Zitto ataka kuandika kitabu kuhusu Chifupa!!

kama mimi ninapendelea kuandika vitabu na wewe unapendelea kuogelea, hivi nikisema niaandika kitabu chochote utaona nina hobby mbaya kuliko ya kwako? ni akili mbovu na uvivu wa kupindukia.

wenzetu walioendelea huandika vitabu juu ya maisha yao, sembuse Zitto kusema ninaandika kitabu kuhusu maisha ya mtanzania mwenzake. tuache kebehi na tuchape kazi huku tukiinua vipaji vyetu.
 
Nadhani kwa wanao mfahamu zito hawatashangaa nini anataka kufanya wasiwasi wangu ni kwa kiasi gani anataka kuthibitisha yale aliyokua anafanya na AMINA ktk harakati zake za kuvunja NDOA ya CHIFUPA.

Nitasubiri Kitabu then tatoa comment kwani we all know kua zito ni OPPURTUNIST sasa najiuliza level yake yake ni ile ya mlimani au imeongezeka?BCS kujinufaisha kwa JINA la Marehemu atakua amevuka kiwango cha kuitwa oppurtunist kwani atakua amesahau kua yeye zito alikua mmoja waliomsababishia matatizo AMINA.

Kwa sababu ametangaza dhamira na kwa jinsi navomfahamu hawezi kubadili msimamo as far as atapata umaarufu sana basi tusubiri ila nategemea ataongelea alivo anza mahusiano na amina ktk kura mpaka alipoanza kutembea nae akijua mke wa mtu,nategemea atatumia kitabu hicho kutuomba radhi watanzania kwa kosa alofanya la kutembea na mke wa mtu

Imefika mahali zito anajisifia uzinifu kwa kuandika kitabu kumsemea mtu alietuhumiwa nae.HAYAAAAAAAAAAAAA NANGOJA.
 
Huyu kweli ni mzee misifa,

Kwa nini asiandike kuhusu Buzwagi? Watu tunameacha misikio yetu wazi tukisibiri hayo atakayoyaona kwenye tume ya madini. Na jimbo lake limeshagawanywa, sijui kama atarudi tena bungeni 2010.

Na sisi wapiga kura tunamsubiri ole wake atuambie kuwa mikataba haina tatizo.
 
This is non-sense. Hivi unaweza ukaandika kitabu kuhusu mtu kwa kuwa naye bungeni kwa muda wa masaa kadhaa; kwa miezi michache?? Zitto do you know what is writing a book on somebody's life? Just stick with Madini Issue will raise you...dont use her name she has given uo her life...please
 
Nilishasema awali kwamba..jamaa huyu amesifiwa sana kupita kiasi, lakini umaarufu wake waweza kuishia within a day kama ataanza kufanya shughuli zenye sura ya namna hii. Kitabu kama anakiandika basi ili kinunuliwe aeleze hata alivyoweza kuingilia ndoa yake Chifupa basi kutanunuliwa sana na ZITTO ataonekana kuwa mkweli wa kuaminika kwa Watanzania. Moto huu wa zitto kula matunda Mr. Mpakanjia ulikuwa unaanza kuzimika lakini sasa naona kijana Zitto anataka ili kuonekana ni kijana msomi na anayefaa kwenye jamii...basi aandike kitabu hicho. Kuandika vitabu si shida.....shida ni kile ulichokiandika...chaweza kukuweka juu au kukumaliza. Ninamshauri bwana mdogo huyu aendelee kujijenga na kujikitika zaidi kwenye mfumo wa kiutendaji hasa katika masuala ya serikali lakini asilete ubishow wa ajabu hapa!
 
Jamani huyu zitto Kabwe amuache mtoto wa watu arest in peace. Mtu keshafariki lakini haishi kutajwa kila siku iendayo kwa mungu lazima Utasikia Amina chifupa sijui kafanya nini.
 
Asalamu alaykum.

Heeee! waswahili wana msemo wao unaoitwa taireni jamani taireni!

Nimesoma maoni takriban ya wajumbe wote kuhusiana na issue hii ya Zitto Kabwe lakini nilichogundua katika michango ya nimeona wengi wamechangia kwa kulaumu na wametumia lugha ya chuki dhidi ya Zitto.

Kwa vile sijaweza kuhifadhi michango yote nitaweza kuchangia kidogo kuhusu mjumbe mmoja amehoji kwa nini Zitto aandike maisha ya Amina kwa kuwa hamfahamu sana eti amesema walikutana wakati wa kuhesabu kura na amekaa nae muda mchache Bungeni.

Kwa hakika naheshimu sana mawazo na maoni ya wengine lakini naomba kuchangia hoja hiyo kwa sababu naona haina uzito sana khasa kwa kuwa Zitto mwenyewe aliwahi kusema kwamba mwanzo wa kujuana na kuzungumza na Amani ilikuwa ni siku ya kuhesabu kura sio kwamba alikuwa hamjui Amina la alikuwa anamjua kama walivyomjua wengine wengi kupitia luninga na magazeti.

Kumjua khasa kiundani Amina, Zitto alisema alianzia kwenye kuhesabu kura. lakini mjumbe mmoja mawazo yake anaona kwamba hakutoshi kuwa ndio leseni ya kujuana kwa kuwa muda ni mfupi sana waliokaa Bungeni na kujuana.

Mimi katika hilo nipo tofauti kwa mawazo yangu naona siku moja inatosha sana kujuana khasa katika jinsia mbili tofauti namaanisha jinsia ya kike na kiume na rahisi sana kujuana kwa saa moja licha ya siku moja maana jicho linaona linampelekea sms moyo na moyo nao unapokea sms na kuipa go ahead kwa hivyo hapo tena mawasiliano ya kimoyo yanakuwa tayari mdomo nao unachukua nafasi yake kutamka unaitwa nani? unakaa wapi? uanfanya shughuli gani? kazi yako ni ipi? nk. jee haitshi kujuana kwa njia hiyo? jee hujapata details za mtu huyo? bila ya shaka umeshapata kutokana na question ndogo tu hizo ambazo zinachukua kama dakika moja tokea kuuliza na kujibiwa.

Sasa baada ya kupata majibu sahihi mnaanza kuzungumza mengine ya kila aina pengine umeipenda kazi yake nzuri aliyoifanya kwa wakati ule jee utashidnwa kumpongeza? laa bila ya shaka una uhuru wa kuuliza na kuulizwa yaani kupokea na kutoa maoni au mawazo yako kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania.

Kuhusu Zitto kuandika kitabu kama muda anao sio vibaya ana khitari yake ana uhuru wake kwa kuzingatia katiba ya Tanzania uhuru alionao kila mtanzania.

ikiwa kuna jambo muhimu amelioan kwa Amina ambapo kwa wengine hakuliona kuna ibaya gani kuliweka wazi wakati jambo hilo litakuwa funzo kwa wananchi wengine hasa vijana? hasa wanawake? si itakuwa faida kwa vijana wanaoinukia katika siasa ambao wataiga ujasiri aliokuwa nao Amina?

Kuna ubaya gani Zitto kuandika kitabu ikiwa yeye ni Mtanzania na anayemuandikia ni Mtanzania? Zitto hata kama sio mwana familia hazuwiwi kutoa maoni hake ana haki hiyo akitaka.

Kuhusu issue ya Zitto kutaka umaarufu mjumbe mmoja anasema eti Zitto anataka umaarufu hivyo kweli hajaupata huo umaarufu au umaarufu gani tena anaousaka zaidi? ikiwa miezi miwili mfululuzo anazungumzwa kwenye vyombo vya habari vyote nchini hajapata umaarufu tu? heee punguzeni kidogo jazba mzungumzie issue na sio chuki binafsi.

Mtu hata kama mnatofautiana kimawazo lakini mumpe haki yake Zitto kwa ukweli amekuwa maarufu sana hivi sasa Tanzania watu wapende wachukukie lakini ukweli ndio huo.

Mie naona nafasi aliyonayo na muda ni mdogo wa kuweza kuandika kitabu lakini kama nitapata kumshauri nataka aandike chengine kuhusiana na woga wa wabunge wa CCM ndani ya Bunge na misimamo yao isiyokuwa na maana na badala ya kutetea hoja za msingi ambazo zinawahusu wananchi wao wanajitetea nafsi yao na serikali yao.

asante na naomba kusasilisha
 
nadhani jamaa alikuja kuomba ushauri hapa na kuona riaksheni ya watu ! sasa kakaa kimya kama sio yeye !
 
Kada mpinzani umeniuliza suali na mimi nakujibu kwa heshima na taadhima kwamba mimi nina mengi sana na nina hakika utayapenda ikitaka.
 
i wonder how long he*ZITTO* has been with amina chifupa mpaka kuandika kurasa zoooote hizo kuhusu amina (alisema alikuwa nae katika kuhesabu kura, na walikuwa wabunge
-je amina huyo amekaa bungeni muda gani mpaka kuelewana na zitto hivyo ?
je zitto alikuwa "rafiki tu" au walikuwa zaidi ya marafiki ?
-je kuna uwezekano zitto akawa anajua nini kilichomsibu amina kama rafiki yake wa karibu sana
-mengine meeengi kuja baadae !
! kama sio hivyo basi ASITUMIE JINA LA AMINA KUPATA UMAARUFU !!

Hiki kitabu kilitoka?
 
Huu uzi wa 2007 ukimsoma vizuri mleta mada na wachangiaji walivyokuwa wanachangia utakubaliani nami kwamba JF ya kipindi na sasa ni kama mlima na kichuguu
 
Back
Top Bottom