Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
what is is true?? kaka? YA WANGWE UNAYAJUA WEWE AU UNATAKA TUFUNUE HUMU??


mimi siamini kama kuna huo mpango, ila siamini kama Zitto eti amejiandikia, kwani nikisema ni wewe son of peasant umeandika kwa lengo lako itakuwa vibaya? ulivyowaza ww ndiyo tutakavyowaza na sisi kuwa wewe ndie uliyeandika
Waberoya! ikiwa mimi nimeshaamua kukutuhumu, kisha nikakushtaki kwenye mahakama ya akili zangu, je watarajia hukumu itakuwa ipi? Mara nyingi (baadhi yetu) tunaandika na kuamini katika yale tunayoyadhani kwamba ni sahihi kuliko ya wengine. pia kwa wakati huohuo tunaamini katika wale tunaowaamini na si wale tunaowachukia hata kama watakuwa wamesema kweli!
 
huyu kila akiamka anakuja na tamko............amefanya hivi ili kuwalainisha na kuwahadaa ili kuwashangaza baadaye...............zitto hana na wala hajawahi kuwa na msimamo isipokuwa ana maslahi binafsi.............itachukua karne nyingi mtu km mimi kumwamini tena
ni wengi tu huja na matamko!! lakini kwa sababu huna chuki nao umeliona tamko la usiyemtaka!!!
Hiki chako sikitofautishi na kisa cha mwanakondoo na mbwa mwitu waliokuwa wakinywa maji mtoni! Mbwamwitu alikuwa akinywa maji juu kwenye chanzo na mwanakondoo alikuwa chini maji yanakotiririkia... lakini kwa sababu mbwa mwitu alikuwa na lake, alimwambia mwanakondoo hana adabu anamchafulia maji!
Nimeeleweka!
 
hivi kuna mtu anaamini habari za magazeti kuwa zitto kabwe angeondoka chadema au kufukuzwa?

chama ambacho ameshiriki kukijenga tangu akiwa shule ya sekondari? na afukuzwe na nani? na hao ambao mpaka 1995 walikuwa ccm damu na waliingia upinzani baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge huko ccm?
HAO NDIO SIWAAMINI KWA ASILIMIA ZOTE!!!! Na ule mwingine ndio ukweli mchungu kabisa ambao unaweza kukuletea machungu pia... (wale wanaohama vyama kwenda vingine ndio wanaitwa MAPANDIKIZI - maana yake hawana uasilia wa asili) mniwie radhi.

nasema hivyo kwa sababu hawana jipya zaidi ya yale walioyarithi kutoka hukoooo.... ndio maana nasema, na nitarudia tena kusema. Upinzani wa kweli utatokana na kizazi cha 1992. Na hawa hawa baadhi ambao hii leo wananangwa na wasiojua siasa.
 
Anajihakikishiaje kama hawezi kunyang'nywa kadi ya Chadema kama anavunja katiba ya Chadema?
UNA UHAKIKA KWAMBA AMEIVUNJA? Nauliza tena (kwa maana sijajibiwa:- Je DEMOKRASIA NI KUWAKUBALIA WENGI, BILA KUJALI WACHACHE WANASEMAJE?)
 
UNA UHAKIKA KWAMBA AMEIVUNJA? Nauliza tena (kwa maana sijajibiwa:- Je DEMOKRASIA NI KUWAKUBALIA WENGI, BILA KUJALI WACHACHE WANASEMAJE?)

Keep it up brother!

Naona mawazo yako nia ya mtu aliyehuru na aliyetayari kutetea UKWELI

Tumeshuhudia wanachadema wengi humu wamtukana sana Zito, wamesema ahame chama, mara fisadi, mara nini na maneno kibao. walikuwa hawajui kuwa kuna adui anawaangalia na kaja kwa style ya chadema inataka kumuua Zitto, ambayo ama kwa hakika imewashtua wengi kuzingatia tuhuma kama hizo zilishakuwepo kwenye kifo cha Wangwe.

Adui kawapata wanatapatapa humu! na kujifanya wanakiua chama ili hali matendo yao wameishakiua siku nyingi.

Tulio nje wanamapinduzi tunaangalia na tuko tayari kusema ukweli daima, pasi kuegemea chama chochote kile

Long Live freedom of mind!!
 
Keep it up brother!

Naona mawazo yako nia ya mtu aliyehuru na aliyetayari kutetea UKWELI

Tumeshuhudia wanachadema wengi humu wamtukana sana Zito, wamesema ahame chama, mara fisadi, mara nini na maneno kibao. walikuwa hawajui kuwa kuna adui anawaangalia na kaja kwa style ya chadema inataka kumuua Zitto, ambayo ama kwa hakika imewashtua wengi kuzingatia tuhuma kama hizo zilishakuwepo kwenye kifo cha Wangwe.

Adui kawapata wanatapatapa humu! na kujifanya wanakiua chama ili hali matendo yao wameishakiua siku nyingi.

Tulio nje wanamapinduzi tunaangalia na tuko tayari kusema ukweli daima, pasi kuegemea chama chochote kile

Long Live freedom of mind!!

Huwa napenda sana kusoma post zako mkuu pamoja na Mwanamageuko japo si kwamba nakubaliana na mawazo yote mnayoyatoa.
 
Sielewi kwa nn nimekosa imani na Zitto kwamba huenda anatumiwa na CCM.

Tunamwangalia kwa macho mawili. Akisema na kufanya zuri, tuko naye, akiendelea na linkage yake na CCM, tutamwacha. Yeye astick kwenye ukweli na kuonesha imani kwa viongozi wengine na kujenga umoja na wa CHAMA. Kama akiendelea na kiburi (na vurugu zake ndani ya chama), ni kweli hatafukuzwa lakini atapoteza umaarufu wake.
 
Eeeh tuepushe CHADEMA na mpasuko wa kisiasa ndani ya chama!!!!! if real Big up brother Zitto
 
mkuu all the best ila uache kuwa msemaji hata kwa mambo ambayo hayakuhusu uzungumze kama kutoka bungeni kwa wabunge wachadema ulihalibu kishenzi unaonekana UNAKIHEREHERE SANA PUNGUZA MKUU!
 
Zito waambie viongozi wako, wanachofanya akina Kibanda, Ngurumo na Kubenea ndiyo kinapeleka haya yote!! magazeti ya chadema ndiyo yanakuandika vibaya ulitaka wengine waanzie wapi kama sio kwenda mbali zaidi

This is just another crap!! Kama ni ukweli kwamba ana mahusiano yenye shaka na mafisadi Kubenea asiseme? Kwani upuuzi aliolopoka kule TBC1 alilazimishwa na Kubenea?

Zitto kachemka big time na yote anayoandikwa nayo ni output ya upuuzi wake!!! Kweli ukipenda chongo.....!!
 
Mh Zitto ametoa tamko. Kwa busara bila kulazimishwa, mjadala unaishia hapo kundelea kujadili ni kupoteza muda na nguvu za kufanya kitu kingine chenye manufaa ama kwako au kwa jamii nzima ya watanzania.

Siku njema.

busara ya wapi wewe? Acha kuwa mwehu, nyie endeleeni kumwamini huyu Punga ndo mtaelewa kwanini wenye akili wanamwita Zitto kirusi ndani ya chadema
 
Uhuru wa mawazo ni mzuri sana popote pale, lakini lazima utumiwe vizuri. Kiongozi lazima upime athali za kauli zako kwa:-
a) Wapiga kura wako
b) Chama chako
c) Kwa viongozi wenzako
d) Wananchi kwa ujumla
e) Kwa familia yako pia

Demokrasia lazima itumike kwa uangalifu kwa mfano kauli moja tu ya kiongozi wa chama inaweza kukijenga au kukimaliza, sasa ukiwa kiongozi pima athari za kauli zako kabla hujaitoa hadharani.

Nasisitiza mwanasiasa asiyeeleweka msimamo wake ni hatari sana. Si busara kwa kiongozi mwandamizi kuongelea mawazo yanayopingana na msimamo wa CHAMA anachokiongoza, kauli hiyo inaonyesha mgawanyiko na kukimaliza CHAMA makusudi.

Kama una dukuduku kwa nini usitumie vikao vya CHAMA? Yaani si lazima utumie akili nyingi kujua Mweshimiwa kwa hilo alichemka vibaya sana, nafikiri ni tukio litakaloweza kufunga mwaka huu.
 
busara ya wapi wewe? Acha kuwa mwehu, nyie endeleeni kumwamini huyu Punga ndo mtaelewa kwanini wenye akili wanamwita Zitto kirusi ndani ya chadema

Kama mtu hayuko huru kueleza mawazo yake ndani ya chadema basi kuna udikteta mkubwa chamani. otherwise, chuki zimepandikizwa dhidi nya zitto kwa vile ana nia ya kugombea uenyekiti na urais 2015.

MBOWE PUNGUZA KUPANDIKIZA MBEGU ZA CHUKI
 
Kama mtu hayuko huru kueleza mawazo yake ndani ya chadema basi kuna udikteta mkubwa chamani. otherwise, chuki zimepandikizwa dhidi nya zitto kwa vile ana nia ya kugombea uenyekiti na urais 2015.

MBOWE PUNGUZA KUPANDIKIZA MBEGU ZA CHUKI

Hakuna anayekataa kiongozi kutoa mawazo yake? kila Chama au Taasisi ina mfumo wake wa kutoa maelezo na hata kama mawazo yako hayasikilizwi pia upo mfumo ndani ya CHAMA husika kuangalia hilo.

Hata ndani ya CCM unafikiri wapo salama? Unafikiri Sita hana duku duku lake? Malecela hana duku duku lake? Mwakalebela hana duku duku lake? Seleli je? sasa umesikia wajibwabwaja hovyo kwenye vyombo vya habari?

Kiongozi kutoa kauli inayopigana na msimamo wa CHAMA unachokiongoza ina maana gani? Jamani hilo nalo linahitaji elimu ya chuo kikuu kulitambua?

Kwa tafsiri yako kama husikilizwi ndani ya CHAMA au Taasisi basi hakuna njia nyingine ni kwenda moja kwa moja kwenye vyombo vya habari kuushitaki uongozi halali kwa umma sivyo?. Sasa huo ni UASI.
 
Katika hili niko tayari kuziamini habari zinazochapishwa na gazeti la MTANZANIA(pamoja na kupauka kwake)kuliko maelezo ya Zitto.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom