Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Ujumbe mfupi wa maneno (SMS) unaohusishwa na mpango wa kijasusi wa kumuua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe umenaswa na Uwazi.

Katika SMS hiyo, aliyeiandika alisisitiza kwamba Zitto atakufa kwa siri lakini kabla ya kutekeleza kifo chake, atanyang’anywa nyaraka zote alizonazo ambazo hazikufafanuliwa kwenye ujumbe.


SMS hiyo, iliyonaswa kwenye simu ya mmoja wa makada wa CHADEMA (jina tunalo), ametajwa kama mmoja wa watakaotekeleza mpango wa kumuua Zitto, inasomeka:

“Nawaarifu kwamba nipo Mara nimemaliza kukutana na viongozi wa Mwanza. Inaelekea hawakubaliani na hoja yetu ya kumfukuza Zitto, sasa nilikwisha kusema kwamba tuweke mkakati kwenye Media JF. Ni …, … na … (yanatajwa majina ya watu).”

SMS hiyo inaendelea: “Ni …, … na … (majina mengine ya makada wa CHADEMA) watatekeleza kazi tuliyowapa na … (anatajwa kiongozi wa CHADEMA) atawapa mtu wa kuwaongezea nguvu.”

Ujumbe huo hauishii hapo, unaendelea: “Kuweni makini, hakikisheni amewapa nyaraka zote alizonazo kabla ya kumuua, usiri unahitajika… atawasaidia kujua nyendo zake na hii tu ndiyo njia ya kukinusuru chama.”

Uchunguzi unaonesha kuwa SMS hiyo ilizunguka kwa watu kadhaa ambao wanadaiwa wapo kwenye mtandao ulioandaliwa kutekeleza mpango wa kukatisha maisha ya Zitto.

Gazeti hili limebaini kuwa mmoja wa wabunge wazoefu wa Viti Maalum (CHADEMA) alitumiwa kisha naye akaituma (kui-forward) kwa mwenzake ambaye ni memba mpya ndani ya bunge.

Gazeti hili lilifuatilia mnyororo wa SMS hiyo na kugundua kwamba wakati ujumbe ukizungushwa kwa wanaodaiwa wana mtandao, uliingia ‘kirusi’ kwa kumfikia mtu ambaye hakukubaliani na wazo la kumuua Zitto.

“Hapa hatari iliyopo ni kwamba kuna mtu ambaye hakubaliani na wazo la kumuua Zitto, ndiyo atakuwa amevujisha,” kilisema moja ya vyanzo vyetu.

Chanzo chetu kilisema kuwa mtu huyo baada ya kupata SMS hiyo, aliituma kwa mama yake Zitto, Shida Salum ambaye naye ‘aliifowadi’ kwa mwanaye.

Gazeti hili lilimpata Zitto na alikiri kupata SMS, ingawa alidai kuwa uchunguzi ndiyo utafanikisha kumnasa mhusika mkuu wa ujumbe huo.
Zitto, akijibu bila uchangamfu, alisema wakati mwingine anahisi kuna watu wanatumiwa ili kukivuruga CHADEMA.

“Nafsi yangu haisemi kama ni kweli. Inawezekana kuna watu wametuingilia, Mungu ndiye anajua,” alisema Zitto.
Alipoulizwa kuhusu kuripoti polisi, Zitto alijibu:

“Nikiripoti ni kwa ajili ya uchunguzi wa kipolisi tu. Sitaki kutoa kwenye vyombo vya habari, sihitaji mgogoro kwenye chama.”
Kwa upande wa Mama Zitto, alikiri kupata SMS hiyo na kueleza kwamba tayari amesharipoti kwenye vyombo vinavyohusika.
“Sitaki kuizungumzia hiyo SMS, inachunguzwa kipolisi,” alisema Mama Zitto.

Gazeti hili lilizungumza na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Regia Mtema ambaye ni mmoja watu wanaodaiwa kutumiwa SMS hiyo ambaye alikiri.

Hata hivyo, Regia aliye pia Ofisa wa Oganaizesheni wa chama hicho alisema: “Hiyo SMS sijatumiwa mimi peke yangu, kila mtu makao makuu anayo.

“Nafikiri kuna watu wametengeneza lakini hakuna mpango wa kumuua na kwanini auawe?”
Baada ya kuzungumza hayo, simu ilikatika na alipopigiwa tena hakupokea mpaka tuliapoamua gazeti kwenda mitamboni.

Wakati Zitto akipuuza ufuatiliaji wa SMS hiyo, chanzo chetu kimoja ndani ya makao makuu ya CHADEMA, kilisema kuwa si vema kudharau vitu kwa sababu ujumbe huo una alama za hatari.

“Mimi sipendi sana kuzungumzia mambo ya marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), lakini naye kifo chake kilitokea akiwa na mvutano na viongozi wengine wa chama kama ilivyo kwa Zitto sasa,” kilisema chanzo chetu.

Mpango wa kumuua Zitto, inakuja baada ya matukio kadhaa ambayo yalikaribia kuondoa uhai wake, ikiwemo kuwekewa sumu kwenye maziwa.

Miaka minne iliyopita, Zitto alikunywa maziwa yenye sumu kwenye hoteli moja jijini Mwanza na kuokolewa na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (CCM), marehemu Amina Chifupa ambaye alimpigia simu na kumueleza asiendelee kunywa.

Hata hivyo, kutokana na wingi wa maziwa aliyokuwa amekunywa dakika chache baada ya kupokea simu ya Amina, aliishiwa nguvu na kukimbizwa kwenye hospitali moja jijini humo ambapo alipatiwa matibabu.

Tags: uwazi11
 
Dah...... kuna watu aisee, yaani kama vile wengine tunavyosema mtume' au yesu wangu, AU MAMA WEEE... KUNA WATU HATA WAKISKIA PAAA' WAWEZA SEMA ZITTOOOOO

balaah
 
Angalau sasa inatia moyo kidogo!
...Nimekuwa naombe Zitto atoe kauli yeye mwenyewe binafsi, na ndiyo njia pekee ya kurudisha imani ya watu, hasa kipindi hiki anachoonekana kama anapishana na wenzie!...Zitto, wewe ni mwanaume, jaribu kubehave accordingly, kuwa na msimamo, ondoa hili wingu la mashaka linalokuzunguka broda!.
PJ Mh. Zito alijieleza sana hapa jamvini, lakini watu hawakutaka kumuelewa. Kuna fitna kubwa zinapikwa kwa ufundi mkubwa - imefikia hatua wanatafutwa vijana wasomi kwa hivi sasa, na kushawishiwa kutoka vyuo vikuu (hususan UDSM) ili waingie CDM kwa gharama zozote ili kufunika pengo za ZK wakifanikiwa kumbandua humo. na hili linafanyika ili kulifanikisha ni lazima kwanza ZK anuke, na akishanuka basi hakuna atakaemtaka (kwa mujibu wa fikra za adui zake na CDM pia)

WASWAHILI WANSEMA:
Ukiona zinduna..........
 
Mimi ningekufa miaka kumi iliyopita nimeshaandikiwa SMS kibao zikinitishia kuniua sijawahi kwenda polisi wala sijawahi kudhuriwa katika kila nchi kuna mahooligan mtu anatishia nyau basi ,kwa hiyo gazeti la uwazi waache siasa za maji taka,hawana la ziada kwenye nchi hii zaidi ya kuchuma fedha za wajinga wanaonunua magazeti hayo na huku Shigongo anayependa kulawiti makaka poa akijifanya mlokole
 
Huu ni uzushi tuu na mimi nahisi zitto mwenyewe ndie mwanzilishi wa hili kuanzia sms mpaka kujiongelesha mbele ya waandishi wa habari,hamna kitu hapa haka kajamaa kanatafuta umaarufu tuu na kana fanya kila njia kaonekane honest ,sio kweli na mimi siamini kabisa kuwa chadema wanaweza kufikia hatua ya kutaka kumuua zitto,kweli amefanya makosa makubwa lakini alifanya kazi kubwa pia na kama chadema imemchoka inaweza kumfukuza mara moja wala hatuna shida na uhai wake yeyey ni kiumbe wa mungu sisi kama chama tukimchoka mtu au mtu akikataa kufuata maadili yetu basi tunamuondoa mara moja bila kuangalia umaarufu,mchango wake au jina na cheo chake hakuna mtyu aliye juu ya chama hata mbowe akikosea leo tunamuondoa kwa taratibu tulizojiwekea.

Nawaomba wananchi wapuuze uzushi huu na naamini zitto ndie aliyeuanzisha na mwisho itajulikana tuu,hii ni tabia yaek tunamjua
 
Hii ndio taarifa tuliyokuwa tunaisubiria kwa hamu.sasa tusonge mbele!
 
Mimi ningekufa miaka kumi iliyopita nimeshaandikiwa SMS kibao zikinitishia kuniua sijawahi kwenda polisi wala sijawahi kudhuriwa ...............

Samahani naomba unikumbushe wewe ni nani tena?
 
vifuata upepo leo mmegeuka? eti zito shujaa, mwanaume na majina mengine, mmesahau juzi mlikuwa wapi? tamko hili linaonesha jinsi gani zitto ndio chadema yenyewe maana mmeanza kupumua.
 
son of peasant umesema ukweli haka kajamaa kameshapoteza umaarufu na sasa kanataka kuurudisha kwa staili hii,watanzania hatudanganyiki labda kigoma
 
hhhahahaha.......hisia za ki-bbc hizo

uongo mtupu
 
bora katamka mwenyewe,maana yamesemwa mengi ili mradi watuharibu kisaikolojia.
 
mmmmh ............hii habari inamaanisha hizo SMS zipo kweli kama gazeti limethubutu kuwanukuu wahusika.
 
Mimi ningekufa miaka kumi iliyopita nimeshaandikiwa SMS kibao zikinitishia kuniua sijawahi kwenda polisi wala sijawahi kudhuriwa katika kila nchi kuna mahooligan mtu anatishia nyau basi ,kwa hiyo gazeti la uwazi waache siasa za maji taka,hawana la ziada kwenye nchi hii zaidi ya kuchuma fedha za wajinga wanaonunua magazeti hayo na huku Shigongo anayependa kulawiti makaka poa akijifanya mlokole
Froida!! Please naomba hayo mengine tuyaache tujadili mada kwanza, kwa sababu yatawatoa wengine nje ya mjadala.

Vema, tulirudi kwenye mada: Inawezekana kabisa, SMS kuwa ni ya kweli na mpango huo ukawepo. Na pia inawezekana kabisa SMS hiyo ikawa ni ya kutungwa ni POLISI na VIONGOZI wa CDM pekee katika uchunguzi wao wanaweza kututhibitishia ukweli wa jambo hilo. Jambo la kutishiwa maisha si dogo hata kama ni la kutungwa. (hii inanikumbusha pia yale ya mkurugenzi mwendeshaji wa makumpuni fulani) sijui uchunguzi wake uliishia wapi? na yule wakili fulani nae sijui yameishia wapi!!

Ila LISEMWALO.....
 
Vizuri sana Zitto umetoa tamko sasa wewe weka kifua mbele simamieni yale munayaamini katika CHADEMA
 
Kwangu mimi taarifa hiyo ingelinipa imani zaidi kama ingelikuwa imeambatana na tamko la kuwataka radhi wale wote aliowakwaza kwa kauli na matendo yake ya hapo awali.
 
Msimlishe maneno Zitto wakati wa kutoa taarifa ukifika atafanya hivyo. Natambua anajua nani anawahitaji zaidi kipindi hiki wale wanaoweza kupata taarifa zake na kuzitamka wazi kabla hajamalizwa na wale wanaomuhitaji kimslahi. Tumewagundua na safari hii hakuna atakayetushinda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom