Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
zito zito zioto zito sasahivi ni mwepesi tu kibaraka wa mafisadi.
Asulubiweeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
enough is enough...kila siku zitto...nyie hamchoki??????? Am tired of this...same story every day...keep quiety pls.this is enough for zitto..
 
SI KWELI HAKUNA MTU WA KIGOMA ALIEMTUMA TENA UKIZINGATIA KIGOMA MJINI BADO WANA HASIRA ZA KUCHAKACHUA MATOKEO YALIYOMPA USHINDI PETER SELUKAMBA AMBAPO WATU WOTE WANAJUA WALICHAKACHUA.

sasa hayo ya zito kayatunga mwenyewe na wala hakupewa ushauri na mtu.
 
Ndugu yangu Bruce, ukisema kayatunga mwenyewe unakosea kwasababu yeye ni mwakilishi wa jimbo lake hivyo akisema yeye maana yake anajua ya jimboni kwake kushinda mwingine yeyote, kama alivyo waziri wa wizara yeyote akisema yeye akiwa kwenye saa za kazi ndio maana itaripotiwa serikali imesema jambo fulani kupitia waziri wake wizara fulani, hivyo mwakilishi wa jimbo akisema maana yake watu wa jimboni kwake wamesema, hayo ya baadaye kama ni uongo au ukweli lakini what we know ni mwakilishi wa jimbo amesema.
SI KWELI HAKUNA MTU WA KIGOMA ALIEMTUMA TENA UKIZINGATIA KIGOMA MJINI BADO WANA HASIRA ZA KUCHAKACHUA MATOKEO YALIYOMPA USHINDI PETER SELUKAMBA AMBAPO WATU WOTE WANAJUA WALICHAKACHUA.

sasa hayo ya zito kayatunga mwenyewe na wala hakupewa ushauri na mtu.
 
Wana JF naomba ufahamu wenu kwa hili.. kipindi Chadema wamesusia hotuba ya rais pale mjengoni(bungeni)..mengi yalisemwa lakini hili la Zitto Kabwe naomba msaada kidogo mimi ni shabiki wa Chadema na ningependa nijue kinachoendelea kwenye chama. Mheshimiwaa Zitto baada ya siku chache nilimsikia TBC akisema kwamba hakubaliani na uamuzi wa wabunge wengine wa Chadema, kwa madai ya kushinikizwa na wananchi wa kigoma akidai kwamba Mh. Kikwete ndie rais aliyefanya mambo mengi kigoma kuliko rais yeyote aliewahi kutawala Tanzania..Swali kwa wanaJF ni kweli madai ya Mh. Zitto ni sahihi? kwa mtazamo wangu Kigoma ndiyo mkoa nambari 1 uliochoka utawala wa ccm na rais wao, kwani ktk majimbo 6 ni 2 tu Ccm wameeza kuchakachua, iweje leo Mh, Zitto aseme alitumwa na wananchi kwamba Kikwete ndiye rais wao bora?? hapo vipi jamani!!

Zitto sio msaliti hata kidogo ila amesema ukweli wake. Kwa vile CHADEMA ni kama chama cha kifalme , na yeye anaonekana anataka kuchukua ufalme wao ndio maana wanamuwekea zengwe . Katika majimbo yote ya Kigoma, jimbo la zitto ndilo lenye barabara za lami, sasa unataka asiseme JK amemfanyia mambo mema??. Acheni kumwandama mtu anapokuwa mkweli, zitto ni kiongozi makini sana
 
I salute you commernder, thats what I was saying. The same words to the dot.

Zitto sio msaliti hata kidogo ila amesema ukweli wake. Kwa vile CHADEMA ni kama chama cha kifalme , na yeye anaonekana anataka kuchukua ufalme wao ndio maana wanamuwekea zengwe . Katika majimbo yote ya Kigoma, jimbo la zitto ndilo lenye barabara za lami, sasa unataka asiseme JK amemfanyia mambo mema??. Acheni kumwandama mtu anapokuwa mkweli, zitto ni kiongozi makini sana
 
Zitto sio msaliti hata kidogo ila amesema ukweli wake. Kwa vile CHADEMA ni kama chama cha kifalme , na yeye anaonekana anataka kuchukua ufalme wao ndio maana wanamuwekea zengwe . Katika majimbo yote ya Kigoma, jimbo la zitto ndilo lenye barabara za lami, sasa unataka asiseme JK amemfanyia mambo mema??. Acheni kumwandama mtu anapokuwa mkweli, zitto ni kiongozi makini sana
duh kwa msingi wa lami basi wabunge wa kilimanjaro walitakiwa wamlambe miguu kwani mtandao wa lami umeenea mpk vijijini lkn nilidhani huo ni wajibu wa government ambao wamechelewa kuuteleza for 49 yrs kwa maeneo ambayo bado watie akili
 
Hizi lugha za matusi na jazba katika forum yetu anazilea nani? Hatuwezi kulumbana mpaka tutukanane. Tunashindana kwa hoja au ujuzi wa kutema matusi? Kwa hilo tunaipa forum yetu sura gani katika forum zingine za kisomi? Ningewaomba, kama ambavyo nimekuwa nikiwaomba wana jamii forum wenzengu tujadiliane kwa heshima na busara.

Baada ya hapo napenda nitofautiane na wachangiaji wanaomlaumu mheshimiwa Zito kwa kuwa na urafiki na Mh Kikwete. Japo sina uhakika na urafiki wao, mtizamo wangu ni kwamba siasa za upinzani sio uadui. Yawezekana kabisa mimi nikawa Chadema na mke wangu akawa CCM. Mfano mzuri ni Mh. Dr Slaa amabaye wakati wa Uchaguzi Mkuu 2005 yeye alikuwa Chadema lakini mke wake alikuwa CCM. Yawezekana pia mimi nikawa CCM baba yangu akawa Chadema. Mfano mzuri ni Mh. Hayati mwalimu Nyerere ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 alikuwa CCM na mwanae mpendwa Makongoro Nyerere alikuwa NCCR Mageuzi. Mfano mwingine ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Masha ambaye yeye ni CCM lakini baba yake alikuwa kada wa Chadema. Ukiacha udugu wa damu, mifano ya marafiki wanaoamini katika vyama tofauti ni mingi sana. Mh. Mwakyembe wa CCM na DR Mvungi wa NCCR Mageuzi ni marafiki wa siku nyingi licha ya tofauti zao za kisiasa.

Kwa hali hiyo mimi sioni tatizo Mh Zito kuwa mbunge na mwanachama wa Chadema na akaendelea kuwa rafiki wa karibu wa Mh. Kikwete. Kama Zito Kabwe kuna kosa lolote alilolifanya sio lazima lihusishwe na urafiki wake na Kikwete. Suala la yeye pamoja na baadhi ya wabunge wenzake kutofautiana na uamuzi wa kumsusia Raisi ni tofauti za kawaida za mitizamo ya kisiasa. Ndio maana Nzito na wenzake kama Mh. Shibuda hawakuwa wanafiki toka mwanzo. Walibainisha misimamo yao ndani ya kikao cha wabunge.

Alafu, urafiki wa Kikwete na Zito nijuavyo mimi sio kitu cha siri ndani ya Chadema. Kwa kujua ukawaida wa jambo kama hilo katika siasa za kistaarabu ndiyo maana Chadema ikampitisha Zito kugombea ubungei katika jimbo lake na akashinda. Na ndio maana Chadema walimpa cheo kikubwa cha Unaibu Katibu Mkuu. Hatuna haja ya kutoa hoja za kumchonganisha Mh. Zito na Chama chake kwa hisia zetu tu.
 
Tatizo kubwa kila mtu anajìfanya mtu safi na ana mchangö mkubwa Chadema na bingwa wa kukosöa kutoa lugha chafu na za kebei kwa ZITO, wengi wenu mnaoponda ZITO nì 'Sycophant' ZITO ni kiongozi makini sana amna anaeweza kujipima nae kisiasa kwa nyie mnaömponda, kama tatizo urafiki na Jk mbona MBOÈ alikuwa mtu wa kwanza kumkombatia JK 2005 kumpongeza mbona awasèmì?achèni majungu
 
Kijana anajitahidi, kwa kuwa atahamia ccm kabla ya 2015, obviously atagombea kinondoni kwa tiketi ya ccm. thanks
 
23 September 2010
Na waandishi wetu

kabwee_fr.jpg

WAKATI kampeni zikipamba moto, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, amekiri serikali ya CCM imejenga uchumi imara. Amepongeza utendaji kazi wa serikali za CCM na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi.

Zitto anayewania ubunge Kigoma Kaskazini, alisema hayo juzi jioni katika Uwanja wa Mashujaa, alipomnadi mgombea ubunge wa Mtwara Mjini, kwa tiketi ya chama hicho, Jetha Othuman. Akizungumzia mafanikio ya serikali ya CCM, Zitto alimmwagia sifa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akisema amefanya mambo makubwa katika uongozi wake na kama kuna makosa ni ya kibinadamu.

“Hakuna anayeweza kila kitu kama yapo yaliyomshinda huo ni ubinadamu,” alisema Zitto na kuongeza kuwa, uchumi imara uliwezesha kushuka kwa mfumko wa bei. Aliwaponda watu wanadai serikali ya CCM inabagua wapinzani, akisema imekuwa ikitekeleza Ilani kwa kufikisha maendeleo hata kwenye maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani.

“Wanaosema serikali ya CCM inabagua katika kugawana keki ya taifa hao ni waongo, imefikisha maendeleo hata kwa wapinzani,” alisema huku akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika majimbo ya Karatu, Kigoma na Sumbawanga. Alisema Kigoma ni ngome ya upinzani, lakini imepiga hatua kubwa katika maendeleo, akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa ya barabara, maji na umeme.

Source: UHURU

Kumbe source ni UHURU-Kongwe la chama cha mafisadi!
 
Zitto sio msaliti hata kidogo ila amesema ukweli wake. Kwa vile CHADEMA ni kama chama cha kifalme , na yeye anaonekana anataka kuchukua ufalme wao ndio maana wanamuwekea zengwe . Katika majimbo yote ya Kigoma, jimbo la zitto ndilo lenye barabara za lami, sasa unataka asiseme JK amemfanyia mambo mema??. Acheni kumwandama mtu anapokuwa mkweli, zitto ni kiongozi makini sana

Maendeleo ya mahali katika nchi si maamuzi ya Raisi ni maamuzi ya wananchi kupitia bunge. Sidhani kama nchi hii itabaki na amani yake ikiwa Raisi anaweza kuwa na nafsi ya kuamuru barabara za jimbo gani ziwekewe Rami. kama hivyo ndivyo haya ndiyo mapugufu ya katiba yetu na hayatakuwepo tena. Zitto hana sababu ya kumpigia magoti Jk ili jimbo lake liwekewe barabara za Rami hili ni swala na Priorities katika maendeleo ya nchi yetu si swala la Mbunge kwenda kumpigia magoti Rais.

Kimsingi Zitto katika hoja hii ameonyesha udhaifu mkubwa maana haelewi jinsi nchi inavyotakiwa iendeshwe na yeye anaonyesha anaunga mkono huu UTUMWA na Rushwa ya kubembeleza. Sioni tofauti na Rushwa ya Ngono wanayodaiwa akina dada wanapotaka kitu fulani kwenye maofisi mbalimbali. Zitto angekuwa mdada tungemfikiria vinginevo katika hili. This is shame to him and he must apologize kama kweli yeye ni mwanasiasa mwadilifu asiyetumia njia za mgongo wa nyuma kufaniksiha mambo binafisi yasiyokuwa na masilahi ya kitaifa.

Naamini Kigoma inahitaji Rami kama mkoa nasiyo jimbo moja la zito pekee. Jimbo moja katika mkoa mzima kuwa na Rami huku barabara zingine zote ni vumbi sidhani kama hayo ni maendeleo. Hizi ni siasa za kuwandanganyia wapiga kura tu ambazo haziwezi kuwa endelevu.

Nasema haziwezi kuwa endelevu kwa sababu ikiwa JK atatoka madarakani, zitto atapata wapi hela za kufanyia mtengenezo ya hizi barabara kama hazitambuliki kama sehemu ya mpango wa maendeleo ya Taifa bali ni favour tu ya JK kwa zitto ili awalaghai wapiga kura wake?

Nadhani kunauhalali wa watu kuhoji mahusiano ya Zitto na JK kwa vile yanamasilahi binafsi tu na si kwa watanzania wote. Zitto katika hili anaangalia masilahi yake tu na simasilahi ya wengi.

Zitto analo swali la kujibu kama kweli yeye ni mwanmapinduzi wa kweli au yamemshinda na ameamua kuwajoini maadui zake?
 
Ndugu Ngonini, kwa kadili nilivyosoma andiko kuhusiana na kauli ya KABWE naona kiini cha maelezo yake ilikuwa ni kutoa shukurani kwa Mh. Raisi kwa kusikiliza kilio cha wapiga kura wake. Mh ZITO hakuwa anajadili mapungufu ya kikatiba juu ya madaraka ya Raisi kufanya hivyo. Bila shaka MH. ZITO alizingatia kwamba mamlaka ya Raisi juu ya hilo hakujipa mwenyewe bali yametokana na katiba ambayo pia hakuitunga yeye. Kama katiba ina matatizo au la sio tatizo la KABWE wala MH KIKWETE bali ni tatizo la watanzania wote. Maana, ni chini ya katiba hiyo hiyo ambayo tunasema ni mbovu ndio MH ZITO na MH KIKWETE wamechaguliwa. Hata kama ina mapungufu kiasi gani wanalazimika kuiheshimu na kuitii mpaka itakapokosa nguvu za kisheria.
 
Bado sijakusoma maana umetoka kwenye pointi ya msingi. Tunachokikataa hapa ni zitto kujipendekekeza kwa jk eti kwa sababu amepeleka rami jimboni kwake hivyo wapigakura wake watamshangaa. Tunasema kupeleka rami jimboni si maamuzi ya jk ni maamuzi ya bunge kama jk anatumia udhaifu wa katiba kutoa upendeleo wa maendeleo basi haya ndo mapungufu ya katiba lakini zitto lazima afahamu kujengewa rami jimboni kwake siyo favour wanastaili wanachi wa jimbo hilo. Hivyo hana haja ya kumramba miguu jk pasipo sababu ya msingi.
 
duh,politics kweli mchezo mchafu,nani wa kuaminiwa sijui bado wanao kuchafua au wewe mwenyewe!
 
Bado sijakusoma maana umetoka kwenye pointi ya msingi. Tunachokikataa hapa ni zitto kujipendekekeza kwa jk eti kwa sababu amepeleka rami jimboni kwake hivyo wapigakura wake watamshangaa. Tunasema kupeleka rami jimboni si maamuzi ya jk ni maamuzi ya bunge kama jk anatumia udhaifu wa katiba kutoa upendeleo wa maendeleo basi haya ndo mapungufu ya katiba lakini zitto lazima afahamu kujengewa rami jimboni kwake siyo favour wanastaili wanachi wa jimbo hilo. Hivyo hana haja ya kumramba miguu jk pasipo sababu ya msingi.

Kiongozi anaposhindwa kutekeleza wajibu wake kwa kuwapatia watu fulani haki yao anapaswa kulaumiwa kwa kutotimiza wajibu. Kwa upande mwingine kiongozi anayetimiza wajibu wake kwa kuwapa watu wake haki wanayostahili anastahili pongezi kwa kutimiza wajibu wake. Misingi ya kumsifia sio kwakuwa alichofanya ni favour bali ni kwakuwa ametimiza wajibu wake. Hamna popote Mh. Zito anajikomba kwa J.K. Na alipokuwa anamsifia JK kwa hili hakuwa anamsifia yeye binafsi bali kama kiongozi mkuu wa dola.

Wapiga kura wa jimbo la Moshi mjini wanapomsifia Ndesambura kwa kuwaletea maendeleo hawajikombi na wala alichokifanya Ndesambura kwao sio favour bali ni jukumu lake. Wanamsifia kwakuwa ametekeleza jukumu lake. Sio tofauti kati ya hilo na hili la Kabwe kumsifia mkuu wa dola na dola na dola yake kutekeleza jukumu lake.

Kama Raisi amefanya chochote kutokana na madaraka aliyonayo yanayotokana na mapungufu ya katiba hilo sio suala la Kabwe na Kikwete peke yake maana katiba haikutungwa wala haiwezi kurekebishwa na Kikwete na Kabwe peke yao.
 
Anayemuandika zitto kuwa ni maarufu kuliko chadema si mkweli na nadhani anashirikiana na zitto aandike then zitto akanushe,kwa kweli simuamini hata chembe moja zitto.mnafiki na msaliti..Yuda alimsaliti Yesu akaishia kujinyonga...zitto ataishia wapi!?!tusubiri tuone
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom