Siku zote chama ni taasisi na huwa inaheshimika kuliko mtu au mwanachama,
siku zote epuka kuwa extrovert(kulazimisha watu wakujue au kukuzungumzia wewe sana na haswa kwa mabaya).
Zitto watu wanakutakia mema ndio maana wanapiga kelele za kukuktaka ubadilike,urudi kwenye mstari na taswira yako ya awali kwa jamii,
mvuto wako unafifia kwa kasi,jamii haitasita kukutema ikiendelea na hisia hizi ilizonazo kwa sasa juu yako.
Heshima hainunuliwi dukani,chama kina wazee na watu wengine wa heshima,
si jambo la busara ukatoa tamko lolote ambalo viongozi ndani ya chama na wanachama hata wapenzi wa chama wakatilia shaka,kamwe zitto hautaweaza kuwa juu ya chama au wanachama,siku zote heshimu hisia za wanachama.
Nimesoma kwenye mwananchi la jana ukisema kuwa masuala yote yatatatuliwa ndani ya chama,sasa kama unaelewa chama ndio chenye uwezo wa kutafuta ufumbuzi wa kila kitu ni bora ukawa na heshima hiyo kwa chama na hata maamuzi yanayofikiwa na vikao halali vya chama
iwe mwiko kwako kutoa tamko lenye utashi binafsi huku ukisahau nafasi yako kama kiongozi ndani ya chama,zitto kumbuka,lolote utakalosema halitachukuliwa kama ni mtazamo wa zitto kama zitto bali ni mtazamo wa moja ya viongozi wa juu wa chadema.
Mdomo uumba,hakuna silaha kali na ya maangamizi kama ulimi,jifunze kuutumia vizuri ulimi wako kwani umri wako ni bado ktk harakati au safari za kisiasa,nikikulinganisha na mzee sitta au dr slaa umri wako ni nusu ya umri wao.kwa mapenzi mema kwako na safari yako ya kisiasa zingatia hayo na ukumbuke chadema haitapita wala kufa kwani ni taasisi ila mimi na wewe tutapita na kufa,
pamoja tunaweza