Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Msimlishe maneno Zitto wakati wa kutoa taarifa ukifika atafanya hivyo. Natambua anajua nani anawahitaji zaidi kipindi hiki wale wanaoweza kupata taarifa zake na kuzitamka wazi kabla hajamalizwa na wale wanaomuhitaji kimslahi. Tumewagundua na safari hii hakuna atakayetushinda

Posti hiyo hapo juu imetoka kwenye facebook yake sasa nani anamlisha maneno ebo
 
Anajihakikishiaje kama hawezi kunyang'nywa kadi ya Chadema kama anavunja katiba ya Chadema?
 
safi sana zitto kwa kujisafisha sisi vijana wenye moyo safi walio kwenye harakati ya kuikomboa nchi yetu zidi ya mazimwi/mafisadi tumepata ufunuo , mie binafsi nimefarijika lakini kwa nini hawa waandishi waliomaliza primary hasa magazeti ya Udaku na Wakora kama jambo leo, Uwazi ya Shingongile, hawa watu badala kuandika mabo ya kukomboa nchi wapo kwa ajiri ya chokochoko sijui kukitokea kumekuwepo umwagaji wa damu uliosababisha na wao itakuwaje? kumbuka Erc alisababisha gogoro la Mhe. Amina Chif.. mpaka mauti yake kwa kumchonganisha na Zitto bado wako nyuma yako kuwa makini, Unakumbuka ya Mange wa pale Africa sana endelea na Erc utaona mengi
 
Nafikiri Zitto anatakiwa ajiulize kwa nini watu wanamsemasema sana, nafikiri ni kwa sababu walimuona kama kiongozi bora (kijana) na mzalendo wa kweli kwa taifa lake. Kapata umaarufu mkubwa tu kisiasa na hizi chochoko zinazodaiwa juu yake kutaka kuvuruga chama chake zinaweza kumchafua na kuondoa imani kwa watanzania juu yake waliojawa na mashaka mengi juu yake kwa sasa.

Zitto jiulize kwa nini wewe tu kila siku? Watanzania na hasa vijana wanakupenda ndio maana wanapiga kelele, wasikilize yao ukichanganya na yako utabaki Zitto yule yule shujaa wa kweli, jisahihishe kila siku, kubali unapokosa na pia wasikilize wazee (wenye busara zao)
 
Hawa Chadema sasa wanaanza kutugawa sisi wananchi tuache kushabikia vyama maana ni uozo mtupu..
 
iTS GOOD U HAVE COME OUT CLEAN,thanks broda we wre worrying!!

I think he has come out dirty by saying he will not be expelled from Chadema, is he the one who is making party decisions? It also seems that this statement is for his friends only including Iteitei Lya Kitee.
 
:embarrassed: who is zito,au yeye mwenyewe amejiandikia kujipa title tena, e.g Koffi alijitangaza kufa ila akumbukwe Congo,baada ya Falii pupa kumfunika ktk muziki
 
Nimefurahi sana kuona Mh. Zitto unasoma post hizi

Good, endelea kupata maoni ya watanzania juu ya tamko lako
 
Mpango wa kumuua Zitto, inakuja baada ya matukio kadhaa ambayo yalikaribia kuondoa uhai wake, ikiwemo kuwekewa sumu kwenye maziwa.

Miaka minne iliyopita, Zitto alikunywa maziwa yenye sumu kwenye hoteli moja jijini Mwanza na kuokolewa na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (CCM), marehemu Amina Chifupa ambaye alimpigia simu na kumueleza asiendelee kunywa.

Hata hivyo, kutokana na wingi wa maziwa aliyokuwa amekunywa dakika chache baada ya kupokea simu ya Amina, aliishiwa nguvu na kukimbizwa kwenye hospitali moja jijini humo ambapo alipatiwa matibabu
.


Hii ndio sababu bado anaishi hadi leo, nadhani na safari hii demu wake aliyendani ya chadema atamuokoa.
 
Mh Zitto ametoa tamko. Kwa busara bila kulazimishwa, mjadala unaishia hapo kundelea kujadili ni kupoteza muda na nguvu za kufanya kitu kingine chenye manufaa ama kwako au kwa jamii nzima ya watanzania.

Siku njema.
 
Ujumbe mfupi wa maneno (SMS) unaohusishwa na mpango wa kijasusi wa kumuua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe umenaswa na Uwazi.

Katika SMS hiyo, aliyeiandika alisisitiza kwamba Zitto atakufa kwa siri lakini kabla ya kutekeleza kifo chake, atanyang'anywa nyaraka zote alizonazo ambazo hazikufafanuliwa kwenye ujumbe.


SMS hiyo, iliyonaswa kwenye simu ya mmoja wa makada wa CHADEMA (jina tunalo), ametajwa kama mmoja wa watakaotekeleza mpango wa kumuua Zitto, inasomeka:

"Nawaarifu kwamba nipo Mara nimemaliza kukutana na viongozi wa Mwanza. Inaelekea hawakubaliani na hoja yetu ya kumfukuza Zitto, sasa nilikwisha kusema kwamba tuweke mkakati kwenye Media JF. Ni …, … na … (yanatajwa majina ya watu)."

SMS hiyo inaendelea: "Ni …, … na … (majina mengine ya makada wa CHADEMA) watatekeleza kazi tuliyowapa na … (anatajwa kiongozi wa CHADEMA) atawapa mtu wa kuwaongezea nguvu."

Ujumbe huo hauishii hapo, unaendelea: "Kuweni makini, hakikisheni amewapa nyaraka zote alizonazo kabla ya kumuua, usiri unahitajika… atawasaidia kujua nyendo zake na hii tu ndiyo njia ya kukinusuru chama."

Uchunguzi unaonesha kuwa SMS hiyo ilizunguka kwa watu kadhaa ambao wanadaiwa wapo kwenye mtandao ulioandaliwa kutekeleza mpango wa kukatisha maisha ya Zitto.

Gazeti hili limebaini kuwa mmoja wa wabunge wazoefu wa Viti Maalum (CHADEMA) alitumiwa kisha naye akaituma (kui-forward) kwa mwenzake ambaye ni memba mpya ndani ya bunge.

Gazeti hili lilifuatilia mnyororo wa SMS hiyo na kugundua kwamba wakati ujumbe ukizungushwa kwa wanaodaiwa wana mtandao, uliingia ‘kirusi' kwa kumfikia mtu ambaye hakukubaliani na wazo la kumuua Zitto.

"Hapa hatari iliyopo ni kwamba kuna mtu ambaye hakubaliani na wazo la kumuua Zitto, ndiyo atakuwa amevujisha," kilisema moja ya vyanzo vyetu.

Chanzo chetu kilisema kuwa mtu huyo baada ya kupata SMS hiyo, aliituma kwa mama yake Zitto, Shida Salum ambaye naye ‘aliifowadi' kwa mwanaye.

Gazeti hili lilimpata Zitto na alikiri kupata SMS, ingawa alidai kuwa uchunguzi ndiyo utafanikisha kumnasa mhusika mkuu wa ujumbe huo.
Zitto, akijibu bila uchangamfu, alisema wakati mwingine anahisi kuna watu wanatumiwa ili kukivuruga CHADEMA.

"Nafsi yangu haisemi kama ni kweli. Inawezekana kuna watu wametuingilia, Mungu ndiye anajua," alisema Zitto.
Alipoulizwa kuhusu kuripoti polisi, Zitto alijibu:

"Nikiripoti ni kwa ajili ya uchunguzi wa kipolisi tu. Sitaki kutoa kwenye vyombo vya habari, sihitaji mgogoro kwenye chama."
Kwa upande wa Mama Zitto, alikiri kupata SMS hiyo na kueleza kwamba tayari amesharipoti kwenye vyombo vinavyohusika.
"Sitaki kuizungumzia hiyo SMS, inachunguzwa kipolisi," alisema Mama Zitto.

Gazeti hili lilizungumza na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Regia Mtema ambaye ni mmoja watu wanaodaiwa kutumiwa SMS hiyo ambaye alikiri.

Hata hivyo, Regia aliye pia Ofisa wa Oganaizesheni wa chama hicho alisema: "Hiyo SMS sijatumiwa mimi peke yangu, kila mtu makao makuu anayo.

"Nafikiri kuna watu wametengeneza lakini hakuna mpango wa kumuua na kwanini auawe?"
Baada ya kuzungumza hayo, simu ilikatika na alipopigiwa tena hakupokea mpaka tuliapoamua gazeti kwenda mitamboni.

Wakati Zitto akipuuza ufuatiliaji wa SMS hiyo, chanzo chetu kimoja ndani ya makao makuu ya CHADEMA, kilisema kuwa si vema kudharau vitu kwa sababu ujumbe huo una alama za hatari.

"Mimi sipendi sana kuzungumzia mambo ya marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), lakini naye kifo chake kilitokea akiwa na mvutano na viongozi wengine wa chama kama ilivyo kwa Zitto sasa," kilisema chanzo chetu.

Mpango wa kumuua Zitto, inakuja baada ya matukio kadhaa ambayo yalikaribia kuondoa uhai wake, ikiwemo kuwekewa sumu kwenye maziwa.

Miaka minne iliyopita, Zitto alikunywa maziwa yenye sumu kwenye hoteli moja jijini Mwanza na kuokolewa na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (CCM), marehemu Amina Chifupa ambaye alimpigia simu na kumueleza asiendelee kunywa.

Hata hivyo, kutokana na wingi wa maziwa aliyokuwa amekunywa dakika chache baada ya kupokea simu ya Amina, aliishiwa nguvu na kukimbizwa kwenye hospitali moja jijini humo ambapo alipatiwa matibabu.

Tags: uwazi11


Pia gazeti la Mtanzania limeandika habari hiyo, likiweka wazi kuwa, "Huo ni mkakati wa CCM uliosukwa kuimaliza Chadema baada ya kuona kinakubalika kwa wengi".

Limeongeza; Miongoni mwa wanaodaiwa kuhusika katika mkakati huo ni voingozi wa CCM ambao wana nia ya kugombea urais mwaka 2015, ambao wanaona umoja ndani ya Chadema ni kikwazo kwao.

Limeongeza: Mmoja wa mgogo hao, Waziri Mwandamizi katika serikali ya Rais jakaya Kikwete, ambaye mara nyingi amekuwa akijipambanua kuwa ni rafiki wa karibu wa rais Jakaya Kikwete, anatajwa kuwa nyuma ya mkakati huo.

Limesema; Moja ya mikakati ya kukisambaratisha chama hicho inayodaiwa kuandaliwa kwa umakini wa hali ya juu ni kuwapo kwa taarifa za viongozi wa Chadema kuandaa mpango wa kumuua naibu Katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe
 
Naendelea kujisomea kwa umakini Katiba ya JMT ili kujua ubora na mapungufu yaliyomo ukizingatia changamoto tulizonaso sasa na zijazo siku za usoni, niko sehemu ambayo inaeleza taratibu za kufuata kumuondoa CAG!!

Nawaacha nyie muendelee kumjadili Zitto, pengine ndiko maslahi ya taifa yalikojikita zaidi!!
 
CCM on the move watumia SMS na email kwenye kampeni hazikufanya kazi sidhani kama sasa zitafanya kazi, wameona Zitto hana mpango wa kutoka CDM na chama kinazidi kupata nguvu kila kukicha wameona watumie silaha yao ya mwisho ya vitisho kwa wananchi, hamtaweza.
 
Mh!lengo ni kuiua chadema!mnataka kutawala milele?mbona mliiua NCCR MAGEUZI makafikiri mmemaliza kazi!hata mkiiua chadema,kitaibuka chama kingine!issue hapa sio chama bali ni ukombozi kwa kupitia njia yeyote!!
 
Zito waambie viongozi wako, wanachofanya akina Kibanda, Ngurumo na Kubenea ndiyo kinapeleka haya yote!! magazeti ya chadema ndiyo yanakuandika vibaya ulitaka wengine waanzie wapi kama sio kwenda mbali zaidi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom