Wakuu habari za punde ni kwamba Zitto Kabwe atahamia NCCR mageuzi, na kwamba atagombea ubunge kigoma kaskazini kwa chama hicho. kwa hiyo basi atakua ametimiza kazi yake ya kuivuruga cdm na mafisadi watashangilia. ila cdm itaendelea kuwepo na kuendelea kufanya kazi uzuri.
By the way where is Aman Wal Kabourou at the moment?
Zitto tatizo lake ni kuwa na blid ambition kupitiliza! Much as people admire him for his guts lakini huyu Bwana is not a consensus builder. Tangu uchaguzi uishe amefanya mambo matatu kuonyesha udhaifu wake;
1) Alikuwa ni mwana-Chadema wa kwanza kutamka kwamba CHADEMA inakusudia kuunda upinzani bungeni peke yake maana namba wanazo. Hata kama ni kweli Chadema walikusudia kufanya hivyo hili lisingetoka kwa Zitto na pengine limefanya vyama vingine kukatishwa tamaa.
2) Zitto alitangaza kugombea Uongozi wa Upinzani Bungeni ndani ya chama chake. In other words he was trying to preempt Chadema wamchague kwa kuruka mstari. Jumping the Que! Ni weakness kubwa.
3) Jana katika hali ya kujikomba ametoboa siri (mapema) kwamba alitofautiana na wenzake kuhusu kususia hotuba ya JK huko Dodoma. What was the aim of going public this early wakati issue ni hot hot kama sio ku-undermine authority and cause ya Chadema?
Kwa mtizamo wangu Zitto is more of a liability than an asset in Chadema and I think Chadema should let go. Wahaya wanasema: AGENDE!
Wakuu habari za punde ni kwamba Zitto Kabwe atahamia NCCR mageuzi, na kwamba atagombea ubunge kigoma kaskazini kwa chama hicho. kwa hiyo basi atakua ametimiza kazi yake ya kuivuruga cdm na mafisadi watashangilia. ila cdm itaendelea kuwepo na kuendelea kufanya kazi uzuri.
mie nadhani atupe sababu kwanini alikuwa hakubaliani na pendekezo hilo,lazima alikuwa na sababu,sasa asiseme tu tulipiga kura wengi wape,vilevile atuambie kwanini hakukubaliana na maamuzi yale then uamuzi utolewe na wana JF.
mbona wenye mawazo km ya zito wakati wa malumbano kabla ya kuingia bungeni walikuwa wengi ,akiwemo ndesa kahigi .
mbona wewe umemlenga zito pekee
Simpo, Zitto siyo meku na wala siyo mgalatia.
You have missed the point entirely. Zitto Kabwe alikuwa na kila haki ya kupingana na wazo la walkout akiwa ndani ya vikao vya chama. Ila baada ya viongozi wa CHADEMA kupiga kura na kuamua kuwa tuna walkout wakati Rais anahutubia Bunge, Zitto alipaswa kuelewa kuwa huo ndio uamuzi wa chama. Kwa kufuata principle ya collective responsibility, yeye alipaswa kuungana na wenzake na kuingia Bungeni halafu ashiriki kwenye walkout hata kama alikuwa haungani na uamuzi huo. Kosa alilofanya la kwanza ni kuamua kutokwenda Bungeni. Lakini kosa kubwa zaidi ni kitendo chake cha kuongea na waandishi wa habari na kutoa siri za vikao vya CHADEMA kuwa kulikuwa na mvutano kwenye hili jambo na yeye hakuunga mkono. CHADEMA wanafaa wamchukulie hatua za kinidhamu, lakini sidhani kwa sasa kosa hili ni kubwa kwa yeye kufukuzwa uanachama. Hapa ni kuandikiwa barua na Katibu Mkuu wa chama kutakiwa atoe maelezo ya kutoa siri za chama hadharani na kupingana na uamuzi wa chama. Ladba kama itokeee ana kaidi na kuonesha dharau kwa uongozi wa chama, hapo ndipo wanaweza kuchukua hatua zaidi.
Kuna wachangiaji wengine humu wamesema, mbona Kamati Kuu ya CCM ilipoamua kumfukuza Spika Samuel kuna wengi walipinga uamuzi huo lakini hawakutoka nje na kutoa siri za kikao cha chama kuwa kulikuwa na mvutano.
Kwa kweli sijamwelewa kabisa Zitto Kabwe kwa kitendo alichofanya.
Mlimwandama Wangwe mpaka mkamuua alipoonesha msimamo wake sasa naona mnataka yatokee pia kwa zitto yaliyotokea kwa Wangwe kutofautiana ndio demokrasi. jiulize mbona si wote ccm waliopenda sita aondolewe hata akina kinana hakupenda na leo mbona hawamlaum?bado najiuliza nani mwenye busara na wapi chadema inaelekea kama wakiwa bungeni wanashindwa kuwa na msmamo mmoja iweje leo hii walalamikie cuf wananuliwa
nilijiuliza na badonajiuliza kati ya hawawatu waliokataa kuingia bungen na kutoka na walioingia na kutoka nani wenye busara
mtafika kwa mtaji huu