Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Wakuu zangu nimemsoma Mbowe pia sielewi kinachoendelea Chadema. Je, aloyasema Mbowe ndio msimamo wa Chadema maanake katibu wake Dr. Alisema hayatambui matokeo, hivyo mtaweza vipi kumtambua rais ambaye matokeo ya uchaguzi wake hamuyatambui?..
 
Kutoka lilikuwa Azimio la vikao si Mbowe, So Zitto ameonyesha tu utovu wa Nidhamu na nina hakika atajadiliwa na vikao kwa kukurupuka kwenye vyombo vya habari, manake sio yeye tu ambaye hakuwa bungeni lakini wenzake wako kimya.
Chama chochote duniani hakiongozwi na hisia binafsi bali maamuzi ya vikao wazee. na yeyote anayekwenda kinyume na maazimio ya vikao anatakiwa kuwajibika. Narudia tena Zitto asipokuwa makini atapotezwa na ccm kama Lamwai Aman Kaburu, Tambwe na wenzao wengi na yeye umaarufu wake unajengwa na upinzani nje ya upinzani he is nobody

Hilo hapo si kweli mkuu, tuliona juzi juzi Democratic walivyokuwa wanahaha kupata kura za kupitisha huduma ya afya kwa wote. Na ni baadhi ya democratic ambao walikuwa wanapingana na Obama wazi wazi kabisa. Mpaka mwisho Obama alipowapa walichotaka ndio mswada ukapita.

Nakubaliana na wewe kusema kwamba Zitto hakutakiwa kutoka media na kuzungumzia maono yake binafsi. Lakini swala la yeye kuto kufika bungeni ni haki yake ya msingi kama aliona linaweza kudhohofisha taaluma yake katika siasa. Narudia ni demokrasia kutokukubaliana katika maamuzi ya kichama.
 
ndugu wana CDM, uvumilivu katika siasa ni kitu muhimusana. ZITO ni mpiganaji kama alivyo kamanda mkuu. Alichokifanya ni MTAZAMO wake, na waweza usimufurahishe mwingine. Hivyo, hii haimanishi kuwa amepotoka U CDM wake au upambanaji wake aliouanza awali. Kwa mawazo yangu, kutoa maoni ni haki kwa Chama cha demokrasia!! kwa ushauri wa baadae kwa kuwa bado twaendelea kujijenga zaidi ili tutwae nchi 2015; ZITO au Kiongozi yeyote wa ngazi ya namna yake, WAJIEPUSHE kutoa maoni mchanganyo (contravesial comments) yanayoweza kuvuta hisia za kuwagawanya wana CDM na kuwawezasha wapinzani wa CDM kutumia mwanya huo KUONGEZA MPASUKO (GAP) ili ya NCCR 1995 yatimie!!!
 
pamoja na yaliyoandikwa kwenye magazzette mh zitto hajafanya kosa la kufanya uongozi wa chadema umfukuze uanachama. Endapo angekuwa ndani ya ukumbi wa bunge na akabaki ndani wakati wabinge wa chadema walipotoka nje hapo angekuwa amekiuka msimamo wa chama chake

kwani nani kasema mambo ya kufukuzwa au kuchukuliwa hatua zozote. Ni watu nje ya chama wanaoongea hayo pamoja na yeye mwenyewe kama aliyasema tbc lakini sidhani kama katika chadema lipo wazo kama hilo.
 
Wakuu zangu nimemsoma Mbowe pia sielewi kinachoendelea Chadema. Je, aloyasema Mbowe ndio msimamo wa Chadema maanake katibu wake Dr. Alisema hayatambui matokeo, hivyo mtaweza vipi kumtambua rais ambaye matokeo ya uchaguzi wake hamuyatambui?..

Mkandara,

Nadhani ulishazungumza kwenye post moja kwamba ni ngumu sana kumkataa raisi wakati katiba inawabana kwenye hilo pale kwenye ibara inayoweka wazi kwamba raisi ni sehemu ya bunge. Hivyo basi, nadhani Mboe ameona labda kuna tofauti kubwa sana ndani ya chama na kuokoa jahazi inabidi asend mix signal ya kumkubali JK.

Sasa swali ni mmoja kwa nini mlimkataa kisha mkamkubali? Hapo ndio nataka kumsikia Kitila akituelimisha hapa jamvini. Nilidhani lengo ni kupata sympathy kutoka kwa international organization ili tuanzishe mchakato wa kufanya ammendment kwa vifungu kadhaa vya katiba kisha kubadilisha mchakato wa uchaguzi wa NEC. Lakini naona imekula kwetu.
 
bado najiuliza nani mwenye busara na wapi chadema inaelekea kama wakiwa bungeni wanashindwa kuwa na msmamo mmoja iweje leo hii walalamikie cuf wananuliwa
nilijiuliza na badonajiuliza kati ya hawawatu waliokataa kuingia bungen na kutoka na walioingia na kutoka nani wenye busara

mtafika kwa mtaji huu

kama hivi tu!!!
 
Zitto kutofautiana na wenzie ni siasa iliyokomaa kabisa. Sababu ni wazi kabisa huwezi kukubali kila wanaloliamua wenzio kwa sababu za eti ni maamuzi ya chama. Swala hilo ndio linawamaliza CCM leo kwa kukumbatia mafisadi kwa kigezo cha protocal za kichama. Sasa, ni wazi kabisa Zitto kabwe alitazama political risk zote associates na uamuzi wake, kisha akaamua lile analoamini ni la manufaa kwake (career wise) na wananchi wa Kigoma Kaskazini.

Ninapo tofautia na Zitto ni kuhold press conference na kutanabaisha bayana mchakato mzima wa yeye kuto kukubaliana na wenzie. Zitto angeweza kusema "kutokana na mambo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu nilishindwa kuwepo bungeni na kuungana na wenzangu kutoka nje wakati Mh. Jakaya akitoa speech ya ufunguzi". Jibu kama hili lingetanabaisha bayana ni kwanini Zitto hakuwepo bungeni, lakini kwa yeye kuja kwenye media na kupayuka kama punguani limeonyesha wazi kabisa uchanga wasiasa uliopo ndani mwa wabunge vijana.

Ushauri kwa wabunge vijana wa CCM, CUF and Chadema, siasa ni mchezo kama drafti au chase hivyo basi sukuma kete zangu kwa kuangalia mwenzio anasukuma vipi zake. Media siku zote ipo kutengeneza story na kuuza, hivyo basi havina rafiki.

MTANGANYIKA UMELIJADILI SUALA HILI VIZURI SANA.







kimsingi mbunge ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo analotoka, hivyo hatakiwi kupeleka maoni yake binafsi bungeni kama wanavyofanya wabunge wengi wa ccm, anatakiwa kupeleka yake aliyokubaliana na waliomchagua.

Hivyo nahisi kigugumizi walichokuwa nacho baadhi ya wabunge kuhusu uamuzi huo ni kutokuwa na uhakika wa maoni ya wananchi wanaowawakilisha hapo bungeni ikikumbukwa kuwa ni siku chache tu wameachana na hawakuwa na vikao vyovyote kukubalina kuhsu uamuzi mzito kama huo. Je wananchi waliowachagua watawaunga mkono au kupinga kitendo hicho.

kwa maoni yangu naona mhe zitto kabwe yuko sahihi kabisa kutoa maelezo ya ziada ya kujitenga na uamuzi huo wa chama kama mtu binafsi mbele ya wapiga kura wake wa kigoma. Ana haki ya kuwaonyesha kuwa ule ulikuwa uamuzi wa chama.

Kwa kufanya hivyo mhe zitto kabwe ametumia ipasavyo mapungufu yaliyopo katika katiba ya tanzania ambayo chadema tunataka ibadilishwe kujisafisha mbele ya wapiga kura wake. Nampongeza sana kwa kujali hisia za wapiga kura wake. Na ni amoni yangu kuwa wasiokuwa wapiga kura wa jimbo lake hawana haki ya kumhukumu kuhusu hilo.

Kimsingi hata wale wanaowanyooshea vidole mhe zitto kabwe na wengine waliojali zaidi matakwa ya wapiga kura wao zaidi ya chama wana hangover ya katiba mbovu ambayo inajali zaidi "party supremacy" yaani "chama kushika hatamu" badala ya wananchi kushika hatamu. Hivyo wanapaswa kupigwa msasa ili waendane na matakwa ya kubadili katiba hii mbovu.


 
Wakuu zangu nimemsoma Mbowe pia sielewi kinachoendelea Chadema. Je, aloyasema Mbowe ndio msimamo wa Chadema maanake katibu wake Dr. Alisema hayatambui matokeo, hivyo mtaweza vipi kumtambua rais ambaye matokeo ya uchaguzi wake hamuyatambui?..

Lazima, narudia, LAZIMA amtambue Rais, vinginevyo itakula kwake na kwa chama chake.

Slaa alikurupuka tu kama ilvyo kawaida yake. Kwa kuwa Mbowe ni mchanga kisiasa, amegundua too late kuwa mambo si mazuri. Woga umemuingia amesahau aliongea nini kwa mbwembwe juzi juzi.

Kwa sasa anaonekana kuongea kwa upole, nidhamu ya woga na kutaka kuomba radhi.

Those are Chadema leaders!
 
Ukiamua kutoka bungeni, fanya kweli. Toka bungeni kwa msingi wenye mantiki, shikilia msimamo wako, chukua hatua zitakazoleta mabadiliko. Sio unatoka bungeni kuuza sura kwenye magazeti na kupiga "kelele" ukiulizwa legal strategy huna much less political. Unabaki kupigwa checkmate !

Mi naona badala ya kuleta mchezo wa kuigiza wa kutoka bungeni, mara humtambui rais, mara unamtambua lakini hutambui matokeo (WTF is that ) CHADEMA wangeamua moja, kama wanao ushahidi hamna kushughulika na shughuli zozote za bunge mpaka waweke mpango kabambe wa angalau kubadilisha katiba, sheria za uchaguzi na NEC, au kukubali kuingia bungeni, kumtambua rais na kushinikiza mambo kutoka bungeni na kwa kuwahamasisha wananchi.

Sasa hivi walichofanya ni kujipunguzia heshima tu, kwenye kumtambua rais wametoka, kwenye kutomtambua rais wametoka, ilimradi wamebaki wanaelea elea tu kama ndumilakuwili wasio na msimamo wanaangalia upepo wa siku unaenda vipi, kama leo kutomtambua rais ndiyo dili basi hatumtambui, kesho tukiona kinaweza kutuwakia ikala kwetu tunamtambua bila aibu tunaweka spin za kitoto eti "rais tunamtambua, hatuyatambui matokeo". Utamtambuaje rais aliyewekwa madarakani kwa matokeo bila ya kuyatambua matokeo?

Mi naona katika strategies hizi mbili, yenye akili ilikuwa ile ya Zitto, ya kuuchuna wamtambue rais kwa sasa wakati wanapanga mipango ya kubadili sheria na katiba. CHADEMA walikuwa hawajajiandaa kwa kitu kikubwa kama kutomtambua rais, rais mwenye dola na bunge. Kwa hiyo kukurupuka na kufanya mambo half baked kumewaumbua tu.

Of course siasa za ushabiki zitaona kutoka ndani ya bunge ni ushindi hata kama hakuna sheria yoyote iliyobadilika na actually hata in the court of public opinion ambako mtu ungeweza kusema CHADEMA wamepeleka kesi yao, watu kibao wanaona hii move fyongo.
 
Ukiwa umetumwa kama kishongo -great thinkers watakuelewa kwamba wewe umetumwa kibraka kibweka. Alichoingea dr slaa na anachoongea mbowe yote sawa. Wote wanapinga uchakachuaji wa kura, wote hawaridhiki na kasoro zote zilizojitokeza wote wanadai uchunguzi, tume huru, na katiba mpya sasa usichoelewa nini, umezoea statement za makamba huwezi kuwaelewa wasomi kama slaa, katafakari urudi upya jamvini
 
Nionavyo Zito alibaki ili kuona kitakachojiri baada ya wenzake.
 
It is official huyu Zitto ni mpayukaji, na ana itaji communication lessons hili kuelewa implications za kauli zake hadharani ki chama (ya kuwa zinazua utata particularly mistrust ambayo amesha jijengea tayari chamani). On the other hand na CHADEMA inabidi ielewe wako major mainly kwa sababu kubwa watanzania wameshaanza kuchoka na CCM kuliko their political wit.

Hivyo hili chama kukua zaidi inabidi kuanza kuwa open and honest na Zitto despite his unthoughful comments in most cases huwa anasema ukweli uliopo within in my opinion (mara nyingi chadema wenye huja hapa na kukiri, lakini umtukana kutokana kuropoka kwake). Sasa inabidi kuwe na reform within the party, political movement requires a team of strong minded individuals ya kuweza kuja na mikakati ya kushinda.

Na kama mnadhani coming 2015 labda mtapanda ushindi wa walk in the park hata kama katiba ikibadilishwa you got another thing coming. CCM ina reseve tank ya watoto wa mafisadi niamini nikikwambia kuna mijizi huko imeisomesha mitoto zao ulaya nusu wa kufirisika wao wenyewe. Na hizo shule hawa watoto wanazosoma huku especial wale mafisadi wenye elimu (achana na elimu ya RZ1 hiko cha mtoto tu) ni za wazungu wenye mihela kupata nafasi yenyewe ni ngumu. Niamini ukikutana na baadhi ya hawa watoto wengine hata miaka 25 hawana, msifanye mchezo nyie wakianza kuelezea mambo.

Hii ni reserve army ya CCM inakipaji cha propaganda, elimu ya juu, fikra za juu na quality zote za modern politicians. Sasa msizani hawa watakuja na tactics za CCM iliyozeeka na bado aija adopt modernity. Kiasi cha raisi kuja kutamka hadharani pumba kama siitaji kura zenu. We subiri kama CCM itaona umuhimu wa kuleta vipaji vyao hakutakalika huko mimi nakwambia nimeshakutana na baadhi ya hii mitoto ni mieruvu nikikwambia.

Sasa chadema na yenyewe inabidi hi reform, ndio atukatai Mh. Mbowe na wenzake wakuu wamepigana vita kubwa na hiyo lazima itambulike. Lakini wakati wa sasa Chadema inabidi hiwe open kwa jinsi inavyoongozwa na kuweza ku attract the young ones, huwezi kujaribu ku-lure all sorts of people into your party wakati asilimia kubwa JF members wanao support Chadema wanakuja na mi signature yenye quotations za biblical writings au avatars zenye mipicha inayo supporet dini. Take or leave hila come two years time utaona mabadiliko ya CCM. JC is rarely wrong hila wengi huwa hawanielewi at first baadae uishia kusema ulisemaga.

Nawasilisha.
 
Nimepata nyeti kuwa majasusi wa ccm wamepania kukisambaratisha (sidhani kama wataweza) chama cha chadema kwa kuanzisha mgogoro bubu kati ya Zitto na Mbowe.

Kama mjuavyo, Chadema wamescore points kibao kisiasa kwa kuondoka bungeni wakati wa speech ya Kikwete. Ile issue imewachanganya ccm na sasa wameanza kutafuta chochote wawezacho ili wabadili upepo huu wa kisiasa.

Kwa siku za karibuni, ccm (na wapambe wao kwenye vyombo vya habari) wameanza kutafuta kila sababu ya kufufua mgogoro bubu kati ya Mbowe na Zitto. Wanataka kuwachonganisha hawa viongozi wawili ili kuleta kambi mbili chadema -- divide and rule.

Wanaanzisha stori za ajabu ajabu tu ili ku-make their case. Mfano mzuri, ni stori zisizoisha hapa toka kwa wanaccm kama zemakopolo (sp?), kishongo, malaria sugu na wenzake ambao wanaonekana kumsifia sana Zitto huku wakipondea viongozi wengine wa chadema.

Kama ulisoma hata ile article ya fisadi la kutupwa la daruso - Maina Owino wa ccm London - ambayo alijidai kutoa ushauri kwa wabunge vijana wa chadema (mdee na mnyika) eti wasikubali kutumiwa na viongozi wa chadema, utagundua kuwa ccm wako hell bent kuigawa chadema. The same can be said kwenye ile thread ya mwanaccm hapa JF (selemani) kuhusu Mdee.

Wanachadema kuweni makini sana na these guys. hawatachoka mpaka wamewavuruga kabisaaa.

Mkiona topic yoyote hapa (au gazetini) kuhusu Zitto au mgogoro wa chadema, jaribuni kufuatilia source ya hiyo stori. Kwa msaada zaidi kwa wale wanachama wageni hapa JF, ukiclick jina la mwanachama yoyote hapa JF, unapewa option ya kusoma post zake zote alizowahi kupost hapa JF.
Jielimishe na mtaona kinachoendelea.

NB - ushauri binafsi wa Zitto, Una nafasi nzuri sana ya kuwaaibisha hawa wanafiki hapa na kwenye media kwa kutoa tamko ambalo litaweka yote haya kaburini.
 
Mbona siyo siri tena? Hata mfuasi wa CCM hapa ukumbini Selemani kishasema kuna mipango ya ku-infiltrate Chadema.
 
Mbona siyo siri tena? Hata mfuasi wa CCM hapa ukumbini Selemani kishasema kuna mipango ya ku-infiltrate Chadema.

Moja ya mbinu zao, ni kutumia watu ambao wanajiita kuwa wapinzani (esp chadema) ili kuleta habari za kipuuzi na wakidai kuwa wao wako upande wa Zitto na sio wa Mbowe or something like that.
 
Kuweni pia na mwanachama anaitwa bonobo (tamka sokomoko) anaandika upumbavu kwa sababu zake!
 
Moja ya mbinu zao, ni kutumia watu ambao wanajiita kuwa wapinzani (esp chadema) ili kuleta habari za kipuuzi na wakidai kuwa wao wako upande wa Zitto na sio wa Mbowe or something like that.

Tena humu jamvini wapo wengi sana.
Ila kwa hili la Zitto na Mbowe naona kama wanaelekea kufanikiwa.
 
Nia yao ni kuigawa kambi ya upinzani inayoundwa na CHADEMA ndani ya Bunge. Ninaamini CHADEMA hawadanganyiki na propaganda za kihuni!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom