Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Nawashangaa sana watu wanaosema eti Zitto ni mwana demokrasia, demokrasia gani aliyonayo Zitto ya kutoheshimu kura za wengi? Aesema kwamba walipiga kura, na wengi wakachagua kutoka nje wakati 'Rais' akianza kuhutubia, sasa yeye kama mpenda demokrasia si alitakiwa aheshimu mawazo ya wengi?

Misingi ya utawala bora inasema kama Zitto bado alikuwa na shaka angeomba dissenting opinion yake irekodiwe au hata kuamua kujiuzuru kama anaona jambo analolisimia ni la msingi kiasi kwamba hawezi kuendelea kuishi katika mfumo huo.

Kitendo cha Chadema kupiga kura na kura za wengi kuheshimiwa ni ishara tosha kwamba ndani ya chama kuna demokrasia, kwa hiyo hoja ya kwamba eti ooh Mh. Mbowe anakiburuza Chama haina mashiko.

Katika hili la kwenda kwenye vyombo vya habari na 'kuropoka' kunadhihirisha Zitto asivyopenda demokrasia, na pengine anapenda chama kiwe kinamsikiliza yeye tu. Lazima tukiri kwamba Zitto either bado ni mchanga sana katika masuala ya uongozi na uwajibikaji ama anatumika na kundi au watu fulani kuchafua hali ya hewa ndani ya Chadema.

Binafsi nilipoteza imani kwa Zitto toka kipindi kile cha mijadala ya kununua mitambo ya Dowans!! Bwana mdogo ana tamaa sana ya madaraka na pia ni mtu wa kupenda sana sifa binafsi. Mtu kama huyu hawezi kuwa na mchango wa maana katika kambi ya upinzani.

Somo kwa Zitto: Kwa mtizamo wake, je kufikia uamuzi wa kumuengua Mh. Sitta kugombea uspika kupitia tiketi ya CCM ni wajumbe wote walikubaliana? Na ni wote waliafiki kuwaengua wagombea wanaume na kuafiki kuwasimamisha wanawake tu?

Naamini atajibu si wote. Je kwa nini hakuna mjumbe zaidi ya Katibu Mkuu wa CCM aliyetoka na kwenda kwenye vyombo vya habari kueleza kwamba yeye hakukubaliana na uamuzi wa wengi?


Kuhusu kwamba eti aliwasiliana na wapiga kura wake kujua msimamo wao kuhusu kutoka nje ya ukumbi wa bunge, ni hoja ambayo inaonyesha dhahiri kwamba Zitto ni muongo. Kwa hali halisi ya kimawasiliano ya jimbo la Zitto, aliwasiliana vipi na wapiga kura wake (idadi ya wapiga kura) na kufikia uamuzi kwamba wengi hawakukubakiana na uamuzi wa Chama?

Zitto anasema yuko tayari kusubiri adhabu atakayopewa na chama kwa utovu wa nidhamu, hiki ni kichekesho cha mwaka......badala ya mtu wa ngazi yake (Naibu Katibu Mkuu wa Chama) kusema anaomba radhi kwa kuwa amefanya kosa yeye analeta jeuri kwamba anasubiri adhabu atakayopewa!! Ni kama anawatishia Chadema..!!

Huyu bwana mdogo anaonyesha jeuri na kiburi ambacho hakina maana kabisa!! Binafsi naona angevuliwa uongozi na kubaki kama mwanachama wa kawaida. Chadema isiogope kuwatosa wanachama wasio na nidhamu kama hawa, ni mzigo kwa chama na ukuaji wa demokrasia.
 
Zitto kwa JK ni kama MBWA kwa CHATU. Lolote utalojaribu kulifanya linalombomoa JK Zito hatakubaliana nawe.


Nakubaliana na wewe mkuu, hata kipindi cha kampeni aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akimsifia JK kwa uchapakazi!! Huwa sipendi kuamini watu wanayosema mtaani kwamba Zitto huwa ni NDIYO MZEE kwa JK!!
 
udini...udini....udini....! kuna vyama muislamu hawezi kukaa salama....na kuna vyamamkristo hawezi kaa salama........na kuna chama mseto ndo unakivuruga zaidi...!
CHAGUA JIBU SAHIHI KATI YA HAYA .....CHADEMA.....CUF......CCM....!
 
Zito anastahili kuwaondolea wasiwasi Watanzania wapenda mabadiliko walio nao juu yake wa kuwa yeye sasa yawezekana yupo CHADEMA lakini kwa maslahi zaidi ya kwake na ya CCM. Kumekuwa na minong'ono mingi juu ya ukaribu wa Zito na viongozi wa CCM. Minong'ono hii inaweza kuwa ya kweli kwa 100% au kwa kiwango fulani au pengine isiwe ya kweli lakini yeye anastahili kuitolea ufafanuzi. Lakini lililo dhahiri ni kuwa Zito anapenda sana umaarufu wake binafsi kuliko mafanikio ya CHADEMA kama taasisi. Unapopiga kura kwaajili ya kupata uamuzi maana yake ni kuwa upo tayari kukubaliana na uamuzi wa walio wengi. Kama walio wengi wa waliopiga kura waliazimia kuwa wabunge wa CHADEMA watoke mara Kikwete akianza kuhutubia, kwa nini Zito alichukua uamuzi tofauti? Ina maana haamini katika demokrasia ya maamuzi ya walio wengi? Yeye kama kiongozi wa Chama alistahili kuonesha mfano katika kukubaliana na maamuzi ya walio wengi kuliko kuona kuwa wakati wote watu wote ni lazima wakubaliane na anachotaka yeye. Huo ni ubinafsi mkubwa!
 
nilipolisoma jina hapo juu nilidhani mjenga hoja wa maana, kumbe pumba zimekujaa kichwani.

Ukweli unauma MUNGI. Na huo ndi ukweli wenyewe Zitto ni mtu makini, amekataa unafiki wa kwenda kinyume na kiapo chake kwa ajili yaku wafurahisa wakina Mbowe.
 
Ukweli unauma MUNGI. Na huo ndi ukweli wenyewe Zitto ni mtu makini, amekataa unafiki wa kwenda kinyume na kiapo chake kwa ajili yaku wafurahisa wakina Mbowe.
Ivi unajua kinachojadiliwa hapa?
 
ANA KIBURI CHA ASILI


mtu gani hashauriki?! anaonekana ni CHOLERIC
 
zito anastahili kuwaondolea wasiwasi watanzania wapenda mabadiliko walio nao juu yake wa kuwa yeye sasa yawezekana yupo chadema lakini kwa maslahi zaidi ya kwake na ya ccm. Kumekuwa na minong'ono mingi juu ya ukaribu wa zito na viongozi wa ccm. Minong'ono hii inaweza kuwa ya kweli kwa 100% au kwa kiwango fulani au pengine isiwe ya kweli lakini yeye anastahili kuitolea ufafanuzi. Lakini lililo dhahiri ni kuwa zito anapenda sana umaarufu wake binafsi kuliko mafanikio ya chadema kama taasisi. Unapopiga kura kwaajili ya kupata uamuzi maana yake ni kuwa upo tayari kukubaliana na uamuzi wa walio wengi. Kama walio wengi wa waliopiga kura waliazimia kuwa wabunge wa chadema watoke mara kikwete akianza kuhutubia, kwa nini zito alichukua uamuzi tofauti? Ina maana haamini katika demokrasia ya maamuzi ya walio wengi? Yeye kama kiongozi wa chama alistahili kuonesha mfano katika kukubaliana na maamuzi ya walio wengi kuliko kuona kuwa wakati wote watu wote ni lazima wakubaliane na anachotaka yeye. Huo ni ubinafsi mkubwa!


uko sawa kabisa. Umaarufu binafsi ndo unamtafuna mtoto huyu!
 
Naogopa sana nkisikia maneno magumu kutoka kwa Zitto. Huyu mtu amekuwa mashuhuri sana,kumbuka si kwa uwezo wake tu,bali na kwa msaada wa chadema! Mh.Zitto naomba uelewe kuwa sisi raia tunakuhamini ila kwa tuhuma zinazoanza kumiminika kwako,pia zikidhihirishwa na matamshi yako,nakujulisha zitakucost. Kumbuka umaarufu wa mtu uundwa na kikosi,ni waandishi wa vitabu peke yao wenye umaarufu wao wenyewe,otherwise ni kutokana na kikosi chake. Mkuu kaa upate hekima na ukubali kuwa ktk kikosi kuliko kutaka kuwa wewe tu. Hao ccm wasikudanganye,ukienda uko utakaa bench,ukidhani wee kichwa sawa ila ccm pia ina vichwa zaidi yako na hawawiki kamwe! Kama unataka umaarufu utafute ukiwa chadema,ukitaka kupoteza kisiasa,toa mguu hapo na utapoteza kisiasa believe my words. Nakuomba uendelee kupinga udhalimu na ufisadi,usiwasaliti wapiganaji,mwache dr.akijenge chama muda wako bado wala si 2015. Nawasilisha.
 
Wakuu habari za punde ni kwamba Zitto Kabwe atahamia NCCR mageuzi, na kwamba atagombea ubunge kigoma kaskazini kwa chama hicho. kwa hiyo basi atakua ametimiza kazi yake ya kuivuruga cdm na mafisadi watashangilia. ila cdm itaendelea kuwepo na kuendelea kufanya kazi uzuri.
 
Zitto anadhani yeye ni superstar

Tatizo ambalo Zitto analitengeneza ama amelitengeneza ndani ya Chama(Chadema) ni kile kitendo chake cha kutoa Kauli tata ambazo mwisho wa siku zinaonekana kama ni za kuvuruga ama kuharibu Chama, Kauli zake nyingi ni kauli za kujionyesha kwamba yeye anauwezo, ni much know,
Baadhi ya Kauli zake ambazo zilikuwa tata na zilizomfanya ashindwe kueleweka na hata kutoaminika ni kama pale alipokuwa anasema sitagombea tena ubunge, naenda shule, kisha akabadilika na kusema nitachangua jimbo la kugombea (Geita, Kinondoni ama Kigoma Kaskazini),

Nilishasema katika post zangu za nyuma kuwa Zitto inampasa kuwa mwangalifu na kujua kusoma alama za nyakati, kama hali yake ndani ya chama ni nguvu au isiyovumilika (Haelewani na mwenyekiti wake na wanaonekana kana kwamba wana bifu) ni bora akaondoka ndani ya chama wakati bado anaheshima yake lakini itafikia kipindi cha kufukuzwa na kutakuwa hakuna wa kumwonea huruma kwani mvuto wake utakuwa umeisha

MIMI kwa mtazamo wangu, Zitto akupenda wala hakumsapoti Dr Slaa kuwania Uraisi, sababu anazijua mwenyewe Zitto, mimi nasema hivyo kutokana na kauli zake katika moja ya kampeni zake, Zitto alisema "Nitagombea uraisi 2015" sasa swali la kujiuliza atatoaje hiyo kauli tata wakti Dr Slaa anagombea uraisi, ina maana Dr angeshinda, Hiyo 2015 angempisha Zitto, na inakuwaje aanze kuzungumzia mambo ya 2015 kugombea uraisi bila hata kujua msimamo wa Chama? Alishajiakikishiaje kuwa Chama kitampitisha, Au Zitto alishakuwa na uhakika kuwa Dr atashindwa tu?, mbona Dr Slaa alikaa kimya mpaka hatua ya mwisho ndio tukajua kuwa anagombea?Pamoja na hayo yote,

nilihuzunika sana siku ile ya kipindi cha Mchakato majimboni kilichorushwa na TBC1, katka maongezi yake yote sikumsikia Zitto hata mara moja akimnadi Dr Slaa wala Chadema, cha zaidi kilikuwa mkinichagua mimi/tena
Kwa kifupi Zitto akumkubali Dr Slaa na wala issue ya kuibiwa kura kwa Slaa kwake sio issue, issue ilikuwa ni ubunge wake na kaupata, the way inavyoonekana Zitto hana time (heshima) na kiongozi yoyote wa Chadema na ndio maana anaweza kwenda media na kuongea chochote bila ridhaa ya wakubwa wake,
Haiingii akili kwa Chama chenye uongozi lakini mtu anakurupuka na kwenda press kutangaza kwamba atagombea kuwa kiongozi wa upinzani bungeni, kwa nini asisubiri chama kiongee, Hizo ndio kauli chochezi na tata, kwa sababu mwisho wa siku akichaguliwa Mbowe watu watasema wamembania Zitto kwani alishasema (kwenye media) kuwa anaitaka hiyo nafasi

Zitto bado una heshima usisubiri adhabu unayoitangaza kwenye media, we toka Chadema ukiwa na angalau una hiyo heshima yako kidogo kabla haijaporomoka kabisa
 
Wakuu habari za punde ni kwamba Zitto Kabwe atahamia NCCR mageuzi, na kwamba atagombea ubunge kigoma kaskazini kwa chama hicho. kwa hiyo basi atakua ametimiza kazi yake ya kuivuruga cdm na mafisadi watashangilia. ila cdm itaendelea kuwepo na kuendelea kufanya kazi uzuri.

Huo ni uchochezi si kweli. Usimuwekee maneno mdomoni. Lakini hata akifanya hivyo ana uhuru wa kufanya hivyo hata kama ni kwa maslahi binafsi.
 
mbona umeandika stori kana kwamba zito keshatoka au kufukuzwa chadema? acha porojo bana, huo uzushi, zito hawezi kucheza huo mchezo hata kama haipendi CDM!
 
Demo-cracy or Demo-crazy?
so what!
Tell me the concept behind,
I will understand you.
it can be either of the two options,
*true* OR *false* sir
PROVE IT just by simple arithmetic or you can use Pythagoras Theorem
but there is Newton 3rd Law of Motion which says,*Any action has an equal and opposite reaction*
 
Huo ni uchochezi si kweli. Usimuwekee maneno mdomoni. Lakini hata akifanya hivyo ana uhuru wa kufanya hivyo hata kama ni kwa maslahi binafsi.

Umenena kama real great thinker

Zitto ana uhuru wa kufanya lolote lile, kuwa msaliti, fisadi, kujiunga CCM, kubaki chadema, hatakuwa wa kwanza, wala taarifa hiyo haitakuwa nja uzito wa kusimamisha jua lisiendelee kuzunguka dunia!

Cha muhimu ni kuwa tunahitaji katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, kuvitafuta hivi au kuvipigani hakujalishi Zito atakuwa upande wetu au la! tuwaze makubwa jamani!!
 
Ishu za Zitto zimeshaanza.....kila kukicha itakua zitto zittooo zittoo...dah!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom