Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Tukubali tukatae Zitto ni kijana kiumuri HIVYO HATA KIFIKIRI. MIENENDO YAKE INAZIDI KUTIA SHAKA. NADHANI ALISAHAU MSINGI WA CHADEMA KUTOKA NJE YA BUNGE KWANI CHAMA KIKISHASEMA HAKIMTAMBUI RAIS KINGEWEZESHA KUKAA ILI AKIHUTUBIE? HAONI KUBAKI KUBAKI BUNGENI ILIKUWA NI KUINYIMA NGUVU HOJA WALIYO IANZISHA?

NI VYEMA ZITTO KUELEZEA MSIMAMO WAKE HADHARANI KAMA ANAONA ANA HAKI/UHURU KUFANYA HIVYO. LAKINI KAMA ALIKUWA HAKUBALIANI NA MAAMUZI HAYO SI ANGEBAKI NDANI YA BUNGE? MAANA BADO ALIKUWA NA HAKI/UHURU KUFANYA HIVYO!

NADHANI ZITTO ATAMBUE KUWA NI MTU MUHIMU SANA NDANI YA CHADEMA NA AELEWE ATABEBA FAIDA AU LAANA YA KUPARAGANYIKA KWA UPINZANI NCHI HII. KUHESHIMU MAAMUZI YA PAMOJA NI MUHIMU LAMSINGI MAAMUZI HAYO YAWE NA MANUFAA KWA WANANCHI WANAO WAKILISHWA. KATIKA HILI NAAMINI UAMUZI WA CHADEMA ULIKUWA NA MANUFAA KWETU TUPENDAO MABADILIKO.

KAMA ZITTO ANADHANI KUJIOSHA KWAKE KUTAMUONGEZEA UMAARAFU, KAKOSEA, MAANA MIMI KAMA MOJAWAPO YA WAFUASI WAKE WA KARIBU AMENIHUDHUNISHA

AELEWE SERIKALI, CCM NA VYAMA PINZANI KWA SASA VINATAFUTA KILA NAFASI KUIANGAMIZA CHADEMA, MOJAWAPO YA NJAMA HIZO NI KUFANYA UPOTOSHAJI NA KUMOBILIZE PUBLIC BIAS AGAINST CHADEMA.

ZITTO JARIBU KUFIKIRI BEYOND PERSONAL INTEREST

Sikubaliani na wewe hata kidogo, hayo mambo ya kumwambia ni muhimu ndio yanayompa kichwa kufanya mambo ya ajabu ajabu, atoke basi aone kama CHADEMA itakufa, sana sana atakufa yeye
 
Take a few loud mouths and give them the support of the disgruntled mob and an unprecedented number of seats in the House matokeo.... dalili tunaanza kuziona. 1000 Zitto Kabwe's would have a difficult time solving the current problems in Tanzania. JF enzi za Nyani kulikua na substantive discussions humu, about real issues.. All that people seem to talk about now is CHADEMA and not even politics, but personalities. This is very poor and JF should aim higher than this... be a thinktank not some forum for the mob to gather and do either virtual lynching or help build personality cults. It is quite appalling... Issues... thats what we ought to discuss, not the self-righteous discourse of certain individuals who at best are trying to solidify a platform for their own political ascension.
 
Akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1, Bw. Kabwe alisema yeye asingeweza kuingia bungeni na kutoka wakati Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, na ambaye amefanya mambo mengine mkoani Kigoma kuliko marais wengine anahutubia. Source: Majira

Based on that inaonyesha kabisa Zitto alikua anamuunga mkono kikwete kama katika nafasi ya Urais na Siyo Dr maweapon hiyo ndiyo sababu ya kutoingia bungeni kabisa na kupinga hoja ya chama ya kutoka bungeni wakati Rais anahutubia. Zitto yupo CHADEMA kimaslahi binafsi sana na siyo ya kichama. Kama kweli haungi mkono ni bora angejiudhuru hata hiyo nafasi ya unaibu katibu mkuu awe mwanachama wa kawaida kabisa, Aige mfano wa Shitambala.
 
Zito kimsingi ana mapungufu kama kijana maana saa nyingine mimi naona kama anawadharau waliomfikisha hapo alipofika.

akumbuke watanzania tunafuatilia sana nyendo zake, na tutamfahamu kwa undani kama ni mtu wa kutetea mananchi masikini.

Vile vile ajue amekuwa anang'aa kwenye siasa kwa sababu ya chadema, kwani wapo vijana wengi sana wanafanya siasa lakini hawajulikani, Zito safari yake ya siasa ilikuwa 2007 alipofukuzwa bungeni. Lakini chadema wakaona isiwe tabu na kuanza kumzungusha kwa wananchi tukamwona wa maana, lakini sasa anakuja kusumbua wazee kichwa mara anataka umwenyeki. etc.

Mimi namshauri kuna vijana wengi sana NCCR, CCM etc. lakini watanzania hawawajui na yeye amepata hiyo bahati asiichezee. kabisa watu wanaikubali sana chadema, na wanaiona tumaini jipya kwa hiyo asione amefika akavimba kichwa.
 
Tatizo Zitto anajikosha kosha kwa Riz1. Kuna ki2 kaahidiwa!
 
Mmeshaanza kuparurana, je tungewapa dola si ingekuwa kiama?
 
huyu zitto ana vielement ambavyo bado sija vielewa vizuri
 
Zito wewe ni kiongozi wa chama unatakiwa uonyeshe njia ya dhati ya kuleta mabadiliko...........kwani wewe hukuona chakachua iliyofanywa na Nec na CCM? Kinachotakiwa sasa hivi ni tume huru ya uchaguzi......kama wewe ni kiongozi na unakaa pembeni hiyo tume huru itapatikaje? Nimekusikia mara nyingi ukisema kuna Udini........jaribu kuwa muwazi anayeleta udini ni nani! Mbona JK hivi majuzi amechagua wabunge 3 wote waislam na hujaliongelea, sasa tusubiri baraza la mawaziri tuone ni akina nani wako huko! Mh. Zito wewe bado ni kijana na nyota yako ilikuwa inaenda vizuri sana.......lakini inaonekana yule Zito wa zamani siye Zito wa sasa, angalia isije ikawa CCM wameshakuingiza mkenge na hela zao......."Hela si kila kitu"! Imani ambayo wantanzaia wameonyesha kwako itunze......ukifanya hila kwa ajili ya kuadaiwa na CCM na kusaliti Watanzania nguvu ya Mungu itakuadhibu ndugu yangu!!! Tetea Chama, tetea maslahi ya Watanzania.

Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, amesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa.

Kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.

Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.

Source: TBC 1 News Bulletin
 
Zitto ana akili ya kitoto sana...Had it been ningekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ningeitisha kikao na kumvua uanachama ili aweze kuwatumikia vizuri hao CCM
 
Take a few loud mouths and give them the support of the disgruntled mob and an unprecedented number of seats in the House matokeo.... dalili tunaanza kuziona. 1000 Zitto Kabwe's would have a difficult time solving the current problems in Tanzania. JF enzi za Nyani kulikua na substantive discussions humu, about real issues.. All that people seem to talk about now is CHADEMA and not even politics, but personalities. This is very poor and JF should aim higher than this... be a thinktank not some forum for the mob to gather and do either virtual lynching or help build personality cults. It is quite appalling... Issues... thats what we ought to discuss, not the self-righteous discourse of certain individuals who at best are trying to solidify a platform for their own political ascension.

Well said, well framed, well put.

Its about time (though we are late) to focus our energy, mind and time on "issues" and not "people"
Issues that have been pulling our nation down ever since, now and long time to come if we dont act "NOW"

The good thing is all these issues are known

Let address them with "all our strength"
With almighty God on our side for sure we will win.
 
Zitto anadhani yeye ni superstar
kabisa.chadema tujue hii ni kansa itatuua siku moja.nashauri akifanya ujinga wake atimuliwe.chadema tukumbuke mchelea mwana kulia hulia mwenyewe
 
Ni haki yake kama binadamu huru kuamua au kutoamua kuunga mkono hoja ya CHADEMA nje ya bunge, lakini alitekeza kwa kutotokea. Kama angeingia bungeni na kubakia wakati Kikuete anahutubia hapo tungesema yupo kinyume.
 
Analeta tabia kama za CCM kila mtu anaongea madhara yake anatoa mpaka siri za chama ooh tulipiga kura wengi ikawa wape.
Zitto nowdays amekuwa muoga kiasi icho ata akasita kuingia bungeni?

Kila mmoja ana uhuru wake wa kutoa mawazo yake na habanwi na chama wala mtu yeyote. Ndani ya CCM wapo wanaopingana na chama na tunawaona wakidunda bila kuvuliwa uanachama wapo kina mhe Samwel Sita, Mzee Malecela na mkewe, yupo selelii na wengine wengi. Zitto anakipa changamoto chadema ili kiwe na ukomavu mkianza kufukuzana mtakiua chama hamjifunzi kwa yaliyotokea kwa kafulila?
 
Zitto ana akili ya kitoto sana...Had it been ningekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ningeitisha kikao na kumvua uanachama ili aweze kuwatumikia vizuri hao CCM

Mi naona sio bure lazima kutakuwa na kasoro flani CHADEMA.
Mtu kama Zitto sidhani kama anaweza kufanya haya bila kuwa na 'kitu flani' ambacho hakiko sawa ndani ya chama chake.
 
Akihojiwa na Kituo cha Televisheni cha TBC1, Bw. Kabwe alisema yeye asingeweza kuingia bungeni na kutoka wakati Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, na ambaye amefanya mambo mengine mkoani Kigoma kuliko marais wengine anahutubia. Source: Majira

Based on that inaonyesha kabisa Zitto alikua anamuunga mkono kikwete kama katika nafasi ya Urais na Siyo Dr maweapon hiyo ndiyo sababu ya kutoingia bungeni kabisa na kupinga hoja ya chama ya kutoka bungeni wakati Rais anahutubia. Zitto yupo CHADEMA kimaslahi binafsi sana na siyo ya kichama. Kama kweli haungi mkono ni bora angejiudhuru hata hiyo nafasi ya unaibu katibu mkuu awe mwanachama wa kawaida kabisa, Aige mfano wa Shitambala.

Huyo bwana mdogo kaonja fedha za mafisadi na sasa ameanza kuwatumikia. Nikirejea chaguzi za ndani ya chama ninamwona kama ni kijana mwenye tamaa sana ya madaraka. Mimi sisemi chadema wamfukuze lakini ninawashauri wawe makini nae vinginevyo atakivuruga chama. Sisi wananchi wengi wengi wanyonge hapa nchini tumefurahi kupata chama tunachoona kuwa ni kimbilio letu yaani chadema. Bila chadema tungejuaje kama umaskini wetu umesababishwa na mafisadi wanaokumbatiwa na ccm!! Endapo chadema ikiachwa ivurugwe na wachumia tumbo na wenye tamaa ya madaraka kama zitto ni wazi kuwa chadema itaporomoka na hiyo itakuwa ndiyo furaha ya ccm na mafisadi wake. Wananchi wanyonge walioanza kuona mwanga wa matumaini wataangamia.
 
ZITTO KABWE

Ninapenda kuingia katika mjadala huuu. Ndani ya chadema wapo vijana ambao wanampenda sana Zitto na wanaamini iko siku atakuwa Mwenyekiti wa Chadema. Niliwahi waambia tatizo la zitto hawakuani. Zitto bado mdogo sana katika siasa anahitaji kukua kisiasa, hivyo niliwaambia wasimdanganye kuwa anaweza kuwa Mwenyekiti kwa sasa, wamshauli afanya kazi atakazopangiwa ndani ya chama tu. Pia niliwaaambia Zitto kwa sasa hana sifa za kuwa kiongozi, kwani anapenda sana kusema ......mimi nimefanya/nilifanya........nikawaambia viongozi waliofanikiwa duniani (Mfano rahisi kabisa Nyerere) husema .......... sisi tumefanya........... Sasa kama hawakunielewa wakati ule, ebu angalieni kauli/matendo zake/yake katika jambo hili la wabunge wa chadema kutoka mjemgoni!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom