Wakuu,
1:Kuna watetezi wa Zitto hapa ambao ni genuine wanaona Zitto alionewa ingawa hawasemi kwamba alipewa barua kujulishwa makosa yakw
2:Kuna watetezi Genuine wa Chama hapa wanaotaka katiba ifuatwe na ukuu wa Taasisi uzingatiwe
3:Kuna watetezi wa Zitto hapa ambao sio genuine bali ni maadui wake na maadui wa Chadema.Ni maadui wa upinzani.Kazi ya kuchochea upande wanaoamua
4:Kuna wasiofungamana na upande wowote ila wanapenda haki na upinzani imara usio na doa na migogoro
5:Kuna wasiojua chochochote
6:Kuna ambao hawataki kabisa kuhoji ukweli wa hoja hii aliyoleta mleta mada na wapo kwenye hayo makundi yote hapo juu na hii inaweza kupelekea hata wanachama kukwaruzana
7:Kuna wahusika wakuu katika suala hili nao wako hapa hawatasema kwa ID zao halisi au wanafuatilia kwa karibu bila kujali credibility ya thread.
Kila mmoja awe genuine na azingatie haki na ubora wa mijadala sasa. I'm out!
Mbowe ameogopa masharti ya zitto akijua wazi kuwa yeye ndio mwenye makosa. Kwanini asikubali kutoa ushahidi kama ni kweli zitto ana kosa
Watu humu ndani mnaongea sana.yani hata hukumu mahakanani haitolewi hivi.mtu lazima ajitetee ajue kosa lake kisha Kama kuomba radhi ndio aombe .Na Kama ameonewa je?ndio maana nayeye anataka kuwe na masharti kwenye kurudi.
Wa TZ, hasa wana Chadema wajinga kweli. Mtu anahoji kosa lake la kuvumiliwa uwanachama imekuwa kero? Mbowe na Slaa ni virusi vya Ebola katika CDM. Zitto alivuliwa uwanachama kwa sababu alionyesha nia ya kugombea uwenyekiti, pili ukanda, tatu dini yake. Baada ya uchaguzi Mbowe alinukuwa akisema ni vigumu CDM kuongozwa na mwislam au CCM kuongozwa na mkristo. Akili na macho ya ziada inaitajika ili uitambue hili.
Hapa unamaana gani?? [/QUOTE] Baada ya uchaguzi Mbowe alinukuwa akisema ni vigumu CDM kuongozwa na mwislam au CCM kuongozwa na mkristo.[/QUOTE]Mtu anahoji kosa lake la kuvumiliwa uanachama
zitto yuko sahihi ...ataomba msamaha kwa kosa lipi?aambiwe kosa ndipo aombe msamaha.....
Kamanda sio mpango huo, yani urudishe kadi kwa reason rahisi hivyo? Mimi kadi hii sitoirudisha kamwe, tena ngoja kesho nikalipie na ada ya uanachama kabisa.