Zitto aitibua CHADEMA

Zitto aitibua CHADEMA

Viongozi wangu Mbowe na Dr Slaa, tunawapenda sana pia tunawaamini, hebu msameheni Zitto, tunataka tuone ile triple army kama ya zamani, msameheni bila masharti.

Zitto na wewe hebu tunaomba utulie kamanda, epukana na kauli tata tujenge chama.

Once a traitor,you will always be,akafie mbele...
 
Last edited by a moderator:
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.

Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.

“Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.

Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.

Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.

Zitto akisamehewa narudisha kadi Yangu CHADEMA
 
Safi sana! Nawe pia unakaribia kuyala matapishi yako. umeshayanusa na kulamba kwa mbaaali.

Nikikumbuka matope uliyowahi kumsiliba Mh.Zitto, nabaki kutahamaki tu.

Najua tatizo lilikua ni uchaguzi maana alikua ni tishio hasa kwenye uenyekiti. Na angeshinda ule ukurugenzi si ungeusikia redioni?

Anyway, ushapata ulichokua unakilinda mnalegeza misimamo.

Maneno kama yenu nyie vibaraka wa CCM ndiyo yanayoonyesha Chadema ni chama makini chenye msimamo na kisichoyumbishwa.
 
1:Hivi alifukuzwa ndani ya chama?

3:Tuwe wakweli ,je hakuelezwa makosa yake tena kimaandishi?

hapa ndio nakupendaga ben, nashangaa humu watu wanashupaliwa aelezwe makosa hake ili atubu, kana kwamba hakusomewa makosa yake

kwa maoni yangu kama zitto anaona yale sio makosa, basi aendelee kukaa hukohuko aliko, nasisitiza sio lazima awe chadema ili afanye siasa, asitafute kiki ya 2015 kwa lazima, awe na huruma na vijana aliowaweka njia panda act
 
Kuna msamaha wenye masharti?

Ndio,Kwa nini wao wasiweke ushahidi wa usaliti wake ili aombe msamaha?na bado wakaenda jimboni kwake kumchafua na kujisifu ujinga eti alilala Kwa Mwenyekiti so what???

Na mwenyekiti Aombe Radhi Kwa kumchafua na kutoa kauli zisizo na uthibitisho...kwani yeye ndo ana haki ya kubeza na kujaji??

Zitto namuunga Mkono hawezi mtu akuchafue ukishafanya jambo jema akusifie huyo ni mnafiki na Zitto anjiamini sana kwa hilo.

Hata hivyo Kazi alioifanya haiusiano na Usaliti waliomuuta ametekeleza majukumu yake ipasavyo..
 
Safi sana! Nawe pia unakaribia kuyala matapishi yako. umeshayanusa na kulamba kwa mbaaali.

Nikikumbuka matope uliyowahi kumsiliba Mh.Zitto, nabaki kutahamaki tu.

Najua tatizo lilikua ni uchaguzi maana alikua ni tishio hasa kwenye uenyekiti. Na angeshinda ule ukurugenzi si ungeusikia redioni?

Anyway, ushapata ulichokua unakilinda mnalegeza misimamo.
Kweli kabisa , ulikuwa ni uoga wa Ucjaguzi.Wamefanikiwa MBOE MCHAGA na MNYIKA MPARE.
 
Mwenyekiti nae anataka kutuaminisha hiki chama ni chake sasa, kwani kuna shida gani wakasameheana kujenga upinzani wenye nguvu, najua Zitto amejutia usaliti wake na sidhani kama atarudia tena, asamehewe tu.

Anajutia vipi wakati hajui kosa lake? Akae huko huko Wasira kijasho kimtoke.
 
Kwa nini Chadema inafikiria kufanya kosa? Achaneni na mpango huo jengeni chama msiyafuate matatizo.
 
Hamna cha pande mbili kukaa na busara kutumika,issue ni Zitto kurudi na kuomba msamaha kwa yote aliyoyafanya.Sababu aliambiwa,barua anayo sasa huu usanii wa kisiasa huu anaouleta hauwezi msaidia kama kweli alikuwa na nia ya dhati ya kurudi CHADEMA.
Kitu kipo wazi kabisa tuache porojo tuokoe muda hii haihitaji hata cheti cha kuhitimu darasa la saba kujua kuwa Zitto alikosea na alipaswa kushughulikiwa kama sheria,kanuni na katiba ya chama ilivyotaka bila kuangalia yeye ni nani vinginevyo ilikuwa ni chama kuonekana kina double standard.

Na Zitto hapaswi kutumia umaarufu wa kilichojiri bungeni akidhani kuwa hiyo pekee imetosha kumpa umaarufu na kukubaliwa,la hasha hiyo ni kwa wale tu wasiojua nini kinaendelea,Zitto kashindwa kupiga nyundo ya utosini juu ya kichwa cha Kikwete wakati mkono wake na influence yake imeonekana ikitumika kwenye kufanikisha ukwapuaji wa fedha kwenye account ya escrow,katuletea yaleyale ya Mwakyembe na kamati yake kuficha baadhi ya mambo kuogopa serikali kuanguka.
Ushikaji wa Zitto na Kikwete umeharibu fursa nzuri sana ambayo tulikuwa nayo wananchi kupitia wawakilishi wetu wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais.Ripoti ya PAC unatarajia itumike kurudisha umaarufu wa Zitto kwenye vichwa vya watu kama kina Pascal na wengineo.
Zitto anapaswa kuomba msamaha ili arudi kundini,hili sharti analoweka linaonyesha ni jinsi asivyo kuwa na udhati wa nia wa kutaka kwake kurudi kundini.
 
Zitto akisamehewa narudisha kadi Yangu CHADEMA

Kamanda sio mpango huo, yani urudishe kadi kwa reason rahisi hivyo? Mimi kadi hii sitoirudisha kamwe, tena ngoja kesho nikalipie na ada ya uanachama kabisa.
 
Nimeguswa!....nimejiona kundi langu, na reserve comments zangu kwenye hili, kuepuka kunyoosheana vidole!.
Asante.
Pasco

umeguswa nini...si useme tu we ni no 3 tunakufahamu...nyambafu
 
Suala lililopo hapa ni kwamba zitto amefanya hesabu ya haraka na kuona kwamba ili aendelee kuwa kwenye kamati za bunge na kufanya kila awezavyo abaki cdm.hii inaamana kwamba kwa huu muda uliobaki ni mchache mno kwa kukitangaza chama chao act.kama watakitangaza je kitapata mafanikio kwa huu muda mchache uliobaki?dec 5 ndio ilikua cku ya kukizindua rasimi lakini mpaka leo atuoni chochote.kwa hiyo hapo ni kama zitto amesharudi kundini ila mtihani kwa wenzie maana chama kilikua kikisubiri mwenyewe sasa mwenyewe ndio uyo tena anaanza kuweka mazingira ya kurudi cdm. Samsoni. Kitila,mmmmhhh mtafakari ndio kunakucha sasa
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.

Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.

“Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.

Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.

Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.
Siungi mkono Zitto kurejea Chadema. Lakini siamini kama Mbowe kwa ukomavu wake kisiasa na busara yake ya hali ya juu aliyonayo tangu Zitto na sisimizi wenzie walipoanza fujo hadi sasa, Mbowe hawezi kukasirishwa na visharti vya kitoto vilivyowekwa na Zitto. Mbowe kiongozi wangu mimi hababaishwi na visharti vya kijinga. Atakuwa amevipuuza hivyo visharti siku nyingi! Mleta thread lengo lako linajulikana. Ni mbinu ile ile, ya watu walewale kwa malengo yale yale. Hamtafanikiwa!
 
Wewe ndo umeongea, Wakubwa acheni fujo hapa! Zito akirudi, UKAWA mtatikisa sana. Kila mmoja wenu ni wasamani kwa Watanzania. Tunahitaji ng'oa mbuyu 2015! Acheni malumbano!
 
Wewe ndo umeongea, Wakubwa acheni fujo hapa! Zito akirudi, UKAWA mtatikisa sana. Kila mmoja wenu ni wasamani kwa Watanzania. Tunahitaji ng'oa mbuyu 2015! Acheni malumbano!
Wasamani=Wa thamani
 
zitto ni mwanasiasa kijana unayeponzwa na kauli za majivuno nakibri.
sikuukijakujitambua na kujisahihisha nyota yako itang'ara zaidi kupitia chadema tu!
kauli za kujikosha na kujitafgutia huruma kwa wafuasi wako walio wachache haitakufikisha popote zaidi ya kukumaliza kisiasa.
kama mbowe angekuwa mmbaya wako angaliacha mjadala uendelee siku ya kwanza ya kujadili sakata la escrow na mwishowe mwmbo yakaharibika kwa kuachia uwajishwaji kwa raisi.
>>>hukumu kubwa na mbaya ingekuehukia wewe ambaye ama kwa weledi wa hali yajuu uliieshia kutamka kuwa"umechoka".
jipime na ujitafakari sana kijana.
 
Mbona hatuelewani Zito hana tatizo na kusamehewa ila kinachompa tabu hanasamehewa kwa Kosa gani anataka kwanza hajue Kosa Lake
 
Back
Top Bottom