Radhi ya Mbowe yaivuruga CHADEMA: Mgogoro mkubwa unaendelea ndani

Irene Darton

Member
Joined
Feb 25, 2024
Posts
22
Reaction score
27
Hali ya sintofahamu imezidi kushika kasi ndani ya chadema, huku kile kinachoelezwa kama “radhi ya Mbowe” kikitajwa kuwa chanzo kipya cha misuguano, mvutano na mpasuko unaoanza kujitokeza waziwazi miongoni mwa viongozi na wanachama.

Kwa mujibu wa taarifa zinazozunguka ndani ya vikao vya ndani vya chama, baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali—kuanzia mikoa, wilaya hadi kanda—wameanza kutoa shinikizo kali wakitaka uongozi wa kitaifa kuchukua hatua ya haraka kumrejesha Freeman Mbowe katika nafasi ya uongozi ili kunusuru kufa kwa chama.

Shinikizo la Chini Kuja Juu

Vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa kundi kubwa la makatibu wa mikoa na wilaya limeungana katika msimamo wa pamoja: kwamba bila juhudi za dhati za kumrudisha Mbowe katika mstari wa mbele, chama kinaweza kupoteza mshikamano wake.

Wengine wameenda mbali zaidi kwa kutishia kujiuzulu nyadhifa zao, wakisema hawapo tayari kushuhudia chama kikiyumba wakati wanahisi suluhisho liko wazi ni Mbowe kurudi kwenye uskani wa mbele katika harakati za chama.

“Tunataka umoja. Na kwa sasa, ishara ya umoja huo ni kumrudisha Mbowe katika nafasi yake ya uongozi,” alinukuliwa mmoja wa makatibu wa wilaya akisema kwa sharti la kutotajwa jina.

Mgawanyiko wa Mitazamo

Hata hivyo, si kila kiongozi anakubaliana na msimamo huo. Ndani ya chama kuna kundi lingine linaloamini kuwa mwelekeo mpya wa uongozi unapaswa kuheshimiwa, na kwamba kurejea kwa Mbowe kunaweza kuleta changamoto mpya badala ya suluhisho.

Tofauti hizi za kimtazamo zimeanza kujenga makundi mawili makuu: wale wanaotaka “maridhiano na urejesho” na wale wanaotetea “mwendelezo wa mabadiliko.”

Hatari ya Wimbi la Kujiuzulu

Tishio kubwa zaidi linalolikabili chadema kwa sasa ni uwezekano wa wimbi la kujiuzulu kwa viongozi wa ngazi za kati na chini. Tayari baadhi wameashiria kuwa wako tayari kuachia nafasi zao na kubaki wanachama wa kawaida—hatua ambayo inaweza kudhoofisha sana miundombinu ya chama katika maeneo mbalimbali.

Wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa hali hiyo ikiachwa iendelee, inaweza kusababisha athari kubwa ambayo inaweza kupelekea Chadema kufa katika ulingo wa siasa.

Je, Suluhisho Ni Lipi?

Swali linalobaki ni kama uongozi wa juu wa chama utachukua hatua za haraka kusuluhisha mgogoro huu, au kama mvutano huu utaendelea kukua na kuathiri mustakabali wa chama.

Wapo wanaoamini kuwa suluhisho lipo katika mazungumzo ya wazi, maridhiano ya kweli na kuweka mbele maslahi ya chama kuliko makundi binafsi. Lakini muda ndio utaamua kama wito huo utasikilizwa.

Kwa sasa, macho ya wanachama na wadau wa siasa yameelekezwa kwenye uamuzi wa viongozi wa juu—uamuzi ambao unaweza kuamua hatima ya chama katika kipindi hiki nyeti.
 
chadema walifanya mzaha sana aise katika siasa,
eti heche ni kiongozi wa kitafa ndani ya chama hicho, dah!

walifanya mzaha na utani mbaya sana kiuongozi hoa machadema ambayo yanaelekea kuvurugana vibaya sana katika muda usio mrefu ujao.
 
Mtu aliyeshindwa kwa kula halali na taifa zima likishuhudia uchaguzi huo hawezi kurudishwa kwa shinikizo la watu flani flani. Chama cha Maendeleo na Demokrasia kitaendelea kumtambua Tundu Antipas Lissu kuwa MWENYEKITI HALALI WA CHAMA hiko. Hao wanaotaka wajiuzuru wajiuzuru tu
 
Nyie ni wale wa nyama na bia za bure🚮🚮
Screenshot_2026-04-20_174503.jpg
 
Nyie wa ELIMU MBALIMBALI kutoka Pakistani hahaha hata kuhesabu 1-10 n shida mafuta Lita dola 800 kwel muwe na uwezo wa kuchambaua hal ya siasa

Najua nikiandika haya moyo unawauma SANA ila mfanye nn

Chadema ipo vizur SANA kiuongoz na namna ya kuchakata taarifa

Imagine mwaka mzma mmekifungia lakn bado kipo midomoni mwenu mda wote mbona hukitaji CHAUMMA maana yake chadema n zaid ya chama

Nje ya mada bint ushaolewa
 
Back
Top Bottom