Zitto aitibua CHADEMA

Zitto aitibua CHADEMA

Zitto hadi kajengewa barabara kwake, ni Mbunge gani wa upinzani kajengewa barabara kama ZZK. Nataka nijue tu.

Mbowe mpaka akasema ameruka angani na kutembea ardhini hayaona kiongozi bora kama Kikwete siku ya ufunguzi wa barabara jimboni kwake.
 
Wadau mmeshasahau Zitto alivyoengua wagombea wa CDM dhidi ya Pinda na Nimrod Mkono? Mmeshasahau vikao vyake na Jacky Zoka kuanzia 2009 kuiua CDM? Mmesahau alivyotudanganya anafuatilia mabilioni ya Uswisi ili kutupumbaza? Mmesahau ana madiwani 2 tu kwenye jimbo lake? Mmesahau kaanzisha ACT ili ipambane na CDM na siyo CCM? Mjadala wa Escrow kawalinda Ikulu na Hazina tena alikubali pendekezo la Chenge ndipo Mbowe akawashtukia? Once a traitor always a traitor. Zitto akafie ACT. Full Stop!
 
Zito akirudishwa CDM atakuwa bado ni tatizo. Sioni sababu ya kuhangaika na zito wakati chama kinasonga mbele bila yeye. Sifa zimemponza sana huyu jamaa
 
Shardcole....hii ni objective comment.

Ben is this real you? Sijui nini kinaendelea kwako but I feel like something is wrong somewhere. Vinginevyo basi nikiri kwamba I am impressed by your recent comments.
 
Last edited by a moderator:
Wadau mmeshasahau Zitto alivyoengua wagombea wa CDM dhidi ya Pinda na Nimrod Mkono? Mmeshasahau vikao vyake na Jacky Zoka kuanzia 2009 kuiua CDM? Mmesahau alivyotudanganya anafuatilia mabilioni ya Uswisi ili kutupumbaza? Mmesahau ana madiwani 2 tu kwenye jimbo lake? Mmesahau kaanzisha ACT ili ipambane na CDM na siyo CCM? Mjadala wa Escrow kawalinda Ikulu na Hazina tena alikubali pendekezo la Chenge ndipo Mbowe akawashtukia? Once a traitor always a traitor. Zitto akafie ACT. Full Stop!
Japo zitto ni msaliti na mla rushwa lakini hakuna chadema bila zitto.
 
Viongozi wangu Mbowe na Dr Slaa, tunawapenda sana pia tunawaamini, hebu msameheni Zitto, tunataka tuone ile triple army kama ya zamani, msameheni bila masharti.

Zitto na wewe hebu tunaomba utulie kamanda, epukana na kauli tata tujenge chama.
tatizo hapa sio MBOWE ni ZITTO mwenyewe.. ameambiwa anaweza kusamehewa akarudi kundini . sasa ZITTO anaweka masharti ya nini ili akubali kusamehewa?? TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

1:Kuna watetezi wa Zitto hapa ambao ni genuine wanaona Zitto alionewa ingawa hawasemi kwamba alipewa barua kujulishwa makosa yakw

2:Kuna watetezi Genuine wa Chama hapa wanaotaka katiba ifuatwe na ukuu wa Taasisi uzingatiwe

3:Kuna watetezi wa Zitto hapa ambao sio genuine bali ni maadui wake na maadui wa Chadema.Ni maadui wa upinzani.Kazi ya kuchochea upande wanaoamua

4:Kuna wasiofungamana na upande wowote ila wanapenda haki na upinzani imara usio na doa na migogoro

5:Kuna wasiojua chochochote

6:Kuna ambao hawataki kabisa kuhoji ukweli wa hoja hii aliyoleta mleta mada na wapo kwenye hayo makundi yote hapo juu na hii inaweza kupelekea hata wanachama kukwaruzana

7:Kuna wahusika wakuu katika suala hili nao wako hapa hawatasema kwa ID zao halisi au wanafuatilia kwa karibu bila kujali credibility ya thread.

Kila mmoja awe genuine na azingatie haki na ubora wa mijadala sasa. I'm out!

Nimeipenda sana namba 4
 
Kwani ripoti ya PAC, aliichambua kwa sababu ya chadema au kwa sababu ya bunge? Hio ni gea ya kutaka zitto alegeze msimamo ili aje bila masharti hapana ,lazima mbowe asimame hadharani aombe radhi.....na pia ztto lazima arejeshewe vyeo vyake vyote ndani ya chama.
 
Simiyu Yetu na Mafisadi woooote malizeni ishu ya Escrow kwanza waachieni wanachadema Chadema yao. Zitto ni CCM per se sasa hivi. Zitto hahitajiki CDM bali CCM na ACT
 
faidha foxy ambaye rafiki yake mkubwa ni mwislam mwenzake lakini kisha mzalau sana zitto hasa kwakuona hana msimamo kwenye escrow mfano alikubali pendekezo la chenge na pia akawapiga kijembe chadema kuwa anajua watachukia kukubali pendekezo lile
 
sisi tusiopenda ccm tunaoishi maeneo yote ya tanganyika kutoa kigoma ujiji na pwani tuna imani sana na viongozi wote wa juu wa cdm na kauri tata za zito zilikua zinatukera sana asirudi tena cdm, cdm ni maarufu kwetu kuliko slaal mbowe sembuse zitto
 
Kimsingi ningefurahi kuona nguvu ile ya 2005-2010 ndani ya CDM ikiendelea. Wakati ule Zitto alifanya mengi na pia kushiriki katika mikutano mbalimbali ndani ya Bunge na kwenye majukwaa kama mwana mageuzi. Kwa pamoja walisimama kama timu imara kabla ya mambo kuanza kwenda harijojo.

Makundi mbalimbali yalianzishwa ndani ya chama kwa nia ya za kuangusha wengine na kujenga wengine, na katika hili tuliona wengi wakipoteza utiifu kwa viongozi wao wakuu (HILI NI LA UPANDE MMOJA KWANI PIA WAPO WALIOKOSA HESHIMA KWA ZITTO KAMA KIONGOZI MWANDAMIZI, ILA HAYAKUPEWA UZITO) hadi kufikia mahali chama kushindwa kendelea nao wengine wakifukuzwa na wengine wakijiengua wenyewe, mfano Kafulila Kafulila, Shoza, Mwampamba, Mkumbo, Mwigamba na wengine wengi. Wapo waliokwenda CCM wakiamua kuachana na siasa za upinzani, na wengine wakijiunga na vyama vya upinzani huenda walikuwa na imani kuwa baadae kuwa Zitto atawafuata huko na watafanya Mapinduzi ili Zitto awe kiongozi wao (rejea Sakata la Kafulila NCCR). Wengine waliafikiana kuanzisha chama kimpya mbadala kwa CDM ambacho kitaweza kusimamia yale waliyoyashindwa wakiwa CDM, na hawa walimwandaa Zitto kuchukua madaraka CDM kabla ya mambo kuharibika. Huenda wanategemea Zitto akamilishe ngwe yake ya Ubunge akawe mwenyekiti wao (ACT Tanzania). Kwa muktadha huu basi, ni dhahiri kuwa endapo Zitto atarejea CDM maana yake ni kuwa ameazimia kuizamisha ACT na litakuwa ni pigo kwa washirika wake (Mwigamba, Mkumbo, Mchange and colleagues). Lakini pia inaweza kumuweka Zitto katika mizani mbaya kuwa mtu asiyeaminika, kwani pale wanapokutana na dhoruba basi yeye anawaacha wenzie wakizama wakati akitumia mbinu mbalimbali kuiokoa nafsi yake tu. Lakini pia, kwa wachambuzi wengine wanaweza kuitizama hii kama fursa ya mwisho kujaribu kutimiza lile lililoshindikana, na endapo atafanikiwa basi anaweza kulirudhisha kundi lililotawanyika, wakati huohuo akisambaratisha kundi lililokuwa zizini endapo ------.
Sijui atachukua lipi katika haya. Ni mtihani MZITO kwa ZITTO.
 
Wadau mmeshasahau Zitto alivyoengua wagombea wa CDM dhidi ya Pinda na Nimrod Mkono? Mmeshasahau vikao vyake na Jacky Zoka kuanzia 2009 kuiua CDM? Mmesahau alivyotudanganya anafuatilia mabilioni ya Uswisi ili kutupumbaza? Mmesahau ana madiwani 2 tu kwenye jimbo lake? Mmesahau kaanzisha ACT ili ipambane na CDM na siyo CCM? Mjadala wa Escrow kawalinda Ikulu na Hazina tena alikubali pendekezo la Chenge ndipo Mbowe akawashtukia? Once a traitor always a traitor. Zitto akafie ACT. Full Stop!

Much as Zitto anaweza kuongeza nguvu sana katika siasa za Chadema, nafikiri waachane nae. Tatizo kubwa la Zitto ni he is not a team player. Ana ujuaji na ubinafsi ambao humfanya awasaliti wenzake. Hata kama wakimrudisha, asiaminike moja kwa moja.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, anachukizwa na kitendo cha Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) la kuweka sharti la kurejesha kundini.

Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote za uongozi mapema mwaka huu, kwa sasa yuko mahakamani akitetea uwanachama wake, baada ya viongozi wenzake wakuu kutishia kutaka kumfukuza.

Habari kutoka ndani ya Chadema zinasema, karibu viongozi wote wa juu wa chama hicho, akiwamo Dk. Willibrod Slaa, wameonyesha nia ya kumsamehe Zitto ili arejee kundini, lakini tatizo lilikuja pale mwanasiasa huyo alipoweka sharti.

Inadaiwa kuwa Mbowe ameweka msimamo mkali baada ya Zitto kutoa kauli inayoonyesha kuwa anataka kuwekwa sharti la yeye kurejea ndani ya chama.

“Kulikuwa hakuna tatizo Zitto kusamehewa na kurejea ndani ya chama. Lakini kauli yake kuwa anaweka sharti la kutaka kusamehewa, ndilo limeonekana kumkera mwenyekiti,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama ambaye hakupenda kutajwa.

Amesema baada ya Kamati ya Bunge ya PAC inayoongozwa na Zitto kufanya kazi kubwa ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kisha kuwasilisha mapendekezo yake bungeni, baadhi ya viongozi wa Chadema akiwamo Mbowe na Dk. Slaa walionekana kuwa wako tayari kusamehe yaliyopita, lakini kitendo cha Zitto kuweka sharti kimewaudhi baadhi yao na kumuona kama mtu anayetaka kuabudiwa.

Mapema wiki iliyopita, Zitto alinukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema, "hajui kosa" lake na kuweka masharti kwamba pale atakapoambiwa kosa lake yuko tayari kuomba radhi na kurejea Chadema.


Wakuu,
hakuna haja ya Zitto KURUDI Chadema. Tuko kwenye mapambano ya kuing'oa CCM. Kwa umaarufu wake ingekuwa vyema aanzishe chama then ajiunge katika UKAWA. Nguvu ya cdm sasa iko katika UKAWA sio kwa mtu (individual). Katika kujenga Taasisi tusitangulize ubabe, kwamba bila yeye au mtu fulani mambo hayaendi. Kila mtu achangie kwa uwezo aliompa MUNGU kuing'oa CCM. Na katika mapambano hayo sio lazima mtu ajiunge chadema. Sio kutanguliza ubinafsi, kuweka masharti na hila. Wakati Mwalimu Nyerere anaingia katika chama cha TAA hakuonyesha ubabe kwa wazee wenye chama. Lengo lilikuwa moja tu kumng'oa mkoloni. Sasa tunataka kumng'oa mkoloni mweusi mwenzetu alietusaliti kwa kugeuka dalali wa mali zetu, tusitangulize ubinafsi kwamba mimi nitakuwa nani. Naomba viongozi wa Chadema wasimpokee Zitto kama anaweka mashart, tusonge mbele. Tuandae vijana wengine wengi kama Naibu Katibu Mkuu Zanzibar watakaojenga uwezo kumzidi Zitto. Tukikubali masharti ndio mwanzo wa kutengeneza viongozi masultani ambao hawako tayari kuwajibika kwa wananchi kama waliop[o sasa tunaopambana kuwang'oa.
 
Wewe leo unatia aibu tu hapa. Unaelekea kuyala matapishi yako. Angalau kwasasa umeyakaribia na umeshayanusa,ila unaona aibu maana ni mapema mno. unajua ni kwanini leo upo hivo;

1. wewe pamoja na kutumika kooote huaminiki na chama kama Zitto ambaye ulishiriki kumchafua kwa kiasi kikubwa

2. Wewe umejikuta ni majeruhi wa chaguzi za chama wakudumu hivyo hakuna sababu ya kuendelea kua radical dhidi ya Zitto

3. Unalijipenyeza kupitia kichaka cha IPTL/Escrow kumsogelea Zitto na kwa bahati nzuri ana ngozi ngumu na amekusitiri tu

4. Leo ungetamani Zitto arejee CDM kama kawaida na kufanya nae kazi, lkn bado unajiuliza uso wako utauficha wapi??

Nawaza tu kwa sauti!

Mentality za kipuuzi kama hizi ndizo zitakazofanya matamanio yenu yasitimie kama mnavyotaka
 
Zitto amesema yupo tayari kurudi kundini lakini wakae yeye na viongozi wa chadema wajue tatizo lilikuwa wapi, kama yeye ndio alikuwa na makosa ataomba msamaha kwa wa TZ. na kama kosa lilikuwa la chama kiwe tayari kuomba msamaha.!
 
Ili nililipost mahala fulani...hapa Jukwaani...na bado naamini lina mashiko
It is possible but difficult to handle Zitto, when he has an access to the locker key. This time we going to spent more energy/resources to counteract his 'ill-motive'; as any of his surprise attack, while in the group, to the Unity of UKAWA will be more less beyond repair.

Ni mawazo yangu. Si mwamini hata kidogo kwenye masuala ya kuleta ukombozi wa wananchi kwenye masuhala ya haki, umoja, na amani na maendeleo. He is more obsessed with Power.
 
Viongozi wangu Mbowe na Dr Slaa, tunawapenda sana pia tunawaamini, hebu msameheni Zitto, tunataka tuone ile triple army kama ya zamani, msameheni bila masharti.

Zitto na wewe hebu tunaomba utulie kamanda, epukana na kauli tata tujenge chama.
Ninyi mnaowataka Mbowe na Slaa wamsamehe Zitto, kwani mmeambiwa wapi kwamba wamekataa? Walichosema ni kwamba asiweke masharti ya kuombana msamaha. Ni vyema mkamwambia ZZK aondoe masharti hayo, vinginevyo status quo iendelee
 
Back
Top Bottom