Zitto aitibua CHADEMA

Sitapepesa Macho.. Hakuna aliye juu ya Chama na atakae kwenda kinyume na katiba nafikiri mamuzi magumu yahusike nimuhimu sana naona kuna wengine hata hapa sidhani kama wanasoma katiba ya chama inasemaje na kama wamesoma basi nimakusudi pia wanafanya nao hawatufai. Chadema Kwanza
 
Hanashidana msamaha huyo akafie mbali na ACT kama ni machozi tumesha lia mpaka ya mekauka.

Tumesha anua matanga tayari asije akatuliza kwa mara nyingine tena.
 
You just hit the nail on the head!

Kuna sehemu nimeeleza katika maudhui kama uliyoeleza.

Kwa sasa wafuasi wa Mhe. Zitto wanaweweseka kwa sababu hawafahamu msimamo wake.

Kuna wengine hapa wanapiga kelele wakisema hawataki Zitto arudi CHADEMA lakini hawafahamu kuwa wanaishi katika maneno ya Mbowe na Dkt. Slaa.

Siku Mbowe au Dkt. Slaa wakubaliane kuyamaliza na Zitto, hata kauli za wale waliokuwa wanapinga zitabadilika.

Tutawasikia wakisema, Oooh, hakuna adui wa kudumu au rafiki wa kudumu.

Yani mkuu unaongea as if CHADEMA ni ya Mbowe na Dr.Slaa tu, hujui kuna kamati kuu? Jamani Mbowe na Slaa ni watu wa kupokea mawazo yetu lakini tatizo linakuja je kamati kuu ya chama au kikao husika kilIchompa adhabu Zitto kitakubali?

Kwa maoni yangu Zitto arudishwe tujenge chama sababu hata wanachama wengi tunaunga mkono hoja hii, Pia kitendo cha Chama kumsamehe Zitto haina maana kumpigia magoti Zitto bali ni uamuzi tu mzuri kwa ustawi wa chama, Pia Zitto kama kaomba aambiwe makosa yake ni vyema aambiwe sababu huwezi kutubu dhambi usiyoijua, Kitendo cha chama kusita kumwambia makosa yake kinatoa sintofahamu nyingi hata kama ni kweli makosa yapo na Zitto alikosea. OVER
 
1:Hivi alifukuzwa ndani ya chama?

2: Je,Kanuni za chama hasa maadili na miongozo ya uongozi ibara ya 8:0 (a) (X) ya katiba ya chama si inakataza kiongozi kupeleka kesi mahakamani vinginevyo atakua amejifukuzisha mwenyewe uanachama?

3:Tuwe wakweli ,je hakuelezwa makosa yake tena kimaandishi?
 
Chadema mwombeni radhi kwanza kamanda Zitto halafu naye atawaomba radhi siasa haina adui wa kudumu.Mtu huyu ni jembe kila chama kinamhitaji lakini ana msimamo hajaoa wala kuolewa na mke/mume mwingine kipindi chote cha mgogoro.
 
Reckless comment....!
 
Salama yako ni hii kauli yako kwenye bold, vinginevyo ningejua tunajadili na watoto waliozaliwa leo!.
Maadani ni hukumbuki vizuri, then its ok, ukitulia utakumbuka!, ila ingekuwa huujui mchakato huo, hapo tungeelimishana!, ila kwa kukusaidia tuu, Zitto hajaondolewa Chadema bali alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya Chadema kinyume cha sheria, taratibu na kanuni za Chadema!.

Pasco.

Pasco, mimi si mjuzi wa kauli za dharau so sitakujibu moja kwa moja juu ya kauli zako za "salama yako" au "watoto waliozaliwa leo".

mimi ni mpinzani huru dhidi ya CCM nisiyefungamana na chama chochote, so si ajabu kwangu kutokujua mambo ya akina Zitto na "kufukuzwa" au "kuondolewa nyadhifa", nk. mimi niko kwenye principles zaidi.

vyovyote vile iwavyo, chama chenye kutengeneza na kuabudu individuals kama miungu si chama serious.
 
Huu ni umbea umetungwa kumchafua mbowe..... Hpa hakna mpya ni umbea wa Lumumba
 
Hapo kwenye rangi nyekundi sio sahihi ! Angalau ungesema "....baadhi ya waliokuwa wanapinga.....". Ukiacha hivyo umeni-include na mimi wakati mimi siamini kila kitu eti kwa sababu Mbowe, Slaa au binadamu mwingine yeyote amesema !

Pamoja na kwamba ninawaheshimu viongozi wangu, lakini najua nao ni binadamu na huwa wanafanya makosa kama mimi na hivyo chochote wanachokisema sikimezi tu, ninaangalia kama kina-make sense....Wakifanya hivyo mimi bado nitasema they are wrong hata kama ni viongozi wangu....

Nimemfuatilia Zitto tangu 2009 na ninaamini amekuwa akikisaliti Chama na so far sijaiona chochote cha kunifanya niwe na mawazo mbadala!. Ninaamini itakuwa ni makosa makubwa kwa CDM kumwamini tena Zitto.

You just hit the nail on the head!

Kuna sehemu nimeeleza katika maudhui kama uliyoeleza.

Kwa sasa wafuasi wa Mhe. Zitto wanaweweseka kwa sababu hawafahamu msimamo wake.

Kuna wengine hapa wanapiga kelele wakisema hawataki Zitto arudi CHADEMA lakini hawafahamu kuwa wanaishi katika maneno ya Mbowe na Dkt. Slaa.

Siku Mbowe au Dkt. Slaa wakubaliane kuyamaliza na Zitto, hata kauli za wale waliokuwa wanapinga zitabadilika.

Tutawasikia wakisema, Oooh, hakuna adui wa kudumu au rafiki wa kudumu.
 
Siku zote tunapotafuta kusameheana swala la nani alikosea na nani alikuwa sahihi au yapi makosa yangu halina msingi. Cha maana ni kusameheana na kusonga mbele kama timu kumuokoa "mama Tanzania"
 
Pasco tukisema na wewe umechagua side kabla ya kujua detail ya pande zote au angalao kuweka tahadhari "For the least info niliyonayo"

Halafu ondoa huo ushauri wako wa chama kumnyenyekea mtu.Huo ni ushauri mbaya kabisa kati ya ushauri niliowahi kukutana nao siku za karibuni.

afadhali umelisemea hili mwanachadema mwenyewe.

kwamba eti chama kimpigie magoti an individual kama anavyoshauri Pasco? mkikubali ku-succumb dhidi ya pressure kama hiyo then sidhani kama kuna mtu atakayekichukulia chama chenu seriously tena!!

nakubaliana hata hivyo na ukweli kuwa hekima inahitajika kutoka pande zote lakini no way at the expense of the integrity of the party as an institution..
 
Last edited by a moderator:
Mwandishi kapotosha sana me tena nakumbuka nimeikuta hii news fb tena zzk akisema anashangaa wanao sema yeye yupo ACT
 
Acheni mambo ya kijinga na wewe mtoa mada acha uongo.Unaona raha kila siku kuja hapa jukwaani kumchafua Zitto.
 
Yalikuwa maamuzi ya kamati kuu si ya Mbowe na Slaa pekee,

By the way watamsamehe kwa makosa yapi ? Kwani Zitto amekwambia amekosa ?

Nataka nikuhakikishie kwamba, nimejitahidi kusoma historia ya chama changu CHADEM kwa muda wa kutosha hasa matukio mbalimbali ya CHADEMA kama chaguzi za BAVICHA na taifa 2009,

Nimefatilia visa mbalimbali vya wanasiasa vijana mahiri waliokuwa CHADEMA kama Juju Ndanda, Kafulia, Machali, Mkosamali na mambo ya Zitto na kugombea uenyekiti, nimejiridhisha bila shaka kwamba kuna makundi yaliyoibuka chamani hapo awali, moja likimuunga mkono Mbowe na jingine Zitto, na kundi la Zitto lilikuwa ni la wahanga wa chaguzi za ndani ya chama pamoja na wahanga wa vyeo mbalimbali pale makao makuu,

Kutokana na hili CCM iliweza kujipenyeza kuleta migogoro. Nataka nikuhakikishie kwamba mgogoro uliokuwepo ulikuwa ni wa Zitto na Mbowe na sio wa Zitto na CHADEMA ila sisi wanachama tuliingia kichwakichwa kwa kuside upande mmoja bila kutaka suluhu, pia wanachama tumechangia kwa mchango mkubwa kukuza mgogoro huu.
 
Zitto hayupo ACT rasmi, hawezi kutangaza kwamba yupo ACT wakati ni mbunge kupitia chama cha CDM....Lakini kwa wafuatiliaji wa mambo tunajua Zitto na Kitila ni kati ya waanzilishi wa ACT.

Mwandishi kapotosha sana me tena nakumbuka nimeikuta hii news fb tena zzk akisema anashangaa wanao sema yeye yupo ACT
 
Hayo ni mawazo yako na kwa kweli sikubaliani nayo........

Kama wewe na baadhi ya wanachama wengine mliingia kichwa kichwa mimi sikuingia kichwa kichwa......Nadhani utakubalina na mimi kwamba hata kamati kuu ambayo ndiyo iliyomvua vyeo Zitto haikuingia kichwa kichwa !

Bila hata kwenda kwenye details nyingine....ambazo naamini unazijua, nikuulize swali moja tu : Hivi unafikiri Zitto alianzisha ACT ili kupambana na CCM au Chadema ?

Nataka nikuhakikishie kwamba, nimejitahidi kusoma historia ya chama changu CHADEM kwa muda wa kutosha hasa matukio mbalimbali ya CHADEMA kama chaguzi za BAVICHA na taifa 2009,

Nimefatilia visa mbalimbali vya wanasiasa vijana mahiri waliokuwa CHADEMA kama Juju Ndanda, Kafulia, Machali, Mkosamali na mambo ya Zitto na kugombea uenyekiti, nimejiridhisha bila shaka kwamba kuna makundi yaliyoibuka chamani hapo awali, moja likimuunga mkono Mbowe na jingine Zitto, na kundi la Zitto lilikuwa ni la wahanga wa chaguzi za ndani ya chama pamoja na wahanga wa vyeo mbalimbali pale makao makuu,

Kutokana na hili CCM iliweza kujipenyeza kuleta migogoro. Nataka nikuhakikishie kwamba mgogoro uliokuwepo ulikuwa ni wa Zitto na Mbowe na sio wa Zitto na CHADEMA ila sisi wanachama tuliingia kichwakichwa kwa kuside upande mmoja bila kutaka suluhu, pia wanachama tumechangia kwa mchango mkubwa kukuza mgogoro huu.
 
Hayo ni mawazo yako na kwa kweli sikubaliani nayo........

Kama wewe na baadhi ya wanachama wengine mliingia kichwa kichwa mimi sikuingia kichwa kichwa......Nadhani utakubalina na mimi kwamba hata kamati kuu ambayo ndiyo iliyomvua vyeo Zitto haikuingia kichwa kichwa !

Bila hata kwenda kwenye details nyingine....ambazo naamini unazijua, nikuulize swali moja tu : Hivi unafikiri Zitto alianzisha ACT ili kupambana na CCM au Chadema ?

Ndiyo ninaamini kama Zitto ni miongoni mwa waanzilishi wa ACT, binafsi simlaum katika hili sababu mwanasiasa yeyote anahitaji kupata platform ya kufanyia siasa hivyo kwakuwa alijua atafukuzwa CHADEMA ndiomana akaamua kuandaa makazi mapema, hili ni kawaida na ni haki ya kikatiba ya mwanachama yeyote kuhamia chama kingine, si unakumbuka hata Drslaa baada ya kutoka CCM? Ilibidi aende CHADEMA japo mazingira ya Slaa kwenda CHADEMA nibtofauti na Zitto kutaka kwenda ACT lakini all in all wote objective yao ilikuwa ni kupata political platform.
 
Wakuu,

1:Kuna watetezi wa Zitto hapa ambao ni genuine wanaona Zitto alionewa ingawa hawasemi kwamba alipewa barua kujulishwa makosa yakw

2:Kuna watetezi Genuine wa Chama hapa wanaotaka katiba ifuatwe na ukuu wa Taasisi uzingatiwe

3:Kuna watetezi wa Zitto hapa ambao sio genuine bali ni maadui wake na maadui wa Chadema.Ni maadui wa upinzani.Kazi ya kuchochea upande wanaoamua

4:Kuna wasiofungamana na upande wowote ila wanapenda haki na upinzani imara usio na doa na migogoro

5:Kuna wasiojua chochochote

6:Kuna ambao hawataki kabisa kuhoji ukweli wa hoja hii aliyoleta mleta mada na wapo kwenye hayo makundi yote hapo juu na hii inaweza kupelekea hata wanachama kukwaruzana

7:Kuna wahusika wakuu katika suala hili nao wako hapa hawatasema kwa ID zao halisi au wanafuatilia kwa karibu bila kujali credibility ya thread.

Kila mmoja awe genuine na azingatie haki na ubora wa mijadala sasa. I'm out!
 
Back
Top Bottom