Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
Ingekuwa pumba wala usingechangia chochote, angalia hii thread viewers wake wako wangapi? mbona wengine wamesoma tu michango ya wenzao na wakaendelea na hamsini zao? wewe kama nani ujione kwamba mawazo yako ndio mchele na wenzio ni pumba! haya hiyo AVATAR yako ina maslahi gani kwa taifa? mnafki mkubwa wewe.
Avatar yangu ndio inakuumiza enhe! nimeiweka makusudi hiyo. Endelea kuumia tu! Nanihino mkubwa wee!
 
Je unadhani kuna mtu anaweza kuwa anajua sababu za Mheshimiwa kujitoa facebook hapa? Labda kama mtu huyo atakuwa ameteuliwa na Zitto mwenyewe kuwa msemaje wake. Vinginevyo muuliza swali afanye utaratibu wa kuwasiliana na Zitto mwenyewe.

Thats why nimemshauri jamaa amtumie Zitto private message.... huwezi kujua labda kuna mdau mwingine aliguswa na tatizo kama la huyu jamaa akamuuliza Zitto akajibiwa...... Hapa kuna marafiki zake Zitto pia uenda wanajua.......
 
Hivi kumbe Mtu Ukijitoa Facebook unatakiwa Kutoa Maelezo eee! Nilikuwa Sijui
 
quote_icon.png
Originally Posted by Waberoya
Paulo mjadala mzuri ni kujua walikuwa wanaongea nini! wasije kuwa walikuwa wanaongea mechi za hispania au UK! Paulo nikisema ulimpigia simu mke wa jirani , mara kumi ndani ya mwezi mmoja, bila kujua na kuweka mazungumzo walikuwa wanaongea nini tutakuwa tunakosea sana hupo? si kila wanachoandika mwanahalisi ukimeze kama kilivyo watu huwa wanameza kasa!

Rostam huyu ni mfanya biashara, majirani zetu, ndugu zetu wamejiriwa na huyu mtu, EL hali kadhalika, nyumba za kupanga hata daladala you never know pengine zao!!


Nilisema miaka mingi , dawa ya mafisadi ni JELA! WAKIWAMO MTAANI NI WASAFI!! , tukisema hatuna uwezo wa kuwapeleka jela kama alivyosema Pinda basi hakuna serikali! we need strategic move ya kuondokana na dhana hizi za kumtafuta mchawi, ni sawa na ukihudhiwa kazini unarudi nyumbani kufokea mke na watoto! unatafuta sehemu za KUPUNGUZIA stress na kinachoonekana ndio hiki! we have failed to do great things, tunakazania kupigana na watu wadogo!


Take time, breath deeply! relax, READ...Kama RA ni fisadi angekuwa jela Zito angepata wapi muda wa kuongea naye?? maana kwa akili ndogo ya wafuata mkumbo itakuwa kuwa Zito anaongea na fisadi! who principally siyo fisadi maana sehemu yake ni JELA!!


Tunakuwa kama mbwa tunabweka watu wakija na kutisha wanachukua mawe tunakimbia na kwenda kubwekea uani.Watanzania tumewashindwa mafisadi, tumefikia muda kila mtu tutamuita fisadi, maskini!!!! hata wale wasio.... kisa yuko tofauti na sisi!!


Kazi iliyo mbele yetu na Kubenea analijua hilo ni kuwapeleka jela hawa mafisadi, tukishindwa hapo tukae kimya, kutupa mawe na kuitana mafisadi pasipo ushahidi ni uonevu mbaya sana , hasa pale tunapowasema watu wazuri.


Unamfahamu PA wa Rostam? unawafahamu waliojiriwa naye? unafahamu kampuni yake ya Caspian imeajiri watu wangapi? then who is Zito?


Zito ni nani hata atuzibe mdomo wa kutokuwaza makubwa ya nchi hii ya kuwaweka mafisadi jela? Zito ni nani? nani aliyewaroga kuwa hoja za Zito zitatufikisha pazuri, why you guys dont think globally? kesho Kubenea atatoa Zito alimpigia simu Pengo! keshokutwa watasema alimpigia simu girlfriend wake! who is Zito is he president?? why you guys feeling inferiority towards Zito??-Slaa chukua hiyo! kama kuongea na wenye tuhuma za mafisadi ni Zito pekee?? makanisa mangapi akina Rostam wanaalikwa na kutoa michango, misikiti mingapo kaijenga?? hivi huu ujinga UTATUONDOKA LINI KUWA TUWEZE KUWAZA YA JUU NA MBALI SANA NA SIO AKINA ZITO!!!!


Kubenea hagawi gazeti kama pipi! anauza!!! note this anauza! na wakati mwingine pengine anaowasema wanahusika kugawana fedha ,....who knows?? umeliwa bongo hii!


Ngau magazeti ya UDAKU yenye picha na waliofumaniwa live!! magazeti ya udaku nchi hii yanafanya vizuri sana kuliko Kubena na mwanahalisi!


Kesho baba yako wakati yuko kazini akimpigia simu housegirl mara 3 kwa siku kwa siku 5 za kazi huwezi ukajua wanaongea nini, the same case kama mama yako akiongea na houseboy!!! why conclude by surmising?


Mwambie lengo la kubenea na hizo article ni nini? anataka tumuite Zito fisadi au tumntenge?? muulize yeye aliyechukua fomu za kutaka kugombea ubunge mafia kwa kutumia CCM, si angekuwa anaishi na kukaa vikao na akina Rostam?? Muulize yule matanzania wa kawaida anayetembea kwa mguu toka ubungo mpaka posta hii habari inamsaidia vipi? Tumezoea majungu na wanasiasa wanakula kwa akili na tabia zetu za kusema ''asulubiwe asulubiwe'


Slaa alikiri kuwa nusu ya usalama wa taifa wanareport kwake! kwa njia gani? maana kama simu basi ili la Zito lina ugeni gani na linataka attention gani? au kusema huyu aliongelea kinampanda na huyu aliongelea Rufiji??


nimekuwa nibishana sana kwa siku mbili sasa na wahariri wa MWANAHALISI kuhusu post zao dhidi ya ZITTO KABWE.
BAINAFSI NAONA UHURU WA MTU( ZITTO) unaingiliwa kwa kiwango ambacho haijapata kutokea na anahukumiwa kwa mambo ambayo sio makosa katika mahakama yoyote duniani.najaribu kufikiria,,,, je kila anayewasiliana na R.A, E.L na USALAMA WA TAIFA anafanya kosa. na je hivi SLAA hakuwa anawasiliana na usalama wa taifa? je MBOWE hakuwa anawasiliana na usalama wa taifa? kama wote walikuwa wanawasiliana na usalama wa taifa mbona leo mawasiliano kati ya ZITTO na usalama ndio iwe BIG STORY??
Ajabu ni kwamba hatuambiwi walikuwa wanaomgea nini zaidi ya kutuonyesha muda,siku na mahali alipokuwa ZITO wakati anaongea.
Wadau wa JF,,,,,, kuna kitu kilichojificha katika mashambulizi haya ya MWANAHALISI dhidi ya ZITO.sijui ni kitu gani kwani bado niko katika uchunguzi.
ila nina wasiwasi na dhana ya kutaka kukidhoofisha CDM kupitia migogoro,kumdhoofisha ZITO binafsi kwa malengo binafsi(siyajui),kukichonganisha CDM na usalama wa taifa na mwisho ni kukichonganisha CDM na wananchi huku MWANAHALISI likiwa pembeni likikenua.
NIMEKUWA nikifuatili mienendo ya wahariri, wamiliki na waandishi wa habari wa kiafrika kwa miaka ya hivi karibuni na nilichokiona ni kitu cha kuogofya sana,, nacho ni...
wamekuwa ni watamani ufisadi kiasi cha kutumia kalamu na mitaji yao kutengeneza mazingira ya kuwa mafisadi watarajiwa,wamekuwa wakitumi vyombo vyao na kalamu zao kuendeleza mapambano binafsi dhidi ya watu wasiowaunga mkono au wapinzani wa kibiashara,wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa pamoja na mafisadi ku-TWIST akili za waafrika(waafrica wengi hatuna uwezo wa kuona uongo wa magazet,radio na tv) NA MWISHO WAMEKUWA WAKITUMIA KALAMU ZAO KUJITENGENEZEA MAZINGIRA YA '''''baba nami unikumbuke katika ufalme wako'''''
tuwe makini sana na hawa watu
 
.....,lakini ili mradi leo kwenye mwananchi ameonyesha kuwa atakuwa mbali na vyombo vya habari hiyo ndio njia sahihi ,kwani Kimya kinalipa

Mmh aliyemshauri hamtakii mema, atakwepa vipi hivi vyombo vya habari wakati ajira yake kuu ni siasa na mdau mkubwa kwa utendaji wake ni vyombo vya habari? Ajitahidi kujifunza more on how to communicate with public. Atambue kuwa kuteleza si kuanguka na hakuna kufuzu bila mitihani. Na kuwa matatizo hayakimbiwi yanatatuliwa. Hiyo ni changamoto katika growth na development katika carrier yake ya politics.

We still need, love him and he is worthy of our praise kwa yote aliyotutendea katika kutetea mnyonge wa Tanzania. Hii haimaanishi hatutamsahihisha atakapo potoka kwa sababu hii ni law of nature, parents use sticks to correct their sibblings not because of hate and doctors too dont use knives to cut the diseased parts of the patients; but because of love through which they would save those whom they love!
 
Hivi kumbe Mtu Ukijitoa Facebook unatakiwa Kutoa Maelezo eee! Nilikuwa Sijui

Sio mtu akijitoa tu.... huyu bwana ni follower wa Zitto na alikuwa anatumia medium ya facebook kupata habari za mbunge wake. Sasa Mbunge huyu anapojitoa hatakiwi kutoa maelezo ila yule ambaye huwa anapata habari pale si vibaya kama akijua kwa nini jamaa kajitoa... je ni short time? je kuna other means ya kuwasiliana? je amehamia sehemu nyingine ambapo huyu jamaa anaweza pata information?, je is it just a technical issue?, sababu ni nyingi za huyu follower kutaka kujua issue hiyo

Tukianza kuanalyze maswali wengine tutakuwa hatupati majibu
 
Wow... nimeipenda hii

can we learn more jinsi wanavyofanana.... maana wanasema kuishi ni kujifunza

Albedo hebu nipe shule hapo aisee

Mkuu Tabia zao zote ni Fitina na Majungu, Marafiki wa Zitto wako Imara Kumfitini Mbowe na Genge la Mbowe liko Imara Kumfitini Zitto na Tabia za Watu wenye Fitna ni kwamba wao huwa wanajadili Hisia zaidi bila Facts.

Na Mwisho wa Wafitini ni Kuumbuka tu na ndiyo maana watu wameanza kufuta Post zao humu baada ya Kugundua Kwamba Kuna siku wataambiwa Wazimeze lakini Watashindwa

Marafiki wa Zitto = Genge la Mbowe = Wafitini na Mbwa Mwitu
 
Sio mtu akijitoa tu.... huyu bwana ni follower wa Zitto na alikuwa anatumia medium ya facebook kupata habari za mbunge wake. Sasa Mbunge huyu anapojitoa hatakiwi kutoa maelezo ila yule ambaye huwa anapata habari pale si vibaya kama akijua kwa nini jamaa kajitoa... je ni short time? je kuna other means ya kuwasiliana? je amehamia sehemu nyingine ambapo huyu jamaa anaweza pata information?, je is it just a technical issue?, sababu ni nyingi za huyu follower kutaka kujua issue hiyo

Tukianza kuanalyze maswali wengine tutakuwa hatupati majibu

Njia nzuri alikuwa atumie PM.
 
Sio mtu akijitoa tu.... huyu bwana ni follower wa Zitto na alikuwa anatumia medium ya facebook kupata habari za mbunge wake. Sasa Mbunge huyu anapojitoa hatakiwi kutoa maelezo ila yule ambaye huwa anapata habari pale si vibaya kama akijua kwa nini jamaa kajitoa... je ni short time? je kuna other means ya kuwasiliana? je amehamia sehemu nyingine ambapo huyu jamaa anaweza pata information?, je is it just a technical issue?, sababu ni nyingi za huyu follower kutaka kujua issue hiyo

Tukianza kuanalyze maswali wengine tutakuwa hatupati majibu



  1. zitto ni a.k.a misifa, sasa siku hizi pale facebook watu wanamchana live, kwani watu si wafata mkumbo tena.
  2. kama mtakumbuka hata hapa MMM juzi alikuja na hoja dhaifu na mnaona kwamba hata wale ambao kazi yao ni kumgongea Thanx MMM hata kabla hawajasoma thread yake, nao waligeuka wakasema hapana hii ni ishara watanzania wanaanza kuziamini akili zao kuliko kumuachia mtu mwingine kufikiri kwa niaba yao.
  3. facebook ni mtandao mpana, kama una friends 5000 mtu akiposti kitu kwenye status yako, basi notification inakwenda kwa wale friends zako wote 5000 na wanasoma nini kinaendelea.
  4. Nawapa changamoto wale wenye fikra na mawazo huru waishauri CHADEMA impe nishani ya heshima John Mnyika, kwani ni yeye ndio alikuwa naibu katibu mkuu, na ndio alikuwa anaongoza ngome ya chadema makao makuu, na kufuatilia kila kitu kuhusu mgombea urais Dr (Phd) na kwa muda huo huo alikuwa na kibaruwa kizito cha kuhakikisha anashinda jimbo la ubungo, hakika katika wagombea wote wa chadema ukimuondoa Dr (Phd) hakuna kamanda aliyetumika na CHADEMA kama John mnyika. Lakini hapa kila siku kelele tu Zitto, Zittooooo, zittoo, hii ni dalili kwamba John mnyika ni kijana makini na hana makundi na atafika mbali kisiasa. kama ZItto ni maarufu sana angegombea kinondoni halafu majibu yake mngeyapata.
  5. big up John Mnyika huna makundi, wewe kundi lako ni moja tu wapenda mabadiliko ndani ya TANZANIA.
 
Wewe Muongo na hufai hata kusikilizwa, mbona mi mwenyewe kwenye facebook ni friend wa huyu ndugu, just check out, atakuwa amekublocK! Omba tena urafiki kwake...
 
Wewe Muongo na hufai hata kusikilizwa, mbona mi mwenyewe kwenye facebook ni friend wa huyu ndugu, just check out, atakuwa amekublocK! Omba tena urafiki kwake...

Hawa vijana wanaotumia visimu vya vitochi kulog in wana shida kwelikweli, hawa ni wa kuwasamehe tu na wakuwaelekeza ili waelemike.
haya sasa bwana mdogo ni hivi, Zitto Kabwe amedelete/remove facebook account yake kwa sababu zake binafsi, alichonacho pale facebook, ni kitu kinaitwa page, na page hiyo ni Zitto Kabwe fans, wala huitaji kurequest friendship, wewe unaingia kazi yako ni kuclick pale kwenye like button basi unakuwa wewe ni fans wake. na ukitaka page ya Mkwere nayo ipo search jina lake kamili utamuona hapo anatabasamu, na ukimtaka Dr (Phd) nae msearch kwa jina lake kamili utampata.
Natumaini hii tuition imekutosha. sasa pima mwenyewe je wewe unafaa kusikilizwa?
 
umeongea kwa confidence mwenyewee,, eti "haya bwana mdogo zitto kabwe amedelete/remove account yake". hivi hizi info mnazitoa wapi ninyi?mbona hata account yake ipo active?au na wewe mzee wa vitochi ameku-block nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom