Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
Kupitia kwa msemaji wake na rafiki yake wa karibu (omarilyas) Zitto amejibu tuhuma alizotupiwa na gazeti la MwanaHalisi alichokuwa anaongea na Rostam Aziz.

Nimesikitika sana kusikia eti Omarilyas ndo msemaji wa ZT. Huyu Omarilyas anaonekana anaupeo finyu na hafai kupewa thread humu JF. Ukifuatilia hii thread toka mwanzo utaona jinsi Omar alivyoshindwa kabisa kutetea hoja zake. Tena mpambano ulivyozidi kuwaka moto ndo akachemsha kabisa na kuanza kuandika mambo ambayo hakika ni kama siri za ZT na hivyo kutafsiriwa kuwa amemvua nguo ZT. Baada ya kumwaibisha ZT na pengine ZT aliyasoma na kuudhika huyu Omar amehamua kuyafuta kwa ridhaa yake mwenyewe. Ushahidi ni huu....Angalia time deleted....

2010-12-16_0958.png

2010-12-16_0956.png

2010-12-16_0957.png

2010-12-16_1003.png
2010-12-16_1005.png


Kama uonavyo Omar aliandika post afu akazifuta tena mwenyewe saa 2:11, saa 2:26, saa 2:36, saa 5:21 na saa 5:56. Ni mtu gani makini anayeweza kuwa msemaji wa mtu afute tena mada zake mara 5 kwwa siku? Jamani let us be serious! Huyu ni mganga njaa tu na wala tusimpe credit zozote humu jamvini
 
Paulo mjadala mzuri ni kujua walikuwa wanaongea nini! wasije kuwa walikuwa wanaongea mechi za hispania au UK! Paulo nikisema ulimpigia simu mke wa jirani , mara kumi ndani ya mwezi mmoja, bila kujua na kuweka mazungumzo walikuwa wanaongea nini tutakuwa tunakosea sana hupo? si kila wanachoandika mwanahalisi ukimeze kama kilivyo watu huwa wanameza kasa!

Rostam huyu ni mfanya biashara, majirani zetu, ndugu zetu wamejiriwa na huyu mtu, EL hali kadhalika, nyumba za kupanga hata daladala you never know pengine zao!!

Nilisema miaka mingi , dawa ya mafisadi ni JELA! WAKIWAMO MTAANI NI WASAFI!! , tukisema hatuna uwezo wa kuwapeleka jela kama alivyosema Pinda basi hakuna serikali! we need strategic move ya kuondokana na dhana hizi za kumtafuta mchawi, ni sawa na ukihudhiwa kazini unarudi nyumbani kufokea mke na watoto! unatafuta sehemu za KUPUNGUZIA stress na kinachoonekana ndio hiki! we have failed to do great things, tunakazania kupigana na watu wadogo!

Take time, breath deeply! relax, READ...Kama RA ni fisadi angekuwa jela Zito angepata wapi muda wa kuongea naye?? maana kwa akili ndogo ya wafuata mkumbo itakuwa kuwa Zito anaongea na fisadi! who principally siyo fisadi maana sehemu yake ni JELA!!

Tunakuwa kama mbwa tunabweka watu wakija na kutisha wanachukua mawe tunakimbia na kwenda kubwekea uani.Watanzania tumewashindwa mafisadi, tumefikia muda kila mtu tutamuita fisadi, maskini!!!! hata wale wasio.... kisa yuko tofauti na sisi!!

Kazi iliyo mbele yetu na Kubenea analijua hilo ni kuwapeleka jela hawa mafisadi, tukishindwa hapo tukae kimya, kutupa mawe na kuitana mafisadi pasipo ushahidi ni uonevu mbaya sana , hasa pale tunapowasema watu wazuri.

Unamfahamu PA wa Rostam? unawafahamu waliojiriwa naye? unafahamu kampuni yake ya Caspian imeajiri watu wangapi? then who is Zito?

Zito ni nani hata atuzibe mdomo wa kutokuwaza makubwa ya nchi hii ya kuwaweka mafisadi jela? Zito ni nani? nani aliyewaroga kuwa hoja za Zito zitatufikisha pazuri, why you guys dont think globally? kesho Kubenea atatoa Zito alimpigia simu Pengo! keshokutwa watasema alimpigia simu girlfriend wake! who is Zito is he president?? why you guys feeling inferiority towards Zito??-Slaa chukua hiyo! kama kuongea na wenye tuhuma za mafisadi ni Zito pekee?? makanisa mangapi akina Rostam wanaalikwa na kutoa michango, misikiti mingapo kaijenga?? hivi huu ujinga UTATUONDOKA LINI KUWA TUWEZE KUWAZA YA JUU NA MBALI SANA NA SIO AKINA ZITO!!!!

Kubenea hagawi gazeti kama pipi! anauza!!! note this anauza! na wakati mwingine pengine anaowasema wanahusika kugawana fedha ,....who knows?? umeliwa bongo hii!

Ngau magazeti ya UDAKU yenye picha na waliofumaniwa live!! magazeti ya udaku nchi hii yanafanya vizuri sana kuliko Kubena na mwanahalisi!

Kesho baba yako wakati yuko kazini akimpigia simu housegirl mara 3 kwa siku kwa siku 5 za kazi huwezi ukajua wanaongea nini, the same case kama mama yako akiongea na houseboy!!! why conclude by surmising?

Mwambie lengo la kubenea na hizo article ni nini? anataka tumuite Zito fisadi au tumntenge?? muulize yeye aliyechukua fomu za kutaka kugombea ubunge mafia kwa kutumia CCM, si angekuwa anaishi na kukaa vikao na akina Rostam?? Muulize yule matanzania wa kawaida anayetembea kwa mguu toka ubungo mpaka posta hii habari inamsaidia vipi? Tumezoea majungu na wanasiasa wanakula kwa akili na tabia zetu za kusema ''asulubiwe asulubiwe'

Slaa alikiri kuwa nusu ya usalama wa taifa wanareport kwake! kwa njia gani? maana kama simu basi ili la Zito lina ugeni gani na linataka attention gani? au kusema huyu aliongelea kinampanda na huyu aliongelea Rufiji??
Kweli kabisa Waberoya!
 
Nimesikitika sana kusikia eti Omarilyas ndo msemaji wa ZT. Huyu Omarilyas anaonekana anaupeo finyu na hafai kupewa thread humu JF. Ukifuatilia hii thread toka mwanzo utaona jinsi Omar alivyoshindwa kabisa kutetea hoja zake. Tena mpambano ulivyozidi kuwaka moto ndo akachemsha kabisa na kuanza kuandika mambo ambayo hakika ni kama siri za ZT na hivyo kutafsiriwa kuwa amemvua nguo ZT. Baada ya kumwaibisha ZT na pengine ZT aliyasoma na kuudhika huyu Omar amehamua kuyafuta kwa ridhaa yake mwenyewe. Ushahidi ni huu....Angalia time deleted....

2010-12-16_0958.png

2010-12-16_0956.png

2010-12-16_0957.png

2010-12-16_1003.png
2010-12-16_1005.png


Kama uonavyo Omar aliandika post afu akazifuta tena mwenyewe saa 2:11, saa 2:26, saa 2:36, saa 5:21 na saa 5:56. Ni mtu gani makini anayeweza kuwa msemaji wa mtu afute tena mada zake mara 5 kwwa siku? Jamani let us be serious! Huyu ni mganga njaa tu na wala hana tusimpe credit zozote humu jamvini

Haya ninyi wenye akili nyingi, kujua mengi na wenye point nyingi and great thinkers wa mapambano ya bora mabadiliko .....samahani kwa kuwagusa pabaya...Zidumu fikira za Mwenyekiti na maslahi yenu....
 
Swali jepesi tu, Zitto na Rostam wataongelea NINI ambalo linahusu MASLAHI yetu WATANZANIA?
 
Omarilyas

Sasa naona umeanza kujichanganya mwenyewe... are you switching role models now??

Unajua wewe ni mmoja wa watu ambao tunatofautiana lakini nakuheshimu sana? Waache kina Quinine na his likes waendelee na hizi siasa za ujanjaujanja.....Mwenzako nilifanya kosa la kubishana nao na sasa nimegundua na kujirudi....nakutafadhalisha nawe kufanya hivyo...huu mjadala hauna maana kama ilvokuwa nia ya huyo aliouleta hapa.....
 
Wapenzi naomba kujua sababu ya zito kujitoa kye facebook, tulizoea kupata information zake kupitia account yake ya fecebook ila kwa sasa haipo kulikoni??

Kha! Sasa hapa unamuuliza nani?. Ts watu wengine bwana! yaani amtaje Zitto tuuuu!.Zahabu ni zahabu tu! Hata ipake tope.
 
Ana uhuru wa kufanya hivyo
We inakuhusu nini sasa?:A S-alert1:
 
Originally Posted by kilimasera
HUWA ninaguswa kwa namna ya pekee na matukio yanayoashiria kuibuka kwa migogoro isiyo na kichwa wala miguu ndani ya vyama vya siasa vya upinzani hapa nchini.
Mguso ninaoupata kutokana na hali hiyo huwa hainifanyi kamwe kusahau wa kupuuza ukweli kwamba, migogoro yenye tija hususan ile inayojengwa katika misingi ya mapambano ya nguvu ya hoja ni jambo la afya ndani ya taasisi yoyote.

Hata hivyo, wakati nikiliamini hilo kwa dhati, bado huwa natambua pia kwamba aina ya migogoro inayojengwa katika uzushi, fitina, majungu, kutojiamini na mambo yanayofanana na hayo ni chanzo kikuu cha kuporomoka kwa taasisi za namna hiyo.

Ni kwa sababu hiyo basi ndiyo maana ushahidi wa kihistoria katika taifa hili umekuwa ni mwalimu mzuri kuthibitisha kwamba, kasi ndogo ya kukua kwa mfumo wa vyama vingi nchini kwa kiwango kikubwa imechangiwa na kuibuka kwa mihemuko ya kisiasa ndani ya vyama vya siasa ambayo mara nyingi imekuwa haina mashiko.

Leo hii, miaka 18 na nusu tangu kuanza kwa mfumo wa kisiasa wa vyama vingi nchini, aina hiyo ya mihemuko ya kisiasa isiyo na msingi imepata kwa nyakati tofauti kuvukumba vyama viwili ya upinzani vya CUF na NCCR Mageuzi ambavyo laiti kama vingeweza kuiepuka hali hiyo, vingeweza vikawa katika ngazi nyingine tofauti na ile vilivyopo leo hii.

Hivi ni mchambuzi gani huru anayeweza akashindwa kutambua kwamba, hatua ya uongozi wa juu wa CUF ya kumtimua kutoka katika chama hicho mwasisi na mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, James Mapalala miaka ya mwanzo ya 1990 ni mzizi wa mkwamo wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara?

Kwangu mimi, uamuzi ule wa CUF kumtimua Mapalala na viongozi wenzake wa juu wa chama hicho kwa sababu ya kile kilichobatizwa jina la usaliti wa kisiasa si tu uliwakatisha tamaa baadhi ya wapenzi wa mwanzo wa vuguvugu la siasa za vyama vingi, bali ulikwenda mbele zaidi na kukizorotesha chama hicho upande mmoja wa muungano.

Matokeo ya dhambi hiyo ambayo huenda ilifanywa kwa nia njema ndiyo ambayo ilikipa mwanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na makachero wake kukitungia kila aina ya majina mabaya CUF.

Kosa hilo lilisababisha CUF kipachikwe majina kama vile ‘chama cha Wapemba’, ‘chama cha Waislamu’, ‘chama cha kibaguzi’ na mengine mengi ambayo yumkini hayakuwa yakifanana kwa namna yoyote ile na sera na itikadi zake.

Katika mazingira ya kushangaza na huku kikitumia makosa ya namna hiyo hiyo, CUF kilijiingiza kwa zaidi ya mara mbili katika mizozo ya kipuuzi ya namna hiyo hiyo pale kilipomtimua mmoja wa makada wake maarufu wa zama zile, Naila Jiddawi na miezi kadhaa baadaye kikamfukuza Mkurugenzi wa Habari aliyekuwa kipenzi kikubwa cha wanahabari miaka ya 1990, Ramadhani Mzee.

Matukio hayo yaliyofuatiwa na yale ya kutiwa misukosuko kwa viongozi wengine wa chama hicho kama Tambwe Hizza na baadaye Wilfred Lwakatare ukiyajumlisha pamoja unaweza ukaona namna chama hicho kilivyoshiriki kujiumiza pasipo kuwa na sababu za msingi.

Matokeo ya matukio ya namna hiyo ndiyo ambayo yamekipokonya chama hicho hazina kubwa ya mashabiki na wapenzi wakati katika majimbo ya Bukoba Mjini na Temeke kwa kuyataja maeneo machache tu ya mfano.

Makosa kama hayo ya CUF kwa zaidi ya mara moja yalipata kufanywa pia na NCCR –

Mageuzi ambayo kwa sababu ya mihemuko ya kisiasa isiyo na msingi kilijipalia makaa kwa kuzalisha mgogoro mkubwa wa ndani kilipoamua kumuingia kihuni Augustine Mrema ndani ya chama hicho na kisha kikajaribu kumng’oa kimizengwe shujaa wao huyo ambaye ghafla aligeuka msaliti.

Mhemuko wa kumkumbatia Mrema kishabiki na kumpa madaraka ya juu ya chama na kisha fursa ya kuwa mgombea urais kidikteta kabla ya kupanga njama za kumuangusha kwa hila si tu kwamba ilikitokea puani chama hicho, bali ilitikisa vuguvugu zima la upinzani lililoibuka mwaka 1995.

Hata kabla ya mtikisiko wa Mrema kung’olewa NCCR Mageuzi haujapoa, chama hicho kilijikuta kikilazimika kuendeleza dhambi yake ile ile ya kutafunana pale, James Mbatia alipojijengea mtandao wa siri ndani ya chama hicho na akatumia sanduku la kura za hila kumngoa madarakani aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mabere Marando.

Makosa hayo ya NCCR Mageuzi yalishuhudia chama hicho kikipoteza ushawishi mkubwa kiliojijengea na kaburi la kifo chake likasilibwa vyema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 kilipojikuta kikiangushwa vibaya.

Kila wakati ambapo vyama vya CUF na NCCR- Mageuzi vilipofanya makosa hayo ya kisiasa, nyuma yake kulikuwa na ushawishi na ushabiki mkubwa ndani ya vyombo vya habari.

Hali hiyo ilisababisha wanasiasa waliokuwa wakiibua washindi katika kila kosa wajione wao ndiyo mashujaa waliofanikiwa kuwashikisha adabu wasaliti ambao kwa mtazamo wao walikuwa ndiyo wavurugaji wa kasi ya kukua kwa mfumo wa vyama vingi.

Kwa nyakati tofauti wanasiasa wa aina ya Mapalala, Jiddawi, Lwakatare, Tambwe, Mrema, Marando na wengine wengi wakaonekana kuwa ni wasaliti na wanasiasa ambao walipaswa kuadhibiwa.

Leo hii unapogeuka nyuma na kuviangalia vyama hivyo viwili na kutazama namna vilivyopoteza ushawishi wake kwa sababu tu ya mihemuko isiyo na msingi unaweza ukashindwa kupata jibu ni kitu gani hasa kinapita katika vichwa vya wanasiasa wetu hususan wale walio ndani ya vyama vya upinzani.

Lakini pengine mawazo ya namna hii huwa ni makali zaidi kwa watu kama mimi ninaposhuhudia mihemuko ya namna hiyo hiyo ikitokea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo hii.

Kile kinachotokea ndani ya CHADEMA sasa katika sura inayoelezwa kuwa ni kosa la usaliti wa baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho dhidi ya misingi ya uwajibikaji wa pamoja kinaonyesha dhahiri kurejewa kwa historia ya kutafunana ndani ya vyama vya siasa vya upinzani.

Yumkini makosa ya kisiasa yanayoaminika kufanywa na wanasiasa wa kariba ya Zitto Kabwe na wenzake wengine ndani ya chama hicho yanaweza yakafananishwa kwa namna moja au nyingine na yale yaliyofanywa na wanasiasa wa aina ya Mapalala, Jiddawi, Mrema na wengi wengine wa kabla yao.

Pasipo kujali iwapo ni kweli Zitto ana makosa au la, CHADEMA inapaswa kutambua kwamba hatua zozote zitakachochukuliwa dhidi ya mwanasiasa huyo na wenzake wengine zinaweza kwa kiwango kikubwa kuathiri ukuaji wa chama hicho.

CHADEMA inapaswa kutambua kwamba, madhara yatakayotokana na maamuzi yoyote dhidi ya Zitto hayataathiriwa kwa namna yoyote na taswira ya ndani ya chama hicho au nje iwe ni ile inayomsuta au kumbeba mwanasiasa huyo.

Kwa sababu hiyo basi, viongozi wa juu wa chama hicho cha upinzani watapaswa kupima matokeo ya siku zijazo dhidi ya hatua zozote za kinidhamu walizopanga au watakazopanga kuzichukua dhidi ya Zitto leo au kesho.

Ili kuweza kufikia malengo yao, Mbowe, Dk. Slaa na wazee wa chama hicho watalazimika kutambua kwamba japokuwa Zitto anaweza akawa tatizo katika mitizamo yao, adui wanayepaswa kushughulika naye yuko nje ya chama hicho na kimsingi ni hatima ya CHADEMA siku zijazo kwa namna ile ile walipojifikisha CUF na NCCR- Mageuzi.



Kwa uchambuzi huu, tungekuwa wote tuna urgue kama hivi kwenye hili jamvi, ingekuwa kweli sehemu ya GREAT THINKERS. Hii ndio inatakiwa mtu mwenye uwezo wa kujibu hoja ya mwenzake aje na guts za kufanya hivyo kuliko kuishia kutukana. Wakati mwingine mtu unagundua umbumbumbu wake au uelewa wake anapoongea kuliko angekaa kimya. Tunatakiwa TUBADILIKE tujadili mambo kwa nia ya kujenga na sio kubomoa. Wakati mwingine sio lazima ukomenti kila kitu hata kama huna uelewa na mada.
 
labda amemtumia Zoka kuchunguza wabaya wake, then akagundua nawe uko kwenye list ndo maana akaamua kukublock
 
Acha uongo wewe zito mbona bado yuko kwa facebook? Hebu fanya utafiti kwanza kabla hujaleta taarifa zako humu jf. Nafikiri wewe ndo kakufungia inawezekana unamfatafata sana allaaaa
 
Zitto ana marafiki wanaoamini katika anachokipigania ambacho ni kubadili mazoea ya ufanyaji siasa ambayo yanalenga kujenga nchi na sio wanasiasa...Mbowe ana genge ambalo ama linaundwa common interest ya kulinda na kutetea maslahi fulani ama na chuki dhidi ya watu na mambo fulani yasiyoendana na kile wanachoamini kuwa ni sawa kwao pamoja na mateka wa siasa za vitisho zilizoshika hatamu katika Chadema.....

Soini Tofauti kati ya Marafiki wa Zitto na Genge la Mbowe
 
Mwache ajitoe...na ikiwezekana ajitoe CHADEMA
kwa faida ya nani!? mbona zito ana wakereketa sana hata akikaa kimya mna msakama tu, alikuja hapa jamvini akatoa ufafanuzi wa makosa aliyo yafaya na kuomba msamaha kama kuna watu ai wakwaza bado tu mna msakama mlitaka awalambe miguu....kuweni fair bannnnnnnnnnnnnnnnnnnnna
 
Zitto kama zitto amejitoa facebook,kwani hata marafiki zake wa facebook wanamweleza ukweli,na wengine wanafikia hata stage ya kumtukana. Akaona ni bora ajitoe. Iliyobaki ni page ya zitto fans peke yake.
 
Bwana Ilyasi,

Nimekuwa nasoma maelezo yako kwenye hii thread. Kuna mambo ambayo naona kama unaongea kwa kutaka kujibu hoja moja na kusahau hoja nyengine ulijibu vipi. Ni wewe ndiye unasema Mbowe yumo kwenye paylist ya RA. Na amekuwa anakwenda kwa RA kwa kificho sijui kavaa kofia na miwani au vipi. Unasema Zitto yeye kama ni mawasiliano na kina RA anafanya bila kificho. Na umesema kuwa hakuna mahali Mbowe amewahi kumsakama RA hadharani a`aliwahi kujaribu ikabidi asafiri haraka kuja Dar kuomba radhi. HUO NI UPANDE MMOJA.

UPANDE WA PILI. Unasema Mbowe anawatumia akina Kubenea kwa maslahi yake Binafsi. Kimsingi wanachofanya akina Kubenea ni kile ambacho Mbowe anakitaka. Nani asiyejua kuwa hakuna Gazeti ambalo limekuwa likiandika habari za ufisadi wa RA kama Mwanahalisi? Hivi huyu Mbowe ambaye 'anamiliki' Mwanahalisi na wakati huo huo 'anamilikiwa' na RA angewezaje kurusu Mwanahalisi 'limchafue' King maker wake?

UPANDE MWINGINE: Inaonekana wewe ni mtu wa karibu sana na Zitto. Unajua kama Zitto anachafuliwa na kina Mbowe. Naomba hatua kwa hatua utueleze Mbowe anahusika vipi na kumchafua Zitto kuanzia pale Zitto alipoamua kwenda TBC kusema kile walichokiamua na wenzake kidemokrasia na yeye akaamua kuikana demokrasia. Hivi ni Mbowe ndiye alimtuma Zitto aende TBC. Hivi ni Mbowe ndiye amekuwa akimtuma Zitto amsifie JK hadharani? Nisaidie ndugu yangu kunipa majibu yenye ukweli na si ushabiki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom