Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
Quinine umeshaona umelikoroga huku umekwenda anzisha thred nyingine ni kama unasahau kuwa kuwa humu ndani wanasoma watu mbalimbali na wana uelewa mbalimbali usitulazimishe kuamini unachotaka ukweli si ukae wazi na mbona zito mwenyewe anapenda mcharuko sana na angeweza kukmbilia hapo tbc 1 akaanza kujizungusha na kuogea na OMO ili atakate kwamba yeye hakufanya makosa lakini amekaa kimya pamoja na kusoma humu ndani shutuma hizi zote huyo dogo ni infomer wa ccm na huenda hakuanza jana wala leo AMEJIMALIZA MWENYEWE ASIMTAFUTE MCHAWI WALA GAZETI LA MWANAHALISI na hata kama mwanahalisi wasingeandika angefikia mwisho tu.

Halafu Quinine! nenda kanijibu maswali yangu niliyokuuliza kwenye ka thread chako ulichoanzisha cha kumsafisha ZIGO
 
Wahenga walisema ukitaka kufahamu tabia za mtu angalia marafiki zake.

Na ukitembea na mwizi . . . . .

Je vitabu vitakatifu havikusema wawili hawapatani isipokuwa lao ni moja?
 
Zitto jibu hizi tuhuma tafadhali, maana tumekuwa dilema kwa hali hii tutashindwa kuamini nani mkweli.

Isijekuwa mlikuwa mnachonga mambo yenu.

We sema tu mlichokuwa mnazungumza, hata kama ni mambo ya kujirusha ama kuzungumzia mambo ya miereka au basketball.
 
Kaka,

Uzalendo wa kuficha ukweli ni uzalendo pofu (myopic patriotism) ambayo daima nimekuwa nikiipiga vita. Uzalendo ni pamoja na kusema ama kusimamia yale wengi hawataki kuyasikia lakini unaamini wanapaswa kujua kwani watu wanapaswa kujua. Uzalendo sio kuacha reactionaries na puppets wao wanatamba na cheap propaganda zao halafu baadae tujutie wanapokuwa ndio MASIHA wa kukimbiliwa na raia wakati wote tunajua hasara yake kwa nchi. Uzalendo ni pamoja na kupambana hata kama wengi watadharau mantiki ya mapambano hayo....

By the way, kama ungenijua vizuri kukubalika ama kutokukubalika na wewe ama mwengine yeyote kwangu sio issue kwani KUSEMA UKWELI DAIMA ni hulka yangu hata kama gharama yake ni kubwa......


As long as with proof, I am convinced kuwa haya yote yana mkono wa kina Mbowe na genge lake sitanyamaza kimya wakiendesha siasa majitaka zao dhidi ya Zitto...


Lakini huoni kama busara yako ni ndogo? hivi zitto hawezi kuja mwenyewe na kusema ? uliomba ruhusa kutoka kwa zitto umsemee? AU NI zITTO alikuomba umjibie tuhuma? au wewe ni msemaji wa Zitto? Yaliyosemwa na Mwanahalisi naamini ni kweli lakini je Zitto alikuwepo wakati wa makabidhiano? Kiasi gani kilikopwa toka kwa RA? Zitto ana act kama middle man kama na wakati wa makabidhiano? so hapa sio vita ya wazalendo na mafisadi ni mafisadi dhidi ya mafisadi akiwepo zitto na mbowe kama kweli walip[okea mkopo toka kwa RA maana pesa za RA ni haramu na kuchukua pesa kwake kwa matumizi ya kampeni ni sawa na money laundering.

Unajitahidi kuwa msemaji na unapendeza kujipendekeza kwa kofia ya uzalendo
 
My CSI movie scenes:

Simple, TISS and RA & Co call him in order to frame him for the phone records he has had with them. Won't people want to know what they talked about? A few will want to know, but most people become emotional with such issues and tend to "naturally" pick sides and defend their "thinking" at any costs.. This is where wadau pick sides. Paulo & Co hating on ZK........ kuna wale wanaom-defend Zk, Omary & Co they too will fight..........kuna wale watakaokuja na kusema "CHADEMA wahuni, hawafai kupewa nchi..........Fujo tupu.. That way, CHADEMA will fight and destroy the party and CCM will walk out victorious............

Mkuu I can say about 80% of your post umeandika vyema na kwakweli inaleta ladha nzuri kwenye ubongo kwa mtu makini kuisoma more than once. Ila nakanusha kwa nguvu zote kuwa I have a side in this. Sina mtu yeyote ninaye mkandamiza wala kumtetea na katu sitofanya hivyo. Kilichopo kwenye thread ni kuhusu huu uhusiano kwa njia ya simu Kati ya ZT na RA ambaye wote tunajua sifa zake. Pili thread inakumbushia maongezi kwa njia ya simu ambayo ZT amekuwa nayo kati yake na JZ (Bosi wa TISS) ambaye alikuwa mwiba kwa CDM kwenye uchaguzi wa juzi. Tatu wana JF wamekuwa wakijadili jinsi tabia ya ZT ilivyobadilika siku za karibuni kiasi cha kufikia wabunge wenzake wampigie kura ya kutokuwa na imani naye. Sasa ukiunganisha haya yote unaona kwamba hii thread ilikuwa inakusanya maoni ya GREAT THINKERS kuhusu adhabu gani apewe ili mwanaharamu aweze kupita. Binafsi sina chuki na Zt ila je,akikosea asiadhibiwe? Hata mama yake anakiri mwanaye ni mkorofi na sii msikivu. Hivyo, akiadhibiwa atajifunza na atajirekebisha na kuwa ktk mwenendo mzuri ili atakapokuja kugombea Urais awe anaaminika zaidi.
 
serious breach of privacy and paranoia... JF is fast becoming a sh*t Hole.
 
kwa haya niliyosikia, pamoja na vitendo vyake ambayo viko kinyume na itikadi yake na si wote tulioamua kuwa wapiganaji, naona anafaa na anatosha kabisa kuhusishwa naye. atubu ili aurudie upiganaji
 
kwa haya niliyosikia, pamoja na vitendo vyake ambayo viko kinyume na itikadi yake na si wote tulioamua kuwa wapiganaji, naona anafaa na anatosha kabisa kuhusishwa naye. atubu ili aurudie upiganaji
 
Lakini huoni kama busara yako ni ndogo? hivi zitto hawezi kuja mwenyewe na kusema ? uliomba ruhusa kutoka kwa zitto umsemee? AU NI zITTO alikuomba umjibie tuhuma? au wewe ni msemaji wa Zitto? Yaliyosemwa na Mwanahalisi naamini ni kweli lakini je Zitto alikuwepo wakati wa makabidhiano? Kiasi gani kilikopwa toka kwa RA? Zitto ana act kama middle man kama na wakati wa makabidhiano? so hapa sio vita ya wazalendo na mafisadi ni mafisadi dhidi ya mafisadi akiwepo zitto na mbowe kama kweli walipokea mkopo toka kwa RA maana pesa za RA ni haramu na kuchukua pesa kwake kwa matumizi ya kampeni ni sawa na money laundering.

Unajitahidi kuwa msemaji na unapendeza kujipendekeza kwa kofia ya uzalendo

Sorry, hivi ni wapi nilisema huo ulikuwa mkopo ama Zitto alihusika katika kupatikana kwa hizo fedha? Unapotaka Zitto aje hapa kujibu tuhuma zinazoandaliwa na haohao viongozi wake mbona hutaki kumtaka Mbowe aje hapa kujibu tuhuma zake pia?


Jana niliamua kutoa post zote ambazo niligundua kuwa zinabomoa zaidi badala ya kujenga, lakini kila tukiendelea naendelea kuamini kuwa ustaarabu na UTU kwenu ni ishara za weakeness hivyo hamtaacha huu ujinga wenu hadi upande mwengine nao utakapoweka ustaarabu na UTU pembeni......
 
kwa haya niliyosikia, pamoja na vitendo vyake ambayo viko kinyume na itikadi yake na si wote tulioamua kuwa wapiganaji, naona anafaa na anatosha kabisa kuhusishwa naye. atubu ili aurudie upiganaji

Itakadi ya Zitto ni ipi? Na ya Chadema? Au unajua maana ya tofauti ya Itikadi na mitazamo?

Kama upiganaji kwenu ni kuendeleza chuki dhidi ya wakosaji na huku mkikumbatia makosa hayohayo mnayojidai kuyapiga vita, then ni wazi ushabiki wenu kwa Zitto una mushkeli. Zitto haamini katika siasa za visa na chuki dhidi ya binadamu wenzake kama mnavyoamini ninyi na mapambano kwake ni suala la style nyingi na sio ile ya kuiga wengi wafanyavyo ama watakavyo....

Style yake ya engagement na objectivity Vs populism na chuki, imesaidia kuokoa mabilioni mengi kuliko hayo ambayo wenzake wameyageuza mtaji wa kisiasa na ambayo hakuna walichowahi kuokoa.......

Tatizo wengi mlivutiwa na Zitto the victim of CCM mob justice wakati ule bungeni na sio umakini wa hoja na style yake ya kupambana ili kuleta mafanikio na sio kupambana ili aonekanae nanyi kuwa ni mpambanaji......No wonder huwa mnaishia kuwakumbatia MASIHA FEKI waliojaa uozo na huku wakikemea Uvundo wa wengine.....
 
Kaka,

Uzalendo wa kuficha ukweli ni uzalendo pofu (myopic patriotism) ambayo daima nimekuwa nikiipiga vita. Uzalendo ni pamoja na kusema ama kusimamia yale wengi hawataki kuyasikia lakini unaamini wanapaswa kujua kwani watu wanapaswa kujua. Uzalendo sio kuacha reactionaries na puppets wao wanatamba na cheap propaganda zao halafu baadae tujutie wanapokuwa ndio MASIHA wa kukimbiliwa na raia wakati wote tunajua hasara yake kwa nchi. Uzalendo ni pamoja na kupambana hata kama wengi watadharau mantiki ya mapambano hayo....

By the way, kama ungenijua vizuri kukubalika ama kutokukubalika na wewe ama mwengine yeyote kwangu sio issue kwani KUSEMA UKWELI DAIMA ni hulka yangu hata kama gharama yake ni kubwa......


As long as with proof, I am convinced kuwa haya yote yana mkono wa kina Mbowe na genge lake sitanyamaza kimya wakiendesha siasa majitaka zao dhidi ya Zitto...

Unatakusema yote haya ni kwa sababu kuna kundi kubwa au genge kama ulivyoliita la Mbowei linaloendesha propaganda kwa Zitko na pia counter kundi/genge lingine linaloendesha propaganda kwa Mbowei ambalo miongoni mwao wewe upo kwenye lile genge la Zitko
 
Sorry, hivi ni wapi nilisema huo ulikuwa mkopo ama Zitto alihusika katika kupatikana kwa hizo fedha? Unapotaka Zitto aje hapa kujibu tuhuma zinazoandaliwa na haohao viongozi wake mbona hutaki kumtaka Mbowe aje hapa kujibu tuhuma zake pia?


Jana niliamua kutoa post zote ambazo niligundua kuwa zinabomoa zaidi badala ya kujenga, lakini kila tukiendelea naendelea kuamini kuwa ustaarabu na UTU kwenu ni ishara za weakeness hivyo hamtaacha huu ujinga wenu hadi upande mwengine nao utakapoweka ustaarabu na UTU pembeni......

mmh...kweli 'Wadanganyika' bado tuna safari ndefu!
 
Unatakusema yote haya ni kwa sababu kuna kundi kubwa au genge kama ulivyoliita la Mbowei linaloendesha propaganda kwa Zitko na pia counter kundi/genge lingine linaloendesha propaganda kwa Mbowei ambalo miongoni mwao wewe upo kwenye lile genge la Zitko


Zitto ana marafiki wanaoamini katika anachokipigania ambacho ni kubadili mazoea ya ufanyaji siasa ambayo yanalenga kujenga nchi na sio wanasiasa...Mbowe ana genge ambalo ama linaundwa common interest ya kulinda na kutetea maslahi fulani ama na chuki dhidi ya watu na mambo fulani yasiyoendana na kile wanachoamini kuwa ni sawa kwao pamoja na mateka wa siasa za vitisho zilizoshika hatamu katika Chadema.....
 
This is ridiculous; hivi kila mtu afuatilie nani anazungumza na nani? Mbona sisi wengine basi tungekuwa na hatia by phone records!

Naheshimu sana mchango wa mawazo yako mkuu...lakini pia ni vizuri ukumbuke kwamba, katika hali ya sasa inayoendelea nchini, ambapo Watanzania wanahitaji forum ya kuwaongoza ili kuleta mabadiliko yatakayopelekea maisha bora, CHADEMA kama chama wameonyesha nia ya dhati,hata kama wana mapungufu yao.. sasa basi, lolote ambalo ni utata, lazima liwekwe hadharani mapema ili mwisho wa siku yasitokee majuto..hivi ukikuta MKEO ANA MAWASILIANO YA SIMU NA MWANAMUME MWENYE SIFA YA KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU UTANYAMAZA TU ETI KWA VILE NI HAKI YAKE KUWASILIANA NA MTU YEYOTE?? Mwisho wa siku mambo yakiharibika???? labda Zitto ajitokeze aseme ni nini huwa anajadili na watu hawa, of koz ni Watanzania na binadamu kama sisi....
 
HUWA ninaguswa kwa namna ya pekee na matukio yanayoashiria kuibuka kwa migogoro isiyo na kichwa wala miguu ndani ya vyama vya siasa vya upinzani hapa nchini.
Mguso ninaoupata kutokana na hali hiyo huwa hainifanyi kamwe kusahau wa kupuuza ukweli kwamba, migogoro yenye tija hususan ile inayojengwa katika misingi ya mapambano ya nguvu ya hoja ni jambo la afya ndani ya taasisi yoyote.

Hata hivyo, wakati nikiliamini hilo kwa dhati, bado huwa natambua pia kwamba aina ya migogoro inayojengwa katika uzushi, fitina, majungu, kutojiamini na mambo yanayofanana na hayo ni chanzo kikuu cha kuporomoka kwa taasisi za namna hiyo.

Ni kwa sababu hiyo basi ndiyo maana ushahidi wa kihistoria katika taifa hili umekuwa ni mwalimu mzuri kuthibitisha kwamba, kasi ndogo ya kukua kwa mfumo wa vyama vingi nchini kwa kiwango kikubwa imechangiwa na kuibuka kwa mihemuko ya kisiasa ndani ya vyama vya siasa ambayo mara nyingi imekuwa haina mashiko.

Leo hii, miaka 18 na nusu tangu kuanza kwa mfumo wa kisiasa wa vyama vingi nchini, aina hiyo ya mihemuko ya kisiasa isiyo na msingi imepata kwa nyakati tofauti kuvukumba vyama viwili ya upinzani vya CUF na NCCR Mageuzi ambavyo laiti kama vingeweza kuiepuka hali hiyo, vingeweza vikawa katika ngazi nyingine tofauti na ile vilivyopo leo hii.

Hivi ni mchambuzi gani huru anayeweza akashindwa kutambua kwamba, hatua ya uongozi wa juu wa CUF ya kumtimua kutoka katika chama hicho mwasisi na mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, James Mapalala miaka ya mwanzo ya 1990 ni mzizi wa mkwamo wa chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara?

Kwangu mimi, uamuzi ule wa CUF kumtimua Mapalala na viongozi wenzake wa juu wa chama hicho kwa sababu ya kile kilichobatizwa jina la usaliti wa kisiasa si tu uliwakatisha tamaa baadhi ya wapenzi wa mwanzo wa vuguvugu la siasa za vyama vingi, bali ulikwenda mbele zaidi na kukizorotesha chama hicho upande mmoja wa muungano.

Matokeo ya dhambi hiyo ambayo huenda ilifanywa kwa nia njema ndiyo ambayo ilikipa mwanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na makachero wake kukitungia kila aina ya majina mabaya CUF.

Kosa hilo lilisababisha CUF kipachikwe majina kama vile ‘chama cha Wapemba', ‘chama cha Waislamu', ‘chama cha kibaguzi' na mengine mengi ambayo yumkini hayakuwa yakifanana kwa namna yoyote ile na sera na itikadi zake.

Katika mazingira ya kushangaza na huku kikitumia makosa ya namna hiyo hiyo, CUF kilijiingiza kwa zaidi ya mara mbili katika mizozo ya kipuuzi ya namna hiyo hiyo pale kilipomtimua mmoja wa makada wake maarufu wa zama zile, Naila Jiddawi na miezi kadhaa baadaye kikamfukuza Mkurugenzi wa Habari aliyekuwa kipenzi kikubwa cha wanahabari miaka ya 1990, Ramadhani Mzee.

Matukio hayo yaliyofuatiwa na yale ya kutiwa misukosuko kwa viongozi wengine wa chama hicho kama Tambwe Hizza na baadaye Wilfred Lwakatare ukiyajumlisha pamoja unaweza ukaona namna chama hicho kilivyoshiriki kujiumiza pasipo kuwa na sababu za msingi.

Matokeo ya matukio ya namna hiyo ndiyo ambayo yamekipokonya chama hicho hazina kubwa ya mashabiki na wapenzi wakati katika majimbo ya Bukoba Mjini na Temeke kwa kuyataja maeneo machache tu ya mfano.

Makosa kama hayo ya CUF kwa zaidi ya mara moja yalipata kufanywa pia na NCCR –

Mageuzi ambayo kwa sababu ya mihemuko ya kisiasa isiyo na msingi kilijipalia makaa kwa kuzalisha mgogoro mkubwa wa ndani kilipoamua kumuingia kihuni Augustine Mrema ndani ya chama hicho na kisha kikajaribu kumng'oa kimizengwe shujaa wao huyo ambaye ghafla aligeuka msaliti.

Mhemuko wa kumkumbatia Mrema kishabiki na kumpa madaraka ya juu ya chama na kisha fursa ya kuwa mgombea urais kidikteta kabla ya kupanga njama za kumuangusha kwa hila si tu kwamba ilikitokea puani chama hicho, bali ilitikisa vuguvugu zima la upinzani lililoibuka mwaka 1995.

Hata kabla ya mtikisiko wa Mrema kung'olewa NCCR Mageuzi haujapoa, chama hicho kilijikuta kikilazimika kuendeleza dhambi yake ile ile ya kutafunana pale, James Mbatia alipojijengea mtandao wa siri ndani ya chama hicho na akatumia sanduku la kura za hila kumngoa madarakani aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mabere Marando.

Makosa hayo ya NCCR Mageuzi yalishuhudia chama hicho kikipoteza ushawishi mkubwa kiliojijengea na kaburi la kifo chake likasilibwa vyema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 kilipojikuta kikiangushwa vibaya.

Kila wakati ambapo vyama vya CUF na NCCR- Mageuzi vilipofanya makosa hayo ya kisiasa, nyuma yake kulikuwa na ushawishi na ushabiki mkubwa ndani ya vyombo vya habari.

Hali hiyo ilisababisha wanasiasa waliokuwa wakiibua washindi katika kila kosa wajione wao ndiyo mashujaa waliofanikiwa kuwashikisha adabu wasaliti ambao kwa mtazamo wao walikuwa ndiyo wavurugaji wa kasi ya kukua kwa mfumo wa vyama vingi.

Kwa nyakati tofauti wanasiasa wa aina ya Mapalala, Jiddawi, Lwakatare, Tambwe, Mrema, Marando na wengine wengi wakaonekana kuwa ni wasaliti na wanasiasa ambao walipaswa kuadhibiwa.

Leo hii unapogeuka nyuma na kuviangalia vyama hivyo viwili na kutazama namna vilivyopoteza ushawishi wake kwa sababu tu ya mihemuko isiyo na msingi unaweza ukashindwa kupata jibu ni kitu gani hasa kinapita katika vichwa vya wanasiasa wetu hususan wale walio ndani ya vyama vya upinzani.

Lakini pengine mawazo ya namna hii huwa ni makali zaidi kwa watu kama mimi ninaposhuhudia mihemuko ya namna hiyo hiyo ikitokea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo hii.

Kile kinachotokea ndani ya CHADEMA sasa katika sura inayoelezwa kuwa ni kosa la usaliti wa baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho dhidi ya misingi ya uwajibikaji wa pamoja kinaonyesha dhahiri kurejewa kwa historia ya kutafunana ndani ya vyama vya siasa vya upinzani.

Yumkini makosa ya kisiasa yanayoaminika kufanywa na wanasiasa wa kariba ya Zitto Kabwe na wenzake wengine ndani ya chama hicho yanaweza yakafananishwa kwa namna moja au nyingine na yale yaliyofanywa na wanasiasa wa aina ya Mapalala, Jiddawi, Mrema na wengi wengine wa kabla yao.

Pasipo kujali iwapo ni kweli Zitto ana makosa au la, CHADEMA inapaswa kutambua kwamba hatua zozote zitakachochukuliwa dhidi ya mwanasiasa huyo na wenzake wengine zinaweza kwa kiwango kikubwa kuathiri ukuaji wa chama hicho.

CHADEMA inapaswa kutambua kwamba, madhara yatakayotokana na maamuzi yoyote dhidi ya Zitto hayataathiriwa kwa namna yoyote na taswira ya ndani ya chama hicho au nje iwe ni ile inayomsuta au kumbeba mwanasiasa huyo.

Kwa sababu hiyo basi, viongozi wa juu wa chama hicho cha upinzani watapaswa kupima matokeo ya siku zijazo dhidi ya hatua zozote za kinidhamu walizopanga au watakazopanga kuzichukua dhidi ya Zitto leo au kesho.

Ili kuweza kufikia malengo yao, Mbowe, Dk. Slaa na wazee wa chama hicho watalazimika kutambua kwamba japokuwa Zitto anaweza akawa tatizo katika mitizamo yao, adui wanayepaswa kushughulika naye yuko nje ya chama hicho na kimsingi ni hatima ya CHADEMA siku zijazo kwa namna ile ile walipojifikisha CUF na NCCR- Mageuzi.


Siungi mkono mtazamo wake kwa ujumla lakini naamini kuna mengi ya kusoma humu. Inaonyesha huyu jamaa ni mzoefu wa siasa za mageuzi nchini na hivyo kuna mengi ya kutusaidia kwa wale wenye utamaduni wa kutaka kujua.....
 
Wapenzi naomba kujua sababu ya zito kujitoa kye facebook, tulizoea kupata information zake kupitia account yake ya fecebook ila kwa sasa haipo kulikoni??
 
Siungi mkono mtazamo wake kwa ujumla lakini naamini kuna mengi ya kusoma humu. Inaonyesha huyu jamaa ni mzoefu wa siasa za mageuzi nchini na hivyo kuna mengi ya kutusaidia kwa wale wenye utamaduni wa kutaka kujua.....
Omarilyas

Sasa naona umeanza kujichanganya mwenyewe... are you switching role models now??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom