Sababu watu wengi humu sio great thinkers hivyo tunapenda digested news sisi tumeze kisha tujigambe kama maexpert wa Tanzania politics and corruption saga.
Kubenea na Zitto walishakuwa marafiki kwa muda fulani, then urafiki ukaenda mrama jee nani anahoji swala hilo? Why urafiki ulikwenda mrama? Jee ni Kweli Kubenea anatumia Mwanahalisi kama tools ya kumkomesha Zitto kwa kumuaribia credibility yake?
Kwa wale ambao hatulukii hadithi tunresearch kwanza, kisa cha wawili hawa kufarakana inasemekana ni mmoja wao kukataaa kuwekeza kwenye biashara ya mwingine, na kwenda kuwekeza kwenye biashara kama hiyo kwenye kampuni nyingine, na ni hapo ndipo beef lilipo anza.
Now go and research.
Jamani, tusiwe Wadanganyika. This is beyond mahusiano binafsi kati ya Zitto na mmiliki wa MwanaHalisi, Kubenea.
Hapa issue ni tuhuma nzito na zenye ushahidi kamili kuwa Zitto amekuwa na mawasiliano ya karibu na mafisadi na vigogo wa usalama wa taifa.
Iwapo Zitto na Kubenea ni maswahiba au maadui siyo issue, ni vijimambo tu. Hata kama unavyodai wewe kuwa Kubenea amenuna eti kwa kuwa Zitto amekataa kuwekeza MwanaHalisi na kwenda kuwekeza kwenye gazeti lingine la wiki kama hilo, bado tuhuma dhidi ya Zitto zinabaki palepale.
CHADEMA ni chama kinachopambana na mafisadi na kuitoa CCM madarakani, iweje tena mmoja wa viongozi wake wenye ushawishi mkubwa, Zitto, akawa swahiba wa mafisadi na vigogo wa CCM? That is the question to ask ourselves. Si upuuzi wa kutafuta the personal relationship between Zitto na mmiliki wa gazeti. Tupime tuhuma zenyewe kwa umakini mkubwa.