Ikiwa kuna mtu atathibitisha kuwa ndoa ya Mut-a ni halali
Tutaomba ushahidi wa wazi juu ya hili
Na ajiepushe na Blaa Blaa
Allah anasema katika Quraan
سورة المعارج

29. Na ambao wanahifadhi tupu zao. 29

30. Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi 30

31. Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.
MAELEZO
Mola ametutaka tuoe sisi Waislam,na inapotokea mmoja wetu,kumiliki wanawake tuliowapata kwa mikono yetu ya kuume(Watumwa wa Kivita Kisheria)
Basi,hakuna shaka katika kuwaingilia/kufanya nao tendo la ndoa
Ni ruhusa kutoka kwa Mola wetu
ZINGATIO
Yeyote,atakaefanya tendo la ndoa,kinyume na mke au yule anaemmiliki kwa mkono wake wa kuume,Basi huyo amepetuka Mipaka(amefanya Dhambi)
Ndoa ya Mut-aa,ukiifanya,wewe umepetula Mipaka Kisheria
Hukmu yako,ni Hukmu ya Mzinifu,unafaa kuadhibiwa kisheria
Sent using
Jamii Forums mobile app