Mpaka hapa nawashukuru sana Safuha na Mfiaukweli kwa mahojiano yenu. Nimenufaika!!
====
Safuha, nikilejea maelezo yako kuwa ruhusa ya ndoa ya mkataba ilitolewa na Mtume (S.A.W) kwa sababu maalumu (vita) kwa sababu ya kukaa muda mrefu nje ya familia na baadaye alikataza (labda baada ya vita kuisha... [naomba maelezo ya ziada sababu ya kusitisha ruhusa hiyo ]).
Je. huoni kuwa sasa ni muda muafaka kurejea ruhusa hiyo kwani siku hizi kuna vita mbali mbali zinazowafanya waumini /wafuasi wa dini wana kuwa mbali na familia zao kwa muda mrefu!? Mfano, kuna vita za ugaidi miaka zaidi ya kumi na tano bado haijaisha.
Pia kuna vita ya kiuchumi watu wako kwenye misheni za vita hii kwa muda mrefu sana tena wengine karibu umri wao wote wa ujana wako kwenye vita hii na hili linaoneka katika familia nyingi hata hapa nchini. Unakuta mama anapigana vita ya kiuchumi Lindi baba anapigana vita ya kiuchumi Kagera ama Baba yupo Katavi vitani mama yupo Tanga ama Kilimanjaro naye anapigana vita ya uchumi kuinusuru familia.... Tena wengine unakuta, Baba yupo Marylland /Detriot (US) na mama yupo Msasani ama Bunju (Tanzania) wote wanapigana vita ya kiuchumi kuinusuru familia!!!
Katika Mazingira haya, huoni kuna haja ya kurejea ruhusa ya ndoa ya mkataba?