Ndoto zenye uzinzi na madhara yake

Ndoto zenye uzinzi na madhara yake

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
368
Reaction score
735
Maana ya Neno Uzinifu
Mtu ambaye hana ndoa lakini anafanya tendo la ndoa huyo anaitwa mzinifu.

Maana ya Pili
Mtu ambaye ameoa au kuolewa anapofanya uzinifu anaitwa mwasherati

Inawezekana watu wengi tuna amini kwamba ndoto zenye kuambatana na vitendo vya uzinzi ni kitu cha kawaida tu , na mara nyingi hatutilii maananu juu ya ndoto hizi

Wakati mwingine tunaona ni sawa tu, kuota unazini na wako wengine wamekwenda mbali zaidi na kuwa wanaona ni furaha kuota ndoto unazini ?

Ndoto ni nini
Kitabu cha Ayu. 33: 13-14, kinatwambia ndoto ni njia ambayo Mungu anatumia kuongea na mtu akiwa usingizini

Kama Mungu anaongea na Mtu kwa njia ya Ndoto, na kwa mujibu wa maandiko Mungu ni Roho maana yake Mungu kama ni Roho anapozungumza nasi kwa njia ya ndoto anasema nasi kwa njia ya kiroho hivyo ni sawa na kusema ndoto ni mlango wa Mungu kusema na roho yangu /nafsi yangu

Ndoto ni mlango ambao Mungu anautumia kwa lengo la kumsaidia mwanadamu kumwondoa katika makusudi yake Ayu 33:17

Kama tulipojifunza hapo juu ndoto ni mlango na mlango hauchagui nani aingie nani asingie , mlango unaweza kutumiwa na mwizi au mchungaji , kadhalika ndoto inaweza kutumiwa na Mungu au shetani

Kuna madhara gani ya kuota ndoto ya uzinifu
Biblia inasema adamu na mkewe walikuwa mtu mmoja kupitia ndoa , kwa hiyo ndoa ni muunganiko wa kimwili na sio wa kiroho

Rom 7:2 Kifungo cha ndoa kati ya Mwanamke na Mwanaume ni pale tu wakiwa katika Mwili ndio maana maandiko yanasema mwanamke amefungwa na sheria ya mume akiwa hai kwa hiyo ndoa ni ya mwili na sio ya rohoni

Kwa hiyo mtu anapoota anafanya uzinzi katika ndoto maana yake anashiriki tendo la ndoa katika ulimwengu wa roho kwa sababu ndoto ni mlango wa kupitisha mambo ya rohoni kwa mwanadamu

Maana ya kuota ndoto za uzinifu / uasherati

Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalo mwanga miza nafsi yake. Mit 6:32

Kwa hiyo mtu anapoota ndoto anafanya uzinzi maana yake , shetani amekusudia kuangamiza nafsi yake

Nini maana ya nafsi kuangamizwa
Kuangamizwa maana yake ni kuhua.

Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.Kut 17:13

Kwa hiyo kupitia ndoto ya uzinzi shetani amekusudia kuua nafsi yako

Madhara ya nafsi iliyokufa
Mtu ambaye nafsi yake imekufa ni mtu ambaye matendo yake yanafananishwa na mtu ambaye hana akili

Madhara mengine ya nafsi yanakwenda kwa kiini cha nafsi ambayo ni kufa kwa fikra, akili na hekima pia

Ndo maana mtu ambaye nafsi yake imekufa ni kawaida kutenda mambo yafuatayo.

ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. 2 Kor 4:4

Mtu ambaye nafsi imekufa ni mbishi sana kwa mambo ya Mungu ni mpinga Kristo

ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao; EFe 4:18

Madhara mengine ya nafsi iliyokufa ni pamoja na kukosa akili , unatenda mambo ya aibu

Ushuhuda
Kijana mmoja ambaye alikuwa anasumburiwa na ndoto za uzinifu akaniambia Mwl natamani sana kuacha zinaa lakini nashindwa kuna wakati nakuwa kama nachanganyikiwa nikimwona mwanamke natamani kulala naye , nimelala ma wanawake wengi na wakati napo jaribu kufunga ili nivuke nashindwa

Madhara makubwa ambayo mtu atapata kwa kuota ndoto za uzinifu ni pamoja na kushindwa kujizuia juu ya dhambi ya uzinzi kwanini?

Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Mathayo 19:6

Kwa hiyo ndoa ni Muunganiko wa kiroho na uzinzi ni hivyo hivyo, unapofanya uzinzi kwenye ndoto maana yake nafsi yako inaungana na roho ya uzinifu ndio maana watu wengi ambao wamekuwa na tabia za kuota ndoto za uzinzi sio rahisi kuhepuka uzinzi kwa sababu nafsi yao inakuwa imefungwa na roho ya uzinzi
Roho ya uzinzi ina ambatana na pepo la uzinzi ndio maana mara zote wale ambao wamekuwa wakufanya uzinzi kwa njia ya ndoto hata maisha yao ya mwili ni hivyo hivyo wamekuwa wakifanya na watu hata ambao uwezi kuzania
 
Kuna haja gani ya kuamini dream state ina nguvu sawa ya kiroho kama physical intimacy?
 
Mtu anayejenga hoja kwa kutumia vitabu kama biblia na quran huyo namuona kama vile ana upeo mdogo sana wa kufikri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom