Shaka-Zulu
JF-Expert Member
- Nov 20, 2018
- 432
- 831
Mkuu nyama ya nguruwe umeruhusiwa endapo tu njaa yako inaweza kupelekea kupata kifo (Hapa dini imethamini uhai ndio maana ikaruhusu kula haramu ili usife kwa sababu ya njaa).
Hapo unapotaka kuhalalisha mutaa kwa mazingira hayo hayo ya ruhusa ya dharura ya kula kiti moto, je ushawahi kusikia mtu amekufa kwa sababu tu nyege zimembana?
Maendeleo hayana chama
Mkuu, mbona kwenye kila amri kuna vilegezo! Saumu ya Ramadhani ni lazima, lakini ukiwa mgonjwa au umesafiri au una dharura fulani, basi unaweza kuziacha na kuzirudia baadaye au unalipia kafara! Wudhu kabla ya Saala ni lazima, lakini maji yakikosekana, unafanya 'tayamum'. Hakika Allah SWT amesema mwenyewe kwamba sijawatakieni ugumu bali nimewatakieni uwepesi, na hii aya inahusu haswa suala ya kujamiana kipindi cha saumu!
Narudia, Uislamu unazingatia sana uhalisia ya maisha, na imelegeza masharti ili maisha ya songe mbele!
Lakini kwenye suala la Mutaa, sijui mazingira yapi ya siku hizi yanaweza kuhalalisha hii ndoa ya muda??? Sijui, kama ni haramu moja kwa moja? Ukweli ni kwamba sijawahi kusikia hata tukio mmoja ya ndoa ya namna hii!