Zimbabwe Election: Progress & Results

Mbeki urges patience on Zimbabwe



The two leaders appeared cordial as they met in Harare today






Spiraling inflation has seen the introduction of a Z$50m note







Zimbabwe - where a drink costs Z$200m





A boy passes a campaign poster of Zimbabwean opposition leader Morgan Tsvangirai in Chitungwiza on Saturday.


Mbeki anasema hakuna crisis zimbabwe sasa nini kimempeleka, rais mzima unakuwa mjinga.
 
Kitila,

Jeshi limeshasema haliwezi kukubali matokeo yoyote ambayo Mugabe hatashinda. Mugabe atashinda kihalali au kwa kuiba.

Kama sijakosea ni kwamba Jeshi la Serikali lilitamka kwamba endapo Mugabe atapata ushindi litampindua, lakini Jeshi la Polisi likaja na tamko mbadala kwamba litahakikisha linamlinda Mugabe.
 
Kama sijakosea ni kwamba Jeshi la Serikali lilitamka kwamba endapo Mugabe atapata ushindi litampindua, lakini Jeshi la Polisi likaja na tamko mbadala kwamba litahakikisha linamlinda Mugabe.

Jamani tusipindishe kilichosemwa, aliyesema ni mkuu wa majeshi tena on his own kwamba hatakuwa tayari kumpigia salute mtu yeyote tofauti na Mugabe. Hivyo siyo jeshi lililosema maana jeshi lina msemaji wake na ndio yuko authorised kutoa tamko rasmi litakaloheshimika kwamba jeshi limesema. Mkuu wa polisi na Magereza wao walikuw wanawashinikiza polisi na askari magereza kuvote for Mugabe na kwamba mtu mwingine yeyote ni sell out na kibaraka.

"at least to set the record straight"
 
Kulikuwa kweli kuna haja gani ya hawa waheshimiwa kukutana Zambia? Si wangebakia tu nyumbani na kutoa matamko haya haya bila kuingia gharama yote hii?
 
Kitila Fratelin anajua propaganda nyeusi ndo maana haoni ubaya wa Mugabe....
 
SADC nao wameogopa kumwambia ukweli matokeo yake wanambembeleza Morgan matokeo yakitangazwa akubaliane nayo.
 
Sadc nao wameogopa kumwambia ukweli, bado wanambembeleza kutangaza matokeo
 
Huu ni unafiki uliopitiliza kwa nini wasimwambie mugabe kuwa ameshindwa? na anatakiwa ajitoe kwa heshima asisubiri atolewe kama Knal Barcar kule commoro, ama hajui kuwa Bush bado anatawala marekani na Brown yupo UK?
 
Hivi nini kinaendelea huko Zimbabwe....wameshapata mshindi?
 
Hivi nini kinaendelea huko Zimbabwe....wameshapata mshindi?

Huko mambo bado magumu sana. Mshindi hajapatikana. Mahakama ilitupilia mbali madai ya wapinzani, na hivyo kura zinahesabiwa upya kwenye baadhi ya majimbo, baada ya serikali kushikilia masanduku ya kura hizo kwa takriban wiki tatu. Wapinzani wameitisha mgomo wa nchi nzima, lakini wananchi wameugomea mgomo huo, hawakujitokeza! Inadaiwa ni kutokana na hali mbaya ya uchumi, watu hawana hela ya kula leo, kwa hiyo wakigoma ndio kufa njaa hivyo! Wafanyakazi hawako tayari kupoteza kidogo wakipatacho makazini, na wananchi waliobaki hawana uhakika wa mlo wa siku, kwa hiyo wameona mgomo ni hatari kwao, wameugomea japo labda kweli wangependa kushiriki. Niliposikiliza habari hii kwenye BBC, nimekumbuka kitabu kiitwacho "KULI" kilichoandikwa na Shafi Adam Shafi, ambacho nilikisoma zaidi ya miaka 25 iliyopita. Katika "KULI", vibarua waliokuwa wanaonewa waliitisha mgomo, lakini baada ya siku 3 mfululizo bila malipo, njaa ilizidi wakarudi makazini kwa majuto, na viongozi wao kina Rashidi wakasalitiwa! Inauma sana kwa kweli. Katika kitabu hicho cha "KULI" Rashidi alijifariji kwa maneno "....yana mwisho haya." Naamini hata ya huko Zimbabwe yana mwisho, lakini mwisho wake lini?
 
Hadi sasa hivi hakuna mshindi hilo ndio agizo la kamati ya uchaguzi, sasa kama nyie mna matokeo zaidi ya hayo tupeni...Na kama nilivyosema toka mwanzo mahakama kuu pia amekatupilia mbali madai ya MDC kwa sababu hawa wote ni matunda ya ZANU - PF...
 
Zimbabwe could be added to UN Security Council's Africa summit
Monsters and Critics


Apr 15, 2008, 18:35 GMT


Mugabe is waiting to take the next move.........
 
Hadi sasa hivi hakuna mshindi hilo ndio agizo la kamati ya uchaguzi, sasa kama nyie mna matokeo zaidi ya hayo tupeni...Na kama nilivyosema toka mwanzo mahakama kuu pia amekatupilia mbali madai ya MDC kwa sababu hawa wote ni matunda ya ZANU - PF...


Kweli hakuna aliyeshinda lakini hayo matokeo mbona hayatangazwi ili duru la pili lifanyike? Kwa nini iwe siri ya ZANU - PF peke yao?
 
Mugabe rival sets run-off terms



The MDC says Morgan Tsvangirai won the presidential vote


Mfano wa uchaguzi umeomekana Italy ambako Silvio amerudi madarakani na uchaguzi umefanyika just over the weekend.

Mugabe amekula nyama ya binadamu ndio sababu hawezi kung'oka maana ni taboo mbaya sana ukishakula tu huwezi kuacha.
 
Dua,
Kweli hakuna aliyeshinda lakini hayo matokeo mbona hayatangazwi ili duru la pili lifanyike? Kwa nini iwe siri ya ZANU - PF peke yao?

Mkuu wewe na mimi pamoja na wengine wote tunajua mshindi nani achana na hizo kura lakini kwa sababu ya ujinga wa mtu mweusi kutumia demokrasia ambayo haiwezi fanya kazi kwetu tumejiingiza ktk kiza kingine kikubwa!..
Tatizo kubwa sio Mugabe isipokuwa chama ZANU PF kwani kama wataachia nafasi hii basi ndio imetoka - wanalijua hili kama ilivyotokea Kenya na baadhi ya nchi ambazo vyama vya upinzani wakipata ushindi basi huchukua zaidi ya miaka 30 kwa chama tawala kuweza kurudi tena madarakani na hawa jamaa wote watakuwa marehemu, kisha ZANU PF hawana tofauti na CCM viongozi wote madarakani ni mafisadi ardhi waliyochukua kwa wazungu wamegawana wenyewe sasa kimbunga kitakuwa pale watakapo shindwa.
Siwezi kuamini kabisa kwamba leo hii CUF ama Chjadema wanaweza peleka mashtaka ya uchaguzi mahakama yetu chini ya Chenge tukategemea haki hata iwe siku moja ama mwezi mzima!
 
Mkandara, maneno mazito. Ila umenikumbusha mfululizo wa vitabu vya "Ujinga wa Mwafrika"..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…