Zimbabwe Election: Progress & Results



Mkuu mi si mwanasiasa ila napenda kuwa realist.

Politics is the art of compromise. Its all about give and take. katika hali tete kama Zimbabwe alot of things are at stake. Kuna watu walishajua wana hati miliki ya kuitawala Zimbabwe forever, leo kupoteza madaraka ghafla ni terrifying nighmare. They can do anything to wretch the nation. I understand your frustrations. But I suppose Morgan has taken a right course. Siasa za Africa ni tofauti sana na huko Europa na USA. Leo Mugabe akijitangaza raisi? what will happen? viongozi wa Afrika watafyata, ulaya wataweka vikwazo-as usual ambavyo vitazidi kuwaathiri wananchi, wapinzani watawekwa ndani..and on..and on... wananchi watazidi kufa kwa hali ngumu za maisha na Mugabe ataendelea kuwepo! Guys think twice before hujacriticize..Zimbabwe is no USA or Europe..its Africa...where rule of law comes second to the rule of man!

Wengi tunaomlaumu Morgan we dont know for sure what it takes to be a credible politician in Africa. Wengi humu tunaandika tuu...lakini ikifika the hour of need..tunafyata..why? unaona siasa ni biashara kichaa....kupigwa, kunyanyaswa..tunaishia kusoma na kuandika academic literatures...Thats why I say mabadiliko makubwa katika jamii yoyote mara nyingi huletwa na rank and file wananchi. Wasomi na elites ni waoga mno. wanaona watapoteza status zao-after all their families are well provided for!

Again Iam not anywhere, but I respect and admire the resilience and courage of Morgan and his colleagues. Mugabe is no joke bana!

Lets think big!!
 
Hakuna tatizo kuwa realist, mbona wengi tu wameshafanya politics za realism.

Kibaya zaidi ya kutokuwa na msimamo ni kutokuwa na msimamo halafu kuwa muongo.

Morgan siyo tu ame compromise vibaya, amecompromise vibaya halafu anaficha ukweli na kusema hajakutana na watu wa Mugabe.Sasa anajiondolea credibility mapema kabisaaa.

Mbona watu wengi hapa hapa Africa hawaku compromise, wapi Mandela? wapi Lumumba? Wapi Machel?
 

Pundit
For some reasons they have to tell lies, actually that is what most politicians do. They even thank God for making them able to die while people are dying.
 
ITS TRUE.....! ITS TRUE.....!
MUGABE AMECHUKIWA KWA KILE UINGIREZA ILISHINDWA KUTEKELEZA.....MORGAN AMEIBUKA KWENYE ISHU YA ARDHI(akitetea wazungu)......SO MUGABE CAN NOT GIVE NCHI MORGAN AMBAYE ANATETEA WAINGIREZA BADALA YA WAZIMBABWE.....BUT MUGABE IS OLD.....!
 

Sasa yaani Wazimbabwe pamoja na kumchagua wanayemtaka kuwaongoza bado sisi hatutaki tunatafuta mzalendo! Nini basi maana ya Uzalendo kama Morgan hawezi ku-fit hapo? Au tunataka kuwachagulia rais? Tuache longo longo na kukemea tabia hii ambayo imepitwa na wakati. Mugabe ameshindwa hata kutoa matokeo halafu anasema re-run, utafanyaje re-run wakati hujui matokeo? Mzee ameadhirika vibaya, wakichapisha matokeo ataaibika maana wizi wake ulikuwa unajulikana hivyo MDC walikuwa macho.

Lets support the people of Zimbabwe na kama waki-fail hapa basi hakuna maana ya Uchaguzi mwingine. Huhitaji kuwa na degree saba kama Mugabe kuua uchumi wa nchi yoyote ile.
 

Can you prove those highlighted words? Au unabwabwaja tu kama kasuku?
 
Unasema kweli.
Wananikumbusha ile hadithi ya kitabu cha kiswahili Darasa la 4 kule Primary.
Tunataka kiongozi.
Awashinde wote kwa urefu
Awashinde wote kwa ufupi
Awashinde wote kwa Akili
Awashinde wote kwa ujinga
Awashinde wote kwa kuongea
Ashinde wote kwa kukaa kimya
Awashinde wote kwa kila kitu.

Huyo ndiyo kiongozi tunaye mtaka kwi kwi kwi kwi!
 
Dua,
Labda hujapenda kuelewa kuwa huu hapa ni mjadala huru ambao tunatoa mawazo yetu nje kabisa na kura zilizopigwa Zimbabwe. Naweza sema hata Bush ama mama Clinton ni chochote kile maadam nimeeleza points zangu. Sii lazima wewe uzikubali ama tukiandika hapa kutatokea changes zozote ama kuleta haki na maendeleo Zimbabwe..
Mbona kuna watu humu mnamzungumzia Mbowe kwa mabaya lakini hatujafikia hatua ya kusema longolongo isipokuwa tunadai hoja kujibiwa na hoja!...JK anasemwa vile vile na hakuna mtu anayeweza beba dhamana ya kiongozi hata mmoja kati yao.
Mkuu Morgan ni kibaraka na hawezi kulikataa hilo inajulikana toka wamweke madarakani kama kingozi wa Upinzani. Mugabe sote tunajua ni mzee tena uzee wake miaka kibao sio uzee ambao waingereza wanaupigia debe baada ya mwaka 2002.. yaani hii miaka 6 tu ndio kawa mzee hivyo ama alikuwa mzee hata kabla ya kuchukua ardhi za wazungu. Mbona kabla ya hapo hawakusema uzee wake?..Oooh mpaka aseme mzungu, sikujua hilo.
Hivyo, ni mawazo yetu kutokana na ukweli kwamba Morgan alitakiwa kuwaambia wananchi kuwa atalazimika kuanzisha mazungumzo na Utawala wa Mugabe kama alivyofanya Raila ambaye hakuanza mazungumzo kwa siri kisha akakana kuwepo kwa mazungumzo hayo mchezo wa Morgan..Hii mkuu inatueleza nini kuhusu Morgan!...kama sio ku prove kwetu kuwa hana msimamo.
Pili, navyofahamu nchi zetu za Kiafrika ukisha kuwa rais basi vyeo vingine vyote ni nafasi za Ulaji tu. Kingine binafsi hainihusu kitu kama Morgan atachukua nchi isipokuwa tunachoizungumzia hapa ni uwezo wake, nafasi yake na pia kuwa yeye ni Kibaraka, kesho akija waonyesha kuwa ni Kibaraka msije sema mbona hatukuyasema haya mwanzoni!..
Kifupi mkuu NDIVYO TULIVYO!..
Mugabe ni reflection ya....hata yeye Morgan ni reflection ya Wazimbabwe wengi wanaompigia kura vile vile.

Aaaah Mkuu Nyani Ngabu na FMES ama kweli maneno haya yanabidi yatungiwe kitabu..
 
Mkandara

Hii thread pamoja na kutoa mawazo huru inahusu uchaguzi uliotokea ambao (Dictator Mugabe) kama wengine waliopita wanavyofanya i.e. Mobutu etc. amezuia usichapishwe au kutolewa kwa sababu ya kushindwa. Well ipo thread nyingine Our relationship with Zimbabwe ni uchaguzi tu lakini huwezi kuzua bila kutoa proof maana hapa ndipo tutakapokuuliza na kama huna proof usizue.

Swala la Mugabe sio uzee kama unavyodai, economy imefeli haijawahi kutokea duniani. Mugabe siku zote ndiye alikuwa kibaraka kwani wakati Lancaster agreement ilipokwisha 1990 alikataa kuchukua ardhi kutokana na makubaliano kwa sababu alikuwa anawalamba miguu wazungu kwa kwenda Ulaya kila week na kufanya shopping za nguvu bila tatizo lolote. Shida ilitokea pale aliposhindwa ku-account pesa aliyopewa na UK kulipia fidia ya mashamba ndipo akaanza kelele. Wazungu walipoamua kumpiga stop ya kwenda ulaya ndio tabu ikawa kubwa, Now wakati Mugabe anafanya biashara na UK na USA sio kibaraka lakini Morgan ambaye amedhalilishwa miaka yote na kushinda kura kihalali ndio amekuwa kibaraka. (Now nini maana ya uchaguzi?)

BTW issue ni hii - Nani kibaraka hapa Anayeshindwa kutangaza matokeo au anayesubiri matokeo? Nafikiri ni muhimu kufahamu vile vile Who (Mugabe) is he Really? Wale wote aliowaua damu zao atazilipa hapa hapa - just wait.

Amekuja na mpya anabwabwaja hovyo kwa kisingizio cha regime change, sasa ni nani aliitisha uchaguzi? Was it UK or USA?

I salute the people of Zimbabwe wako katika amani na hawana haja ya mtafaruku na hivi anatafuta sababu kuweka Marshal Law. Hizo billions za value ya pesa na shida zote walijua watazimaliza kwenye uchaguzi na ndivyo wamefanya. Mwacheni akae Ikulu na kura za urais bila kutangaza AIBU!
 


Mugabe unleashes thugs in Harare in final bid to stay in power


Nothing to add even if they win they are not accepted by the democrats (Mugabe and his henchmen).


MAIL COMMENT: Mugabe must pay for his genocide
 
Hapana bana Waafrika Hatuko Hivyo!!! Wanatupakazia tu

Du unakataa ukweli? Inatakiwa kuukubali ukweli, then utafute njia ya kurekebisha. Mzee Kibaki katoa shule kwa Mzee Mugabe. aibu
 
Kuna mtu alisema kwenye thread hii awali kuwa kama si watu wa zimbabwe, hali ingekwua nyingine kabisa. Kutokana na msingi huo, I want to salute the People of Zimbabwe kwa kuamua kuwa watulivu wakati wanasiasa wanacheza gimmicks zao. Ni kweli kuwa ingekuwa sehemu nyingine, wangeshakuwa incited kuingia mitaani kufanya fujo, wale wa Morgan wakidai matokeo yatangazwe, polisi wakiwadhibiti na humu wafuasiw a Mugabe wakishangilia ushindi, Nchi ingekuwa imeshachafuka, lakini hadi hivi sasa wazimbabwe wameamua kuwa watulivu na kusubiri. nawaomba waendelee na moyo huo huo hata baada ya matokeo kutangazwa.
Lolote litakalotokea wawe na subira kwani linaweza kutatuliwa bila kurushiana risasi mitaani.
 
Watanzania tunajadili tu kuhusu Zimbabwe mimi nijuavyo kuna uwezekano mkubwa kuwa mugabe anapendwa na wazimbabwe.

Kuna siku nilikutana na Mzimbabwe katika kuzungumzia nikawa namponda Mugabe na Uzee na Siasa zilizopitwa na wakati. Yule jamaa alikuwa anafanya kazi kama Machinga type hivyo siyo kusema wa serikali. majibu aliyoyatoa niliogopa nikafuta usemi wangu na kukoma kuzungumzia siasa za watu.

Wazimbabwe wanajuana kwa vilemba
 

..una maana kuna wa-zimbabwe wanampenda,sio!

..hilo halina shaka hata kidogo! hata hitler alipendwa pia!
 
..mugabe..oops!..zanu-pf walifanya makosa pale walipojiridhia kwamba mugabe agombee!walipaswa kutambua kwamba hauziki na kumshauri accordingly.

..tatizo ni kuwa mugabe kwasasa hauziki hata ukim-recondition vipi. watu husahau kwamba hamna marefu yasiyo na ncha!.wananchi wamechoka kutaabika kila siku,mwezi hadi mwaka bila sababu ya msingi,eti kisa mugabe amekingiana kifua na nchi za magharibi!

..awali nilidhani uchaguzi huu angepita kwa shida na kwamba angekuwa on his way out. naona wananchi wa zimbabwe knows better!

..he must leave with the little grace that remains,ama sivyo ataondoka vibaya!

..its only a matter of time!
 
Bwahahahahahahaaaaa....hivi leo ni siku ya ngapi vile tokea uchaguzi ufanyike? I ask coz I've lost count..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…