Zimbabwe Election: Progress & Results

The New York Times reports the state run Paper in
Zimbabwe predicts a run off.

Could it be that Bob is testing the waters before tossing his hat in the second round?

This is his mouthpiece after all

www.nyt.com
 
Msione kimya kingi Mugabe amewekwa kiti moto na wakuu wa vyombo vya dola ,mkuu wa majeshi ya misituni mkuu wa Usalama na jeshi la polisi na vingunge wengine ambao wamemwambia kuwa mambo ni mazito na hawataweza kutekeleza yale aliyowafundisha akina karume na Kibaki ,kwani watakaokufa ni wengi na ni miongoni mwa ndugu na jamaa hivyo akubali matokeo kwa vyovyote vile yatakavyotokea asilazimishe kitu ,kwani zaidi ya mbinu zote za wizi bado ametupwa nyuma kwa mbali sana katika kura za uraisi.
 

Nashukuru kwa post yako nzuri,naomba wapenda mabadiliko wote tushiriki kuhamasisha kitu kilichofanywa zimbabwe cha ngos kutengeneza Zimbabwe Election Support Network. Hizi jumuia zimetoa elimu kwa nguvu zote ndio maana wazimbabwe wameweza kuamua richa ya vitisho vilivyotolewa.Naomba sana taasisi zetu za dini na ngos za haki za binadamu waige kitu hicho TEMCO haiaminiki.Huo mtandao uanze sasa hivi bila kuchelewa kujenga ujasiri kwa wapiga kura wa tanzania, waache kutoa lawama kwa viongozi wa upinzani tu.
 
ZEC: 200 constituencies announced; Zanu-PF loses parliamentary majority

Sokwanele - Enough is Enough - Zimbabwe
PROMOTING NON-VIOLENT PRINCIPLES TO ACHIEVE DEMOCRACY





Siri ya MDC kushinda ni mbinu za kisasa za kutokomeza wizi wa kura alioufanya 2000 election kwa hiyo this time around pamoja na matatizo ya kiuchumi wakati Mugabe akitegemea Wazimbabwe waandamane Ili atumie nguvu za jeshi wao wamekuwa wametulia wakimuangalia tu, AIBU KUBWA. Ameshindwa kupata sababu ya kutumia jeshi.

Sasa waliobaki ni wale makuwadi wanaoangalia matumbo yao yaliyokuwa yanalindwa na Dictactor.
 
Hivi ni nini kinachosababisha haya matokeo kutotangazwa? Afrika bana....inashangaza sana!! Mambo kama haya ndiyo yanasababisha tuonekane Ndivyo Tulivyo!!
 
Kitila Mkumbo,
Tofauti kati yangu na wewe ama pengine wengi humu ni kwamba hamtazami yajayo mbele.. na nini athari zake. Hata siku moja huwezi kukubali kuweka mazungumzo na mtu ambaye KASHINDWA uchaguzi mkuu. Ukikubali ku share Uongozi ina maana umekubaliana na matokeo ya uchaguzi na pia kuonyesha wazi kuwa demokrasia fulani ya mchoro imefanyika nje ya matakwa ya wananchi waliokuchagua. What if Mugabe ndiye angeshinda! kungekuwepo na mazungumzo ya aina yoyote?

Mkuu kama Watanzania asilimia 70 wamekuchagua wewe kutawala kisha wewe kwa woga wa maisha yako ukakubali kufanya muafaka na yule aliyeshindwa!... Hapo mkuu kwa nafasi utakayo pewa utakuwa una represent nani?..Je, kulikuwepo na haja ya wananchi kupiga kura in the first place?...

Pili, nachoshindwa kuelewa ni pale anapokana kufanya mazungumzo na Mugabe hali amefanya.. Je, hii sio kuwadanganya wananchi hao hao waliokupigia kura besides for whose interest unakana?..Kesho utadanganya nini tena pindi ukishindwa kutimiza ahadi ambazo uliwaahidi wananchi walikuchagua..
Mwisho mkuu wangu ikiwa Jeshi limeisha sema haliwezi kutambua uchaguzi huu nje ya Mugabe.. Je, sio jambo la busara kufanya mazungumzo na wakuu wa jeshi kutokana na kauli yao badala ya kufanya mazungumzo na Mugabe!. Pengine yawezekana kabisa kuwa Jeshi linasema hivyo kutokana na interest za kijeshi maanake nchi zetu za Kiafrika na hasa dunia ya Tatu.. mara nyingi Jeshi huwa linajitegemea kimawazo inapofikia swala la kiongozi, wanaweza chukua wao madaraka ya kuongoza nje kabisa ya matokeo ya uchaguzi ama matakwa ya Mugabe.
Je, nini hatma ya uchaguzi huu na kutakuwepo na faida gani ku share uongozi na Mugabe hali wananchi wameridhika na sera za chama chako sdhidi ya zile za chama kilichoshindwa!..Je, haitakuwa mnajaribu kuwahadaa wananchi na hizo kura kumbe ni pambo tu la ukutani kufurahisha nchi za western..
Kibaya kwa Wa Zimbabwe, westerners wataendelea kuweka vikwazo kwa sababu Mugabe kamwe hatakubali kurudisha ardhi na pili ataendelea kuwa rais ama kuwa na nafasi ya juu ktk maamuzi mengi ya serikali mpya.. Na kama swala ni kutopelekwa kortini, mkuu wangu hiyo korti ya dunia haihitaji baraka za rais Morgan ama mjomba wake... Hawa wakisha kuwekea wanted huna pa kujificha na wala sio jukumu la Morgan tena.. he has no say kama wanavyowatafutwa wale Ma- Nazis,Serbian ama Wahutu waliohusika na mauaji.
 
mbona matokeo yamechelewa mno....what is going on.....?
 
Bob I feel you bro. Lakini tuwekane sawa.

1. Kwanza lazima tukubalia na kuappreciate mazingira MAGUMU wapinzani wanayofanyia kazi katika bara letu la Africa. Incumbents wanatumia resources za serikali kama za Chama wakati wapinzani hawana kitu. Hata nyumbani hapa angalia CCM inavyotumia resorces za walipa kodi kufanya shughuli zake, rais au waziri mkuu akienda mkoani kwa shughuli za "maendeleo" ni kuifanyia campaign CCM wakati bill tunalipa sisi. Kifupi kuanzia kwa mtendaji wa kata mpaka raisi..wote wanakifanyia kazi Chama! Sasa jiulize mtu kama Mbowe au Mrema et al, katika mazingira kama hayo watafanya shughuli zao kivipi? bila kusahau CCM kila mwezi wanajilipa millions and millions. we all have tons of explanations lakini ukweli ni kwamba kujitoa muhanga kwenye opposition politics zetu za kiafrika lazima uwe na kichwa cha mwenda wazimu!

2. Personally namsifu sana Morgani he has shown maturity ya hali ya juu sana. Zimbabwe ilipo hata MUGABE ALIJUA "ATASHINDA" KWA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA, LAKINI AS KENYANS HAVE SHOWN WANANCHI HAWAKUTAKA KUPELEKWA HUKO WALIMNYIMA HIYO NAFASI MUGABE YA KUTUMIA JESHI-ATLEAST NOT YET. MPAKA WAKILAZIMISHWA!

3. Tutakuwa wanafiki tusipokubali umakini na juhudi za Morgan (as any other politician he has his own failings) lakini tumeona hata humu JF jamaa alivyopigwa na kuswekwa ndani mara kadhaa, kifupi he was truly after liberation of Zimbabwe. Mugabe kamnyanyasa sana, lakini jamaa kavumilia na wala hajawahi kuadvocate violence kama wengi tunavyotaka kuamini humu. Na wala hajaenda UHAMISHONI Sasa katika hali kama ya Zim, what kind of politician do you want?

4.Kumuita Morgan kwamba ni kibaraka I guess we miss a Point. Hivi hata ungekuwa wewe kweli kama unataka kuendelea kuwa politically relevant, how can you compete without resources? Mugabe anatumia hela za walipa kodi, kitu ambacho Morgan hana! sasa kweli hata kama anapewa hela na Britain nk, what is wrong? wanasiasa wangapi hata huko ulaya wanakuwa financed na outsiders? Kifupi hata kama ni wewe ungekuwa kwenye upinzani katika siasa zetu za kinazi na kizandiki Africa..ungefanya nini? Harafu hii ya kuitana vibaraka nadhani ni hoja MUFILISI, not that everything which comes from the west is BAD kama wanasiasa wetu wanavyopenda tuamini. No way. Kuna mengine mazuri na mengine mabaya, ni sisi kupima. Tujenge hoja. Morgan had no access to resources, Mugabe anacontrol media yote, everything! na leo unategemea kwamba Morgani apambane na Mugabe? lets stop kidding on serious issues as if tunaishi kwenye sayari ya Mars!

5. Mugabe his time is up, hata wale big wigs ambao leo wamepoteza uchaguzi wanamlaumu Mugabe kwa sababu ndiyo chanzo, na wamepoteza mkate... kifupi ni kwamba people were tired. and he can hardly manuevre kwa sababu his political base is fractured to the core. He must accept graceful exit. Swala la jeshi siyo issue kubwa, unafikiri wao wanaishi mbinguni? wale wakubwa walikuwa wanamsupport Mugabe kwa sababu in Africa lazima uonyeshe loyalty yako, otherwise you will be in trouble!

6. Mwisho, swala la kushare power katika nchi za kiafrika haliepukiki na ni la busara sana. Imagine kama Zanzibar incumbent anashinda kwa less than 1%! hata mjinga anajua kwamba waliiba kura, haya angalia Angola, Chad, nk angalia nchi nyingi za kiafrika pale ambapo incumbents wamekuwa na mawazo na msimamo mkali kama unaoonyesha hapa, wapinzani wameishia msituni ambako madhara yake yamekuwa mabaya zaidi. kWA SABABU UCHAGUZI WETU aFRICA HAUNA TRANSPARENCY WALA ACCOUNTABILITY. KIFUPI HATA WATAWALA HAWAAMINI PROCESS YENYEWE. Kifupi sharing of power promotes healing and enables the nation to move forward.

make no mistake, opposition is not a panacea of our woes especially in africa, but if we have decided to follow certain process lets have a level playing field. Sitegemei Morgan hata akipata madaraka kuwa malaika, but kama wananchi wameamua hivyo kwenye open and transparent process, why should one man for his own and selfish reasons hold hostage the whole nation? Let Zim move forward. Tanzania itafuata.

Lastly, I say, when people are tired of you, you will never impose yourself on them. Mugabe had taken for a ride his people..whetever the outcome of the election-He will have a tale to tale in his remaining days!
 
ELECTION RESULTS SO FAR
Parliamentary constituencies
MDC-Tsvangirai: 99
Zanu-PF: 97
Breakaway MDC faction: 10
Independent: 1
Undeclared: 3
Presidential results
None so far
Winner needs more than 50% to avoid run-off
Source: ZEC
 
Wananchi wa Zimbabwe wanatufundisha mengi, wameonyesha ujasiri wa hali ya juu kwa kupiga kura kwa amani na utulivu na kuchagua mtu/chama wanachokihitaji kwa wakati huu. Huu ni ukomavu wa democrasia. Afrika tujifunze kutoka kwa wananchi wa Zimbabwe. Kwa upande mwingine, suala la tume za uchaguzi ni nyeti. Ni upuuzi kwa tume ya uchaguzi kubaki kimya siku 5, hakuna matokeo wala sababu za kucheleweshwa. MDC wametoa matokeo yao, bado tume ipo kimya hata kuyakanusha basi kama si ya kweli. Bila tume huru za uchaguzi, amani yetu inakuwa imewekwa rehani.
 
Mkandara tatizo unataka kuspin mambo hapa kwa kujifanya unauma na kupilizia,tunajua msimamo wako kuhusu zimbabwe na unaamini Tvangarai ni kibaraka wa magharibi,sasa dont come here ukijidai unaplay nice huku roho inakuuma Mugabe is done and he will never come back,yaani jitu limekaa kwenye power 28 yrs na lina 86 yrs lakini bado linataka kuwa raisi...napata wasiwasi na hao wanaompigia kura maana inawezekana nao ni mapunguani tuu
 
Sasa hawa viongozi wa SADC wako wapi? Kwa nini hawamwambiii huyu jamaa his time is up? Anatutia aibu au wanasubiri Bush na Tony opssss.......Brown waseme ndio wakurupuke?

Halafu siku ya kuapishwa Morgan utaona wanaanza kujipeleka na kusema tulikuwa tunaku support what hypocrites
they are?


Wazimbabwe wametulia na Mugabe is going, there is no going back!
 
Lakini hata wangeshinda Zanu-PF bado wananchi wangekuwa wameonyesha ukomavu wa kisiasa. I strongly do not believe kuwa kukomaa kisiasa ni kuchagua wale ambao hawakuwa madarakani bali kuchagua kile kilicho bora kwa manufaa yako na ya kizazi kijacho.

Nawapongeza MDC kwa ushindi huu na kuwaombea wasije pokwa ushindi baada ya mrejeo wa uchaguzi.

Naamini upinzani wa Tanzania wanapata somo hapa; lazima mkubali kuwa ni muhimu sana kushinda nafasi za uwakilishi bungeni ili kujiimarisha. Kwa matokeo ya ODM na MDC naamini mtarudi nyuma na kuhakikisha mnaweka watu competent (wanaouzika mbele ya jamii na si losers) katika chaguzi zijazo na kuhakikisha mnapata ushindi wa kishindo. Safari ni ndefu lakini tambueni wananchi wanahitaji mabadiliko na mnakosea sana pale mnapowapelekea watu ambao tayari walishapoteza imani nao. Lengo lisiwe kuing'oa CCM tu bali kuwahudumia watanzania bila kujali itikadi zao kisiasa na kiimani ili wapunguze machungu ya maisha.

Hali ya Zimbabwe katika maisha ipo kwa asilimia kubwa ya watanzania achia mbali walio mijini. Tunahitaji kina MDC na ODM wa kutosha kuibadili sura ya siasa ya Tanzania.

Heri mimi nimesema
 
Halafu siku ya kuapishwa Morgan utaona wanaanza kujipeleka na kusema tulikuwa tunaku support what hypocrites
they are?
Hiyo ndiyo kawaida ya viongozi wetu mkuu Dua, watajifanya walikuwa wanamuunga mkono tu. Wanafiki tu. Si uliona Kibaki alipommwaga Moi? Hata siku Morgan akimmwaga Bob basi watammwagia sifa kedekede.

Zimbabwe will rejoice soon though that's not total salvation!
 
Mugabe defeated: Britain leads move for £1bn rescue package
 

Mimi kwa mtizamo wangu,naona watu wakichoka wanapiga kura za hasira.Kilichotokea kwenye zim vote ni kwamba wanachi wameamua kumpa Tsivingarai kwa sababu ndiye aliyehimili vitisho vya Bob.Hivyo basi wapiga kura wakaona kuwa kwa hali hiyo ndiye anayefaa.Tafsiri yake Morgan anafaidika na hasira dhidi ya Mugabe.Kumbukumbu zangu zimenikumbusha uchaguzi wa zambia(1991),Malawi(1994) na Cote de Voire(Gen Robert Gue Vs Bagbo).

Ukiona watu wamefikia hapo hawataki wasomi maana wanajua hawawezi kurisk,kwa hiyo wanahitaji Lech Walesa(asiye msomi) kutengeneza mazingira ya wasomi kuingia kwenye ushindani wa kisiasa.
 
TUTAAMKA TU tupeni muda mana hawakutegemea zimbabwe kufikia hapo walipo leo.
 
Allafrica.com published a report citing a Harare correspondent with links to the Mugabe inner circle saying Mugabe has conceded defeat to his close people and confidants.


This is getting tired, it is Thursday already, what will it take a week? Do us a favour Bob and drop out before something nasty happens.
 
RELAXED: Mugabe made first public appearence since voting ended on Saturday

ZIMBABWEAN President Robert Mugabe made his first public appearance on Thursday since weekend polls when he met election observers from the African Union, footage on state television showed.

Mugabe did not make any comment in the brief footage in which he appeared alongside former Sierra Leone president Ahmed Tejan Kabbah.

Kabbah was the head of the African Union mission, which monitored the joint parliamentary, and presidential elections held on Saturday.

While there has still been no word on the outcome of the presidential ballot, the opposition Movement for Democratic Change (MDC) has already won control of parliament.

In an interview with the television, Kabbah said Mugabe appeared "relaxed" during their meeting.

"He looked very relaxed. He is of the view that the problems facing the country will be resolved amicably. He hopes the rest of the results will be forthcoming," he said.

Kabbah also played down criticism from Western governments and from the opposition over the delay in announcing the results.

"We discussed the fact that Zimbabwe is leading the world in terms of elections ... It's the business of the people of Zimbabwe to decide whom they want."

He also revealed that he had earlier met with MDC leader Morgan Tsvangirai who believes he has beaten Mugabe in the presidential election.

"Tsvangirai also had some good words to say about the president," said Kabbah, without giving further details.
--------------------------------------------------------

Je, hii ni clear msg kwamba Mugabe kashindwa na sasa AU wameamua kufanya kazi ya kumshawishi akubali matokeo na kuachia madaraka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…