Ndicho ulichobakiza, ushirikina sio uchawi, ushirikina ni kumshirikisha mwenyezi mungu na vitu vingine/viumbe vingine yaani kuamini asiyekua Mwenyezi mungu sasa hapo sijui umeona wapi nimeweka "chanting" ambayo imekuwa judge as ushirikina?
Na kama umemaanisha uchawi bado hapo requirement au elements za kichawi sijaweka hata moja,
Usilolijua mkuu.
Rakims
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ushirikina ni dhambi. Mwenyezi Mungu wa Mbinguni hana ushirika na giza.
2 Wakorintho 6:14-16 SUV
"Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu."
Kumbukumbu la torati 18:9-14 SUV
"Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. Uwe mkamilifu kwa BWANA, Mungu wako. Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, BWANA, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo."
Mwenye akili aelewe.
Sent using Mikoyan MiG-29