joely sandu
JF-Expert Member
- Nov 24, 2017
- 1,962
- 1,819
OK mkuu ngoja nikae mkao wa kula
OK mkuu ngoja nikae mkao wa kula
sawa lakini situmii makalio kufikria kama wewe
Tatizo wao hupenda sana kudharau imani za wenzao,na wakati imani zao hazijitoshelezi.ukiona watu wanapiga sana vita kitu ujue kinawazidi ubora.Na mtu ukiona kitu akikufai unaachia wengine, ndio maana mimi nikabase huku kwenye intelligence mkuu, nikienda siasa au jokes n.k huwa napita tu, without comments, nashangaa hawa yani hawapiti sehemu bila kusema kitu, ukiuliza watakwambia tunamtangaza mungu mwishoni wataenda casino kutangaza mungu sasa
Rakims
Sent using Jamii Forums mobile app
huwezijua unaemtukana huenda ni babaako wa kamboStill you are Stup*d
Low thinking, you are stup*d and if you think that too you are deadly stup*d, unafikiri kuwa mjinga ni tusi???? Hapana ni ukweli unaouma you were Stup*d you are now and you will always be mkuuhuwezijua unaemtukana huenda ni babaako wa kambo
Wewe waweza kuwa na macho ya muonaji;Mkuu, nimekuwa nikikutana na vioo vyenyewe ukubwa Kama ukuta WA nyumba kwenye ndoto Halafu ndani ya hivo vioo Vina vitu like crystal Au anga na mawingu linavoonekana. Pili hii haikuwa ndoto,Kuna siku nilipita nje ya kanisa ndani nikaona ukuta WA kioo.. Lakini hofu ikaniingia. Hii ina maana gani?
Mkuu nadhani umeeleweka, mimi huwa nahisi behind their quotes ni kwamba wanahofu mtu akitoa elimu ya ziada watu hawatakuwa na uhitaji wa kukemewa mapepo hivyo watakosa wateja, ndio maana siachi kufundisha mkuuAma kweli, Elimu Haina Mwisho.
Waungwana,nimepitia comments za watu kwenye Uzi huu,nimeona na kuamini kweli ' Akiki ni nywele,kila mtu anazake'. Kuna wanao mdharau rakim na kumuita mchawi,wengine wanakuwa wachungaji kuhubiri kisha wanatukana (utumishi wa siku hizi...!!??),wengine wanataka kujua zaidi na hata wengine kutaka kujaribu.
Mie naungana na wanaotaka kufahamu zaidi juu ya kioo,maana,sio mara ya kwanza kusikia habari za kioo kuwa sio vizuri kujitazama usiku au kujitazama kwa muda mrefu,mama yangu mzazi nakumbuka alikuwa ananizuia kujitazama kwenye kioo na alikuwa mkali akinikuta najitazama hasa usiku.
Sasa alichokieleza ndugu Rakims,bila shaka kina ukweli mkubwa na usiopingika...haijalishi uaamini au haukiamini. Nashauri jamaa endelea kutoa darsa ili tuyafahamu mambo ambayo wakati mwingine ni vigumu kuyajua katika hali ya kawaida ili mtu awe na tahadhari. Wehenga walijua mambo mengi sana.
La mwisho,ni ujinga wa kiwango cha juu sana kuamini kuwa wewe eti kwa vile unajua biblia kidogo,basi unadharau elimu zingine...!! Usiwe mjinga,wazungu hao walikutawala kupitia biblia hy,na waarabu wakaufanya mtumwa kwa Qur'an hy.....kuwa wa kujiongeza,tambua na ujue kichwani mwako,kuna elimu nyingi na za maana kimwili na kiroho ambazo ziko nje ya vitabu vya dini. ACHA UJINGA....!! Sikuzuii kuamini unachokiamini,ila nakuzuia kupinga na kudharau taaluma zilizo nje ya imani yako. Dunia ina mengi ya kujifunza,ukichagua ya kujifunza,usithubutu wala kujaribu kudharau wenzako pia walichochagu,maana kuna walipofanyaga ujinga huo,wakajuta baadaye.
Nimemmiss sana mcungaji Kibwetele.
Karibu mkuuNaona umekuja na somo zuri sana mkuu. Wengi wetu hatupendi kujishughulisha na mambo yasiyo na faida.
Nimejifunza jambo hapa, elimu za dunia zina mapana yake. Nami narudi maktaba kusaka maarifa zaidi kuhusiana na bandiko lako. Nitarudi.
Asalaam
huyu jamaa kama angelikuwa na uwezo wa kuona ulimwengu usioonekana basi pia angelikataa hiyo reality naamini kiongozi katika ulimwengu huo una watoto wengi sana.Mithali 26:5 Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
Proverbs 26:5 Answer a fool according to his folly, Lest he be wise in his own eyes.
Acha utoto Rakims kuna watu ndani ya chumba kizima kuna vioo vya kujiangalia pande zote za kuta..........ndio maana nikauliza wanafunikaje?
Halifu sio kila kinachokudhuru wewe lazima kinidhuru na mimi....kwenye ulimwengu wa kiroho kuna imani tofauti tofauti usitake kuniaminisha cha kwako
kazi ya kichwa ni zaidi ya kufuga nywele na kushikilia masikio.Tumia vizuri kichwa chako.
and what u dont know is endless ocean.Salaam, ndio mkuu yote hayo uliyoyasema ni kweli na ndio iliyopelekea mimi kuwafundisha wanajamii ili kuweza kukwepa lakini kwa kuwa wengi uelewa wao ni finyu point walioiona hapo ni kuwa huu ni uchawi hivyo mtu anaehisi hii ni uchawi moja kwa moja hana imani na Mwenyezi mungu kwa maana ukishaamini huu ni uchawi kwamba hadi utengeneze ndio upokee imani ya uwepo wa viumbe visivyoonekana na kama huamini kama hakuna viumbe visivyoonekana basi hata aliyekuumba pia humuamini, pia kwa sisi waislamu kuna sehemu Qur.an inasema vimeumbwa viumbe vingi na tofauti lao mwenyezi mungu angetaka vyote vingekaa pamoja?Asalaam
Nimerudi tena baada ya kushinda maktaba nikipekua nondo kuhusiana na bandiko hili.
Kwa miaka mingi binadamu amekuwa mtumiaji wa kioo kwa ajili ya kitazama taswira yake. Yapo mengi ya imani za wanadamu yanayo husishwa na kioo. Hasa uwezo wake wa kuweza kuwasiliana na roho za kuzimu. Haya ni baadhi tu ambayo yanatanabaisha;
Kioo kinaaminika kuwa na uwezo wa kuvuta nafsi ya mtu. Hivyo mara nyingi haishauriwi kuwepo kwa kioo kwenye chumba cha mgonjwa mahututi au maiti. Kama kioo kitakuwepo inashauriwa kifunikwe kwa kitambaa au kigeuziwe ukutani. Uwepo wa imani hii ni kuepuka kioo kuweza kuchukua nafsi ya mtu pindi roho inapoacha mwili.
Pia inaaminika kioo ni mlango au radar ya mapepo, mashetani au majini. Hivyo tunashauriwa kukiweka mbali visiweze kuchukua taswira ya vitanda vyetu pindi tunapolala usiku. Hii itaepusha viumbe hivyo hatari kuweza kutuona na kutudhuru usiku wa manane. Pia nafsi kutochukuliwa na vioo wakati tupo kwenye usingiza mzito ambao ni nusu ya kifo.
Aidha ili madhara haya yasimpate mtu inashauriwa kioo kisikae sehemu moja katika chumba. La sivyo kuna uwezekano mkubwa wa kugeuka kuwa lango kati ya ulimwengu wa kawaida na ulimwengu wa kiroho ambao una viumbe vingi ambavyo ni hatari.
Pia inashauriwa kutokuwa mtumiaji wa kioo unacho kikuta katika mazingira mageni kwako. Mfano hotelini, kwenye nyumba usiyoifahamu vizuri au kioo ulichokiokota sehemu usiyoijua.
Hizi ni baadhi tu ya imani ambazo binadamu wanazo kuhusiana na kioo. Lakini nijuavyo mimi imani ya jambo inaweza kijidhihirisha pale unapoingia deep na kuamini haswa. Maana zipo imani nyingi kuhusianna na wanyama kama paka, bundi n.k pia kuna imani za vitu kama kioo, midoli n.k Kikubwa ni kushikilia ulichonacho. Binafsi siamini katika haya.
Nawasilisha. Asalaam
Rakims Mshana Jr