Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Sasa akina mkandamizaji watajua kuwa 'kuna sheria' Tanzania.
Manji amewadanganya sasa wataula wa chuya.

Sasa wanaanza kukandamiza kihindi . Na Ndipo watakapojua kipi kitamu.Kihindi au kizenji. Poleni kina Masanja
 
hawa jamaa wa eatv inaonyesha kuwa walikuwa wanashibisha matumbo yao kwa kupitia ZE comedy kwa nn wamewang'ang'ania wasitumie vipaji vyao??
Nao hao COSOTA inabidi wamulikwe labda kuna mkono wa mtu.
Lakini tuangalie upende wa shilingi labda kitendo cha hawa jamaa kuomba ulezi kwa Manji utakuwa umewaletea matatizo....si mnajua fika eatv ni ya Mengi sasa Mengi na Manji paka na panya...wanakomoana wakubwa huku wadogo wakiumia sasa.

siungi mkono EATV asilani!!!!! they could have done better; lakini tuangalie pia sheria za hakimiliki [ambazo wasanii huzipigania bila kuzijua vizuri]; vilevile nahisi kwamba EATV wametumia ile chachu ya "branding" kuwamaliza wavuja jasho.

Wazo: ili kuwaweza EATV, ningeshauri Ze Comedy wacheze mchezo huo huo wa EATV; how? badili jina kuwa Ze Komidy [with same pronouciation maana najua huzuiwi kutamka kitu kwa namna fulani, branding iko kwenye writings]; Joti anaweza kuitwa Jyoti [or Gyoti] lakini matamshi yaleyale ya zamani; Masanja akawa Masancha, Seki akawa Syeki; and then they make fun of EATV for the rest of their lives

Ni wazo tu...
 
muhimu ni kuhusisha wataalam wa kisheria wakati wa kusaii mikataba,na kupitia sehemu zote za mkataba.wanachoweza kufanya sasa hivi ze comedy ni kwenda na mkondo wa sheria,huko peke yake ndo wanaweza kufuata ufumbuzi.sio kukimbilia kwa waziri au raisi.ianbidi tujifunze kuendesha mambo kitaalam...
 
Kabisa MTM, inawezekana kubadili kidogo tu majina na wakaendeleza libeneke, lakini kwasasa ni vyema wakatafuta mtaalamu wa mikataba awasaidie wasijikute wanaingia matatani tena wafahamu kwamba sasa Tz ni nchi ya kibepari na mabepari wanafaidi kwa jasho la watu kama hao kina joti, masanja ambao wanatalent lakini hawajabukua vya kutosha kujua haki zao.
 
Waanze upya na majina mapya na kila kitu kipya. Baada ya mwingine waanze upya tena, waendelee kuanza upya. Ndio watajifunza! Wakubali kubadilika, Huyo
Masanja ataendelea kuwa Masanja mpaka lini!! Si aitwe Masatu, Maganga, Ngosha kama anataka kuendelea kuwa msukuma! Au hata Sinclair, au Manji kabisa!
 
Sina undugu na Kajura wala Seikh Yahya, lakini haya niliyatabiri hapa...

varangati la ze comedy

KIKUNDI cha Sanaa za Maigizo ya Luninga nchini maarufu kama 'Ze Komedi' kimeulalamikia uongozi wa East Afrika Television (EATV) kwa kuwazuia kutumia majina na uhusika wa uigizaji waliokuwanao katika kituo kingine cha TV kwa madai kuwa ni hati miliki yao.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ze Komedy Production, Isaya Mwakisyala alisema uamuzi wa Cosota kukubaliana na ombi la EATV kuwa Ze Komedy ni mali yao katika barua walioiandika Juni 9 na kujibiwa na Cosota Juni 10 kuwa ni mali yao si sawa kwa kuwa wao ni kikundi kinachojitegemea.

"Hatukuanzishwa na EATV bali tulikuwa ni waigizaji kipindi kirefu kabla hata hatujaonekana huko, kinatushangaza na kustaajabisha kitendo cha EATV kudai kuwa Ze Komedy ni mali yao, sisi tuanchosema tutaendelea kuwa huru na kubakia vile vile katika uigizaji huo kama kawaida," alisema Mwakisyala.

Alisema mkataba wa uhalali wa kumiliki kikundi cha Ze Komedy waliupata Julai Mosi mwaka 2007 kwa cheti halali baada ya kusajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) tofauti na EATV ambao wanadai kupewa umiliki wa Ze Komedy Juni 30 mwaka huu.

Alisema endapo kutatokea kutoelewana kokote baada ya uamuzi wao wa kuingia mkataba na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1) ambao uhamasishaji wa matangazo ulianza jana, watakwenda kumuona Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo na ikishindikana watafika kwa Waziri Mkuu na hatimae kwa Rais.

Hata hivyo kurushwa kwa vipindi vya kundi hilo TBC1 kutaanza baada ya wiki mbili zijazo kutokana na safari ya kundi hilo nchini Uingereza baada ya kuahirisha ya kwanza nchini Afrika Kusini kutokana na ghasia zilizokuwapo nchini humo.

Source:www.issamichuzi.blogspot

I love this story
Naona COSOTA wameamua kuwa MAFISADI.... Lets see na mwaka huu unga robo
 
Sheria Ifwate Mkondo Wake
Waziri Hana Jipya La Kufanya Hapo
Vijana Rudini Kaeni Chini Na Eatv..msidanganyike Na Waziri Yoyote
Mtaishia Porini Na Kusahaulika....

Mwenye Masikio ya kusikia amesikia, na mwenye Macho ya kuona/kusoma amesoma hii.
Vijana Wazeni na kuwazua "Fisadi Manji" anawadanganya.
 
siungi mkono EATV asilani!!!!! they could have done better; lakini tuangalie pia sheria za hakimiliki [ambazo wasanii huzipigania bila kuzijua vizuri]; vilevile nahisi kwamba EATV wametumia ile chachu ya "branding" kuwamaliza wavuja jasho.

Wazo: ili kuwaweza EATV, ningeshauri Ze Comedy wacheze mchezo huo huo wa EATV; how? badili jina kuwa Ze Komidy [with same pronouciation maana najua huzuiwi kutamka kitu kwa namna fulani, branding iko kwenye writings]; Joti anaweza kuitwa Jyoti [or Gyoti] lakini matamshi yaleyale ya zamani; Masanja akawa Masancha, Seki akawa Syeki; and then they make fun of EATV for the rest of their lives

Ni wazo tu...
watanzania tumekuwa na kawaida ya kutothamini utaalamu au ushauri wa kitaalam in this case wanasheria.... utasikia wasanii wakilia hakimiliki hakimiliki...ukiwauliza maana yake nini..sidhani hata kama they have a clue... pamoja na ubutu huo..nadhani kama alivyosema mkuu hapo juu we need to help them ila in so helping we shouldnt mislead them kuwafanye waone it is that simple..katika kubadilisha majina inashawishi ku maintain majina yanayofanana..lakini mtu akitaka kuwabana kisheria bado wanaweza kuwa cornered....perhaps the only way out is to change the brand all together..wawe hata na new identity ...kwani kinachojalisha ni hayo majina ya joti,masanja au wakuvanga?.. i dont think so..nadhani wahusika wanapendwa tu..wasihofu kujibadili big tme... go on comrades!!
 
Ninalo somo zuri kwa hawa wasanii wa ze-comedy
kwanza kabla ya yote nitaanzia safari yangu COSOTA kisha tutajua kwa nini ndizi zilizooza zikaiva tena??

Ze comedy wana haki zoooooote za kumiliki majina yao na kila kitu but only productions za mikataba zitakuwa ktk custody ya mwenye kumiliki mkataba.... kuna vijiswali hapo naamini vitajitokeza ila kama mnataka somo la hakimiliki naweza kudodosa hapa.... ila hawa wasanii wanahitaji msaada wa wadau....
 
Mheshimiwa Mengi na menejimenti yake pale EATV wanatia aibu sasa maana kwa nini waendelee kuwa fuatafuata hawa vijana wajasiriamali,kama walimaliza mkataba basi wawaache waende zao,COSOTA nao wanatia aibu hivi ni nani asie jua kwamba wale vijana mfano Joti na Mpoki kwamba haya ni majina yao kisanii tangu enzi hizo???
Hiyo yote ni roho mbaya tu waachieni hao vijana waendelee popote pale kani ule ni ubunifu wao
 
Maskini wakandamizaji!inasikitisha sana Watanzania kufanyiana hivi!badala ya kuinuana tunapelekana chini!
 
hivi mnafikiri Seinfield anaweza kwenda NBC na kuanzisha comedy yake aipe jina hilo la "Seinfield" na character wa Kramer, George na yule binti bila kusababisha mgongano wa hati miliki na watu wa CBS? Ze Comedy kabla ya kuamua kuachana na EATV walitakiwa kuconsult wanasheria wa haki miliki siyo kukurupuka tu.

Sasa kama Manji anataka kweli kuwasaidia Ze Comedy itabidi alipe sum kubwa ya fedha kwa EATV (Mengi) ili kununua haki za kumiliki na shows ya Ze Comedy. Ina maana Manji amlipe Mengi... patakuwa patamu hapo!
 
unajua til today sijui wats the secret kubwa behind the bifu la hawa mafahali wawili MAnji na Mengi......as kama tuonavyo sasa nyasi ndio zaumia wakigombana majamaa hawa wawili....
 
Mtanzania anaewawekea vingingi the comedy

Kwani ze comedy wamewekewa vigingi na mtu ama wamejiwekea vigingi wenyewe?

Kukumbatia mafisadi ndo kinachowaua kwa sasa. Kulikuwa na safari ya kupelekwa SA na sasa imekuwa UK baada ya mipango ya kwenda kwa Butherez kupanguka. Sina uhakika kama hizo ni safari za kikazi ama za ki-biashara, na ikiwezekana biashara haramu (wajinga ndio waliwao).
 
Hapa Naona Manji amepigwa chenga mbaya!!!!! Kumlipa Mengi itakuwa ngumu!

Mimi nasisitiza watu tuache, kuchanganya mambo. Hawa vijana wameshauriwa vibaya, wameondoka bila utaratibu halafu wanataka waonewe huruma! Hii si tabia nzuri kuanza kumtukana mtu (EATV) aliyekuinua. mwakani si ajabu wakaanza kuitukana TBC (Tido) na Manji! Mimi nadhani wakubali sheria ifuatwe, kama ni kuanza upya waanze tu. Mimi naamini wameshajenga majina yao na haya ya uigizaji yatasumbua muda mfupi tu.

La sivyo Manji awalipie! Itakuwa ngumu! Naona atakuwa tayari kuwapeleka hata mwezini lakini sio kuwalipia kwa Mengi!!!!

Vijana wa Ze Comedy acha kuchukua ushauri wa jazba kutoka kwa wapenzi wenu na maadui wa Mengi! Mmekosea jisahihisheni!!!!
 

...ndio yale yale, mke anakukataa unamnyang'anya kanga, mpaka chupi ulizomnunulia, kisa weye ndio uliyemnunulia, hivyo aondoke mwenyewe kama alivyokuja!

mimi nawashauri ikiwezekana kina Seki na wenzake wawaachie EATV hilo jina na hizo characters, tuone kama EATV wataendeshaje ZE Comedy na actors wapya,

...au ndio itabakia 'kujifariji na harufu ya nguo', eti umemkomoa mtu!

Hizo sheria na hakimiliki zinakuwa 'valid' sababu Ze Comedy wameachana na EATV tu? kuna mangapi na wangapi Tanzania hii wanadhulumiwa hakimiliki zao hapa Tanzania kunakochangiwa na vituo 'kama' hivi vya radio na Tv,

...au ndio mnyonge hana haki, na kwakuwa EATV imeshika mpini, vijana wamekamata makali?

Acheni roho mbaya jamani,
 

...ndio yale yale, mke anakukataa unamnyang'anya kanga, mpaka chupi ulizomnunulia, kisa weye ndio uliyemnunulia, hivyo aondoke mwenyewe kama alivyokuja!

mimi nawashauri ikiwezekana kina Seki na wenzake wawaachie EATV hilo jina na hizo characters, tuone kama EATV wataendeshaje ZE Comedy na actors wapya,

...au ndio itabakia 'kujifariji na harufu ya nguo', eti umemkomoa mtu!

Hizo sheria na hakimiliki zinakuwa 'valid' sababu Ze Comedy wameachana na EATV tu? kuna mangapi na wangapi Tanzania hii wanadhulumiwa hakimiliki zao hapa Tanzania kunakochangiwa na vituo 'kama' hivi vya radio na Tv,

...au ndio mnyonge hana haki, na kwakuwa EATV imeshika mpini, vijana wamekamata makali?

Acheni roho mbaya jamani,

Wewe ni Mdogo wake Manji nini ? ? ? au Nawe "anakufadhili"?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom