Ze Comedy wana haki kuhamia TBC-Serikali

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
52,883
25,249
Ze Comedy wana haki kuhamia TBC-Serikali


*Kesi yao dhidi ya EATV kusikilizwa Jumatano
*Mengi asema hana chuki nao na anawapenda

Kulwa Mzee, Dodoma na Grace Michael, Dar

SAKATA la kikundi maarufu cha uchekeshaji cha 'Ze Comedy' na Kampuni ya East Africa Televisheni (EATV), limeibukia bungeni ambapo Serikali imesisitiza kuwa kina haki ya kwenda Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwani mkataba wao wa awali ulishamalizika.

Sakata hili liliibuka jana, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Bi Suzan Lyimo (CHADEMA), kuitaka Serikali kutoa tamko juu ya kundi hilo, ambalo ni kipenzi cha wananchi.

Mbunge huyo alitaka kujua hayo alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, aliitaka pia Serikali kueleza sababu za kikundi hicho kuzuiwa maonesho yake.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. Joel Bendera, alisema Serikali inalifahamu tatizo lililopo kati ya 'Ze Comedy' na EATV.

Hata hivyo, alisema Serikali imekiagiza Chama cha Hatimiliki (COSOTA), kukaa na wahusika wote kulimaliza tatizo hilo.

“'Ze Comedy' wana hatimiliki na EATV nao wana hatishiriki, 'Ze Comedy' wamemaliza mkataba wao na EATV, wana haki ya kwenda TBC ... hivi karibuni tatizo hili litakwisha,” alisema Bw. Bendera.

Awali, Bw. Bendera alikiri kuwapo tatizo la COSOTA kutekeleza majukumu yake, ikiwamo kushughulikia matatizo yanayowakabili wasanii na kusisitiza kwamba Serikali itajitahidi kukiimarisha chombo hicho, kwa lengo la kuwasaidia wasanii hasa katika kupigania haki zao.

Bw. Bendera alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maaluumu, Bibi Martha Mlata (CCM), aliyeuliza iwapo Serikali ina mpango wa kuisaidia COSOTA kifedha, ili iweze kusimamia vyema kazi za wasanii, baada ya kuonesha chombo hicho kushindwa kufanya kazi zake kutokana na kutokuwa na fedha.

Wakati huo huo, kesi iliyofunguliwa na 'Ze Comedy' dhidi ya EATV, Msajili wa Nembo za Biashara na COSOTA, inatarajiwa kusikilizwa Jumatano mchana Katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.

Hatua hiyo ilifikiwa jana baada ya walalamikiwa katika kesi hiyo, kuwasilisha ombi la kuongezwa muda wa kujibu hati ya madai iliyowasilishwa na kikundi cha wasanii hao kupitia wakili wao, Bw. Peter Swai.

Kwa ombi la walalamikiwa la kuongezwa muda ambalo liliwasilishwa kupitia wakili wao, Bibi Blandina Gogadi, upande wa wadai nao uliiomba mahakama kutoa kibali cha kuendelea na biashara yao, huku upande wa walalamikiwa ukiendelea kujibu maombi hayo.

Baada ya Jaji Catherine Urio kukutana na pande zote mbili, walikubaliana kusikilizwa kesi hiyo Jumatano mchana katika mahakama ya wazi, ili kila mtu aweze kuisikiliza.

Wasanii hao walifika mahakamani hapo ili kujua hatma ya kesi yao, ambapo mmiliki wa EATV, Bw. Reginald Mengi naye alihudhuria.

Akiwa mahakamani hapo, Bw. Mengi alikutana faragha na vijana hao huku akisema hana chuki nao na anawapenda.

Wasanii hao waliwasilisha maombi wakiiomba mahakama kuwazuia walalamikiwa kuingilia biashara zao na kuruhusu kutumia jina lao.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyoko mahakamani hapo inaiomba mahakama hiyo kutoa tamko kuwa walalamikaji hao ni wamiliki wa jina la 'Ze Comedy' kabla na baada ya kuingia makubaliano na walalamikiwa.

Mbali na maombi hayo, pia wasanii hao wanaiomba mahakama hiyo kuamuru walalamikiwa hao kulipa fidia ya sh. milioni 200 kama adhabu kwa usumbufu waliowasababishia.

Walalamikaji hao wanaiomba mahakama kuwaruhusu kuendelea na biashara yao huku kesi ya msingi ikiendelea, ambayo ni kuthibitisha madai ya walalamikiwa, wanaodai kuwa wao ndio waliounda kikundi hicho na wamiliki halali wa nembo ya 'Ze Comedy'.

Maombi hayo yataanza kusikilizwa mahakamani hapo Jumanne saa 4 asubuhi mbele ya Jaji Catherine Urio.

Hati ya walalamikaji iliyopo mahakamani hapo inadai kuwa wao ni kikundi cha sanaa ambacho kimesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa na kinatimiza taratibu zinazotakiwa katika kazi za sanaa.

Inadaiwa kuwa wasanii hao baada ya kuondoka EATV, kampuni hiyo iliwazuia kutumia jina la kikundi hicho na majina yao ikidai kuwa ndiye mmiliki halali wa nembo hiyo.

Walalamikaji katika kesi hiyo ni Isaya Mwakilasa (Wakuvanga), Mujuni Sylivester (Mpoki), Lucas Muhuvile (Joti), Emmanuel Mgaya (Masanja), Alex Chalamila (McRegan), Joseph Shamba (Vengu) na Sekioni David (Seki).
 
Serikali Acheni Kuwa Watumwa Wa Mawazo Imefika Wakati Mnasema Kusaidia Kuhalalisha Hati Miliki Matokeo Yake Ushabiki Wa Wake Zenu Unawafanya Kutaka Kuvunja Haki Za Mtu....nawapebnda Sana Ndugu Zanguni Lakini Kwa Style Hiyo Na Nilishawaomba Kaeni Chini Muelewane Else Hata Muende Kwa Raisi Haki Itaoneka /hamuitaji Kutumia Nguvu Nendeni Cosata ,,hay Majina Yamemilikishwa Kwa Eatv,,labda Tatizo La Ufahamu Na Ushabiki Linawasumbua...kuna Tofauti Kati Ya Hati Miliki Na Mkataba Nduguzanguni!!!!!!
Karibuni Sana!@##$
 
Na hao COSOTA jamani nisaidieni hapa. Mbona wanatuma invoice kwenye mabaa, hotel, clubs , groceries n.k yaani sehemu za starehe wakidai ni mirahaba ya kuangalia TV na kusikiliza muziki.

Criteria gani wanatumia kucharge hiyo mirahaba? Maana unaletwa tu invoice ya 350,000.00 amabayo haina kichwa wala miguu. Tuelimisheni hapa tafadhali
 
Na hao COSOTA jamani nisaidieni hapa. Mbona wanatuma invoice kwenye mabaa, hotel, clubs , groceries n.k yaani sehemu za starehe wakidai ni mirahaba ya kuangalia TV na kusikiliza muziki.

Criteria gani wanatumia kucharge hiyo mirahaba? Maana unaletwa tu invoice ya 350,000.00 amabayo haina kichwa wala miguu. Tuelimisheni hapa tafadhali

Dah hii kali! ila niliwahi kusikia kuwa cosota huwa wanafwata kwenye mabaa kudai fedha za matumizi ya juke box ili wakalipe wasanii ambao nyimbo zao zimeingizwa kule...sasa sijui km kweli wasanii wabongo wanapata huo mshiko wanaochukua cosota!!
Nchi yetu imejaa usanii mtupu..
 
Serikali Acheni Kuwa Watumwa Wa Mawazo Imefika Wakati Mnasema Kusaidia Kuhalalisha Hati Miliki Matokeo Yake ...........Ushabiki Wa Wake Zenu:

Na kwa nini si ushabiki wa waume zao........... angalia lugha hii inayotumika. Kwani kila mtu anaweza kuwa shabiki wa kitu fulani.

This is only comedy!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom