Augustoons
JF-Expert Member
- Oct 31, 2007
- 409
- 31
Ze Comedy yapigwa ‘Stop' TBC
na Sarah Kassim
Katika hali ya kusikitisha haya ndiyo yanayowapata vijana wetu kipenzi wa zecomedy sasa. Hii yote inatokana na uhasama wa tembo wawili wao ni nyasi tu hapa. Je tutaacha kundi hili life je, jf tunawasaidiaje? Maana kinachowapata wao ndio kilichoipata iliyokuwa jambo forums hadi tulipopiga chenga kwenye domain rights na copy right hadi kuwa jamii forums. Hawa nao wakisaidiwa huenda wakpiga bao kama sisi. Na huko TBC naona kama ndio wamekweisha sasa. Mnasemaje wana jamvi?
na Sarah Kassim
SERIKALI jana ilitoa tamko kuwa kundi la sanaa ya maigizo la Ze Comedy, lililoasisiwa na Televisheni ya East Africa (EATV), halipaswi kutumia jina hilo katika televisheni nyingine kwa sababu, ni alama ya huduma (trade mark), mali ya EATV.
Akizungumza katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki, Yustus Mkinga alisema, Ze Comedy ni mali ya EATV iliyo na hakimiliki (Copy right) ya kazi za Ze Comedy.
"Ze Comedy ilianzishwa na EATV na kwamba, kabla ya hapo, hapakuwa na kipindi wala kikundi kilichoitwa Ze Comedy.
"Ze Comedy kama alama ya huduma (service mark) ni mali ya EATV ambayo pia ina hakimiliki (copy right) ya kazi za Ze Comedy," alisema ofisa huyo mkuu wa Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA).
Mkinga alisema, EATV ndicho kituo pekee chenye haki za kipekee, za kiuchumi za kazi zote za Ze Comedy kwani ndiyo waanzilishi wake, ikijumuishwa kuwaunganisha wasanii husika kuanzia hatua ya awali hadi mwisho, kurushwa kwa kipindi kwani wasanii walikuwa wakilipwa haki zao zote kila baada ya kipindi.
Alisema, kitendo cha kituo kingine kurusha kama inavyotaka kufanya Kituo cha Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), si tu ni ukiukwaji wa haki za EATV na kinyume cha sheria ya Hakimiliki, pia ni ushindani usio halali (unfair competition), kinyume cha sheria ya ushindani Na. 8 ya mwaka 2003.
Mkinga alisema kwa mujibu wa barua za EATV kwa COSOTA, TBC ndiyo inayotarajia kurusha kipindi cha Ze Comedy, hivyo EATV ikaomba ufafanuzi wa kisheria kwao (COSOTA) kuhusu suala hilo huku nakala zikitumwa kwa mkuu wa kikundi cha wasanii hao, Isaya Mwakilasa ‘Wakuvanga'.
Alisema, COSOTA iliitaka EATV kueleza namna Ze Comedy ilivyoanzishwa na kuelezwa kuwa awali wasanii 15 walishindanishwa ili kupata sita kati yao na kuhusu uhusiano wa kikazi kati ya EATV na wasanii, watayarishaji, waongozaji na wapiga picha na EATV ikasema, ukitoa wasanii, wengine walikuwa na mkataba wa kikazi.
Kuhusu onyo la hakimiliki, EATV ilijitetea kuwa kila baada ya kipindi, kulikuwa na maneno yaliyosomeka EATV(c) kwa maana kwamba, kazi na ubunifu wote unaofanywa katika kipindi hicho, ni mali ya EATV na si vinginevyo.
Alisema, kwa kuwa Ze Comedy ni kipindi kinachomilikiwa, baada ya kuanzishwa na EATV kwa kushirikisha na wasanii, kipindi hicho kinalindwa chini ya Ibara ya 7 (1) (a) na 13 (a) ya mkataba wa Roma wa Ulinzi wa Wasanii, Wazalishaji wa Mkanda na Mashirika ya Utangazaji mwaka 1961 na kifungu cha 34 (1) ( a) cha sheria na. 7 ya Hakimiliki ya 1999.
Mkinga alisema, kwa vile kipindi cha Ze Comedy kinajumuisha maigizo ambayo yanabadilika kutokana na ujumbe uliokusudiwa, hata majina yanayotumika katika uigizaji, yaani Joti, Masanja Mkandamizaji na mengineyo, vyote ni mali ya EATV vinavyoweza kuendelea kutumiwa.
Katika hali ya kusikitisha haya ndiyo yanayowapata vijana wetu kipenzi wa zecomedy sasa. Hii yote inatokana na uhasama wa tembo wawili wao ni nyasi tu hapa. Je tutaacha kundi hili life je, jf tunawasaidiaje? Maana kinachowapata wao ndio kilichoipata iliyokuwa jambo forums hadi tulipopiga chenga kwenye domain rights na copy right hadi kuwa jamii forums. Hawa nao wakisaidiwa huenda wakpiga bao kama sisi. Na huko TBC naona kama ndio wamekweisha sasa. Mnasemaje wana jamvi?