Mtu akisema wewe ni mgonjwa unaweza kusema sio kweli eti kwa sababu anayekusema kuna wakati alishaugua?
Slaa alishakuwa mtunza fedha wa vilema? Hao Ze Comedy, na bootlickers wengine wa viongozi wezi ndani ya CCM, hawajui ukweli kwamba mtu huwezi kufukuzwa upadri? Mtu unaweza kusimamishwa upadri, lakini upadri haufukuziki. Ni wa milele, na hata ni zaidi ya milele kwani ukishakuwa padri basi unabaki ni padri hata kuzimu. Acheni uongo!
Sisi tunawafahamu wezi wetu. Hata wakitapatapa namna gani ukweli unabaki pale pale. Wanaoshirikiana na wezi wa nje kupora mali asili yetu, walioiba shilingi nusu trilioni kupitia BoT, na wanaoendelea kuwaibia Watanzania hadi leo, ni viongozi wa ngazi za juu wa CCM na washirika wao ndani na nje ya nchi.
Mnajisumbua bure mnapojaribu kumgeuzia kibao Slaa. Sisi tuko naye bega kwa bega kupambana nanyi.