Zawadi ya maneno matamu. Maalumu kwa ajili ya mwanamke bora wa Kiafrika

Dec 2, 2023
1
3
Zawadi ya maneno matamu. Maalumu kwa ajili ya mwanamke bora asilia wa Kiafrika

"Mama Africa", ujumbe maalumu kwenda kwa mwanamke asilia wa kiafrika, mwenye tabasamu angavu, uso wenye nuru, sauti ya upole pamoja na rangi asilia, anayeteka utayari na hisia za wanaume, mwenye mapenzi ya dhati pasi na kutanguliza pesa mbele, asiyejisikia wala kujikweza

Mama Africa
By: African Melki



1.
Mama Afrika,
Nakupenda sana,
Njoo moyoni,
Ukae kifuani,
Nikutamke mdomoni,
Ulimwengu wote ujue,
Amani yangu ilipo

Oh Baby,
Kwako taabani,
Niseme nini uniamini?
Sibishani na moyo,
Amani yangu ilipo

Bridge:
Ukitabasamu moyo wajawa na furaha,
Ununapo uzuri huo mwenzio mpaka nashangaa,
Sauti ya upole mahaba moto wa jiji la Dar,
Haki ya nani unafaa,
Nyota yako inang'aa

Ukini-whitelist mimi nakufa na wewe,
Hilo figure wacha n'chezee mwenyewe,
Ubavu wangu nahisi alikuumbia wewe,
Haki ya nani unafaa,
Nyota yako inang'aa,

Chorus:
Naomba n'kuulize,
Nikikufumania n'fanyeje?
Siwazi one day uniumize,
Kesho nlipize,
Sasa itakuwaje!

Nami naomba unijuze,
Ukinitazama unanionaje?
Mi nakuona wangu zeze,
Michezo ukaicheze,
Bila wewe ntaishije?

2.
Mama Africa,
Look at Your Body Colour,
Very Wonderful,
Very Beautiful,
Nimpende nani?
Wa kuendana nami,
Anayeijua kiu yangu,
Hakuna kama wewe

Kila ninapokuona, nakuona mpya kabisa,
Your Shape is Cocacola Premium akili ushaitesa,
Sinaga wivu, wivu kwako nsije kukukosa,
Ila yote tisa, tabasamu na visa,

Huo mwondoko wa digitali,
Na mdondoko nyuma hatari,
Hicho kikanga alfajiri,
Kuhatarisha maliasili,
Kiuno cha kushitushwa na,
Kilio cha burudani,
Na wivu kwa majirani,
Mie kwako taabani.​
 
Back
Top Bottom