"Mama Africa" ni mwanamke wa namna gani? African Melki amuelezea kwa namna ya pekee

E Motherland

Member
Oct 1, 2023
20
10
Unafikiri ipi ni maana sahihi? Msanii wa kiafrika anayechipukia kwa kasi, African Melki amehojiwa na moja ya kituo cha runinga cha mtandaoni (Online media) na kutoa maana ambayo aliifikiria huenda kwa mawazo yake ni sahihi. "Mama Africa ni mwanamke kutokea Africa mwenye mwonekano asilia wa ngozi, nywele, kucha na uso wake, mwanamke mwenye mvuto kimwonekano, tabasamu na namna azungumzavyo. Anayeteka hisia za wapenzi, mwenye kujituma na kujali familia na watu wake wa karibu", alizungumza African Melki

"Mama Africa is a woman from Africa with the natural appearance of her skin, hair, nails and face, a woman with an attractive appearance, smile and the way she speaks who captures the feelings of lovers, who is dedicated and cares about his family and close people".

Ulazima wa kuulizwa swali hili ulijitokeza kwa kuwa jina la wimbo, Mama Africa lilizungumziwa kwa namna tofauti na jinsi ambavyo neno hili linavyosikika masikioni mwa watu walio wengi huku wengine wakijaribu kupinga hoja kwa kusema kuwa wimbo wa Mama Africa haujasadifu title ya wimbo huo. "Tulitegemea kusikia juhudi za mama zikielezwa katika muziki huo. Namna ambavyo mama hulea wanae kwa shida, kuhakikisha wanapata mahitaji n.k".

Ipi ni dhana sahihi ya neno "Mama Africa" ?
 
Back
Top Bottom