Jinsi ya kumpa mwanamke zawadi siku ya Valentine kwa kujua hatua mliyopo

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Zawadi yako lazima iwe na uzito na itoke kwa moyo mmoja. Wanaume wengi hutoa zawadi kwa wanawake ili kuomba msamaha au ili apendwe au ili amshawishi mwanamke awe naye kimapenzi, hii hupunguza nguvu ya zawadi. Mwanamke atapokea zawadi yako na kukushukuru. Ili zawadi yako iwe na uzito kwanza inabidi ujue nafasi yako kwa mwanamke na mpo hatua gani katika mahusiano yenu.

Hatua ya kutongoza. Kama bado hamjaanza mahusiano rasmi lakini umeona anaelekea vizuri unaweza ukampigia simu na kuongea naye kumtakia heri ya siku ya valentine. Kisha panga siku mtoke, hauna haja ya kuwaza sana kuhusu zawadi hatua hizi za mwanzo mana utaonekana una haraka au unajipendekeza.

Hatua ya mahusiano machanga. Hapa umpigie simu (kama hampo pamoja) kumtakia heri ya valentine na upange siku mtoke pamoja. Siku mnayokutana mnunulie zawadi ndogo tu ya kumfanya afurahi, nzuri apa ni kadi zenye maneno mazuri ya kufurahisha. Mchombeze kwa maneno mazuri ajisikie wa thamani kwako.

Hatua ya mahusiano yaliyokomaa. Hapa namaanisha upo kwenye mahusiano na mwanamke anakupenda vizuri (sio kimaigizo). Siku ya valentine mtoe out, mfanyie surprise ya zawadi nzuri pia na kadi yenye maneno mazuri itapendeza. Kama mpo mbali, mtumie zawadi au maua au kadi pia hakikisha unampigia (hasa video call). Kwake haya yote maana yake ni kwamba unamkubali kimapenzi na ana umuhimu kwenye maisha yako na wewe una umuhimu kwenye maisha yake (si ni kweli?).

Kama mwanamke amekuacha au amekuchunia. Au mwanamke ambaye haeleweki yani humuelewi elewi. Hatua hii usifanye chochote, hata kama ulikua unampenda kiasi gani lakini kitendo chake kimeshakuambia kuwa we huna umuhimu kwenye maisha yake kwa sasa, ya nini sasa uendelee kujipendekeza? Mwache aende zake.

Ila akikutafuta ongea naye vizuri, mwache yeye ndo akutakie heri ya valentine basi, usianze kuongea ya moyoni kwamba unateseka bila yeye. Pia kama ndo mmejuana, umemkubali lakini hamjuani hata kidogo si vyema kuanza kufikiria zawadi au kumfanya ajisikie wa muhimu sana kwako kabla hata hajajithibitisha kuwa wa muhimu kwako.

Kumbuka unapomtafuta mwanamke siku ya valentine unamaanisha una muwaza na ana umuhimu kwenye maisha yako, hivyo ni muhimu ujue hatua uliyopo na maneno ya kumuambia mwanamke ili kudumisha na kuboresha mahusiano.
 
Nimecheka sana mkuu mpaka watu wamenishangaa hapa.

Siku hizi kinachopendwa ni pesa. Leo ni Valentine Day lakini mimi nimetoka kuambiwa hivi na mchumba wangu. Hapa tupo hatua gani katika mahusiano yetu?

Wanaume tutafuteni pesa

Screenshot_20230214-111322_WhatsApp.jpg
 
Nimecheka sana mkuu mpaka watu wamenishangaa hapa.

Siku hizi kinachopendwa ni pesa. Leo ni Valentine Day lakini mimi nimetoka kuambiwa hivi na mchumba wangu. Hapa tupo hatua gani katika mahusiano yetu?

Wanaume tutafuteni pesa

View attachment 2517038
Apo hatua ya mwisho hiyo, maana yake huna umuhimu kwake japo sijajua imekuaje mpaka amekuambia hivyo
 
Sikukuu Ya Makafr Ina Nguvu Mno Mpaka Ule Upande Wa Pili Wanahangaika Nayo
 
Zawadi yako lazima iwe na uzito na itoke kwa moyo mmoja. Wanaume wengi hutoa zawadi kwa wanawake ili kuomba msamaha au ili apendwe au ili amshawishi mwanamke awe naye kimapenzi, hii hupunguza nguvu ya zawadi. Mwanamke atapokea zawadi yako na kukushukuru. Ili zawadi yako iwe na uzito kwanza inabidi ujue nafasi yako kwa mwanamke na mpo hatua gani katika mahusiano yenu.

Hatua ya kutongoza. Kama bado hamjaanza mahusiano rasmi lakini umeona anaelekea vizuri unaweza ukampigia simu na kuongea naye kumtakia heri ya siku ya valentine. Kisha panga siku mtoke, hauna haja ya kuwaza sana kuhusu zawadi hatua hizi za mwanzo mana utaonekana una haraka au unajipendekeza.

Hatua ya mahusiano machanga. Hapa umpigie simu (kama hampo pamoja) kumtakia heri ya valentine na upange siku mtoke pamoja. Siku mnayokutana mnunulie zawadi ndogo tu ya kumfanya afurahi, nzuri apa ni kadi zenye maneno mazuri ya kufurahisha. Mchombeze kwa maneno mazuri ajisikie wa thamani kwako.

Hatua ya mahusiano yaliyokomaa. Hapa namaanisha upo kwenye mahusiano na mwanamke anakupenda vizuri (sio kimaigizo). Siku ya valentine mtoe out, mfanyie surprise ya zawadi nzuri pia na kadi yenye maneno mazuri itapendeza. Kama mpo mbali, mtumie zawadi au maua au kadi pia hakikisha unampigia (hasa video call). Kwake haya yote maana yake ni kwamba unamkubali kimapenzi na ana umuhimu kwenye maisha yako na wewe una umuhimu kwenye maisha yake (si ni kweli?).

Kama mwanamke amekuacha au amekuchunia. Au mwanamke ambaye haeleweki yani humuelewi elewi. Hatua hii usifanye chochote, hata kama ulikua unampenda kiasi gani lakini kitendo chake kimeshakuambia kuwa we huna umuhimu kwenye maisha yake kwa sasa, ya nini sasa uendelee kujipendekeza? Mwache aende zake.

Ila akikutafuta ongea naye vizuri, mwache yeye ndo akutakie heri ya valentine basi, usianze kuongea ya moyoni kwamba unateseka bila yeye. Pia kama ndo mmejuana, umemkubali lakini hamjuani hata kidogo si vyema kuanza kufikiria zawadi au kumfanya ajisikie wa muhimu sana kwako kabla hata hajajithibitisha kuwa wa muhimu kwako.

Kumbuka unapomtafuta mwanamke siku ya valentine unamaanisha una muwaza na ana umuhimu kwenye maisha yako, hivyo ni muhimu ujue hatua uliyopo na maneno ya kumuambia mwanamke ili kudumisha na kuboresha mahusiano.
Sisi mashahidi wa jehova Mambo yenu hayo hayatuhusu

Tesekeni na mapenzi huko
Upendwe ili iweje kua na shekeli tu mengine yatajileta
 
Ni feminist sana. Ndo shida yake kubwa!
Kwangu mimi ni red flag. Mana ntajikuta natumia nguvu nyingi kumfanya mwanamke awe mtii kwangu kama kiongozi badala ya kutumia muda huo ku have fun...
Heri kuwa na mwanamke mtiifu, maisha yanakua rahisi pia.
Ila sijui kuhusu wewe...
 
Dogo acha ujinga wa kuendekeza wanawake. Mbona wewe umejisahau ivo inamaana wewe huitaji hizo zawadi siku ya valentine's....? Bro you are special too.
 
Back
Top Bottom