Muuza Kangala
JF-Expert Member
- Jul 21, 2021
- 1,126
- 4,169
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza Siku ya Mwaka Mpya wa Kiislamu kuwa Sikukuu ya Kitaifa Zanzibar.
Dkt. Mwinyi ametangaza siku ya Jumatano ya Julai 19, 2023 sawa na Mwezi Mosi Muharram kuwa siku ya mapumziko Kitaifa Zanzibar ili kuadhimisha siku ya mwaka mpya wa Kiislamu.
---
Raisi wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amesema serikali itatoa tamko kuifanya siku ya mwaka wa kiislamu kuwa ya mapumziko, Dk Hussein Mwinyi alisema hayo Julai 31, 2022 katika kongamano lililofanyika msikiti wa Jamiu Zanzubar, Mazizini, mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Mwinyi alisema maadhimisho hayo yatafanyika kwa mzunguko kati ya Unguja na Pemba ili kutoa nafasi kwa waislamu kushiriki. Alisema utaratibu wa kuadhimisha mwaka mpya wa kiislamu utawasaidia waislamu kuujua mwaka wao kidini.
Waislamu wanatumia Kalenda ya Hijiri ambayo miezi yake huanza na kuisha kulingana na mbalamwezi. Kutoweka kwa mwezi kunaashiria mwisho wa mwezi. Kalenda hii iliundwa rasmi mwaka 622AD wakati wa utawala wa Khalifa Umar ibn al-Khattab. Kalenda hii inatumika kuashiria matukio na tarehe muhimu za kiislamu kama vile Ramadhani, Eid al-Fitr, Eid al-Adha na mwanzo wa msimu wa Hija.
Mwaka wa Hijiri una miezi kumi na miwili; Muharram, Safar, Rabi’Al-Awal, Rabee’Al-Akhir, Jumada Al Ula, Jumada Al-Akhirah, Rajab, Shaabani, Ramadhani, Shawwal, Dhu Al Qa’da na Dhu Al Hijja.
Waislamu husherekea mwaka mpya wa Hijiri (unao chukuliwa kuwa likizo rasmi katika baadhi ya nchi za kiislamu) katika mwezi wa kwanza wa kalenda ya kiislamu ya Muharram kila mwaka.