Zanzibar hongereni kwa kuipa heshima Siku ya Mwaka Mpya wa Kiislamu

ikhlas

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,038
1,278
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ametangaza Siku ya Mwaka Mpya wa Kiislamu kuwa ni Sikukuu ya Kitaifa Zanzibar “Mwaka Mpya wa Kiislamu ni siku muhimu katika kalenda ya Kiislamu duniani kote”.

“Siku hii huadhimishwa kila mwaka kwa kumbukumbu ya Hijra, ambayo ni safari ya Mtume Muhammad (S.A.W) kutoka Makkah kwenda Madina mnamo mwaka 622 AD, Hijra ilikuwa hatua muhimu katika historia ya Uislamu kwa kuanzishwa utawala wa Kiislamu Madina”.

“Mabadiliko hayo ya kihistoria yaliunganisha Waislamu katika kutekeleza imani na kujenga jamii yenye misingi ya kidini, kwa mamlaka aliyopewa Kikatiba chini ya kifungu 6 (1) (a) cha Sheria ya Masuala ya Rais wa Zanzibar, Namba: 3 ya 2020, Rais wa Zanzibar Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi ametangaza rasmi kuwa siku ya Jumatano tarehe 19 Julai 2023 sawa na Mwezi Mosi Muharram itakua ni siku ya mapumziko Kitaifa Zanzibar kuadhimisha siku ya mwaka mpya wa Kiislamu”.

“Tamko hili limetolewa tangu tarehe 14 Julai 2023, kwa kuchapishwa rasmi kwenye gazeti la Serikali”

#MillardAyoUPDATES
 
Back
Top Bottom