Katika ulimwengu wa sasa hivi dunia imekuwa ni kijiji kimoja kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Katika eneo ambalo ninaishi MBEZI-KImara nimezungukwa na wakristo dhehebu la RC na wasabato,na Lutherans kwa mbali.Nyumba nayoishi inatizamana na muumini "kindakindaki"wa kanisa katoliki. Tokea mwaka 2008 nilivyomaliza A-level hadi leo 2018 ni karibu miaka 10 nashirikiana na ile jamii kiasi kwamba hata habari ya dini ni kama haipo sababu tumetengeneza bond moja kubwa.Wakati wa misiba,sherehe sikukuu za pasaka wananialika tunajumuika na kufurahi.Maana yake ni kwamba sisi ikija kwaresma ukarimu unaendelea kama kawaida,ikija RAMADHANI ukarimu unaendelea.Sasa vijana wa siku hizi mlio wengi mnapenda kuiga vitu vya kijingajinga bila kuwaza athari za unachokifanya halafu unajidai umeelimika? Kuelimika ni kufanya jambo au kuamua kitu bila kupima athari zake.Na ndio maana kizazi cha sasa kitaendelea kuangamia kwa kukosa maarifa kwa kujitia wajuaji kwa mambo yanayohitaji kutumia akili na busara.
MYTAKE
Kila mtu anao uhuru wa kuwa na imani na dini aitakayo.Kila mtu anatakiwa kuheshimu imani za watu wengine hata kama huipendi,kila mtu abaki na utashi wake wa kuabudu.Chokochoko za kidini zikianza usifikirie wewe uliye na fake ID utakuwa salama maana na wewe utakuwa ni mhanga wa hiyo vita ya kidini.Katika vitu ambavyo tunapaswa kuviepuka ni kuleta MIHEMKO kwenye masuala ya kiimani/kidini na kuleteana dharau zisizo na msingi. Umri wa ujana wako unapaswa umuombe MUNGU uwe na BUSARA na HEKIMA.