Kibumbula
JF-Expert Member
- Mar 26, 2018
- 3,697
- 3,413
Utakula kwenye mgahawa wa nani kama wenye migahawa wamekatazwa kuifungua mchana?Hao wasio waislam wamekatazwa wasile?
Utakula kwenye mgahawa wa nani kama wenye migahawa wamekatazwa kuifungua mchana?Hao wasio waislam wamekatazwa wasile?
Unaongea vitu ambavyo huvijui mkuu.Ngoja nikusaidie na wewe ukue kiakili iko hivi kwa upande wa ZANZIBAR migahawa mingi inamilikiwa na waislam na wasio waislam wanamiliki migahawa michache. Kwa kipindi hiki cha mfungo kwa ZANZIBAR kama ilivyo "DESTURI "yao wao hufunga migahawa mpaka mida ya jioni watu wanapofuturu. Kwa hiyo hapa kuna mambo 2Kwa hiyo migahawa inakuwa katikati ya viwanja vya michezo? Au vituo vya magari?.Au haifunikwi juu ya mapaa yake?.Nyie watu mbona mko hopeless hivyoo.
Kwani lazima ule kwenye mgahawa?Kwako huna au huwezi pika?Utakula kwenye mgahawa wa nani kama wenye migahawa wamekatazwa kuifungua mchana?
Mimi ni mkristo. Lakini sipendi kuona kuwa imani hizi tulizonazo zinatufanya tukose busara. Kwa mfano, sipendi kuona tukinyosheana vidole. Iwe wakristo kwa wakristo au wakristo kwa waislamu. Kuna baadhi yetu hatuli nyama siku ya ijumaa kuu. Lakini wapo wanaokula. Hatupaswi kuwanyoshea vidole.wewe dini gani mkuu?
Vizuri kijana kwa kunielewesha baadhi ya mambo ambayo kwangu ni faida pia. Umeongelea zaidi migahawa inayomilikiwa na waislamu ambao kimsingi kwenye kipindi hiki hawastahili kufungua migahawa yao. Vipi kuhusu migahawa inayomilikiwa na wasio waislamu?Unaongea vitu ambavyo huvijui mkuu.Ngoja nikusaidie na wewe ukue kiakili iko hivi kwa upande wa ZANZIBAR migahawa mingi inamilikiwa na waislam na wasio waislam wanamiliki migahawa michache. Kwa kipindi hiki cha mfungo kwa ZANZIBAR kama ilivyo "DESTURI "yao wao hufunga migahawa mpaka mida ya jioni watu wanapofuturu. Kwa hiyo hapa kuna mambo 2
1. Wenye migahawa wengi ambao ni waislam hawawezi kufanya biashara ya chakula muda wa mchana na wanajua kufanya hivyo ni dhambi maana inakuwa kama unachochea watu wasifanye ibada ya funga badala yake upingane na sheri za mfungo.
2. Hakuna mtu asiye muislam ambaye mpaka sasa amekatazwa kula,ingawaje kuna wasiojielewa wanajaribu kutafuta kiki za kipumbavu lakini zimebuma. hoteli za 5 star zipo wazi na hoteli za kitalii zipo na zinaoperate kwa utaratibu maalum. Na mpaka sasa hakuna complain yoyote sanasana sisi wa BARA tumejipa usemaji wa muda kwa mambo ya ZANZIBAR wakti hata kufika hatujafika.
Kwa hiyo befor jumping into conclusions ni vizuri kufatilia jambo kuliko kuongea mambo usiyoyajua. Kwa ZANZIBAR hakuna jipya miaka yote migahawa inafungwa sasa kama wewe ni mgeni jaribu kuulizia historia upate habari.
Hayo ndiyo tusiyoyapenda. Kwa nini unipangie sehemu ya kula?.Binadamu tunatofautiana saana. Kama watu tunalijua hilo,basi pasingekuwa na migahawa, maana kila mtu ana kwake .Ninaomba majibu yetu yawe yenye upeo na sio blah blah.Kwani lazima ule kwenye mgahawa?Kwako huna au huwezi pika?
Mkuu, umefanya vizuri kuleta mambo haya. Tena umemjibu bujibuji kuwa kuota unafanya mapenzi siyo kosa.Vizuri kama unaongozwa na INJILI na mimi Ulamaa nikusaidie wewe kitu kimoja kwamba sisi waislam tunafata utaratibu wa kufunga kulingana na maamrisho ya ALLAH (S.W) na kupitia maandiko matakatifu ya QURAN nakupa elimu ya bure ndugu usome na uelewe usidhani UISLAM hauna misingi yake
Maana ya Funga
Neno swaumu ambalo ni funga katika lugha ya Kiswahili, kilugha lina maana ya kujizuilia. Ama katika sheria, funga [swaumu] ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kujizuilia na vyenye kufuturisha [kufunguza] kuanzia kudhihiri alfajiri [ya pili] mpaka kuchwa [kuzama] kwa jua na kwa kunuilia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).
Historia ya Funga
Kwa hakika funga si ibada ngeni, bali ni ibada iliyofaradhishwa kwa umati zilizotangulia na pia kufaradhishwa katika umati huu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {{Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga [saumu] kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu}} (2:183).
Ama katika umati huu wa Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) funga ilifaradhishwa katika mwezi wa Shaaban mwaka wa pili baada ya Hijrah (2H).
Hukumu ya Funga
Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo katika nguzo za Uislamu, nayo ni wajibu kwa dalili ya kitabu (Qur-aan), Sunnah na Ijmai (makubaliano) ya wanavyuoni wote wa Kiislamu.
1: Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) : {{Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu. Siku chache tu ( kufunga huko)…(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo hii Qur-aani ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. …}(2:183-185) .
2: Na imepokewa hadithi kutoka kwa Abdullah ibn ‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhuma) amesema: Nimemsikia Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) akisema: “Umejengwa Uislamu juu ya nguzo tano; kushuhudia ya kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kwamba hakika ya Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) ni Mtume wa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na usimamishaji Swala na utoaji zakah na kuhiji katika nyumba (tukufu) ya Alkaaba na funga ya Ramadhani. (Al Bukhariy na Muslim).
Na kuna hadithi nyingine nyingi zinazojulisha wajibu huo, na wanavyuoni wote wamewafikiana juu ya uwajibu huo.
Inayemuwajibikia Funga ya Ramadhani
Funga ya Ramadhani inamuwajibikia kila Mwislamu, baleghe, mwenye akili, aliye katika mji wake (asiwe msafiri), mwenye siha (afya – asiwe mgonjwa), asiwe na mambo yanayozuia kuswihi kwa funga (kama hedhi na nifasi kwa wanawake).
Na inatakikana kwa wazazi kuwafundisha kufunga watoto wao wanapofikia umri wa miaka saba (7) na kuwalazimisha hadi ikibidi kuwapiga wanapofikia umri wa mika kumi (10), na hili inabidi pia kuzingatia afya na ukuaji wa mtoto.
Nyudhuru za Kufunga
Nyudhuru za kuacha kufunga zinatofautiana na kila udhuru una hukumu yake, na hapa nitazielezea nyudhuru hizo kwa ufupi.
1. Hedhi (damu ya mwezi) na nifasi (damu ya uzazi). Huu ni udhuru ambao unamlazimisha mwanamke kuacha kufunga, na inakuwa haramu kwake kufunga na iwapo atafunga haitosihi (haitokubaliwa) funga yake, na ni wajibu kwake kulipa funga hiyo.
2. Maradhi au safari. Na mwenye udhuru wa maradhi (yanayotibika kwa kawaida) pamoja na msafiri wanaruhusiwa kutokufunga na itawawajibikia kulipa. Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) :{{Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizoacha kufunga) katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito.. .}} (2:185). Na kama maradhi yatazidi au kumletea madhara iwapo atafunga basi itakuwa lazima kwake kutokufunga.
Ama safari ambayo inaruhusiwa kwa sababu yake kutokufunga, wanachuoni wengi wemesema: Ni safari ya siku mbili kwa ngamia au kwa mwendo wa miguu (mar-hala mbili) ambayo ni sawa na umbali wa takribani kilomita (85km). Na ruhusa hii inapatikana kwa msafiri anayesafiri kwa chombo cha aina yoyote atakachosafiria, ijapo kwa dhahiri safari hiyo haimpi uzito wowote.
3. Vizee (vikongwe) na wenye maradhi sugu (yasiotarajiwa kupoa). Na haya mawili iwapo yanamsababishia madhara, basi ni katika udhuru na ruhusa ya kuacha kufunga, na itamlazimikia atoe fidia kwa kumlisha masikini kibaba (mudi) cha chakula (ambacho ni sawa na uzito wa gramu 600 takribani) au chakula kinachomshibisha masikini mmoja kwa kila siku aliyoacha kufunga.
4. Waja wazito na wanaonyonyesha. Nao ni katika wenye ruhusa ya kutokufunga, na inawabidi kulipa siku walizoshindwa kufunga kwa sababu ya udhuru huo.
5. Iliyemzidia njaa au kiu na akahofia kuangamia, huu pia ni katika udhuru wa kuacha kufunga, bali wamesema wanachuoni kwamba yule mwenye kuhofia kuangamia inakuwa kwake ni wajibu kufungua, na itamuwajibikia kulipa kama mgonjwa.
Nguzo za Kufunga
Nguzo za kufunga ni tatu:
1. Kwanza ni kunuia. Nia ni kukusudia kufunga usiku wa kuamkia siku ya kufunga, kwa funga ya faradhi.
2. Kujizuilia na vyenye kufunguza (kufuturisha).
3. Muda wa kufunga (mchana kuanzia alfajiri mpaka kutwa (kuzama) kwa jua).
Unavyothibiti kuingia Mwezi wa Ramadhani
1. Kwa kukamilika siku thelathini (30) za mwezi wa Shaaban.
2. Kwa kuonekana mwezi mwandamo siku ya 29 ya mwezi wa Shaaban. Imepokewa hadithi na Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) amesema: {Fungeni kwa kuonekana kwake (mwezi mwandamo) na fungueni kwa kuonekana kwake}. (Al Bukhariy na Muslim).
Na mwezi wa kuingia Ramadhani inatosha kuonekana na Muislamu mmoja mwadilifu ama mwezi wa kumalizika Ramadhani ni lazima uonekane na Waislamu waadilifu wawili au zaidi.
Yanayobatilisha (kuharibu) Funga
Mambo yafuatayo hubatilisha (huharibu) funga. Nayo ni:
1. Kula au kunywa kwa kukusudia.
2. Kila kinachoingia tumboni au kooni kwa kukusudia.
3. Kukutana kimwili (kuingiliana) kati ya mume na mke.
4. Kujitoa manii (mbegu za uzazi) au kusababisha kutokwa na manii (kwa kujichezea sehemu za siri, kukumbatiana au kupigana mabusu na kadhalika).
5. Kujitapisha kwa makusudi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) amesema: Amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam): {…na mwenye kujitapisha basi inamuwajibikia kulipa}
(wameipokea maimamu watano).
6. Kutokwa na damu ya mwezi (hedhi) au damu ya uzazi (nifasi).
Wakati wowote yanapomtokea mwanamke mawili hayo, funga yake ya siku hiyo itakuwa imeharibika na itamlazimikia kuilipa siku hiyo baada ya mwezi wa Ramadhani.
Yasiyofunguza
1. Kula au kunywa kwa kusahau. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hurayrah amesema, {amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam): {Mwenye kusahau naye amefunga, basi akila au akinywa na aikamilishe funga yake….} ( Al Bukhariy na Muslim ).
2. Kusukutua au kupandisha maji puani wakati wa udhu (bila ya kubalighisha).
3. Kuoga au kujiburudisha kwa kujimwagia maji katika kiwiliwili (hasa katika maeneo yenye joto kali).
4. Kuonja chakula kwa mpishi (kwa sharti ya kutokumeza alichokionja).
5. Kutokwa na mbegu za uzazi (manii) katika usingizi (ndoto) au bila ya kukusudia.
6. Kuamka na janaba. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mamama Aishah na Ummu Salamah (Radhiya Allahu ‘anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) alikuwa akiamka na janaba kutokana na kukutana kimwili na wake zake, kisha anaoga na kufunga (Al Bukhariy na Muslim).
7. Kupiga mswaki (wakati wowote).
8. Kuchoma sindano ya kawaida ya tiba.
9. Kung’oa jino na mfano wake.
10. Mwanamke kuamka kabla ya kuoga kwa hedhi au nifasi.
Considering the ZANZIBAR population 95% ni Moslems. Hata hao wamiliki wa migahawa wakristo nao wameifunga migahawa yao mpaka kuanzia saa kumi na mbili inakuwa wazi.Na jioni ndio migahawa inasheheni wateja kwa sababu muda huo watu wanakula hadi usiku mwingi.Kwa maneno mengine biashara ya chakula kwa mwezi huu inakuwa na faida zaidi sababu kiwango cha ulaji kinaongezeka.Vizuri kijana kwa kunielewesha baadhi ya mambo ambayo kwangu ni faida pia. Umeongelea zaidi migahawa inayomilikiwa na waislamu ambao kimsingi kwenye kipindi hiki hawastahili kufungua migahawa yao. Vipi kuhusu migahawa inayomilikiwa na wasio waislamu?
Nani kakupangia sehemu ya kula? Unaweza kwenda kwenye jamii yenye tamaduni ya kutokunywa pombe ukawaambia wasikupangie sababu unakunywa pombe?Hayo ndiyo tusiyoyapenda. Kwa nini unipangie sehemu ya kula?.Binadamu tunatofautiana saana. Kama watu tunalijua hilo,basi pasingekuwa na migahawa, maana kila mtu ana kwake .Ninaomba majibu yetu yawe yenye upeo na sio blah blah.
Wadhani sababu ya migahawa ya wasio waislamu kufungwa mpaka saa 12 jioni ni kukosa wateja au wanalazimishwa?Considering the ZANZIBAR population 95% ni Moslems. Hata hao wamiliki wa migahawa wakristo nao wameifunga migahawa yao mpaka kuanzia saa kumi na mbili inakuwa wazi.Na jioni ndio migahawa inasheheni wateja kwa sababu muda huo watu wanakula hadi usiku mwingi.Kwa maneno mengine biashara ya chakula kwa mwezi huu inakuwa na faida zaidi sababu kiwango cha ulaji kinaongezeka.
Naona mavichwa box mnatetea upuuzialiyewaambia wagonjwa wanakula hadharani katika mwezi mtukufu ni nani?
Nadhani ndugu umechanganya mafaili nikusaidie kitu kimojaMkuu, umefanya vizuri kuleta mambo haya. Tena umemjibu bujibuji kuwa kuota unafanya mapenzi siyo kosa.
Pili, turejee kwenye hoja yako, andiko la Qur'an 2:182-185, nimeisoma kwa kutafakari. Sijaona watu wanalazimishwa kufunga, labda kama kiswahili changu hakipo sawa.
Maandiko yanasema atakayefanya vema ni heri kwake.
Aidha, funga ni kwa walioamini. Sasa nani kasema zenji yote wote wanaaamini? Kwa nini kulazimisha mtu asiyeamini awe sawa na wewe uliyeamini?
Mmeagizwa kujizuia na vyakula, hii ina maana unaweza kutana na mazingira ambayo vyakula utapishana navyo, yakufaa ujizuie na siyo kulazimisha asiyeamini awe sawa na wewe unayeamini.
View attachment 782701
Mimi ninadadisi kutokana na majibu yako. Mpaka sasa hivi bado hujaja na majibu yenye mantiki.Nani kakupangia sehemu ya kula? Unaweza kwenda kwenye jamii yenye tamaduni ya kutokunywa pombe ukawaambia wasikupangie sababu unakunywa pombe?
Hizo ndio mamlaka za kule zinavyoamua mkuu mim na wewe tutaendelea kubishana humu JF lakini kila mwaka wao ndio hufanya hivyo ndio taratibu zao walizojiwekea.Wadhani sababu ya migahawa ya wasio waislamu kufungwa mpaka saa 12 jioni ni kukosa wateja au wanalazimishwa?
wewe dadisi tu ila ukweli wa mambo ndio huo.huenda huoni mantiki yangu lakini nachokueleza ndicho kilivyoMimi ninadadisi kutokana na majibu yako. Mpaka sasa hivi bado hujaja na majibu yenye mantiki.
Hizi kauli tushazizoea ni za wale watoto ambao wako kwenye "ADOLESCENT PERIOD"ambapo anajiona ana akili sana,nguvu kuliko hata mama yake aliyemzaa na kumwambia yeye angechelewa angemzaa. Sijaona jipya kwako.Jitahidi ukue.Naona mavichwa box mnatetea upuuzi
Kuna wakati inatulazimu tuu kufumba macho. Ukweli ni kwamba hizo taratibu sio kwamba wamejiwekea. Hizo zimewekwa na watu fulani kwa kudhani kuwa wampendeza Mungu.Hizo ndio mamlaka za kule zinavyoamua mkuu mim na wewe tutaendelea kubishana humu JF lakini kila mwaka wao ndio hufanya hivyo ndio taratibu zao walizojiwekea.
"Tokea 2008 nilivyomaliza A--level."Katika ulimwengu wa sasa hivi dunia imekuwa ni kijiji kimoja kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Katika eneo ambalo ninaishi MBEZI-KImara nimezungukwa na wakristo dhehebu la RC na wasabato,na Lutherans kwa mbali.Nyumba nayoishi inatizamana na muumini "kindakindaki"wa kanisa katoliki. Tokea mwaka 2008 nilivyomaliza A-level hadi leo 2018 ni karibu miaka 10 nashirikiana na ile jamii kiasi kwamba hata habari ya dini ni kama haipo sababu tumetengeneza bond moja kubwa.Wakati wa misiba,sherehe sikukuu za pasaka wananialika tunajumuika na kufurahi.Maana yake ni kwamba sisi ikija kwaresma ukarimu unaendelea kama kawaida,ikija RAMADHANI ukarimu unaendelea.Sasa vijana wa siku hizi mlio wengi mnapenda kuiga vitu vya kijingajinga bila kuwaza athari za unachokifanya halafu unajidai umeelimika? Kuelimika ni kufanya jambo au kuamua kitu bila kupima athari zake.Na ndio maana kizazi cha sasa kitaendelea kuangamia kwa kukosa maarifa kwa kujitia wajuaji kwa mambo yanayohitaji kutumia akili na busara.
MYTAKE
Kila mtu anao uhuru wa kuwa na imani na dini aitakayo.Kila mtu anatakiwa kuheshimu imani za watu wengine hata kama huipendi,kila mtu abaki na utashi wake wa kuabudu.Chokochoko za kidini zikianza usifikirie wewe uliye na fake ID utakuwa salama maana na wewe utakuwa ni mhanga wa hiyo vita ya kidini.Katika vitu ambavyo tunapaswa kuviepuka ni kuleta MIHEMKO kwenye masuala ya kiimani/kidini na kuleteana dharau zisizo na msingi. Umri wa ujana wako unapaswa umuombe MUNGU uwe na BUSARA na HEKIMA.
Hawa ndio waliofunga hawa!!.Hoja mufilisi kama hizi ndizo zinafanya vijana wa kitanzania mshindwe hata kuajiriwa sababu hamna maarifa.Wewe mwenyewe mtupu kichwani huna ujualo kuhusu elimu ya MADRASSA.Buy the way wenye akili kubwa tunafahamu makundi ya waasi duniani yana mkono wa wazungu sasa kwa **** kama wewe kwa kuwa hujielewi huwezi ukaelewa sababu unaendeshwa na mihemko badala ya akili.