Zanzibar: Ole wao watakaouza vyakula mchana

Zanzibar: Ole wao watakaouza vyakula mchana

Status
Not open for further replies.
Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi imesema itawachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wenye migahawa wanaouza vyakula mchana kwani tayari imeshapiga marufuku uuzaji wa vyakula kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

My take :
Pamoja na kwamba Zanzibar ni nchi yenye waislamu wengi lakini hawapaswi kunyanyasa wengine hasa kipindi hiki cha mfungo, Zanzibar wanaenda watu wengi wa imani tofauti kuzuia hawa wenye migahawa kufungua biashara zao kutawafanya wageni na wasio waislamu kukosa sehemu za kula, lakini pia kufunga ni hiari ya mtu, na kufunga ni pamoja na kujizuia hasa pale unapomuona mwenzako anakula.
Waislam ni watu wanaoishi kwa unafiki, na funga yao imejaa unafiki. Wakristo tunafunga, siyo kama utamaduni, bali kwa kusudi maalumu, na hatusumbui mtu.

Nawasihi wajiamini na imani yao, wasilazimishe Imani
 
Anzisha hizo harakati if you are man of actions.Usijipe ujasiri nyuma ya keyboard wakati vitendo zero. I dare to tell you that.
Mkuu usije sababisha mtume wako akatukanwa ni kosa.

Watu kama hao pita nao mbali huenda hajui kua huo ndo taratibu zao tangu mwanzo wao.[emoji120]
 
Waislam ni watu wanaoishi kwa unafiki, na funga yao imejaa unafiki. Wakristo tunafunga, siyo kama utamaduni, bali kwa kusudi maalumu, na hatusumbui mtu.

Nawasihi wajiamini na imani yao, wasilazimishe Imani
Kiongozi wako ndivyo alivyokufundisha hivyo kukashifu imani za watu wengine? Bila shaka na wewe unafiki utakuwa nao maana hata comment yako inaonesha hivyo.
 
Hata waislam tunafunga kwa malengo maalum. Wewe huna elimu katika eneo hilo ndugu unaongea kwa MIHEMKO na ndio maana reasoning yako ipo chini
 
Hata waislam tunafunga kwa malengo maalum. Wewe huna elimu katika eneo hilo ndugu unaongea kwa MIHEMKO na ndio maana reasoning yako ipo chini
Sasa funga ni yako, mimi nisiyefunga nahusikaje na funga yako kama kweli unafunga kwa kumaanisha? Hivi wapi kula imeandikwa ni dhambi?

Naongozwa na injili....

Soma Math 6:16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Kiongozi wako ndivyo alivyokufundisha hivyo kukashifu imani za watu wengine? Bila shaka na wewe unafiki utakuwa nao maana hata comment yako inaonesha hivyo.
Muache unafiki. Soma hii Bukhari uifuate.

Na Quran 3:55 ff
Screenshot_20180521-144651.jpg
Screenshot_20180516-114717.jpg
 
Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi imesema itawachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wenye migahawa wanaouza vyakula mchana kwani tayari imeshapiga marufuku uuzaji wa vyakula kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

My take :
Pamoja na kwamba Zanzibar ni nchi yenye waislamu wengi lakini hawapaswi kunyanyasa wengine hasa kipindi hiki cha mfungo, Zanzibar wanaenda watu wengi wa imani tofauti kuzuia hawa wenye migahawa kufungua biashara zao kutawafanya wageni na wasio waislamu kukosa sehemu za kula, lakini pia kufunga ni hiari ya mtu, na kufunga ni pamoja na kujizuia hasa pale unapomuona mwenzako anakula.

Nenda pale Kanisani St Monica utakula swafi.
 
Usijifanye mjuaji kwa kitu ambacho hukijui kabisa. Migahawa ya kilocal karibia yote inamilikiwa na waislam. Hivo kwa maamuzi yao wenyewe wameamua kuifunga mchana. Ila migahawa ambayo hutumika kuhudumia wageni ipo wazi kama kawaida, mfano six degrees ambayo ipo stone town, sitegemei kama unaijua wala stone town kama unaijua lakini utajua kuwa ni mjini, kgahawa huu upo wazi na unahudumia wanaokula mchana, mmiliki wa huu mgahawa sio muislam lakini ni mstaarabu na humfikii ata chembe ya ustaarabu, hakuna bastard aliekuwa na ustaarabu duniani. Huweka mapazia makubwa ili anaepita nje asijishughulishe na kutizama watu wanachokula akaja kupatwa na hamu ya kula na kuvunja funga yake.

Na cha kushangaza, unalalamika wewe wakati wakiristo Zanzibar hawakuwahi kuilalamikia serikali ikiwa vibarazani wala kwenye medias. Wala hakuna mkiristo anaelalamika kuwa mfungo wa ramadhan kwao ni adhabu, only bastards complain about that. Migahawa ipo, kwako unapo, eti unalalamikia choice ya mtu kufunga duka!
Kwahiyo mwenye huo mgahawa ametoa rushwa ili kukwepa agizo la huyo RC kilaza? Au migahawa ikiwekwa mapazia inakuwa exempted? Tufahamishe vizuri
 
alienda kwa nani?
kuna lodge zina cafteria na bei ni affordable,
Acheni kupokea maneno na kuyasambaza bila ushahidi na utafiti,

Zanzibar kipindi hiki kinachizuiliwa ni kula/kupika hadharani tu lkn haina maana kama watu hawali mchana....sio kweli.
Naomba kujua sababu za kuzuia kupika na kula hadharani
 
Sehemu yyte yenye watu walioenda shule na wakawa educated huwa hawana upuuzi wa kushabikia dini. Nchi siyo ya kidini mnaendekeza udini huu ni ujinga.
Mkuu ufahamu umefungwa ndio maana wapo kimwili sana
 
Katika ulimwengu wa sasa hivi dunia imekuwa ni kijiji kimoja kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Katika eneo ambalo ninaishi MBEZI-KImara nimezungukwa na wakristo dhehebu la RC na wasabato,na Lutherans kwa mbali.Nyumba nayoishi inatizamana na muumini "kindakindaki"wa kanisa katoliki. Tokea mwaka 2008 nilivyomaliza A-level hadi leo 2018 ni karibu miaka 10 nashirikiana na ile jamii kiasi kwamba hata habari ya dini ni kama haipo sababu tumetengeneza bond moja kubwa.Wakati wa misiba,sherehe sikukuu za pasaka wananialika tunajumuika na kufurahi.Maana yake ni kwamba sisi ikija kwaresma ukarimu unaendelea kama kawaida,ikija RAMADHANI ukarimu unaendelea.Sasa vijana wa siku hizi mlio wengi mnapenda kuiga vitu vya kijingajinga bila kuwaza athari za unachokifanya halafu unajidai umeelimika? Kuelimika ni kufanya jambo au kuamua kitu bila kupima athari zake.Na ndio maana kizazi cha sasa kitaendelea kuangamia kwa kukosa maarifa kwa kujitia wajuaji kwa mambo yanayohitaji kutumia akili na busara.
MYTAKE
Kila mtu anao uhuru wa kuwa na imani na dini aitakayo.Kila mtu anatakiwa kuheshimu imani za watu wengine hata kama huipendi,kila mtu abaki na utashi wake wa kuabudu.Chokochoko za kidini zikianza usifikirie wewe uliye na fake ID utakuwa salama maana na wewe utakuwa ni mhanga wa hiyo vita ya kidini.Katika vitu ambavyo tunapaswa kuviepuka ni kuleta MIHEMKO kwenye masuala ya kiimani/kidini na kuleteana dharau zisizo na msingi. Umri wa ujana wako unapaswa umuombe MUNGU uwe na BUSARA na HEKIMA.
Safi kabisa, na ndio maana imani ya mtu isimtie kifungoni yule asieamini katika imani yako, wewe ukifunga isiwe bughdha na kero kwa asie husika nanimani hiyo
 
Katika ulimwengu wa sasa hivi dunia imekuwa ni kijiji kimoja kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Katika eneo ambalo ninaishi MBEZI-KImara nimezungukwa na wakristo dhehebu la RC na wasabato,na Lutherans kwa mbali.Nyumba nayoishi inatizamana na muumini "kindakindaki"wa kanisa katoliki. Tokea mwaka 2008 nilivyomaliza A-level hadi leo 2018 ni karibu miaka 10 nashirikiana na ile jamii kiasi kwamba hata habari ya dini ni kama haipo sababu tumetengeneza bond moja kubwa.Wakati wa misiba,sherehe sikukuu za pasaka wananialika tunajumuika na kufurahi.Maana yake ni kwamba sisi ikija kwaresma ukarimu unaendelea kama kawaida,ikija RAMADHANI ukarimu unaendelea.Sasa vijana wa siku hizi mlio wengi mnapenda kuiga vitu vya kijingajinga bila kuwaza athari za unachokifanya halafu unajidai umeelimika? Kuelimika ni kufanya jambo au kuamua kitu bila kupima athari zake.Na ndio maana kizazi cha sasa kitaendelea kuangamia kwa kukosa maarifa kwa kujitia wajuaji kwa mambo yanayohitaji kutumia akili na busara.
MYTAKE
Kila mtu anao uhuru wa kuwa na imani na dini aitakayo.Kila mtu anatakiwa kuheshimu imani za watu wengine hata kama huipendi,kila mtu abaki na utashi wake wa kuabudu.Chokochoko za kidini zikianza usifikirie wewe uliye na fake ID utakuwa salama maana na wewe utakuwa ni mhanga wa hiyo vita ya kidini.Katika vitu ambavyo tunapaswa kuviepuka ni kuleta MIHEMKO kwenye masuala ya kiimani/kidini na kuleteana dharau zisizo na msingi. Umri wa ujana wako unapaswa umuombe MUNGU uwe na BUSARA na HEKIMA.

Mkuu unacho sema nikweli kabisa kabisa. Hata hapa ninapoishi (TANGA) nimekaa hapa toka 1982. Mtaa ninao kaa una Waislam na sisi Wakristo. Huwezi amini tunavyoshirikia hakuna mwenye dini tunapokuwa pamoja. Wote tunakuwa kitu kimoja haijalishi una dini gani kichwani mwako. Wakati kama huu ikifika sikukuu huwa tuna letewa vitu vya sikukuu na hata wa kati wa pasaka sisi tuna peleka vyakula kwajili ya sikukuu kwao. Christmas ndio kabisa tuna pika na kula pamoja.

Ila tunacho shangaa kwanini kuwe na matangazo ya kukataza kupikwa hadharani na kula hadharani kama kweli tunaishi nchi moja??
Hili halipo sawa udini mnautafuta wenyewe je na kipindi cha Kwaresma mtavumilia mkisikia mikoa yenye Wakristo wengi kumekatazwa kula hadharani??
 
Kwahiyo mwenye huo mgahawa ametoa rushwa ili kukwepa agizo la huyo RC kilaza? Au migahawa ikiwekwa mapazia inakuwa exempted? Tufahamishe vizuri
Alaa, sasa ivi kumbe unatambua kama agizo la RC sio dini? Nakushangaa sana ulipokuwa ukijitia kifua mbele kukashifu watu. Labda hamkumfahamu RC amekusudia nini, au ingekuwa vyema kama ungemuuliza mwenyewe, nafikiri kwenye FB anaweza kuwemo.

Jifunze kutofautisha NENO LA RC NA NENO LA DINI. Uislam haujakataza kumuuzia asiekuwa muislam chakula, uislam unakataza kumuuzia muislam mwenzako chakula wakati wa kufunga hali ya kuwa hana sababu ya kuacha funga.

Miaka nenda miaka rudi, kwenye mahoteli vyakula vinauzwa kama kawaida! njoo utembee, au mwenzangu unaogopa kuvuka bahari?
 
Sasa funga ni yako, mimi nisiyefunga nahusikaje na funga yako kama kweli unafunga kwa kumaanisha? Hivi wapi kula imeandikwa ni dhambi?

Naongozwa na injili....

Soma Math 6:16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Vizuri kama unaongozwa na INJILI na mimi Ulamaa nikusaidie wewe kitu kimoja kwamba sisi waislam tunafata utaratibu wa kufunga kulingana na maamrisho ya ALLAH (S.W) na kupitia maandiko matakatifu ya QURAN nakupa elimu ya bure ndugu usome na uelewe usidhani UISLAM hauna misingi yake

Maana ya Funga

Neno swaumu ambalo ni funga katika lugha ya Kiswahili, kilugha lina maana ya kujizuilia. Ama katika sheria, funga [swaumu] ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kujizuilia na vyenye kufuturisha [kufunguza] kuanzia kudhihiri alfajiri [ya pili] mpaka kuchwa [kuzama] kwa jua na kwa kunuilia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala).

Historia ya Funga

Kwa hakika funga si ibada ngeni, bali ni ibada iliyofaradhishwa kwa umati zilizotangulia na pia kufaradhishwa katika umati huu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {{Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga [saumu] kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu}} (2:183).

Ama katika umati huu wa Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) funga ilifaradhishwa katika mwezi wa Shaaban mwaka wa pili baada ya Hijrah (2H).

Hukumu ya Funga

Funga ya mwezi wa Ramadhani ni nguzo katika nguzo za Uislamu, nayo ni wajibu kwa dalili ya kitabu (Qur-aan), Sunnah na Ijmai (makubaliano) ya wanavyuoni wote wa Kiislamu.

1: Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) : {{Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu. Siku chache tu ( kufunga huko)…(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo hii Qur-aani ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili). Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. …}(2:183-185) .

2: Na imepokewa hadithi kutoka kwa Abdullah ibn ‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhuma) amesema: Nimemsikia Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) akisema: “Umejengwa Uislamu juu ya nguzo tano; kushuhudia ya kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na kwamba hakika ya Muhammad (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) ni Mtume wa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) na usimamishaji Swala na utoaji zakah na kuhiji katika nyumba (tukufu) ya Alkaaba na funga ya Ramadhani. (Al Bukhariy na Muslim).

Na kuna hadithi nyingine nyingi zinazojulisha wajibu huo, na wanavyuoni wote wamewafikiana juu ya uwajibu huo.

Inayemuwajibikia Funga ya Ramadhani

Funga ya Ramadhani inamuwajibikia kila Mwislamu, baleghe, mwenye akili, aliye katika mji wake (asiwe msafiri), mwenye siha (afya – asiwe mgonjwa), asiwe na mambo yanayozuia kuswihi kwa funga (kama hedhi na nifasi kwa wanawake).

Na inatakikana kwa wazazi kuwafundisha kufunga watoto wao wanapofikia umri wa miaka saba (7) na kuwalazimisha hadi ikibidi kuwapiga wanapofikia umri wa mika kumi (10), na hili inabidi pia kuzingatia afya na ukuaji wa mtoto.

Nyudhuru za Kufunga

Nyudhuru za kuacha kufunga zinatofautiana na kila udhuru una hukumu yake, na hapa nitazielezea nyudhuru hizo kwa ufupi.

1. Hedhi (damu ya mwezi) na nifasi (damu ya uzazi). Huu ni udhuru ambao unamlazimisha mwanamke kuacha kufunga, na inakuwa haramu kwake kufunga na iwapo atafunga haitosihi (haitokubaliwa) funga yake, na ni wajibu kwake kulipa funga hiyo.

2. Maradhi au safari. Na mwenye udhuru wa maradhi (yanayotibika kwa kawaida) pamoja na msafiri wanaruhusiwa kutokufunga na itawawajibikia kulipa. Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) :{{Atakayekuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizoacha kufunga) katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito.. .}} (2:185). Na kama maradhi yatazidi au kumletea madhara iwapo atafunga basi itakuwa lazima kwake kutokufunga.

Ama safari ambayo inaruhusiwa kwa sababu yake kutokufunga, wanachuoni wengi wemesema: Ni safari ya siku mbili kwa ngamia au kwa mwendo wa miguu (mar-hala mbili) ambayo ni sawa na umbali wa takribani kilomita (85km). Na ruhusa hii inapatikana kwa msafiri anayesafiri kwa chombo cha aina yoyote atakachosafiria, ijapo kwa dhahiri safari hiyo haimpi uzito wowote.

3. Vizee (vikongwe) na wenye maradhi sugu (yasiotarajiwa kupoa). Na haya mawili iwapo yanamsababishia madhara, basi ni katika udhuru na ruhusa ya kuacha kufunga, na itamlazimikia atoe fidia kwa kumlisha masikini kibaba (mudi) cha chakula (ambacho ni sawa na uzito wa gramu 600 takribani) au chakula kinachomshibisha masikini mmoja kwa kila siku aliyoacha kufunga.

4. Waja wazito na wanaonyonyesha. Nao ni katika wenye ruhusa ya kutokufunga, na inawabidi kulipa siku walizoshindwa kufunga kwa sababu ya udhuru huo.

5. Iliyemzidia njaa au kiu na akahofia kuangamia, huu pia ni katika udhuru wa kuacha kufunga, bali wamesema wanachuoni kwamba yule mwenye kuhofia kuangamia inakuwa kwake ni wajibu kufungua, na itamuwajibikia kulipa kama mgonjwa.

Nguzo za Kufunga

Nguzo za kufunga ni tatu:

1. Kwanza ni kunuia. Nia ni kukusudia kufunga usiku wa kuamkia siku ya kufunga, kwa funga ya faradhi.

2. Kujizuilia na vyenye kufunguza (kufuturisha).

3. Muda wa kufunga (mchana kuanzia alfajiri mpaka kutwa (kuzama) kwa jua).

Unavyothibiti kuingia Mwezi wa Ramadhani

1. Kwa kukamilika siku thelathini (30) za mwezi wa Shaaban.

2. Kwa kuonekana mwezi mwandamo siku ya 29 ya mwezi wa Shaaban. Imepokewa hadithi na Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) amesema: {Fungeni kwa kuonekana kwake (mwezi mwandamo) na fungueni kwa kuonekana kwake}. (Al Bukhariy na Muslim).

Na mwezi wa kuingia Ramadhani inatosha kuonekana na Muislamu mmoja mwadilifu ama mwezi wa kumalizika Ramadhani ni lazima uonekane na Waislamu waadilifu wawili au zaidi.

Yanayobatilisha (kuharibu) Funga

Mambo yafuatayo hubatilisha (huharibu) funga. Nayo ni:

1. Kula au kunywa kwa kukusudia.

2. Kila kinachoingia tumboni au kooni kwa kukusudia.

3. Kukutana kimwili (kuingiliana) kati ya mume na mke.

4. Kujitoa manii (mbegu za uzazi) au kusababisha kutokwa na manii (kwa kujichezea sehemu za siri, kukumbatiana au kupigana mabusu na kadhalika).

5. Kujitapisha kwa makusudi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) amesema: Amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam): {…na mwenye kujitapisha basi inamuwajibikia kulipa}

(wameipokea maimamu watano).

6. Kutokwa na damu ya mwezi (hedhi) au damu ya uzazi (nifasi).

Wakati wowote yanapomtokea mwanamke mawili hayo, funga yake ya siku hiyo itakuwa imeharibika na itamlazimikia kuilipa siku hiyo baada ya mwezi wa Ramadhani.

Yasiyofunguza

1. Kula au kunywa kwa kusahau. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hurayrah amesema, {amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam): {Mwenye kusahau naye amefunga, basi akila au akinywa na aikamilishe funga yake….} ( Al Bukhariy na Muslim ).

2. Kusukutua au kupandisha maji puani wakati wa udhu (bila ya kubalighisha).

3. Kuoga au kujiburudisha kwa kujimwagia maji katika kiwiliwili (hasa katika maeneo yenye joto kali).

4. Kuonja chakula kwa mpishi (kwa sharti ya kutokumeza alichokionja).

5. Kutokwa na mbegu za uzazi (manii) katika usingizi (ndoto) au bila ya kukusudia.

6. Kuamka na janaba. Imepokewa hadithi kutoka kwa Mamama Aishah na Ummu Salamah (Radhiya Allahu ‘anhuma) kwamba Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi Wasallam) alikuwa akiamka na janaba kutokana na kukutana kimwili na wake zake, kisha anaoga na kufunga (Al Bukhariy na Muslim).

7. Kupiga mswaki (wakati wowote).

8. Kuchoma sindano ya kawaida ya tiba.

9. Kung’oa jino na mfano wake.

10. Mwanamke kuamka kabla ya kuoga kwa hedhi au nifasi.
 
Mkuu unacho sema nikweli kabisa kabisa. Hata hapa ninapoishi (TANGA) nimekaa hapa toka 1982. Mtaa ninao kaa una Waislam na sisi Wakristo. Huwezi amini tunavyoshirikia hakuna mwenye dini tunapokuwa pamoja. Wote tunakuwa kitu kimoja haijalishi una dini gani kichwani mwako. Wakati kama huu ikifika sikukuu huwa tuna letewa vitu vya sikukuu na hata wa kati wa pasaka sisi tuna peleka vyakula kwajili ya sikukuu kwao. Christmas ndio kabisa tuna pika na kula pamoja.

Ila tunacho shangaa kwanini kuwe na matangazo ya kukataza kupikwa hadharani na kula hadharani kama kweli tunaishi nchi moja??
Hili halipo sawa udini mnautafuta wenyewe je na kipindi cha Kwaresma mtavumilia mkisikia mikoa yenye Wakristo wengi kumekatazwa kula hadharani??
ndugu wewe ndiye ambaye hujui bado.Aliyetamka watu wasile hadharani ni nani? Kama hujui sema uelimishwe mkuu
 
Ila tunacho shangaa kwanini kuwe na matangazo ya kukataza kupikwa hadharani na kula hadharani kama kweli tunaishi nchi moja??
Hili halipo sawa udini mnautafuta wenyewe je na kipindi cha Kwaresma mtavumilia mkisikia mikoa yenye Wakristo wengi kumekatazwa kula hadharani??
Kwanini wasivumilie na agizo limetolewa na Serikali?
Katika hawa wote wanaochangia hakuna mwenye ustaarabu hata mmoja wote wamejawa na chuki na mihemko ya kipumbavu sana kisa waislamu kufunga.
Shida yao wamekosa elimu, wanaona labda elimu ni kuwa na phd wakati tunawakuta kabisa maprofesa nchini mwetu wanafanya vituko na walokosa elimu wakiwa wapo mbali sana! Wanajisifia usomi kumbe hawana walijualo, sijui kama wanatamabua kama chizi siku zote humuona mwenye akili kuwa ni chizi na yeye ndo ana akili 😀
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom