Zanzibar ni member wa SADC?

Zanzibar ni member wa SADC?

Hata kama inapambwa hii kitu inazo kasoro Pascal . Nenda Zanzibar halafu utamke kuwa makamu wa Rais wa JMT, ana nguvu kuliko Rais wao kama utaeleweka !!.
Jibu lilikuwa very simple tuu... Kwamba rais wa zanzibar atabaki kuwa mkuu kwa mambo yasiyo ya Muungano ama kwa mujibu wa ile katiba ya zanzibar ya 1984
Mama Samia atakuwa mkuu kwa masuala yasiyo ya Muungano...
 
Tanzania ni JMT ya TZ Bara na TZ Visiwani, Rais wa Zanzibar ni mmoja wa viongozi 5 wakuu wa JMT wakiongozwa na President, VP, PM, Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi kwa mujibu wa katiba ya JMT, au Makamo wa I na II kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ambapo rais wa Zanzibar ni mjumbe wa cabinet ya JMT kama Waziri asiye na Wizara maalum. Hivyo amehudhuria kama kiongozi wa kitaifa.
P
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio Bars na Visiwani maana hata Ukerewe ni Tanzania Visiwani
 
Kwa hiyo Spika wa Bunge hayumo kwnye 5 bora za JMT?
Kuna viongozi wakuu wa aina mbili, kisiasa na kiutawala, kisiasa watu wanaitwa viongozi wakuu kitaifa ni watano. Rais, VP, PM, Rais wa Zanzibar na CM.

Kimamlaka nchi ina mihimili mikuu mitatu ambao ni rais Mkuu wa the executive, serikali, Spika Mkuu wa the legislature , Bunge na Jaji Mkuu, Mkuu wa the Judiciary, Mahakama. Hawa wakuu wa mihimili ndio the top kwenye mihimili yao.

Hawa wakuu wa mihimili wako sawa Kimamlaka. Rais, Spika na Jaji Mkuu wana hadhi na mamlaka sawa kupitia kanuni ya usawa wa mihimili "the principal of separation of powers, checks and balances. Rais ndiye mkuu wa wote, huu ndio mhimili uliojichombia chini zaidi,analiunda Bunge analivunja na kuteua mtendaji mkuu wa Bunge. Ndie anateua Jaji Mkuu. Spika ni mkubwa kuliko Waziri Mkuu ndani ya Bunge. Bunge nalo lina ukubwa kuliko rais wa JMT linaweza kumuondoa rais madarakani.
Japo rais anamteua Jaji Mkuu hawezi kumtengua na rais akivunja katiba Jaji Mkuu ndio anamchunguza na kuliarifu Bunge linamuondoa rais madarakani.
P
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar sio Bars na Visiwani maana hata Ukerewe ni Tanzania Visiwani
Hapana Tanzania Visiwani kwa maana ya visiwa ni Zanzibar na Pemba. Hata Mafia japo ni kisiwa au Kilwa sio Tanzania visiwani, Tanzania Visiwani ni lile eneo lililokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pekee.
P
 
Elimu ya uraia kuhusu SADC inahitajika, Kenya na Uganda sio members wa SADC.
P
Asante nikuwa sijui. Ila nijuze marais wangapi wamehudhuria mkutano huu ?
Leaders
 
Hivi Shen kahudhuria mkutano anawakilisha nchi gani?

Uzi tayari

Je, Mhe Mkapa au Kikwete, Karume,kahudhuria mkutano wa SADC kuwakilisha nchi gani? Please try to ask a question which is beneficial for our nation and not otherwise! Pili Zanzibar in Tanzania Visiwani Ndiyo maana ya The UNITED(Muungano) Republic of Tanzania kama ilivyo United States of America ziko 50 + 1(Puerto Rico), na kila State ina serikali ila Federal Government ndiyo mama! I have just tried to simply this for you.
 
Kuna viongozi wakuu wa aina mbili, kisiasa na kiutawala, kisiasa watu wanaitwa viongozi wakuu kitaifa ni watano. Rais, VP, PM, Rais wa Zanzibar na CM.

Kimamlaka nchi ina mihimili mikuu mitatu ambao ni rais Mkuu wa the executive, serikali, Spika Mkuu wa the legislature , Bunge na Jaji Mkuu, Mkuu wa the Judiciary, Mahakama. Hawa wakuu wa mihimili ndio the top kwenye mihimili yao.

Hawa wakuu wa mihimili wako sawa Kimamlaka. Rais, Spika na Jaji Mkuu wana hadhi na mamlaka sawa kupitia kanuni ya usawa wa mihimili "the principal of separation of powers, checks and balances. Rais ndiye mkuu wa wote, huu ndio mhimili uliojichombia chini zaidi,analiunda Bunge analivunja na kuteua mtendaji mkuu wa Bunge. Ndie anateua Jaji Mkuu. Spika ni mkubwa kuliko Waziri Mkuu ndani ya Bunge. Bunge nalo lina ukubwa kuliko rais wa JMT linaweza kumuondoa rais madarakani.
Japo rais anamteua Jaji Mkuu hawezi kumtengua na rais akivunja katiba Jaji Mkuu ndio anamchunguza na kuliarifu Bunge linamuondoa rais madarakani.
P
Nisije nikaonekana nakupinga tuu ila hakuna big 5 politically nchi hii hakuna mamlaka ya kisiasa na ya kiutawala popote nchi hii... Hilo la muhimili wa raisi kuwa ndio mkuu nalo Ni jipya hapa....mihimili yote Ni sawa na mmoja haupasi kuuingulia nwingine... Executive Hana madaraka popote pale... Isipokuwa in the matter of check and balance ambapo hata yeye anachokonolewa sana tuu na bunge hata na mahakama.
 
Msilete kujuana kwenye mali za watu , Sadc si mali ya ccm , ni mali ya nchi wanachama tu , Zanzibar haimo , hizi ndio kero za Muungano , ni kama vile mlivyoihujumu Zanzibar kule CAF
huyu ndugu ni mpotoshaji sana
 
Mkuu Mwala, kwanza uheshimu muungano usiuite feki, bali una changamoto.

Makamo wa rais ni structural issue kuwa rais akitoka upande mmoja wa muungano Makamo lazima atoke upande mwingine, hivyo Samia sio mwakilishi wa Zanzibar kwenye serikali ya JMT ni rais mwenza wa JMT, in case of anything, kama kutimia kwa ile ndoto ya Lema, yeye ndiye anaapishwa kuwa rais wa JMT.

In case rais akitoka Zanzibar, makamu atatoka Bara huwezi sema makamu ni mwakilishi wa bara ndani ya serikali ya JMT.

Mwakilishi halali wa Zanzibar ndani ya serikali ya JMT ni rais wa Zanzibar anayeingia kwenye cabinet ya JMT kama Waziri asiye na Wizara maalum.
P
Mkuu Paschal,
Unajitahidi sana kuelimisha watu humu.Nakuomba sana jitahidi kujipa muda wa kutafakari kabla ya kuanza kueleza unachokielewa kwa sababu kuna watu wanatumia nondo zako kujibia mitihani ilhali baadhi ya unayoyaeleza hayana ukweli wowote.
Kwenye mada inayoendelea nimejitahidi kukufuatilia huku nikiomba Mungu ugundue makosa yako na kujirekebisha ili kuokoa wafuasi wako lakini naona unaendelea kuwazamisha Porini.
Katika Serikali hii ya awamu ya tano hakuna Waziri asiye na wizara maalum.Ni utovu wa Nidhamu kumwita Rais wa Zanzibar kama Waziri asiye na Wizara Maalum.
Katiba inamtambua kama Rais wa Zanzibar na anaingia kwenye Baraza la Mawaziri kwa cheo hicho.
Anaapishwa na Judge Mkuu wa Zanzibar na anaapisha Mawaziri wa Baraza la Mapinduzi.Ana mamlaka ya juu kabisa kwa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ).
Kwa ufupi naomba ufanye utafiti na ujipe muda wa kutafakari kabla ya kuchangia humu ili kudhibiti hadhi yako isiporomoke kwa kasi kama inavyoanza kuonekana kwa siku za hivi karibuni.
 
Ndani ya muungano zanzibar si nchi, nje ya muungano zanzibar ni nchi. Wadhifa wa Shein ndani ya Muungano ni sawa na waziri. Na pia anaweza kuingia bungeni kama waziri. Hivyo Shein ni sawa na waziri.
unaposema nje ya muungano unamaanisha nini wakati Tanganyika na Zanzibar ndizo ziliunda Muungano huo ? je nje ya muungano Tanganyika ina nafasi gani ? kutetea hili jambo unapaswa kujiondoa utu kwanza , si rahisi kulitetea
 
Wanehudhuria hao waliohudhuria, wanatangazwa live
P
Nimeshajulishwa 😎
Marais wa nchi 11 wamehudhuria mkutano wa kilele wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaofanyika jijini Dar es Salaam, Nao ni:

John Magufuli (Tanzania),
Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini),
Azali Assoumani (Comoro),
Danny Faure (Shelisheli),
JoaoManuel Goncalves (Angola).
Edgar Lungu (Zambia),
Felix Tshisekedi (DRC),
Andry Rajoelina (Madagascar),
Emerson Mnangagwa (Zimbabwe),
Filipe Nyusi (Msumbiji) na
Dk Hage Geingob (Namibia).
Huyu wa MALAWI kutokuja nilitarajia
 
Back
Top Bottom