Hakuna kero yoyote hapo, Rais, Makamo na Waziri Mkuu ndio viongozi wakuu wa JMT wakifuatiwa na Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi kwa mujibu wa katiba ya JMT.
Ndani ya setup ya muungano kabla ya vyama vingi, Rais wa Zanzibar alikuwa ndie Makamo wa rais wa JMT. Kufuatia Tanzania kuwa ni nchi ya vyama vingi, kukitokea possibility ya Zanzibar kushikwa na chama kingine, lolote likitokea kwa rais wa JMT, Makamo anaapishwa kuwa rais
Hivyo katiba ikabadilishwa rais wa Zanzibar ni nobody kwenye setup ya muungano ila ni mjumbe wa cabinet, ili kuingia cabinet lazima uwe Waziri, hivyo rais Zanzibar anateuliwa kuwa waziri na kuapishiwa Dodoma ndipo anaingia Cabinet.
Tena nahisi hiki kipengele cha rais wa Zanzibar kuingia cabinet ndio kikwazo kinachosababisha yale mambo, utampaje halafu aje kuhudhuria cabinet?.
Matokeo yake ndio hivyo tena
P