nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 810
- 2,851
Juhudi za Mkoa wa Morogoro kuwakwamua wakulima wa karafuu kupata mnunuzi mwenye bei nzuri zimegonga mwamba baada ya kulazimishwa kuwa lazima karafuu inayozalishwa Morogoro basi iuzwe kwa SMZ ili wao wauze nje kwa bei kubwa zaidi.
Kwa wasiojua, Morogoro vijijini wanazalisha karafuu nyingi kuliko Zanzibar yote. Uongozi wa Morogoro kwa muda mrefu umekuwa ukipambana ili ipate wanunuzi watakaoshindana badala ya kuendelea kulanguliwa na SMZ na wao kupata bei kubwa katika soko la dunia.
Siku ya leo Waziri wa Viwanda, Kilimo na Biashara wa Zanzibar anafanya ziara huko Morogoro vijijini wanakolima karafuu. Awali walilazimisha Uongozi wa Mkoa wa Morogoro uingie nao mkataba wa kuwa hakuna mtu mwingine kununua karafuu ya Morogoro isipokuwa wao SMZ.
Ikumbukwe karafuu ni zao ghali sana duniani. bei yake kimataifa ni kubwa sana. Siku zote SMZ ilikuwa inajificha chini ya mawakala kuinunua lakini sasa wamekuja wenyewe.
sasa huu Muungano ni kama hauna maana kama utakuwa unanufaisha kasehemu kadogo huku majority wakiumia. haya maagizo kutoka juu yanatuumiza watanganyika. Walianza kukopa pesa nyingi kupeleka kwao, wamekuja kubinafsisha bandari zetu zote, wakasema wana ardhi yao Bagamoyo huku watu wa bara hawaruhusiwi kumiliki ardhi kule, sasa leo wamekuja kwenye karafuu Morogoro.