SoC03 Mfumo wa taarifa za kijiografia na jinsi ya kuunganisha mifumo ya wadau wa kilimo na wakulima kwa kumuwezesha mkulima

Stories of Change - 2023 Competition

Hapana What

Senior Member
Dec 24, 2017
119
47
UTANGULIZI
Kuna fasihi pana ambayo inaunga mkono kwamba urasimishaji wa ardhi utawapa wamiliki wa ardhi manufaa ambayo ni pamoja na: dhamana ya kupata mikopo; kuongeza motisha ya kuwekeza kwa
wawekezaji; kupata haki za ardhi kwa wanawake na vijana; kutoa usalama wa kupanua ukodishaji na
masoko ya mauzo yanayohusiana na ardhi huku yakiboresha ufanisi wao kupitia shughuli zao za kila siku kwa kuwasaidia maskini kupata utajiri kwa kugeuza "mtaji wao uliokufa" kuwa halisi "mtaji" kwa maana ya kupata hati miliki inayovutia uwekezaji kutoka nje; na kupunguza migogoro ya ardhi ambayo
itaunda na kukuza maelewano na kukuza amani na utulivu.

KILIMO
Kulingana na matokeo ya Sampuli ya Kitaifa ya Sensa ya Kilimo 2019/20 yanaonyesha kuwa, milioni 7.8 ya kaya ambayo ni (asilimia 65.3) zilishiriki katika shughuli za kilimo. Kati ya jumla ya kaya, milioni 7.7 ziko Tanzania Bara, na 180,219 ziko Zanzibar. Takriban asilimia 65 ya kaya hizo zilijihusisha na kilimo cha mazao, asilimia 33 zilijihusisha na mazao na ufugaji na asilimia 2 walijihusisha na ufugaji pekee. na zaidi ya 90% ya ardhi inalimwa, sekta hii ya kilimo inatoa takriban 65.5% ya ajira na hutoa riziki kwa zaidi ya 70% ya watu, mchango wa asilimia 29 ya Pato la Taifa; 30% ya mauzo ya nje na 65% ya pembejeo kwa sekta ya viwanda (ASDP II).

MANTIKI YA MRADI
Tangu miaka ya 2000 Tanzania imezindua mpango kabambe wa urasimishaji biashara kupitia mkakati wake maarufu MKURABITA pamoja na washirika wa maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali wakiunga mkono juhudi hizo, urasimishaji wa mali ikiwa ni pamoja na urasimishaji wa ardhi na hii kazi na gharama kubwa na zoezi hili kwa kiasi kikubwa linategemea zana za kimsingi za kuchora ramani ya ardhi. Mara nyingi mchakato umekuwa ukitegemea kwa kiasi kikubwa
mfumo wa karatasi ambapo urejeshaji wa habari ni wa kuchosha na rekodi sio sahihi kila wakati
na huleta ugumu ili kufanya maamuzi kwa wakati. Hii imesababisha kuwaacha nyuma wananchi wa vijijini ambapo mali zao nyingi ni mali ya ardhi isiyo na hati miliki ambayo inaweza kufanya mtaji wao kfa mtaji uliokufa. Zaidi ya hayo, upatikanaji wa taarifa(data) kwa wakati na ubora kwa uamuzi imekuwa changamoto.

LENGO LA SERIKALI KUONGEZA KODI
Tanzania pia imepiga hatua mbele kwa Wananchi kulipia kodi ya ardhi na majengo yao kwa maendeleo ya nchi. Ili kulipa kodi ya ardhi na majengo mali hizi lazima ziwe maeneo rasmi.
Mradi huu utarasimisha kwa kiasi kikubwa mali hizi na kuruhusu serikali kukusanya kodi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ulioanzishwa kidigital ambao utatoa nafasi ya kusaidia juhudi za serikali na itakamilisha juhudi hizi za kupanua wigo wa kodi kwa nchi.

PENDEKEZO
Uandaaji wa kitovu thabiti cha data

Kujenga mfumo wa gharama nafuu, jumuishi na wenye kubeba taarifa za ardhi ya wakulima habari zihusuzo mali kama vile nyumba, idadi ya watu, na maelezo mengine muhimu. mfumo wenye kutoa taarifa za kimasoko unaojumuisha wadau wengine kama Benki, Bima, Wawekezaji, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wakulima, Mifuko ya hifadhi ya Jamii, mamlaka za serikali kuu na za mitaa kupata taarifa.
Mfumo huu ni wa Taarifa za Kijiografi wenye uwezo wa kutoa zana madhubuti ya uchambuzi na usimamizi wa matumizi ya ardhi, wenye kuruhusu kima mdau kujisajili kwenye mfumo kwa utaalam wa kiografia (Geographical information system GIS) mfumo huu huwezesha kupima ardhi na kuchukua taarifa za wamiliki kwa kutumia simu (smartphone) kwa lengo la kuwasaidia kupata hati miliki na kuwaunganisha kwa watoa huduma kupata mikopo, masoko, mifuko ya pensheni, bima, huduma za afya n.k.

UKUFANYAJI WA TAARIFA (GMDS APP)
Upatikanaji wa taarifa za wakulima na ukuaji wa mipaka ya mashamba hutegemea mfumo maalumu ulioandaliwa na wenye kufanyika na chombo kinachoruhusu ukusanyaji wa data kwa kutumia vifaa kama simu,viskwambi nk vya Android au ios ili kuwezesha uwasilishaji wa data kwenye kanzi data (seva) ya mtandaoni, hii application ya ukusanyaji data ni maalumu kwa ukusanyaji data za kijographia ambapo itawezesha kupokea dodoso liliandaliwa kwaajili ya ukusanyaji data lilipo kwenye kanzi data na inauwezo wa kukusanya data katika mazingira yasio na mtandayo na yenye mtandao wa intaneti ili kuwezesha mkusanyaji wa data aweze kufanya kazi pasipo na ugumu.

Mfumo wa kukusanya na APP ni kubadilisha fomu za karatasi za jadi na kupelekea kua na fomu za kielektroniki ambazo huruhusu maandishi, data ya nambari, GPS, picha, video, misimbo pau, na upakiaji wa sauti kwenye seva ya mtandaoni. matumizi haya yatasaidia kupunguza gharama za upimiwaji wa ardhi ambapo mkulima hawezi kuzimudu

1688371793823.png

sehemu ya picha inayoonyesha application ikwa kwenye simu

UTOAJI HUDUMA NDANI YA MFUMO
Katika kuhifadhi data kupitia mfumo huu wadau wanaweza kuwasilisha hoja na kupata ufafanuzi kupitia Unstructured Supplementary Service Data (USSD) itakayokua ndio njia ya kupata msaada juu ya jambo, wadau wanaweza kufikia mfumo na kupata taarifa wakati wowote popote walipo. Wakulima wanaweza kupata taarifa mbalimbali mfano ripoti ya kutopatikana au ubora wa mbolea na zana nyingine za kilimo. Wakulima wanaweza kufikia watoa huduma kupitia mfumo na kuwasiliana nao kwa huduma zao kupitia mfumo. Wadau kama vile taasisi za fedha, mifuko ya pensheni, NGOs, wawekezaji, Mamlaka za serikali kutafuta data/maelezo ya maslahi yao. Hii pia itakuwa mchakato wa mwingiliano ambapo timu ya huduma kwa wateja itaunga mkono na kufafanua maswali yoyote yanayoulizwa wateja. Taasisi ya mikopo itapata taarifa kwa mfano ikiwa mkulima ana mkopo mwingine katika taasisi nyingine, ukubwa wa ardhi, aina ya mazao yanayolimwa nk. Serikali itaweza kupata taarifa za wakati halisi kuhusu tija na mahitaji ya wakulima ili waweze kufanya maamuzi muhimu

UWEZO WA MFUMO KUONYESHA UHALISIA
Mfumo utaweza kuunda maumbo (polgons) za ardhi inayoonyesha ukubwa wa ardhi, umiliki, aina za mazao yanayolimwa kulingana na dodoso liliwekwa kwenye kanzi data. kutakuwa na fursa ya kujua vipengele vingine vinavyopatikana kwenye eneo fulani mfano mito, miti n.k. Aina hii ya data itatumika kwa madhumuni tofauti Kwa teknolojia ya picha za satelaiti kwa kua huu mfumo mzima ni wa kijiografia hivyo vifaa vya ukusanyaji data ni vya mfumo huu wenye kwezesha kuona nini kilichopo kwenye uso wa dunia, hizi taarifa zinaweza kutumika na wadau mbalimbali kama vile wadau wa mabadiliko ya tabianchi, miundombinu na mengine ya huduma za kijamii . Data iliyomo kwenye mfumo inaweza kutazamwa kwenye ramani na katika mfumo wa picha za satelaiti na sifa zake zote p
.
1688373474797.png


Mfano wa picha au ramani zinavyo weza kuwekwa kwenye mfumo
USAJILI
Faida ya mfumo huu ni ya kisasa ni kwamba ni uundaji wa benki ya data yenye data/maelezo ambayo yana lenga zaidi upataji wa hatimiliki kwa wakulima na kuunganisha wadau. Badala ya usajili wa karatasi tutaunda sajili ya kielektroniki ambayo ni rahisi. hii itaondoa mchakato wa urasimu wa kupata karatasi kutoka wilaya au serikali kuu ambayo inachukua muda na matatizo katika kurejesha taarifa ambayo inahitaji nafasi ya kuhifadhi faili halisi.
Hii itapunguza gharama na itafanya mchakato kuwa mwepesi. Wakulima wanaweza kupata taarifa zao wakati wowote walipo na wadau watapata taarifa kwa kubofya mara moja tu popote walipo na
eneo wanalotaka kutoa huduma zao kulingana na aina ya mazao wanayotaka kuwekeza na
wataweza kuona ni wakulima wangapi wenye hati miliki, aina za mazao yanayolimwa au kufugwa mifugo, kiwangoi n.k. Kupitia hili, itakuwa rahisi na kwa wakati unaofaa kwa wakulima kupata habari nk.

Mfumo shirikishi
Mfumo unaweza kuzungumza na mifumo mingine yoyote kwa IPI. Hii inafanya kuwa rahisi kupata na
kubadilishana taarifa muhimu toka mifumo mingine na hivyo kupunguza gharama na kuifanya iwezekane fikia taarifa za wakati halisi bila gharama ya ziada. Mfumo unasomana na mifumo mingine kwa mfano mwenye ardhi anatakiwa kuingiza namba ya uraia na kisha mfumo unapokea
nambari na kuzituma moja kwa moja kwa mfumo wa Nida ili kupata usajili kamili wa mkulima katika mfumo huU

UMUHIMU
Mradi huu unalenga kumwezesha mkulima na mshirika yeyote wa kilimo anayekusudia kufanya kilimo biashara kwa mfano mifuko ya hifadhi ya jamii imesajili wanachama katika sekta ya ajira lakini wanachama wengi wako vijijini ambao wangetumia dhamana za ardhi zao nao kuingizwa kwenye hifadhi za mifuko ya kijamii.
ukosefu wa hatimiliki kwa mashamba kwa wakulima hupelekea kushindwa kutoa mikopo ya kibiashara kutokana na kikwazo hicho lakini huu mfumo utasimama kama mwanga kati ya mkulima na wadau, mfano benki hazina taarifa za mtu wanapohitaji kukopesha lakini akiingia kwenye mfumo na kuomba taarifa atazipata kwa kulipa gharama flani.
 
Sasa peleka hili andiko wizarani kama mbunifu ili liweze kusaidia watu na serikali. Kikubwa kuza weredi kwenye wazo hili na omba uatamizi wa wizara
 
Back
Top Bottom