Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
Wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanzania. Wanasahu kuwa hata Tanganyika ilikuwa part ya Zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?
mie naona muungano uvunjike kila watu wajijue wenyewe hili swala limekuwa sugu sana na nashindwa kuelewa bara wana ng'ang'ana nini ili hali kila kukicha tabu haziishi mogogoro haiishi.kila mmoja anahisi anapata zaidi ya mwenziwe.
 
Ndugu yangu hizo ni ndoto za alinacha za Wazanzibari. Jitahidi ujifunze ili ujue maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu mipaka ya nchi. Kwa mataifa yote ambayo yalikuwa makoloni, kwa kadiri ya sheria za kimataifa, mipaka inayotambulika ni ile tu iliyokubaliwa Berlin wakati wakoloni walipokutana na kugawana Afrika. Hizo habari za Sultan wanazijua Wazanzibari kwa nia ya kujifurahisha.
ngugu zanguni wabara tuwe makini. tukivunja muungano, maili 10 kutoka pwani ya bahari ya hindi zitachukuliwa na znz. miji mingi ya pwani na sehemu kubwa ya dar ilikua chini ya sultan. wazanzibari wakifungua kesi UN, hii ya malawi itakua cha mtoto. wana zaidi ya 70% kushinda na kuchukua pwani yote. bila bandari na dar kuna uchumi hapo? tafakari! wakubwa wanaijua siri hii thats why hawataki muungano uvunjike
 
Ngugu yangu hayo ya kuwa wengi waliutaka muungano utakua unawazulia wazanzibari,kwani asilia 69 walisema wanataka muungano wa mkataba na hili hata Jaji Warioba alilisema pale alipotangaza rasimu ya mwanzo ya katiba,Labda nikwambie tu muungano wa mkataba ni kuwa na mamlaka kamili kila nchi na kuwepo mambo madogo ya mashirikiano.Napenda ujue kwamba muungano unaotakiwa na wazanzibar ni wa kijamii au mashirikiano na sio huu wa kisiasa.
Muungano wa kijamii hauwezi kuuvunja lazima hilo ujue kwani tayari tumechanganya damu ila kuchanganya kwetu damu isiwe ndio sababu ya kukubali kuendelea na muungano huu wa kisiasa kwani siasa ndio uchumi wa nchi .kama utasoma historia utaona kwamba kabla ya muungano nchi hizi mbili zilikua zinashirikiana kwa karibu kuliko nchi nyengine zozote za east africa na wala hakukua na bughdha baina ya nchi moja na nyengine,wala hakuna aliekua analalamika ,wabara alikua anakuja zanzibar kufanya shughuli zake na wala haulizwi na mtu halkadhalika na wazanzibar pia.Lakini baada ya muungano tumeona malalamiko hayeshi kila mmoja analalamika upande wake.
Hapo kwenye nyekundu, ndicho hasa ambacho na mimi nakisema. Kwamba wazanzibar, wanaonekana bado wanautaka muungano, hata kuthubutu kutaka hata huo muungano wa mkataba ambao watanganyika hawautaki. Sisi kama watanganyika tunataka either Zanzibar na Tanganyika zote zife, na tuwe na nchi moja Tanzania yenye mikoa 27 bila kuwa na marais wawili, au tuuvunje kabisa huo muungano kila mtu achukue chake. Hii habari ya sijui serikali mbili au tatu, au mkataba, kwetu sisi ni karaha tu. Tumechoka kusikia kelele za muungano. Liweke sawa, principle yetu iwe ni, "you are either on our side, or against us".
kuhusu uhusiano na ukaribu wa tangu enzi, kabla ya muungano, hilo nalifahamu vema na nimemuelekeza punde dadako FaizaFoxy. Idadi kubwa ya wazanzibari, origin yao ni Tanganyika, hilo lipo wazi, lakini sasa tunaposhindwa kukaa kwa amani hata kama ni watoto wa baba mmoja, yafaa kila mmoja achukue hamsini zake au akubali tuwe kitu kimoja. Na si kitu kimoja huku mwingine anaendelea kuwa na sovereignty yake pembeni tena. Ni lazima iwe wazi, kwamba upo upande wetu au upo kinyume nasi, na si habari ya kuwa katikati.
 
Heeeee...! ww wa wapi ww? eti watu wachache,, hicho ndo kipimo? kajipange!!!
Watanzania wengi sana wana tatizo kama lako! Wanasoma na kutoa comments harakaharaka bila kuelewa kwanza muktadha wa statement iliyotolewa. Au wewe hujaona kwamba hiyo hoja imetolewa kama comparative analysis kati ya mkoa wa Mbeya na Zanzibar?

Ninachoongelea hapa ni suala la sehemu ya nchi yenye watu sawasawa na wa mkoa wa mbeya. Kupewa mamlaka ya kujiamulia mambo yao kama nchi, huku wale wa mbeya wakipelekewa hadi mkurugenzi wa wilaya? Hiyo haki inatoka wapi, ilihali wote wapo chini ya nchi moja inayoitwa Tanzania? Jifunze kusoma na kuelewa.
 
Asante kamanda kwa ku-upload hii video.
muungano wa kisawa ni huu hapo chini.. sote kwa pamoja washirika wa muungano tunaongoza jeshi letu.. sote kwa pamoja tunaongoza nchi.. yako wapi leo hii... liliobakia sasa kwa sisi wana wa kizanzibari ni kuendelea kudai cha kwetuna kuwaelimisha tanganyikaz.. mlikua mnatuona machizi but now mpo kila mahala mnajadili tuloanzisha na kuendeleza sisi wazanzibari.. mnaona eihhhhh.. nyote sasa mnajadili hii kitu muungano.. angalia picha hiyoangalia step zote.. nani kamzidi mwenzake hapo.. huo ulikua usAWA.. SASA LEO IWEJE KUJIFANYA KAMIZINGA MNATAKA MPIGIWE NYINYI TUUUU NA MNAUMIA MZENJ AKIPIGIWA.. AKILI NDOGO HIZO KUTOKA KWA WASEMAJI WENU BUT IT IS WHAT IT IS.. TUKO IMARAA WAZANZIBARI TUNASONGA MBELE.. MTATUFATA TUU KUDAI CHA KWENU...
999243_587092064658151_1359582755_n.jpg
 
Watanzania wengi sana wana tatizo kama lako! Wanasoma na kutoa comments harakaharaka bila kuelewa kwanza muktadha wa statement iliyotolewa. Au wewe hujaona kwamba hiyo hoja imetolewa kama comparative analysis kati ya mkoa wa Mbeya na Zanzibar?

Ninachoongelea hapa ni suala la sehemu ya nchi yenye watu sawasawa na wa mkoa wa mbeya. Kupewa mamlaka ya kujiamulia mambo yao kama nchi, huku wale wa mbeya wakipelekewa hadi mkurugenzi wa wilaya? Hiyo haki inatoka wapi, ilihali wote wapo chini ya nchi moja inayoitwa Tanzania? Jifunze kusoma na kuelewa.
Pitia/ soma hii mada. Ni ushauri tu. Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiinimacho-cha-muungano.html
 


Sumbawanga.
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.

Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.

Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari ya muungano kuvunjika.

“Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa wenzetu wa Zanzibar.

Source: Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Binafsi naunga mkono hoja! Zanzibar ina watu wachache kuliko hata mkoa wa Mbeya, inatoa wapi sifa ya kuwa nchi. Iwe tu mkoa wa Tanzania.
Haitasaidia kitu zanzibar kuwa Mkoa kwani hivi sasa tunashuhudia malumbano ya migawanyiko ya mikowa. Tutayawezaje sisi ikiwa tuko na serikali yetu chuki na choyo kinatuandama, wakati huo tena itakuwaje? Si unajuwa tulivyo dhaifu sisi kina yakhe!
 
Wakuu naomba mnisikilize:

Siungi mkono muungano wa serikali mbili kwa sababu hata tukisema tutatue kero za muungano wa haina hiyo leo; kesho zitakuja nyingine na nyingine. Kwa kifupi kero zake ni endelevu!

Mimi nadhani kilichotufanya tuungane kwanza ni kutaka kuonesha njia kwa mataifa mengine ya Afrika. Kuonesha njia ambayo baadaye ingetufikisha pale ambapo Afrika nzima ingekuwa moja. Nyerere alikuwa na haki na wajibu wa kuipoteza Tanganyika ili kuidhihirishia Afrika na dunia imani yake kwenye Muungano wa Afrika! Kipindi kile ilikuwa ni sifa kubwa sana kupigania Umoja wa Afrika.

Sababu ya pili ilikuwa ni ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwa wakati ule!

Sababu zote hizo hapo juu hazina mashiko tena kwenye zama hizi za ubepari! Sasa kwa nini tuendelee kuishi imani zisizokuwepo!

Ikumbukwe kuwa zile juhudi za kuliunganisha bara la Afrika zilikufa hata kabla hazijafika mbali kwa sababu wengi wa waliokuwa wanaamini kwenye umoja wa Afrika walitoweka na mawazo yao!

Hata zile juhudi za kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki hazina uhai tena. Sisi ni mashuhuda wa kifo chake kitakatifu; tunasubiria tu kitangazwe rasmi siku za usoni!

Nauliza maswali hapa: Ni kwa nini kuwepo na muungano ambao mshirika mmoja anakubali kupoteza ili kumwokoa mwingine? Hata kwenye ndoa haiwezekani ndugu ni lazima walete chokochoko mwenzi mmoja akitoweka!
Eti serikali tatu haiwezekani kwa sababu Zanzibar haina uwezo! Ni kwanini nchi ijione haina uwezo wakati ilitafuta uhuru wake ili ijiendeshe?

Kama kujiendesha kwake ni kwa kutegemea taifa lingine haioni kuwa ina uhuru wa bendera tu?
Kama Zanzibar wa hofu wakiungana rasilimali zake kama mafuta n.k zitapotea; je, Tanganyika yenye gesi, mafuta, wanyamapori, makaa ya mawe, madini ndiyo iendelee kujitoa sadaka???! Basi Tanganyika itakuwa ni nchi nzuri sana ya kuishi kwa sababu haina hofu ya kuishiwa rasilimali!

Endapo atajitokeza mtu wa kuainisha pasipo shaka mipaka ya mapato na matumizi baina ya Tanzania Bara, Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitafarijika sana! Nasema hivi kwa sababu ninachokiona mimi ni kuwa chochote kipatikanacho Tanzania Bara ni faida ya wote na cha Zanzibar ni kwa faida ya Zanzibar tu pekee.

Je, hii inaonesha kuwa Tanzania Bara inajiamini kuwa yenyewe ndiyo yenye uwezo wa gharamia serikali ya muungano na inaona fahari kufanya hivyo?! Au labda kuna masuala mengine Tanzania Bara inanufaika nayo ambayo sisi wananchi hatujui!
Je, Zanzibar nayo inaona fahari tu kuhudumiwa kila kitu kwenye muungano na wala haioni kuwa Tanzania Bara imebeba jukumu zito? Na je Zanzibar isipotimiziwa mambo kadhaa watakuwa radhi kulalamika ilhali wamebebwa katika mambo mengi?

Nionavyo mimi kama tatizo ni gharama za kuendesha serikali tatu ambazo ndo halali ni sharti tutafute mfumo wa kudumu kutatua tofauti zetu! Tukumbuke kuwa upande mmoja wa muungano umeingia gharama kubwa kuhudumia serikali ya muungano kwa zaidi ya miaka 49 sasa! Au iaonekana Tanganyika hajichoka kulea muungano na Zanzibar nayo haijachokaa kubebewa!

Tusijidanganye; Tanzania ni jina! Nchi ni sisi wananchi! Na wananchi wa pande zote za Muungano wamechoka kulazimishiwa muungano wa serikali mbili! Tunaowaona wanatetea ni baadhi ya watawala ambao muungano uliopo sasa unawanufaisha kwa namna fulani.
Kama wananchi wengi wanadai muungano hauwatendei sasa inabidi tuseme imetosha tutafute kitakachotupa haki na usawa. Na hiki si kingine zaidi ya nchi zote kuungana na kuwa chini ya serikali moja itakayohakikisha kila raia anakuwa na haki sawa na mwenzake bila kujali atokako!

Ingependeza tuwe na serikali tatu kila nchi ijihudumie kwani kila nchi ilidai uhuru ili iwe huru! Lakini watu wanaeneza mawazo hasi ya ukubwa wa gharama!Umaskini na uvivu wa fikra! Ikumbukwe chochote kizuri ni sharti kiwe na gharama yake; tena gharama kubwa!
Kama tunakimbilia unafuu wa serikali mbili tufahamu wazi kuwa nafuu mara zote ni ghali zaidi na mara zote hazidumu!

Muungano wa serikali mbili vilio vya unyonyaji! Muungano wa serikali tatu tunaogopa gharama! Basi muungano unaotufaa ni wa serikali moja. Kama hatuwezi muungano wa serikali moja, muungano wowote ule utakaokuwepo aidha wa serikali mbili, tatu au zaidi hautatuliza kiu ya wananchi! Narudia tena: Tanzania ni jina; nchi ni wananchi!

Nashangaa nchi zenye watu zinaogopa kujiwekea mifumo ambayo itawastawisha na kumaliza chokochoko kwa visingizio visivyoisha! Ina maana pamoja na rasili mali tulizonazo viongozi wetu wanataka kututhibitishia kuwa hawawezi kuweka mifumo ya kuliendesha taifa kwa ustawi!

Hoja ya kuwa kuna udugu wa damu kati ya Tanganyika na Zanzibar ni hoja ya kibaguzi kwani uhusiano wa damu upo pia baina ya Tanganyika na nchi nyingine. Swali hapa: Ni kwa nini tusiungane na Kenya, Uganda, Msumbiji, Burundi, Malawi, Zambia, n.k kwa sababu hata huko wapo watanganyika wana ndugu zao?
Kama hoja ni udugu ni kwanini Zanzibar wanapochagua wabunge wa kuja kwenye bunge la Jamhuri wa Muungano, upande wa Tanzania Bara nao wasichague wawakilishi wachache kwenye Baraza la Wawakilishi ili kuukuza zaidi huo unaoitwa udugu???
Udugu unaonufaisha upande mmoja zaidi ya mwingine si mzuri jamani! Tuache propaganda. Kama tunaamini umoja ni nguvu utengano ni udhaifu basi tuungane tuwe nchi moja, serikali moja, rais mmoja na Tanzania moja ili tuwe ndugu kweli!

Watasema ni chuki lakini kama hatuwezi kumaliza tofauti zetu kwa kuunda serikali tatu au moja basi ni bora kila nchi ijendee kivyake! Hata Kenya na Uganda ni ndugu zetu lakini hatujaugana nao kutengeneza taifa la kusadikika!

Litakuwa ni kosa sana kuendelea kuwa na muungano ambao upande wa Tanganyika tu ndiyo unaendelea kupoteza historia yake wakati mshirika wake Zanzibar akibakiwa na ziada hata kama ni sawa na wilaya moja ya Tanganyika!

Wakuu; naombeni kuwasilisha hoja!
 
Hapo kwenye nyekundu, ndicho hasa ambacho na mimi nakisema. Kwamba wazanzibar, wanaonekana bado wanautaka muungano, hata kuthubutu kutaka hata huo muungano wa mkataba ambao watanganyika hawautaki. Sisi kama watanganyika tunataka either Zanzibar na Tanganyika zote zife, na tuwe na nchi moja Tanzania yenye mikoa 27 bila kuwa na marais wawili, au tuuvunje kabisa huo muungano kila mtu achukue chake. Hii habari ya sijui serikali mbili au tatu, au mkataba, kwetu sisi ni karaha tu. Tumechoka kusikia kelele za muungano. Liweke sawa, principle yetu iwe ni, "you are either on our side, or against us".
kuhusu uhusiano na ukaribu wa tangu enzi, kabla ya muungano, hilo nalifahamu vema na nimemuelekeza punde dadako FaizaFoxy. Idadi kubwa ya wazanzibari, origin yao ni Tanganyika, hilo lipo wazi, lakini sasa tunaposhindwa kukaa kwa amani hata kama ni watoto wa baba mmoja, yafaa kila mmoja achukue hamsini zake au akubali tuwe kitu kimoja. Na si kitu kimoja huku mwingine anaendelea kuwa na sovereignty yake pembeni tena. Ni lazima iwe wazi, kwamba upo upande wetu au upo kinyume nasi, na si habari ya kuwa katikati.

Mlipeleka mawazo hayo kwa warioba?hapo kwenye nyekundu ni matokeo ya hadidu rejea za tume muungano uboreshwe usivunjwe ili kuuboresha wazbr wameamua mkataba kwenye maoni,je watanganyika mlitoa maoni yepi?zanzbr kwanza.
 
Sijataka kwenda kujibu hii hoja kule kwenye thread iliyowekwa na Wiliam Malecela. Lakini ukweli ni kwamba mfumo wa serikali tatu, ni mfano kutoka EU. Ambao hadi hivi sasa hata currency yao ni moja kwa nchi zote za EU, na wana serikali ya EU huku wakiwa bado kila nchi ina serikali yake binafsi. Likewise, na sisi tutakuwa na serikali ya muungano huku tukibaki na serikali za nchi zetu.
 
Mlipeleka mawazo hayo kwa warioba?hapo kwenye nyekundu ni matokeo ya hadidu rejea za tume muungano uboreshwe usivunjwe ili kuuboresha wazbr wameamua mkataba kwenye maoni,je watanganyika mlitoa maoni yepi?zanzbr kwanza.
Kulikuwa na maoni ya aina tatu kutokea Tanganyika, wengi wakitaka muungano uvunjwe, wachache wakitaka serikali tatu (CHADEMA), na wengine wakitaka serikali moja. Serikali mbili zilipendekezwa na CCM peke yao. Na haya yalisemwa na walioba pia wakati wa uzinduzi wa rasmu ya katiba, na akasema kwa kuangalia strength na weakness ya kila pendekezo, wameonelea kwamba hoja ya serikali tatu ndiyo inafaa zaidi. Kwahiyo tulisema lakini wachambuzi wa mambo walifanya maamuzi yao tofauti.
 
wanasahau kuwa zanzibar ilikuwepo kabla ya tanzania. Wanasahu kuwa hata tanganyika ilikuwa part ya zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?
naona kabang yako inakubipu ama kuwasha. Ni lini tanganyika ilikuwa sehemu ya upuuzi wa kwenu zenji? Natamani nije na bomu hapo uislamuni niwape ndonga hadi muache huu ujinga wenu. Nani aliwaambia sisi tunapenda 0713?????????????????????????????? Kabang!
 
Wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanzania. Wanasahu kuwa hata Tanganyika ilikuwa part ya Zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?



Fafanua hapo kwenye red....:A S-frusty:
 
PRINTABLUE, kama hutajali naomba uondoe neno uislamuni kwenye hiyo post namba 116. Tusiingize udini kwenye suala hili. Tujadili kwa kuzingatia hali halisi ya maisha na historia, na si udini. Kama mna differences nyingine na Faizafaxy basi mrushiane madongo bila kuingiza udini. Sorry for that mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom