Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
Tatizo lako kubwa ni kuwa umejazwa ujinga ndani ya kichwa chako na wewe umeupokea mzima-mzima.

Ni vigumu sana kuanza kukusomesha historia ya uhakika, lakini hapa umefika, utalipata somo hilo.

Kwanza, elewa kuwa umedanganywa kuwa Waarabu "walifikia", napenda kukujuza kuwa Waarabu hawakufikia pahala, Waarabu hii Afrika ni yao na hata jina la Afrika linatokana na Kiarabu na Uarabu si nchi, Uarabu ni lugha, hapa Afrika lugha inayoongewa na wengi kuliko wowote ni Kiarabu na Waarabu wako wengi Afrika kuliko kwingine kokote. Na nna-kuhakikishia hawakuja kama ulivyodanganywa.

Isitoshe, hivi wewe katika akili yako, aje Mwaarabu asafiri kwa miguu kutoka Bwagamoyo mpaka Kigoma na Kongo, akamate watumwa njiani kote huko, vijikaka vya kibantu vilivyojaa vigimbi kwa kumbizana na ndezi, wawakamate tu wawapeleke kama mizoga? inakuingia akilini? wakati hao hao wanaoambiwa walikuwa wakikamatwa utumwa tunasoma kuwa walifanya "resistance" walipokuja wazungu (soma visa vya Mkwawa, Kimweri, Majimaji, Mirambo na wengineo). Sasa jiulize, hivi vipi hawakufanya "resistance" kwa Waarabu wafanye ressistance kwa wazungu?

Ukipata jibu, njoo, tuendelee na darsa.
Nimesoma neno kwa neno, toka mwanzo hadi mwisho sijaona hoja yako ni nini zaidi ya dharau tu! Nimekwambia Waarabu waliwachukua baadhi ya waafrica wakawatumia kuwakamata baadhi ya waafrica wenzao. Wewe unaniuliza waarabu wangewezaje kukimbizana na waafrika ambao wamezoea kukimbiza ndezi. Sasa hapa tunaongea lugha gongana au kitu gani?
 
Kitendo cha Zanziba kuifanya nchi. Ni upotevu wa pesa za kuendesha hiyo nchi. Watanganyika tunapata hasara.
 
Bora iwe kijiji au kitongoji!!! hahahaa jiti limewabana serikali ya muungano.

mimi nasema turejeshewe tanganyika yetu, Zanzibar imemshinda Nyerere had anastaafu kaiacha ikiwa kama ni Nchi huku akiyspinga maoni ya G55.

Wale jamaa tunawachukia bure wana hoja za msingi, na taifa halipimwi kwa idadi ya watu kuna Nchi haizid watu elfu kumi na ina kiti U.N.

Itabidi twende U.N tuwaambie iwe wilaya ya Tanzania??

Tokea afe Nyerere na Karume Muungano umekufa wamekuja kuuzika wazanzibari 2010 walipobadilisha katiba yao na kusema zanzibar ni Nchi!! mfaateni Pinda atakusaidieni juu ya hili.

Tanganyika kwanza.

Mkuu ID yako ilikuwa likizo. Baada ya zile nyingine kula Ban jana naona umekurupuka na hii
 
Nimesoma neno kwa neno, toka mwanzo hadi mwisho sijaona hoja yako ni nini zaidi ya dharau tu! Nimekwambia Waarabu waliwachukua baadhi ya waafrica wakawatumia kuwakamata baadhi ya waafrica wenzao. Wewe unaniuliza waarabu wangewezaje kukimbizana na waafrika ambao wamezoea kukimbiza ndezi. Sasa hapa tunaongea lugha gongana au kitu gani?

Hapana hiyo si dharau, ni sifa a mababu zetu.

Mbona kipande hiki chenye swali hujakijibu?

inakuingia akilini? wakati hao hao wanaoambiwa walikuwa wakikamatwa utumwa tunasoma kuwa walifanya "resistance" walipokuja wazungu (soma visa vya Mkwawa, Kimweri, Majimaji, Mirambo na wengineo). Sasa jiulize, hivi vipi hawakufanya "resistance" kwa Waarabu wafanye ressistance kwa wazungu?

Ukipata jibu, njoo, tuendelee na darsa.
 
Hapana hiyo si dharau, ni sifa a mababu zetu.

Mbona kipande hiki chenye swali hujakijibu?



Ukipata jibu, njoo, tuendelee na darsa.
Faizafox sikuona hoja ya kujibu katika hilo. Maana inaonekana unashindwa kutofautisha invasion ya wajerumani na ile ya waarabu. Waarabu hawakuja kama wavamizi wa moja kwa moja kama walivyofanya wajerumani ambao walikuwa wanaingia moja kwa moja na kutaka kuwageuza wenyeji kuwa chini ya utawala wao. Wakatumia hadi ubabe. Lakini waarabu wenyewe walikuja na maneno mazuri, vitu vizuri kama vile vioo vya kujitazamia, shanga nk, na kuwadanganya waafrika kwamba wanawapeleka kwenye neema, na mahali penginepo, walifanya alliance na waafrika wachache waliodanganyika na vizawadi vidogo vidogo kama vile shanga na nguo, na kuwatumia hao kwenda kuwakamata waafrika wengine. So haikuwa atack kama ile ya wajerumani, ya kuja na bunduki na kutaka kuingia kinguvu, waarabu walikuja kama wafanyabiashara, wakavaa ngozi ya kondoo huku ndani yao ni mbwa mwitu.
 
Tatizo lako kubwa ni kuwa umejazwa ujinga ndani ya kichwa chako na wewe umeupokea mzima-mzima.

Ni vigumu sana kuanza kukusomesha historia ya uhakika, lakini hapa umefika, utalipata somo hilo.

Kwanza, elewa kuwa umedanganywa kuwa Waarabu "walifikia", napenda kukujuza kuwa Waarabu hawakufikia pahala, Waarabu hii Afrika ni yao na hata jina la Afrika linatokana na Kiarabu na Uarabu si nchi, Uarabu ni lugha, hapa Afrika lugha inayoongewa na wengi kuliko wowote ni Kiarabu na Waarabu wako wengi Afrika kuliko kwingine kokote. Na nna-kuhakikishia hawakuja kama ulivyodanganywa.

Isitoshe, hivi wewe katika akili yako, aje Mwaarabu asafiri kwa miguu kutoka Bwagamoyo mpaka Kigoma na Kongo, akamate watumwa njiani kote huko, vijikaka vya kibantu vilivyojaa vigimbi kwa kumbizana na ndezi, wawakamate tu wawapeleke kama mizoga? inakuingia akilini? wakati hao hao wanaoambiwa walikuwa wakikamatwa utumwa tunasoma kuwa walifanya "resistance" walipokuja wazungu (soma visa vya Mkwawa, Kimweri, Majimaji, Mirambo na wengineo). Sasa jiulize, hivi vipi hawakufanya "resistance" kwa Waarabu wafanye ressistance kwa wazungu?

Ukipata jibu, njoo, tuendelee na darsa.

Hiki kichwa Kweli either katoroka milembe au binge la genius. Kazi kwenu . Mie nduki
 
Mtoto hata akijitambulisha kwa watu kuwa yeye ni baba, bado haisaidii. Cha msingi hapa ni kuangalia katiba ya Muungano inasemaje, sio katiba ya Zanzibar inasemaje!

You're totally lost.

Hapo hakuna cha mtoto kujitambulisha baba kwa sababu Zanzibar haijawahi kuwa mtoto in the first place.

Kabla ya kuungana Zanzibar ilikuwa nchi kama Tanganyika.

Tena kama wewe ni Mtanganyika ujionee aibu mwenyewe maana baada ya muungano Tanganyika ilikufa kifo cha mende lakini Zanzibar iliendelea kuwepo mpaka sasa.

Wakati wewe unaangalia katiba ya muungano ambayo haina hata meno, Zanzibar wanaangalia Katiba ya Zanzibar iliyoboreshwa mwaka 2010 na kuifanya Zanzibar nchi kama ilivyokuwa zamani.

Mnang'ang'ania kuwa na Zanzibar kwani ya baba yenu?

Kama umechokwa ni umechokwa tuu hata ung'ang'anie vipi hutapendwa tena. Sana sana utaishia kubaka.
 
Naunga mkono mia kwa mia pendekezo kuwa Zanzibar iwe ni mkoa. Kama Pemba itaonewa katika uongozi wa huo mkoa mpya, basi Pemba iwe ni mkoa peke yake, na Unguja iwe ni mkoa wa kujitegemea pia.

Lazima tutambue ukweli kwamba katika huu Muungano, Tanganyika ilijitolea sana kwa kujilinganisha na Zanzibar, na inaonekana hata Zanzibar haioni hilo.

Kama Zanzibar hawataki, basi wajitoe na tuwe na nchi mbili. Zenji wasiogope. Wapemba wataendelea na biashara zao bara. Tunawahitaji.
 
ni maoni kama yalivyotolewa; kama yanaboresha muundo wa MUUNGANO yatumike!
 
Ngugu yangu hayo ya kuwa wengi waliutaka muungano utakua unawazulia wazanzibari,kwani asilia 69 walisema wanataka muungano wa mkataba na hili hata Jaji Warioba alilisema pale alipotangaza rasimu ya mwanzo ya katiba,Labda nikwambie tu muungano wa mkataba ni kuwa na mamlaka kamili kila nchi na kuwepo mambo madogo ya mashirikiano.Napenda ujue kwamba muungano unaotakiwa na wazanzibar ni wa kijamii au mashirikiano na sio huu wa kisiasa.
Muungano wa kijamii hauwezi kuuvunja lazima hilo ujue kwani tayari tumechanganya damu ila kuchanganya kwetu damu isiwe ndio sababu ya kukubali kuendelea na muungano huu wa kisiasa kwani siasa ndio uchumi wa nchi .kama utasoma historia utaona kwamba kabla ya muungano nchi hizi mbili zilikua zinashirikiana kwa karibu kuliko nchi nyengine zozote za east africa na wala hakukua na bughdha baina ya nchi moja na nyengine,wala hakuna aliekua analalamika ,wabara alikua anakuja zanzibar kufanya shughuli zake na wala haulizwi na mtu halkadhalika na wazanzibar pia.Lakini baada ya muungano tumeona malalamiko hayeshi kila mmoja analalamika upande wake.
Pamoja na malalamiko haya yote, wakati tume ya katiba ikiwa Zanzibar, ilikuwa ni aghalabu kuwasikia wazanzibar wakipendekeza muungano uvunjwe. Wengi wao walikuwa wanaishia kutaka uboreshwe, akiwemo Seif. Sasa ninachojiuliza, kama hadi leo mnaona muungano unawaumiza mbona hamuamui kujitoa? Kwani kinachowazuia ni nini? Watanganyika wanalalamika usiku na mchana kwamba Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika na wanataka muuangano uvunjwe, mbona nyie hamuungi mkono kampeni hizo?
 
Hapa naona kunatatizo! Wanaojiita wazanzibari saivi wanataka mwarabu wa Oman arudi. Wanajua wakiongea kiarabu watakuwa watuwema bila kujua uarabu ni lugha ya kihuni tu. Sasa wanaotaka Zanzibar iwe nchi waende Oman na sisi tubaki na mikoa yetu ya Unguja na Pemba!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Tanzania ni wachanga sana katika mambo ya Inchi moja kuungana na Inchi ingine na inchi moja kati ya hizo ikakubali kupoteza jina lake kwa sababu tu ya ukubwa wake. Naturally samaki mkubwa anammeza samaki mdogo lakini kwa muungano huu kati ya Zanzibar na Tanganyika samaki mdogo kammeza samaki mkubwa.
Huyu samaki mdogo kutokana na udogo wa umbo lake ameshindwa kummeza samaki mkubwa na amebaki kuendelea kumlalamikia samaki mkubwa kuwa anataka kummeza.
Ukianzisha kitu ambacho hakijawahi kuanzishwa na inchi yoyote Duniani basi ujue hilo jambo lina ambiguity (maana zaidi ya moja). Hutuwezi kuanzisha muungano wenye maana zaidi ya moja. Hatuwezi kuwa na marais watatu na katiba tatu katika inchi moja. Au marais wawili makamu wa rais wawili katika inchi moja.
Tujiulize wenzetu walifanyaje katika muungano wao. Tuangalie inchi za ulaya, China na Marekani walifanyaje katika kuungana kwao. Hawa hawana kero za muungano kwa sababu hawakuwa na muungano ambao ni ambiguous.
Tufanye kama Marekani, tuigawe inchi yetu katika majimbo na majimbo haya yawe na nguvu ya kujiendesha yenyewe yakiwa chini ya rais moja. Vinginevyo Tanganyika ibaki kama inchi na rais wake na Zanzibar ibaki kama inchi na rais wake ingawaje watakaoumia zaidi ni Wazanzibar kwa sababu utajitokeza uunguja na upemba na pia uzanzibara na uzanzibari.
Hali kadhalika wazanzibari waliowekeza Bara hawatakaa salama. Haya aliyasema hayati Mwalimu Nyerere.
Tusiogope kufanya mabadiliko kwa sababu waasisi wa muungano wetu walikuwa na sababu zao za kuanzisha muungano na hasa swala zima la usalama wa inchi zote mbili jambo ambalo halipo tena baada ya kukoma au kupungua kwa viongozi wa Afrika kupinduliwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom