Hapo kwenye nyekundu, ndicho hasa ambacho na mimi nakisema. Kwamba wazanzibar, wanaonekana bado wanautaka muungano, hata kuthubutu kutaka hata huo muungano wa mkataba ambao watanganyika hawautaki. Sisi kama watanganyika tunataka either Zanzibar na Tanganyika zote zife, na tuwe na nchi moja Tanzania yenye mikoa 27 bila kuwa na marais wawili, au tuuvunje kabisa huo muungano kila mtu achukue chake. Hii habari ya sijui serikali mbili au tatu, au mkataba, kwetu sisi ni karaha tu. Tumechoka kusikia kelele za muungano. Liweke sawa, principle yetu iwe ni, "you are either on our side, or against us".
kuhusu uhusiano na ukaribu wa tangu enzi, kabla ya muungano, hilo nalifahamu vema na nimemuelekeza punde dadako
FaizaFoxy. Idadi kubwa ya wazanzibari, origin yao ni Tanganyika, hilo lipo wazi, lakini sasa tunaposhindwa kukaa kwa amani hata kama ni watoto wa baba mmoja, yafaa kila mmoja achukue hamsini zake au akubali tuwe kitu kimoja. Na si kitu kimoja huku mwingine anaendelea kuwa na sovereignty yake pembeni tena. Ni lazima iwe wazi, kwamba upo upande wetu au upo kinyume nasi, na si habari ya kuwa katikati.