Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,210
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.

Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.

Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari ya muungano kuvunjika.

"Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa wenzetu wa Zanzibar.

Source: Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Maoni:
Binafsi naunga mkono hoja! Zanzibar ina watu wachache kuliko hata mkoa wa Mbeya, inatoa wapi sifa ya kuwa nchi. Iwe tu mkoa wa Tanzania.
 
Naona Wazimu tayari kichwa tele. Watu Kama Hawana cha kuzungumza bora wanyamaze kuliko kuzungumza Kama wako club ya pombe wana kunywa CHIBUKU. Pinda mmoja huyu
 
Inawezekana kabisa walitoa hayo mapendekezo hawajawahi kuisoma katika ya Zanzibar.

Pengine hata hawajui kama kuna katiba ya Zanzibar inayotambua Zanzibar kama nchi.

Mnapoteza muda kuongea muungano mfu. Ikitokea mkiongelea muungano ongeleeni in past tense.

[video=youtube_share;Vhs8BMxY4Fg]http://youtu.be/Vhs8BMxY4Fg[/video]
 
Bora iwe kijiji au kitongoji!!! hahahaa jiti limewabana serikali ya muungano.

mimi nasema turejeshewe tanganyika yetu, Zanzibar imemshinda Nyerere had anastaafu kaiacha ikiwa kama ni Nchi huku akiyspinga maoni ya G55.

Wale jamaa tunawachukia bure wana hoja za msingi, na taifa halipimwi kwa idadi ya watu kuna Nchi haizid watu elfu kumi na ina kiti U.N.

Itabidi twende U.N tuwaambie iwe wilaya ya Tanzania??

Tokea afe Nyerere na Karume Muungano umekufa wamekuja kuuzika wazanzibari 2010 walipobadilisha katiba yao na kusema zanzibar ni Nchi!! mfaateni Pinda atakusaidieni juu ya hili.

Tanganyika kwanza.
 
Watu kama huyo anaetoa maoni si hasha wanaamini nyerere ni rais hadi leo.
 
Imemshinda nyerere kuifanya mkoa ataifanya yeye aliekuwa hujui hata maana yw nchii nini nenda kamulize Pinda(waziri mkuu) aliposema zanzibar sinchi na kam wasema zanzibar akamulize Benad Membe (waziri waambo ya njee) hiyo TANGANYIKA MPYA(iliozaliwa 1964) Umoja wa Mataifa watumia kiti cha nani,then utasema Zanzibar iwe mkoa ila kabla kuwa mkoa nayeye tukampime akili
 
haya ndo madhara ya mabaraza yaliyobemendwa. hvi kunawatu hawaelewi hali ya kisiasa ilivyosasa kati ya ZNZ na BARA. Nivyema watu wakazungumzia mambo yanayowezekana kufanyika jaman.
 
Na hivi huu muungano una faida zipi kwa sote? bara na visiwani.
 
Wanasahau kuwa Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanzania. Wanasahu kuwa hata Tanganyika ilikuwa part ya Zanzibar.

Mimi nauliza hivi huu muungano una faida zipi kwa wote hata ukae ujadiliwe miaka nenda miaka rudi?
 
Ila kiukweli Zanzibar uwe mkoa maana ni mali ya Tanganyika toka enzi na enzi. Sema wanaotaka iwe nchi ni waarabu na chotara wa kiarabu kama Hamad Rashid ila wenyekisiwa tunajua Tumetokea Tanganyika

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom