Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
Naunga mkono hoja ya Zanzibar kuwa mkoa na napendekeza uitwe mkoa wa Zanzibar!

Sumbawanga.
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.

Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.

Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari ya muungano kuvunjika.

“Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa wenzetu wa Zanzibar.

Source: Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Binafsi naunga mkono hoja! Zanzibar ina watu wachache kuliko hata mkoa wa Mbeya, inatoa wapi sifa ya kuwa nchi. Iwe tu mkoa wa Tanzania.
 
ngugu zanguni wabara tuwe makini. tukivunja muungano, maili 10 kutoka pwani ya bahari ya hindi zitachukuliwa na znz. miji mingi ya pwani na sehemu kubwa ya dar ilikua chini ya sultan. wazanzibari wakifungua kesi UN, hii ya malawi itakua cha mtoto. wana zaidi ya 70% kushinda na kuchukua pwani yote. bila bandari na dar kuna uchumi hapo? tafakari! wakubwa wanaijua siri hii thats why hawataki muungano uvunjike
 
Faiza hivi kumbe kuna wakati unaweza kupingana na CCM?

Nawashangaa ambao hawaelewi kuwa CCM kuna demokrasia na kila mmoja anaweza kutoa maoni yake na mwisho wa siku tunajadili na kuafikiana.

Tatizo mnalo nyinyi mliopo kwa magwanda mpo kama misukule hamuwezi hata kutoa maoni yenu.
 
...Wakati wewe unaangalia katiba ya muungano ambayo haina hata meno, Zanzibar wanaangalia Katiba ya Zanzibar iliyoboreshwa mwaka 2010 na kuifanya Zanzibar nchi kama ilivyokuwa zamani. ...
Tena baada ya kuiboresha katiba ya Zanzibar mwaka 2010, 'rais' wa Zanzibar baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2010 alifunga safari kutoka mkoani Zanzibar ili kuja kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri !! Nchi hiyo, ambayo rais wake anaenda kuapishwa nchi nyingine ili awe anajadiliana na akina Mulugo !! Na iliyomlazimisha kuja huku ni katiba ya Muungano, ambayo wewe umesema haina meno!!! Chezeya Nyerere wewe!
attachment.php
 
Nakubaliana na mwananchi wa Sumbawanga 100% kwamba Zanzibar iwe ni mkoa tu wa Tanzania. Kama watalalamika mno, basi Unguja iwe mkoa na Pemba mkoa mwingine.

Tanganyika tulijitolea mno mwaka wa 1964, kukubali eti sisi ni sawa na kanchi kadogo kama Zanzibar. Wamefaidika kubebwa na Tanzania Bara, kifedha na kwa maslahi mengine ya kisiasa, kiuchumi na kijamii; lakini licha ya hayo hawaridhiki. Wamekuwa kama yule ngamia aliyeomba kuingiza kichwa chake kipate ubaridi kidogo katika hema la Mwarabu, na aliporuhusiwa, akataka kuingia mzima mzima.

Waachiwe waondoke, kama hawataki kuwa mkoa.
 
Tena baada ya kuiboresha katiba ya Zanzibar mwaka 2010, 'rais' wa Zanzibar baada ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2010 alifunga safari kutoka mkoani Zanzibar ili kuja kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri !! Nchi hiyo, ambayo rais wake anaenda kuapishwa nchi nyingine ili awe anajadiliana na akina Mulugo !! Na iliyomlazimisha kuja huku ni katiba ya Muungano, ambayo wewe umesema haina meno!!! Chezeya Nyerere wewe!
attachment.php

Hahahah... I like this
 
Kama ni hivyo basi tueleze ni kwa nini kila wakati wa kikao cha Baraza la Waziri hiki kiti kwenye picha hapo chini huwa kinakuwa wazi?

Mjumbe gani wa Baraza la Mawaziri ambaye huudhurui vikao vya baraza let alone kutuma hata mwakilishi?

Tena ngoja nikuwekee picha za vikao mbalimbali vya baraza hilo.

8E9U1074.JPG

jk3.jpg

d2.jpg

012.jpg

Dkt.jpg

jk.jpg
 
...Mjumbe gani wa Baraza la Mawaziri ambaye huudhurui vikao vya baraza let alone kutuma hata mwakilishi?...
Kwa katiba ya sasa, hata mbunge asipohudhuria vikao haimuondolei ubunge wake, ili mradi alikubali kula kiapo. The same kwa rais wa Zanzibar, amekula kiapo kwa matakwa ya katiba ya Muungano 'isiyo na meno' kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri. Sasa asipohudhuria, ni sawa tu na naibu waziri wa mifugo aliyeshindwa kuhudhuria kikao, lakini bado ni mjumbe kwa kiapo chake mwenyewe, tena alichokifuata Dar es Salaam!
 
Kama ni hivyo basi tueleze ni kwa nini kila wakati wa kikao cha Baraza la Waziri hiki kiti kwenye picha hapo chini huwa kinakuwa wazi?

Mjumbe gani wa Baraza la Mawaziri ambaye huudhurui vikao vya baraza let alone kutuma hata mwakilishi?

Tena ngoja nikuwekee picha za vikao mbalimbali vya baraza hilo.

8E9U1074.JPG

jk3.jpg

d2.jpg

012.jpg

Dkt.jpg

jk.jpg

jamaaa kumbe mtoro sana huyu!
 
Kwa katiba ya sasa, hata mbunge asipohudhuria vikao haimuondolei ubunge wake, ili mradi alikubali kula kiapo.

Wewe kweli hamnazo. Sijui kama ni ignorance ya kujitakia au unafanya makusudi tuu kwa sababu una computer na internet access. Whatever the case, hii ni aibu.

The same kwa rais wa Zanzibar, amekula kiapo kwa matakwa ya katiba ya Muungano 'isiyo na meno' kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri. Sasa asipohudhuria, ni sawa tu na naibu waziri wa mifugo aliyeshindwa kuhudhuria kikao, lakini bado ni mjumbe kwa kiapo chake mwenyewe, tena alichokifuata Dar es Salaam!

Kiapo chake kinasemaje? Unaweza kukiweka hapa ili tukichambue?

Wakati wewe unaongelea theory, wengine tunaongelea practice.

Mtu anakula kiapo cha kuwa mjumbe wa baraza halafu asiuhudhurie vikao, then hicho kiapo ni useless.
 
Imemshinda nyerere kuifanya mkoa ataifanya yeye aliekuwa hujui hata maana yw nchii nini nenda kamulize Pinda(waziri mkuu) aliposema zanzibar sinchi na kam wasema zanzibar akamulize Benad Membe (waziri waambo ya njee) hiyo TANGANYIKA MPYA(iliozaliwa 1964) Umoja wa Mataifa watumia kiti cha nani,then utasema Zanzibar iwe mkoa ila kabla kuwa mkoa nayeye tukampime akili
Yote tisa kumi muulizeni naibu waziri wa elimu jina nani vile?alisema muungano wetu ni kati ya kisiwa cha pemba na zimbambwe!!!!teh,teh,teh,teh.
 
Miaka hii ya karibuni hakuna Mtanganyika anayeutaka Mwungano. Wengi wanaona kuwa Zanzibar ni mzigo wa kuchumi ambao tungeweza kuutua. Tanganyika haifaidi chochote katika Mwungano huu. Zanzibar amekuwa kama motto anayedeka ambaye leo anataka hiki, kesho kile, na wala hakui.Sasa hivi ni Wazanzibari ndiyo wanaoung'ang'ania mwungano huku wakitaka kuishi kwa ile kauli, 'chako chetu, change ni changu'. Sasa ni wakati wa kuwapa masharti Wazanzibari, kama wanataka mwungano, tuwe na nchi moja, serikali kuu moja, na bunge moja. Au la tuwape mkono wa kwa heri, tukutane kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom