Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania

Status
Not open for further replies.
Mliwahi kusikia wapi nchi au taifa likapotea na kuwa mkoa ? Hivi kama Kenya italeta wazo kama hili la Tanganyika kuwa mkoa na rais atakaeongoza atakuwa mkenya hili wazo litaridhiwa na watanganyika ?

Nadhani hata sheria zilizopo huko BMK haziruhusu mjadala wa serekali moja, hii sio bure hili suala halijadili kabisa mbele ya wazanzibari.

P:S
**Huo muungano ni kulamishana tuu, lakini nina uhakika kama kutakupigwa kura ya maoni wengi wataukana na kudai waachwe wajitenge!
 
Kura ya maoni ikipigwa itachakachuliwa na CCM matokeo yatasomeka hv 97 % wanataka muundo wa serikari 2 na 3% wanataka serikari 3 . Sina imani na kura ya maoni Maana matokeo yalishapangwa na Wakora wa ccm.
 
Huu muungano ni wa Nchi moja Kujipendekeza kwa ingine,Zanzibar wanataka Talaka Tanganyika anawang'ang'ania kwa kuwahonga Mijihela kibao wasikimbilie Oman
 
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.

Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.

Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari ya muungano kuvunjika.

“Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa wenzetu wa Zanzibar.

Source: Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania - Habari Ya Ndani - mwananchi.co.tz

Maoni:
Binafsi naunga mkono hoja! Zanzibar ina watu wachache kuliko hata mkoa wa Mbeya, inatoa wapi sifa ya kuwa nchi. Iwe tu mkoa wa Tanzania.

Uko huru kujifurahisha ,lakini jiulize Tanganyika imepotelea wapi? Serekali yenu Nyiyi ni ya ccm Wabara ndio inayo waongoza kwa sasa ,huo Muungano ni Geresha Tuu haupo na umevunjika zamani nchi yenu ni ccm nyie nyote ni watu wa itikadi moja ya ccm.

ukiskia ccm wanasema tunalinda Muungano usivunjike basi ujuwe wanalinda ccm na maslahi yake , Muungano kwatarifa yako haupo nenda deep utaona usiwe mvivu wakutuma mawazo yako ya kufikiri.

Zanzibar ndio nchi ina kila kitu cha kua nchi kamili , jee Tanganyika ina nini ?
 
Ni kweli Zanzibar ni Nchi : swali lako ni Tanganyika ina nini ? Jibu Tanganyika ina pesa za kuilea na kuibembeleza Zanzibar tu , huku hizo pesa zikitumiwa na Zanzibar kujijenga na kujiandalia namna ya kujitenga baada ya Kugundua Kuwa CCM Nao wanapata cha juu kwenye Pesa inayotoka Tanganyika kwenda ZNZ ,kuna mianya mingi ya Ulaji kwenye hizo pesa, ikiwemo pesa ya kutatua Kero za muungano inayopitia Wizara ya muungano, nayo inaliwa kijanja na wajanja huku Kero zikizidi,badala ya kupungua ! Hii mianya ya Ulaji kwa wajanja wachache wa Tanganyika na wajanja wengi wa Zanzibar ,Ndio imepelekea Tanganyika Kuwa Koloni la ZNZ , Maana imenyonywa hadi Damu sasa ,japo Watanganyika wameshituka kidogo lakini hawana jinsi,Maana akina Kinana wamewazidi maarifa kwenye kuukumbatia muungano.
 
Huu ni muungano wa CCM na Zenji Uliosalia tu, muungano wa Nyerere na karume Ulivunjika siku Zenji alipoanzisha Katiba yake, wimbo wake,bendera yake na sasa wanaandaa Sarafu yao,yaani tayari wameshavunja miiko ya mkataba wa Muungano,na Hakuna wa kuthubutu kuwauliza ! imebakia Tanganyika kujikomba komba kwao kwa kuwamiminia pesa nyingi ili wazuge waihadae Dunia Kuwa Muungano upo, wakati hamna kitu tena,yamebakia Mazoea tu !.
 
Muungano wa marekani una Nchi 52 hawana Kero za Muungano,wala Wizara ya muungano,Hakuna Ukwepaji kulipa Gharama za muungano Kama ZNZ Miaka 47 amekwepa lakini Bara wamegwaya kuwauliza,zile Nchi ndogo ndogo hazina Utitiri wa Wabunge,Watumishi, Ulalamishi,Udini,Ubaguzi wala Uchoyo wa Ardhi Kama Zanzibar ,Muungano wao upo kisayansi zaidi, Hakuna cha Nchi kubwa kutumia Chama tawala kulazimisha Jambo hata Nchi kubwa kujipendekeza kwa zile Nchi ndogo haipo. Kwa nini Tanzania hawajifunzi kupitia Muungano huo wa Marekani ?
 
Kama kweli tunahitaji muundo wa muungano uwe imara hatuna budi kuifuta zanzibar iitwe Tanzania kwa sababu hata Tanganyika ilifutwa inakuaje nchi moja iwepo nyingine ife wakati zimeungana au zanzibar yenyewe ina nguvu gani mpaka iiue Tanganyike?

kama Zanzibar inaendelea juwepo na Tanganyika iwepo ili kuwepo na usawa.

Vinginevyo napendekeza zanzibar ife kabisa tuwe na nchi moja ya Tanzania na si bara wala visiwani ila Tanzania tuu.
 
Katika kipindi cha baragumu cha channel 10 wachangiaji wengi walisema kwakuwa Wazanzibar wamekuwa wakilalamika kwamba Tanganyika imevaa koti la muungano,kiasi Raisi wa muungano kimsingi ndiye Raisi wa Tanganyika basi ni vema sasa wazanzibar watupokee koti hili na Bara waunde serikali ya Tanganyika na wao waue jina la Zanzibar waitwe tu Jamhuri ya muungano wa Tanzania basi.
Na Raisi yoyote atakaye chaguliwa atakuwa anakaa Ikulu ya zanzibar.
Tufanye hivyo kwa muda wa miaka hamsini ndipo koti hilo lirudi Tanganyika tena ilikuondoa malalamiko kwamba Tanganyika ina itawala Zanzibar kimabavu na kijanjakijanja.
 
Itakuwa vizuri maana serikali ya tanganyika itakuwa ikishugulikia ya tanganyika pekee, na serikali ya muungano ambayo ni znz itakuwa ikishugulikia garama zote za muungano bila kugusa mapato ya tanganyika.
 
Ni wazo zuri hivi kuna mtu anaangalia uchumi wetu unavyokwenda kwa sintofahamu ya namna wanasiasa wanavyotaka kuendesha nchi.
 
Katika kipindi cha baragumu cha channel 10 wachangiaji wengi walisema kwakuwa Wazanzibar wamekuwa wakilalamika kwamba Tanganyika imevaa koti la muungano,kiasi Raisi wa muungano kimsingi ndiye Raisi wa Tanganyika basi ni vema sasa wazanzibar watupokee koti hili na Bara waunde serikali ya Tanganyika na wao waue jina la Zanzibar waitwe tu Jamhuri ya muungano wa Tanzania basi.
Na Raisi yoyote atakaye chaguliwa atakuwa anakaa Ikulu ya zanzibar.
Tufanye hivyo kwa muda wa miaka hamsini ndipo koti hilo lirudi Tanganyika tena ilikuondoa malalamiko kwamba Tanganyika ina itawala Zanzibar kimabavu na kijanjakijanja.

wewe vipi uko tayari kuvaa koti alivaa babu yako kwa miaka 50 ? Unataka kuvisha watu mitumba imechakaa
 
Hii nayo njema tu twende nayo tuone mchawi anatokea wapi tena.
 
Itakuwa vizuri maana serikali ya tanganyika itakuwa ikishugulikia ya tanganyika pekee, na serikali ya muungano ambayo ni znz itakuwa ikishugulikia garama zote za muungano bila kugusa mapato ya tanganyika.
Gharama zote za Muungano analipa aliye vaa koti la Muungano ambayo litakuwa jukumu la Zanzibar kama ilivyo kuwa kwa miaka hamsini kwa Tanganyika
 
hakuna haja ya hayo yote, cha msingi bunge lisitishwe, katiba ya sasa irekebishwe na kuingizwa kipengele cha kurusu kura ya maoni, then wananchi tuulizwe kama tunautaka muungano ama laa. kama jambo hili litachukua muda mrefu, basi nawashauri wazanzibar washinikize kufanyika kura ya maoni ya kuamua hatma ya muungano kwakuwa wao katiba yao inaruhusu kura ya maoni
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom